Sidebar with Floating Button
AckySHINE SMSπŸ’ŒπŸ’•
☰
AckyShine

Kisa cha kusisimua: Funzo kwa mabinti

Featured Image

Kijana maskini na mwenye maisha duni alimpenda msichana mmoja
Baada ya kutumia muda mwingi kumfikiria msichana huyo,
Siku moja akaamua kumwita na kumwambia ukweli ya kwamba amempenda na angehitaji kumuoa.

Msichana kwa nyodo na jeuri akasema "sikiliza tena unisikilize kwa makini wewe maskini mshahara wako unaopokea kwa mwezi hautoshi hata kwa matumizi yangu ya siku moja sasa utawezaje kunitunza mm!

Kwaufupi mm sio levo zako hivyo basi sahau kabisa kuhusu kunipata mimi
Nenda katafute maskini mwenzio atakae endana na maisha yako,
Mwisho akamwangalia kwa dharau na kisha akaenda zake.

Kwanzia siku ile kijana hakubahatika tena kumuona msichana yule lkn kwakuwa alimpenda basi hakuweza kumsahau kirahisi rahisi siku zilienda na miezi ikasonga,
Miaka 10 baadae wawili hawa walikuja kukutana katika supermarket moja hivi mjini

Kijana alipomwona msichana alitabasamu lakin kabla hajasema chochote msichana kama kawaida yake kwa dharau akasema "we maskin upo! hivi na ww unaingiaga supermarket eh!

Akaongeza huku akisema walau sasahivi nakuona umependeza inaonekana boss wako kakuongeza mshahara
ila kwa kifupi naomba nikwambie sasahivi nimeshaolewa mume wangu anafanya kazi kwenye kampuni moja hivi ya mtu binafsi kampuni maarufu sana na mshahara wa mume wangu ni shilingi milioni moja na laki mbili kwa mwezi na malupulupu mengine kibao,
Unafikiri ww na umaskini wako kuna siku utakuja kufikia kiwango cha mshahara anachopokea mume wangu!

Macho ya kijana yalitokwa na machozi kwa kuona msichana hajabadilika na anaendelea kuwa na maneno ya kejeri na dharau.

Mara hii mume wa yule dada akaingia ktk supermarket
Ile kumuona yule kijana mume akasema "ooh! Kiongozi upo hapa! Leo imekuwa bahati umekutana na mke wangu!" Kisha akamgeukia mke wake na kusema "mke wangu huyu ndo boss wangu

Na unajua nn mke wangu usishangae kumuona boss wangu anakuja kununua vitu mwenyewe hapa supermarket ukweli ni kwamba boss wangu hana mke, anasema alisha wahi kumpenda msichana mmoja lakini hakufanikiwa kumpata na amekuwa na ndoto ya kuja kukutana tena na msichana huyo ndio maana mpaka sasa bado hajaoa.

Akaendelea kusema hebu fikiria ni bahati kiasi gani alikuwa nayo msichana huyo kama angekubali kuolewa na boss wangu leo hii siangekuwa
maisha!

Muda wote msichana alikuwa kimya hajui hata ajibu nn kwa dharau alizomuonyesha kijana tangu mwanzo.

UJUMBE WANGU
Kwenye maisha mambo huweza kubadilika kama vile upepo unavoweza kubadili mwelekeo kulingana na masaa Hivyo basi usimdharau na kumbeza mtu yeyote kwa sababu ya hali aliyonayo,
Maana kila mtu anafungu lake alilopangiwa na Mungu,

Lakini pia kumbuka hakuna ajuaye kesho
Wakati mwingine mtu unayemdharau leo ndiye huyohuyo ambaye kesho utasimulia mafanikio yake.

Kwako unayesoma ujumbe huu nakuombea Mungu akakufungulie milango ya baraka na kuyapa thamani maisha yako ili pale ulipozomewa ukashangiliwe na wale wote waliokudharau punde wakapate kukupigia magoti kwa uweza wa Mungu.

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

Director J (User) on May 15, 2025

Good story πŸ’ͺ

Related Posts

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kukuza na kudumisha stadi za mawasiliano

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kukuza na kudumisha stadi za mawasiliano

Leo, tutajadili jinsi ya kusaidiana na mpenzi wako katika kukuza na kudumisha stadi za mawasilian... Read More

Jinsi ya Kuonyesha Heshima kwa Msichana Wako

Jinsi ya Kuonyesha Heshima kwa Msichana Wako

Jinsi ya Kuonyesha Heshima kwa Msichana Wako

Wanawake ni vipenzi vya thamani sana katika m... Read More

Je, watu wanapendelea ngono/kufanya mapenzi ya asubuhi au jioni?

Je, watu wanapendelea ngono/kufanya mapenzi ya asubuhi au jioni?

Habari wapenzi wa blogu yetu! Leo, tutazungumzia suala la ngono na wakati bora wa kufanya mapenzi... Read More

Je, watu wanapendelea kutumia kinga wakati wa kufanya ngono/kufanya mapenzi?

Je, watu wanapendelea kutumia kinga wakati wa kufanya ngono/kufanya mapenzi?

  1. Kutumia Kinga Hupunguza Hatari za Maambukizi ya Ngono Kutumia kinga ni hatua muhimu kat... Read More

Kukabiliana na Mazoea ya Kutokuwa na Ushirikiano na Kutoelewana katika Familia Yako

Kukabiliana na Mazoea ya Kutokuwa na Ushirikiano na Kutoelewana katika Familia Yako

  1. Kukabiliana na Mazoea ya Kutokuwa na Ushirikiano na Kutoelewana katika Familia Yako
  2. Read More
Kujenga Utamaduni wa Amani na Furaha katika Familia Yako

Kujenga Utamaduni wa Amani na Furaha katika Familia Yako

Kujenga Utamaduni wa Amani na Furaha katika Familia Yako

Familia ni sehemu muhimu sana kat... Read More

Njia za Kuimarisha Ushirikiano na Kujenga Upendo katika Familia Yako

Njia za Kuimarisha Ushirikiano na Kujenga Upendo katika Familia Yako

Familia ni kitovu cha upendo na ushirikiano. Ni mahali pa kujifunza na kukua kwa pamoja. Hata hiv... Read More

Kujenga Mipaka na Heshima katika Mahusiano ya Familia

Kujenga Mipaka na Heshima katika Mahusiano ya Familia

Kujenga mipaka na heshima katika mahusiano ya familia ni jambo muhimu sana kwa afya ya familia ya... Read More

Jinsi ya kujua kama mwanamke anakupenda kweli kwa dhati

Jinsi ya kujua kama mwanamke anakupenda kweli kwa dhati

Yafuatayo ni maswali ya kujiuliza ili kujua kama mwanamke anakupenda kweli.

Anajitoa kwa ... Read More

Njia za Kuimarisha Ushirikiano wa Kijamii na Urafiki katika Mahusiano

Njia za Kuimarisha Ushirikiano wa Kijamii na Urafiki katika Mahusiano

Hakuna kitu kizuri kama kuwa na marafiki wengi na mahusiano bora ya kijamii. Uhusiano mzuri unahi... Read More

Kujenga Hali ya Kuaminiana katika Kufanya Mapenzi: Kuweka Mipaka na Kuweka Wazi

Kujenga Hali ya Kuaminiana katika Kufanya Mapenzi: Kuweka Mipaka na Kuweka Wazi

Kujenga Hali ya Kuaminiana katika Kufanya Mapenzi: Kuweka Mipaka na Kuweka Wazi

Upendo ni ... Read More

Kujenga Ushirikiano wa Kifedha na Kuweka Malengo ya Pamoja katika Familia

Kujenga Ushirikiano wa Kifedha na Kuweka Malengo ya Pamoja katika Familia

  1. Kuweka malengo ya pamoja katika familia ni jambo muhimu sana katika kujenga ushirikiano... Read More