Updated at: 2024-05-27 07:11:42 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Upendo wa kweli hauambatani na chuki. Huwezi kusema una Upendo wakati kuna watu wengine unawapenda na wengine unawachukia. Ni sawa na kusema kitambaa ni cheupe lakini kina madoa doa, maana yake sio cheupe.
Updated at: 2024-05-27 07:11:52 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Kukosa hata mara moja inahesabika ni kukosea mbele ya Mungu. Kwa kuwa kwa Mungu hakuna kusema, 'Kukosea mara moja sio kosa bali kurudia kosa ndio kosa'. Mbele ya Mungu kila kosa lina uzito wake haijalishi ni kosa la mara ya kwanza.
Mungu ni zaidi ya Mzazi na upendo wake ni zaidi ya wa Wazazi
Updated at: 2024-05-27 07:11:51 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Wakati wazazi waliweza kuaamua kuzaa mtoto tuu, Mungu yeye alikuchagua wewe utungwe mimba na kukulinda ungali tumboni mwa mama yako….Wakati wazazi wanasubiri kwa shauku kuona muonekano wako wewe, Mungu anawaweka wajukuu wa wazazi wako/ watoto wako ndani mwako…. Wakati wazazi wakitafuta chakula kwa ajili yako, Mungu yeye aliwawezesha kukipata…. Wakati wazazi wakingoja kuona unavyoendelea kukua huku wakiwaza hatima ya maisha yako Mungu anakuendeleza na alishapanga maisha yako tangu alipokuchagua uwe mtu ukiwa tumboni mwa mama yako…. Wazazi wanaweza kukuombea kwa Mungu lakini Mungu ndiye anayeamua akufanyie nini maana Wewe ni wa kwake….Wewe na wazazi wako ni watoto wa Baba mmoja ambaye ndiye Mungu.
Updated at: 2024-05-27 07:12:02 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Mungu anasubiri sala zako kila siku. Anasubiri sala zako akujibu ili uone utukufu wake. Anasubiri sala zako ili akuze mahusiano yake na wewe. Sali daima kwani Mungu yupo milele kukusikiliza na kukuhudumia.
Updated at: 2024-05-27 07:12:01 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Kama mtu anasali kila siku katika maisha yake hakuna kitu kitakachokuwa kigumu. Sala ni njia ya kujipatia neema za kuendesha maisha yetu. Usiache kusali kila siku hata kama upo katika hali gani.