Ili kutoka hapo ULIPO uweze kwenda HATUA inayofuata kuna SWALI muhimu sana unahitaji kujiuliza. Watu ambao huwa wanashindwa kupiga hatua katika maisha yao ni kwa sababu huwa wanajiuliza kinyume cha swali hili. Swali hili ndilo wanalojiuliza watu wote waliofanikiwa:
Swali: "Hivi kwa sasa nina nini ambacho naweza kuanza kukitumia kama mtaji wa kwanza kuanza kufanya ninachotaka"?
Updated at: 2024-05-23 16:07:18 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Ili kutoka hapo ULIPO uweze kwenda HATUA inayofuata kuna SWALI muhimu sana unahitaji kujiuliza. Watu ambao huwa wanashindwa kupiga hatua katika maisha yao ni kwa sababu huwa wanajiuliza kinyume cha swali hili. Swali hili ndilo wanalojiuliza watu wote waliofanikiwa:
Swali: "Hivi kwa sasa nina nini ambacho naweza kuanza kukitumia kama mtaji wa kwanza kuanza kufanya ninachotaka"?
Siku moja wakati nasoma biblia niliona Mungu alipotaka kumtumia Mussa kuokoa wana wa Israel akamuuliza-
“Una nini mkononi mwako”-
Mussa akajibu kwa kudharau alichonacho kuwa “Nina fimbo kavu tu ya kuchungia mifugo”.
Ndipo Mungu alianza kumuonyesha miujiza kutumia fimbo ambayo siku zote alikuwa nayo na kujidharau ndiyo ambayo ikatumika kwenda kuokoa wana wa Israel.
Watu wengi sana wanashindwa kuanza kwa sababu huwa wanajiuliza-
"Hivi ninakosa nini ili niweze kuanza" badala ya 'Hivi nina nini cha kuanzia'.
Cha kuanzia sio lazima iwe pesa-Inawezekana ni uwezo wa kufanya jambo fulani la kipekee,inawezekana ni mahusiano mazuri uliyonayo na watu fulani(mtandao wako),inawezekana ni uzoefu ulionao,inawezekana ni kipaji n.k Leo unapoanza siku yako naomba ijiulize-
“Nina nini mkononi mwangu ambacho naweza kutumia katika hatua ya kwanza”?.
Kumbuka hakuna mtu ambaye hana kitu kabisa-KITAFUTE HADI UKIPATE NA ANZA KUKITUMIA KUCHUKUA HATUA.
Share ili wengine wajifunze…..uwe na Jumatatu njema……..