Sidebar with Floating Button
AckySHINE SMSπŸ’ŒπŸ’•
☰
AckyShine

Jinsi ya kumfanya mwanamke afurahi na akupende kwa kumfanyia mambo anayoyataka

Featured Image

Kuna mambo ya msingi ambayo mwanamke anahitaji kutoka kwa mwanamme ili kufurahi na kutulia katika mahusiano japokuwa sio rahisi kukwambia mojakwa moja.

Mambo hayo ni kama ifuatavyo;

Kupewa nafasi na kipaumbele.

Wanawake wanapenda kuwa namba moja au kupendwa kuliko yeyote. Kumpenda mwanamke haikuishii kwenye kumpata na kumliki, kisha kujisahau kwa kisingizio kuwa umemuoa au umemvisha pete ya uchumba, ni zaidi ya hapo. Wanawake wanapenda watangulizwe katika mapenzi na kusiwepo na mwingine wa kuchukua nafasi yao katika mazungumzo na mapenzi kwa ujumla na katika maisha yao.

Kuheshimiwa

Wanawake wanapenda kueshimiwa kwa maneno na matendo. Wanawake hawapendi kuitwa majina mabaya kwa mfano mjinga, Malaya au kulinganishwa na wanawake wenzao wabaya. Wanawake hawapendi kukosewa heshima hasa mbele za watu, hata kama ni kwa mambo madogo madogo.

Kuridhishwa Kwenye tendo la ndoa

Mwanamke anapenda aridhishwe Kwenye tendo la ndoa. Hata kama utakuwa na kiwango kikubwa cha mapenzi juu ya mpenzi wako kwa kiwango gani, ukiwa dhaifu katika tendo la ndoa utayumbisha penzi lako. Utundu na ufundi unahitajika ili kumkata kiu mpenzi wako. Mwanamme anatakiwa kuhakikisha kuwa anamtosheleza mpenzi wake katika tendo hilo.

Nafasi ya kuongea na kujieleza

Wanawake wanapenda wapewe nafasi ya kuongea na kujieleza vile watakavyo. Mpe uhuru mpenzi wako kuzungumza na kumsikiliza bila kumkatiza kwa ukali pale anapoongea sana. Kwa kawaida wanawake wanatajwa kuzungumza maneno 25,000 kwa siku, wakati wanaume wakibaki na kiwango cha maneno 5,000 kwa siku, wanawake hupenda zaidi kujieleza walivyo mbele ya wengine. Kwa hiyo wakizuiwa wasiongee hujiona kama wanakosa nafasi muhimu ya kueleza mawazo yao.

Kusaidiwa katika shida na matatizo yao

Wanawake wengi hutegemea kuwa wanapokuwa na wapenzi watasaidiwa katika matatizo ya kimaisha na migogoro ya kimawazo. Kwa mfano ushauri juu ya maisha yao, kulindwa na hatari za kimaisha, kusaidiwa katika shida na kuongozwa pale wanapohisi kushindwa kufanya jambo. Kama mwanaume hatamfanyia mpenzi wake hili atakuwa amekosa sifa za kuteka penzi la mwanamke.

Kubembelezwa

Wanawake hupenda kubembelezwa hasa pale wanapokuwa na huzuni. Wanawake wengi hupenda kuelimishwa zaidi kuliko kufokewa. Wanawake hawapendi kukaripiwa, mara nyingi hupenda kuungwa mkono wanapokuwa na misuguano na wengine. Ili mwanaume amteke kimapenzi mwanamke lazima awe nyuma yake hata kama atakuwa na kosa.

Mfahamu zaidi Mwanamke kwa Kupitia Kitabu hiki kizuri cha SIRI ZA MWANAMKE

[products columns="2" ids="30827"]

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya haki za binadamu na usawa

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya haki za binadamu na usawa

Upendo ni muhimu katika kila uhusiano na kila mtu anapaswa kuheshimiwa kwa usawa. Katika uhusiano... Read More

Kusisimua Mwili na Akili: Jinsi ya Kuleta Msisimko katika Kufanya Mapenzi

Kusisimua Mwili na Akili: Jinsi ya Kuleta Msisimko katika Kufanya Mapenzi

Kusisimua Mwili na Akili: Jinsi ya Kuleta Msisimko katika Kufanya Mapenzi

Mapenzi ni moja ... Read More

Njia za Kuimarisha Imani na Uaminifu katika Mahusiano

Njia za Kuimarisha Imani na Uaminifu katika Mahusiano

Mahusiano ni kitu muhimu sana katika maisha yetu. Lakini kuwa na uhusiano mzuri na mwenza wako ku... Read More

Siku Maalum za Kufurahia na Kusherehekea na Familia Yako

Siku Maalum za Kufurahia na Kusherehekea na Familia Yako

Kila familia ina siku maalum za kufurahia na kusherehekea pamoja. Siku hizi zinabeba uzito wa kih... Read More

Kuweka Kipaumbele cha Ubora wa Mahusiano: Jinsi ya Kutunza Ushirikiano wako

Kuweka Kipaumbele cha Ubora wa Mahusiano: Jinsi ya Kutunza Ushirikiano wako

Kuweka Kipaumbele cha Ubora wa Mahusiano: Jinsi ya Kutunza Ushirikiano wako

Mahusiano ni s... Read More

Je, ngono/kufanya mapenzi ni jambo la faragha au unajisikia huru kuzungumzia kuhusu hilo?

Je, ngono/kufanya mapenzi ni jambo la faragha au unajisikia huru kuzungumzia kuhusu hilo?

Jambo la faragha kabisa ni ngono au kufanya mapenzi. Kila mtu ana hisia tofauti kuhusu suala hili... Read More

Njia za Kuimarisha Mawasiliano katika Uhusiano wako

Njia za Kuimarisha Mawasiliano katika Uhusiano wako

Njia za Kuimarisha Mawasiliano katika Uhusiano Wako

Mawasiliano ni kitu muhimu sana katika... Read More

Jinsi ya Kuelewa na kushughulikia tofauti za kiutamaduni na lugha na mpenzi wako

Jinsi ya Kuelewa na kushughulikia tofauti za kiutamaduni na lugha na mpenzi wako

Uhusiano wa mapenzi una mambo mengi yanayohusika, ikiwa ni pamoja na tofauti za kiutamaduni na lu... Read More

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kujenga na kudumisha mazingira ya ushirikiano kazini

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kujenga na kudumisha mazingira ya ushirikiano kazini

Kazi ni sehemu muhimu katika maisha yetu na ina jukumu kubwa kwa ustawi wa kila mtu. Kama wapenzi... Read More

Jinsi ya Kujenga Uaminifu na Kuimarisha Ushirikiano katika Familia Yako

Jinsi ya Kujenga Uaminifu na Kuimarisha Ushirikiano katika Familia Yako

Kujenga Uaminifu na Kuimarisha Ushirikiano katika Familia Yako ni muhimu sana kwa ustawi wa famil... Read More

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya utamaduni na sanaa

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya utamaduni na sanaa

Kuwa na mpenzi anayeshiriki maslahi yako ya utamaduni na sanaa ni zawadi kubwa. Ni muhimu kuwa na... Read More

Jinsi ya Kuweka Mipango ya Mbeleni na Kuishi Kwa Pamoja na mke wako

Jinsi ya Kuweka Mipango ya Mbeleni na Kuishi Kwa Pamoja na mke wako

Kuweka mipango ya mbeleni na kuishi pamoja na mke wako ni muhimu katika kujenga maisha ya ndoa yenye... Read More