Sidebar with Floating Button
AckySHINE SMSπŸ’ŒπŸ’•
☰
AckyShine

Jinsi ya kuongeza mvuto kwa mpenzi wako

Featured Image

Kama umeshushwa thamani unakuwa kwenye hatari ya kuachwa. Hata kama mwenzako alikuwa ameshafikiria suala la kuingia kwenye ndoa na wewe lakini kwa sababu ameshakushusha thamani ndoa inaweza kuyeyuka. Ukiwa kwenye ndoa ni hatari zaidi maana mwenzako hukuchukulia wa kawaida mazoea huzidi na hapo ndipo uhitaji wa kuwa na mwingine wa pembeni unapoanzia. Haoni cha muhimu tena kwako, ndiyo maana wazo hilo huvamia ubongo wake kwa kasi sana.

Itafikia hatua, kama upo ndani ya ndoa, mwenzako atagoma kuongozana na wewe na kama ikitokea hivyo mkikutana na rafiki zake njiani hatakutambulisha. Hisia kwamba hamuendani humwingia.

UNAFANYAJE SASA?

Kubwa unalotakiwa kufahamu rafiki yangu mpendwa, suala la kupanda au kushuka thamani lipo mikononi mwako. Yapo mambo ambayo ukiyazingatia, mwenzako hawezi kukuchoka na kufikia hatua ya kukushusha thamani.

Tayari tumeshaona athari zake lakini hapa sasa nataka kukupa mbinu ambazo ukiwa nazo makini basi itakuwa rahisi kwako kubaki namba moja na mtu muhimu zaidi (ndiyo inavyotakiwa kuwa) kwa mpenzi wako maana ni haki yako.

ANZIA MWANZO

Ni rahisi zaidi kulinda thamani yako kuanzia mwanzo wa uhusiano wenu. Ikiwa tayari mmeshakomaa halafu tatizo hilo likajitokeza, hutumika nguvu nyingi zaidi kulirekebisha kuliko kujizatiti kuanzia mwanzo wa uhusiano. Ni mambo gani hayo? Twende hapo chini.

CHUNGA KAULI ZAKO

Naomba ieleweke wazi kuwa mada hii ni maalum zaidi kwa wanawake. Kitu muhimu cha kwanza kabisa kwa mwanamke ambaye anataka kuilinda thamani yake kwa mpenziwe ni kupima sana kauli zake.

Acha kuropoka hovyo, pima maneno yako na ikiwezekana kama unadhani kuna jambo huna uhakika nalo usizungumze kabisa. Katika eneo hili, uwe makini zaidi mnapokuwa na watu wengine. Kama mwanamke usiwe mchangiaji hoja sana.

Utulivu wako unaweza kuwa silaha kubwa ya kukufanya ubaki na thamani yako kama mwanamke anayejitambua.

USIRUHUSU MAPENZI

Msichana mwenye kujitambua na kufahamu thamani yake sawasawa hawezi kuruhusu mwili wake ujulikane na mwanaume harakaharaka. Onesha unajitambua na usikubali kirahisi kuuacha mwili wako uchezewe.

Mpe hoja; kwanza mapema, hajakuoa wala kukuchumbia, haraka ya nini? Wakati unawaza kuhusu kutoa penzi lako, lazima ufikirie kuhusu athari zinazoweza kukupata kwa kukurupukia mapenzi. Mwanaume ambaye bado hamjachunguzana na huna uhakika naye wa kutengeneza maisha, kichwani mwake hakuweki kwa asilimia kubwa.

Ukumbuke kwamba, ukipata matatizo yoyote – binafsi au yanayosababishwa na uhusiano wenu, anakuwa hana uwajibikaji wa asilimia kubwa kwa tatizo hilo. Utabaki wewe na matatizo yako!

Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE

[products columns="2" ids="30827"]

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Je, mawasiliano ni muhimu katika kuboresha uzoefu wa ngono/kufanya mapenzi?

Je, mawasiliano ni muhimu katika kuboresha uzoefu wa ngono/kufanya mapenzi?

Je, wewe na mwenzi wako mnahisi kama hamjawai kufurahia tendo la ndoa? Kila wakati mnafikiri kuwa... Read More

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu maadili na imani za kiroho

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu maadili na imani za kiroho

Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu maadili na imani za kiroho ni muhimu katika kujenga uelewa na hesh... Read More
Kujiamini Katika Kufanya Mapenzi: Jinsi ya Kukuza Kujiamini

Kujiamini Katika Kufanya Mapenzi: Jinsi ya Kukuza Kujiamini

Kujiamini Katika Kufanya Mapenzi: Jinsi ya Kukuza Kujiamini

Mapenzi ni sehemu muhimu sana ... Read More

Jinsi ya Kuwa Msaada wakati wa Shida na Msukumo wa mke wako

Jinsi ya Kuwa Msaada wakati wa Shida na Msukumo wa mke wako

Kuwa msaada wakati wa shida na msukumo kwa mke wako ni jambo muhimu katika kuimarisha uhusiano na ku... Read More
Vidokezo vya Kuwa na Msichana Mzuri wa Kuwa Naye

Vidokezo vya Kuwa na Msichana Mzuri wa Kuwa Naye

Vidokezo vya Kuwa na Msichana Mzuri wa Kuwa Naye

Kila mwanaume anapenda kuwa na msichana m... Read More

Kuhamasisha Mazungumzo ya Amani na Furaha katika Familia Yako

Kuhamasisha Mazungumzo ya Amani na Furaha katika Familia Yako

  1. Kutafuta Muda Mzuri wa Kuongea

Kuwa na familia yenye furaha na amani inahitaj... Read More

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kujenga na kudumisha usawa wa kazi na majukumu ya nyumbani

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kujenga na kudumisha usawa wa kazi na majukumu ya nyumbani

Kuna mambo mengi mazuri katika uhusiano wa kimapenzi, lakini changamoto kubwa zinaweza kutokea wa... Read More

Njia za Kuimarisha Ushirikiano na Kuunda Amani na Furaha katika Familia

Njia za Kuimarisha Ushirikiano na Kuunda Amani na Furaha katika Familia

Familia ni kitovu cha mahusiano, lakini mara nyingi mahusiano haya yanaweza kuwa magumu na kusaba... Read More

Jinsi ya Kuwa na Uhuru katika Uhusiano wako na Msichana

Jinsi ya Kuwa na Uhuru katika Uhusiano wako na Msichana

Kila mtu anataka kuwa na uhuru katika uhusiano wao na msichana wao. Lakini wakati mwingine inawez... Read More

Njia za Kupunguza Mizozo ya Kifedha katika Mahusiano yako

Njia za Kupunguza Mizozo ya Kifedha katika Mahusiano yako

Tofauti za kifedha zinaweza kuwa sababu ya migogoro katika mahusiano yako. Hata hivyo, unaweza ku... Read More

Jinsi ya Kuimarisha imani na kuaminiana katika uhusiano na mpenzi wako

Jinsi ya Kuimarisha imani na kuaminiana katika uhusiano na mpenzi wako

Kuimarisha imani na kuaminiana katika uhusiano wako na mpenzi wako ni muhimu sana kwa kujenga uhusia... Read More
Kutafuta Furaha: Mambo Mazuri Katika Kufanya Mapenzi

Kutafuta Furaha: Mambo Mazuri Katika Kufanya Mapenzi

Kutafuta Furaha: Mambo Mazuri Katika Kufanya Mapenzi

Kila mtu anatamani furaha katika mape... Read More