Sidebar with Floating Button
AckySHINE SMSπŸ’ŒπŸ’•
☰
AckyShine

Kisa cha kusisimua cha kijana na mke wake na mama yake

Featured Image

Kuna kijana mmoja daktari alikwenda kuposa. Binti aliyemposa akamuwekea masharti mazito. Akamwambia chagua mawili imma kunioa mimi au kukaa na mama yako, kwa sababu ukinioa mimi sitokubali mama yako aje hata harusini kwangu! Yule kijana aliemewa. Hakujua la kufanya. Mke anamtaka, lakini mama yake pia anampenda.

Hivyo aliamua kuomba ushauri kwa mwalimu wake wa chuo kikuu. Alimwambia: moyo wangu unampenda mno binti niliyekwenda kumposa, lakini pia siwezi kuishi mbali na mama yangu. Nifanye nini?

Yule mwalimu mwenye hekima ambaye alikuwa anajua tabu alizopitia mama wa kijana yule, alimjibu kwa kumwambia: Kabla ya kukueleza uchague yupi kati ya wawili hao, rudi nyumbani, na leo usifanye chochote, ila kuikosha mikono ya mama yako. Yule kijana alifanya kama alivyotakiwa na mwalimu wake. Alipofika nyumbani aliomba idhini kwa mama yake amruhusu kuikosha mikono yake, na yule mama alimkubalia bila ya ajizi yoyote.

Yule kijana alipoanza kuikosha mikono ya mama yake na kuona jinsi ilivyogugutaa kwa kazi za sulubu, alilia sana. Muda wote huu alikuwa hajawahi kuangalia viganja vya mama yake. *Je, na wewe umewahi kukaa na kuangalia viganja vya mama au baba yako kuona tabu walizopitia kukulea?* Kumbe baba wa yule kijana alifariki dunia yeye akiwa bado mdogo, yule mama aliamua kusamehe kila kitu kwa ajili ya mustakbali wa mwanawe. Alijitolea kufanya kazi za sulubu. Alikubali kuwa mtumishi wa ndani, kukosha nguo, kupiga deki na kila kazi ambayo alihisi ingelimletea chumo la halali bila ya kujali ugumu wa jkazu hiyo.

Juhudi zake zilizaa matunda na kufanikiwa kumlea na kumsomesha mwanawe hadi chuo kikuu na sasa ni daktari ambaye ana mustakbali mzuri. Baada ya yule kijana kukumbuka yote hayo, alifanya haraka kumpigia simu mwalimu wake huku macho yakiendelea kububujikwa na machozi akimwambia, siwezi kusubiri hadi kesho. Jibu nimeshalipata. Siwezi kumtupa mama yangu kwa ajili ya mtu asiyejua thamani ya mama. Ahsante sana kwa kunionesha njia sahihi! Kamwe siwezi kumuuza mama yangu kwa ajili ya leo yangu wakati yeye ameuza maisha yake yote kwa ajili ya mustakbali wangu.
NANI KAMA MAMA?!? Maa! Tabasamu lako ni ufunguo wangu wa ofanisi.
Kama umeipenda.

Share kwa wengine ili nao wazinduke.

Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE

[products columns="2" ids="30827"]

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Njia za Kujenga Ushawishi na Msichana katika Uhusiano

Njia za Kujenga Ushawishi na Msichana katika Uhusiano

Njia za Kujenga Ushawishi na Msichana katika Uhusiano

  1. Kuwasiliana kwa Ukaribu Ha... Read More

Jinsi ya Kuweka Mawasiliano Mzuri katika Familia: Njia na Vidokezo Vyema

Jinsi ya Kuweka Mawasiliano Mzuri katika Familia: Njia na Vidokezo Vyema

Mawasiliano mzuri katika familia ni muhimu sana kwa ustawi wa kila mmoja. Kwa uhusiano mzuri, wat... Read More

Njia Rahisi za Kufanya Msichana Awe na Hamu ya Kuwa na Wewe

Njia Rahisi za Kufanya Msichana Awe na Hamu ya Kuwa na Wewe

Wapenzi, kama unapenda msichana fulani na unataka kuwa na uhusiano naye, inaweza kuwa ngumu kumsh... Read More

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu maadili na imani za kiroho

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu maadili na imani za kiroho

Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu maadili na imani za kiroho ni muhimu katika kujenga uelewa na hesh... Read More
Kujenga Ushirikiano wenye Mshikamano na Kuweka Nafasi ya Kushiriki Wajibu

Kujenga Ushirikiano wenye Mshikamano na Kuweka Nafasi ya Kushiriki Wajibu

Kujenga ushirikiano wenye mshikamano na kuweka nafasi ya kushiriki wajibu ni muhimu sana katika k... Read More

Kujenga Ushirikiano wa Kiroho na Kuweka Mazingira ya Ibada katika Familia

Kujenga Ushirikiano wa Kiroho na Kuweka Mazingira ya Ibada katika Familia

Kujenga Ushirikiano wa Kiroho na Kuweka Mazingira ya Ibada katika Familia

Familia ni mahal... Read More

Jinsi ya Kukuza Ushirikiano na Ushirikiano wa Familia katika Mirathi na Mali

Jinsi ya Kukuza Ushirikiano na Ushirikiano wa Familia katika Mirathi na Mali

Kujenga ushirikiano na ushirikiano wa familia katika mirathi na mali ni muhimu kwa maendeleo ya f... Read More

Jinsi ya kuimarisha furaha na ustawi wa kihisia na mke wako

Jinsi ya kuimarisha furaha na ustawi wa kihisia na mke wako

Kuimarisha furaha na ustawi wa kihisia katika ndoa ni muhimu sana kwa uhusiano mzuri na wenye afya n... Read More
Kuhamasisha Ushirikiano wa Kujenga katika Mahusiano ya Mbali

Kuhamasisha Ushirikiano wa Kujenga katika Mahusiano ya Mbali

Mahusiano ya mbali ni changamoto kubwa sana kwa watu wengi, haswa katika ulimwengu wa leo ambapo ... Read More

Jinsi ya Kusimamia mzigo wa kazi na majukumu ya familia katika uhusiano

Jinsi ya Kusimamia mzigo wa kazi na majukumu ya familia katika uhusiano

Kusimamia mzigo wa kazi na majukumu ya familia katika uhusiano ni changamoto inayoweza kutokea kwa w... Read More
Jinsi ya Kujenga Ushirikiano wenye Msingi imara katika Mahusiano yako

Jinsi ya Kujenga Ushirikiano wenye Msingi imara katika Mahusiano yako

Karibu kwenye makala hii ambayo itakupa mbinu mbalimbali kuhusu jinsi ya kujenga ushirikiano weny... Read More

Jinsi ya Kuzungumza na mpenzi wako kuhusu matarajio ya kifamilia na jamii

Jinsi ya Kuzungumza na mpenzi wako kuhusu matarajio ya kifamilia na jamii

Kuzungumza na mpenzi wako kuhusu matarajio ya kifamilia na jamii ni muhimu katika kujenga msingi wa ... Read More