Menya viazi na kisha vikate katika vipande. Tia mafuta kwenye chuma cha kukaangia, yakisha pata moto tia viazi nauviache vikaangike mpaka upande mmoja uwe wa brown na kisha geuza upande wa pili na upike mpaka uwe wa brown. Vikisha iva ipua na uweke kwenye kitchen towel ili vikauke mafuta. Kachumbali: Katakata vitunguu katika bakuli na kisha tia chumvi kwa ajili ya kuondoa ukali wa vitunguu. Baada ya hapo vioshe mpaka chumvi yote iishe. osha nyanya, Pilipili tango na kisha katakata slice nyembamba na uchanganye na vitunguu. Baada ya hapo tia chumvi, kamulia limao na uchanganye zote pamoja .Baada ya hapo viazi na kachumbali vitakuwa tayari kwa kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:34:46 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji:
Unga sembe glass 1 Unga ngano glass 1 Sukari glass 1 (unaweza kupunguza kidogo) Maziwa glass 1 Mafuta 1/2 glass Mayai 4 Iliki iliosagwa 2tbs Bp 2tbs
Jinsi ya kupika:
Saga sukari yako uweke kwenye bakuli safi pamoja na mayai. Tumia mashine ya cake kusagia hadi ifure/ivimbe. Weka mafuta saga, weka maziwa saga, weka unga wa ngano na bp(bp imix kwenye unga kabla kumimina kwenye mchanganyiko) changanya vizuri halafu malizia kwa kuweka unga sembe na iliki usage vizuri.
Chukua trey au sufuria safi weka baking paper Mimina mchanganyiko wako na uoke.
Ukiwiva utoe na uwache upoe. Mkate wa sembe utakua tayari kwa kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:37:42 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Maini (Cow liver) 1/4 kilo Vitunguu (chopped onion) 2 Nyanya (chopped tomato) 1 Kitunguu swaum/tangawizi (ginger /garlic paste) 1 kijiko cha chai Mafuta ya kupikia Chumvi Coriander Curry powder 1 kijiko cha chai Limao (lemon) 1/4 Pilipili (scotch bonnet ) 1
Matayarisho
Safisha maini na ukate vipande vidogovidogo na uweke pembeni. Baada ya hapo kaanga vitunguu kidogo(visiwe vya brown) kisha tia ginger/ garlic paste,carry powder kaanga kidogo kisha tia nyanya. Kaanga nyanya mpaka zitoe mafuta kisha tia chumvi, pilipili na vimaji kidogo. Acha vichemke kidogo kisha tia maini na uyapike mpaka yaive. Malizia kwa kukamulia limao na kutia coriander kisha ipua na hapo yatakuwa tayari kwa kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:23:12 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Viambaupishi Vya Masala
Nyama vipande - 3 LB
Mtindi - ½ kopo
Kitunguu (thomu/galic) - 1½ kijiko cha supu
Tangawizi - 1½ kijiko cha supu
Nyanya - 2
Pilipili mbichi - kiasi
Nyanya kopo - 4 vijiko vya supu
Vidonge supu - 2
Pilipili nyekundu paprika - kiasi
Bizari zote saga - 2 vijiko vya supu
Viazi - 4
Mafuta - 2 mug
Samli - ½ kikombe
Vitungu - 6
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika masala
Kwenye sufuria tia nyama, saga nyanya na thomu, pilipili mbichi, tangawizi. Mimina kwenye nyama na mtindi, tia na nyanya kopo, bizari paprika, vidonge vya supu, chumvi kisha changanya vyote pamoja weka motoni. Katika sufuria nyengine tia mafuta na samli kaanga vitungu mpaka viwe rangi ya hudhurungi toa weka pembeni. Kanga viazi weka pembeni. Chukua mafuta kidogo uliyokangia tia kwenye nyama acha katika moto wa kiasi mpaka nyama iwive na maji ya punguke. Tia viazi na vitunguu vivunje vunje tia ndani ya nyama acha moto mdogo.
Vipimo Vya Wali
Mchele - 5 mug
Maji - kiasi
Chumvi - kiasi
Mafuta uliyokaanga vitungu - kiasi
Rangi ya biriani - ¼ kijiko cha chai
*Zafarani - ½ kijiko cha chai
*roweka rangi na zafarani
Namna Ya Kutarisha Na Kupika Wali
Osha mchele roweka muda wa saa. Chemsha maji kama magi 10 hivi na chumvi tia mchele. Uache uchemke ukishaiva kiini nusu, mwaga maji chuja. Mimina juu ya nyama tia rangi na mafuta kwa juu funika. Aacha kidogo katika oveni kwa muda wa dakika 20 hivi kisha epua ikiwa tayari.
Updated at: 2024-05-25 10:37:42 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Samaki (Tilapia 2) Nyanya ya kopo (Tomato tin 1) Kitunguu (Onion 1) Tangawizi (ginger kiasi) Kitunguu swaum (garlic clove ) Mafuta (Vegetable oil) Pilipili (scotch bonnet pepper 1) Tui la nazi zito (coconut milk 2 vikombe vya chai) Curry powder 1/2 cha kijiko cha chai Binzari nyembamba ya unga (ground cumin 1/2 kijiko cha chai Binzari manjano (turmaric 1/2 kijiko cha chai Chumvi (salt) Limao (lemon 1) Giligilani (fresh coriander)
Matayarisho
Marinate samaki na chumvi, limao, kitunguu swaum, tangawizi kwa muda wa masaa 6 au zaidi. Baada ya hapo wakaange au waoke katika oven mpaka waive ila usiwakaushe sana. Baada ya hapo saga pamoja nyanya ya kopo, kitunguu maji, kitunguu swaum na tangawizi. Kisha bandika huo mchanganyiko jikoni na upike mpaka ukauke maji kisha tia mafuta, binzari zote, curry powder, chumvi na pilipili na upike kwa muda wa dakika 5. Baada ya hapo tia maji kidogo (kama 1/2 kikombe) pamoja na tui la nazi. Acha uchemke mpaka tui liive na mchuzi ubakie kiasi. Baada ya hapo waweke samaki kwenye sufuria ya kuokea na kisha umwagie huo mchuzi juu ya hao samaki na owaoke (bake) kwa muda wa dakika 20. Ukisha toa kwenye oven katakata giligilani na utie kwenye hao samaki na hapo watakuwa tayari kwa kuliwa. unaweza kuwala na wali, ugali au chapati
Updated at: 2024-05-25 10:37:48 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Makongoro (miguu ya ng'ombe) kiasi Limao 1 kubwa Kitunguu swaum Tangawizi Chumvi Pilipili
Matayarisho
Safisha makongoro kisha yatie kwenye pressure cooker. Kisha tia kitunguu swaum, tangawizi, chumvi,limao na maji kiasi. Baada ya hapo yachemshe mpake yaive na yawe malaini na pia ubakize supu kiasi inaweza kuchukua kama dk 45 au saa 1 hivi. Baada ya hapo yaipue na upakue supu yako kwenye bakuli katia pilipili kiasi kisha itakuwa tayari kwa kuliwa.
Note: Ukiwa unanunua makongoro hakikisha unachukuwa yale yasiyokuwa na manyoya na pia hakikisha usiyachemshe kupitiliza kwani yakiwa malaini sana utashindwa kuyaenjoy.
Bizari ya unga (cummin powder) - 1 Kijiko cha chai
Mafuta ya kukaangia - Kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Safisha daal kwa kutoa mawe ikiwa yapo, kisha osha na roweka dakika 15 hivi. Kisha chemsha kwa kutia maji, bizari ya manjano, chumvi, pili pili ya unga na maji ya ndimu hadi iive na kuvurujika. Halafu chukua kisufuria na kaanga kitungu, kisha thomu na mwisho tia bizari ya pilau. Kisha mimina mchanganyiko wa kitunguu kwenye sufuria ya daal (iliyokwisha iiva)na uchanganye na iwache motoni kidogo itokote. Ukipenda mimina mchanganyiko kwenye blenda na usage mpaka iwe laini. Tia kwenye bakuli na itakuwa tayari kuliwa na wali na samaki ukipenda
Mapishi ya Biriani Ya Samaki Nguru, Njegere Na Snuwbar (UAE)
Updated at: 2024-05-25 10:23:13 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Mchele wa basmati - 4 cups
Samaki nguru (king fish) - 7 vipande au zaidi
Kitunguu - 5
Nyanya/tungule - 3
Njegere - 1 kikombe
Snuwbar (njugu za pine) - 1 kikombe
Viazi - 2 kata kata mapande makubwa
Tangawizi mbichi - 1 kijiko cha supu
Kitunguu saumu - 1 kijiko cha supu
Pilipili nyekundu - 1 kijiko cha chai
Bizari ya biriani/garama masala - 1 kijiko cha supu
Namna Ya Kupika:
Kaanga samaki mbali kwa viungo upendavyo umkoleze vizuri. Au choma (bake/grill) katika oveni ukipenda. Weka mafuta katika sufuria, tia vitunguu kaanga hadi vigeuka rangi. Gawa sehemu mbili. Sehemu moja bakisha katika sufuria kisha tia tangawizi mbichi na kitunguu thomu ukaange. Tia nyanya kaanga kisha tia bizari zote endelea kukaanga, tia njegere, njugu za snuwbar na ndimu kavu. Tia viazi ulivyokwishakaanga, na vitunguu vilobakia. Tia mapande ya samaki, changanya na masala bila ya kumvuruga samaki. Chemsha wali kisha mwagia juu yake, funika upike ndani ya oveni au mkaa hadi wali uive kama unavyopika kawaida ya biriani. Epua pakua huku ukichanganya na masala ya samaki.
Updated at: 2024-05-25 10:37:47 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Dagaa (dried anchovies packet 1) Unga wa ugali (corn meal flour 1/4 kilo) (unaweza kutumia unga wa choice uipendayo) Nyanya ya kopo (tin tomato 1/2) Kitunguu maji (onion 1) Limao (lemon 1/4) Pilipili mbuzi nzima bila kukata (scotch bonnet pepper1, do not chop) Chumvi (salt 1/4 ya kijiko cha chai) Mafuta (vegetable oil) Hoho (green pepper)
Matayarisho
Chambua dagaa kwa kutoa vichwa vyao na utumbo, baada ya hapo waloeke katkika maji ya moto kwa muda wa dakika 5 na uaoshe tena katika maji ya baridi na uwakaushe uwaweke pembeni. Ukishamaliza katakata kitunguu na uandae nyanya tayari kwa upishi. Bandika sufuria ya kupikia dagaa jikoni na utie mafuta, yakishapata moto tia vitunguu pamoja na dagaa. Kaanga mpaka dagaa wawe light brown kisha tia nyanya, chumvi na pilipili. Pika nyanya mpaka ziive (ukitaka kujua kama nyanya zimeiva utaona zinatengana na mafuta) Baada ya hapo kamulia limao kidogo sana na tia pilipili hoho na zipike kama dakika mbili. kisha ipua. Ukisha maliza kupika dagaa andaa chungu cha ugali. Kwanza unatakiwa kuchemsha maji ya moto, kisha koroga pembeni unga kiasi katika maji ya baridi na utie kwenye maji yanayochemka, Fanya kama unatengeneza uji, uji wa ugali ukishachemka tia unga na uanze kuusonga mpaka ugali uive. Ukisha iva pakua na usevu na mboga tayari kwa kuliwa.