Sidebar with Floating Button
AckySHINE SMSπŸ’ŒπŸ’•
☰
AckyShine

Mambo ya Msingi kuyajua Ili uishi na watu vizuri

Featured Image

Nimezipenda hizi nasaha. Naamini na nyinyi wenzangu hamtakosa japo machache ya kujifunza:-
1. Epuka hasira za ovyo na kila mtu, kuwa msikivu kabla ya kukimbilia maamuzi (elewa kuwa ukiwa na hasira huwezi kupata suluhu ya jambo)
2. Usiwatendee wengine ubaya ukadhani kuwa utakuwa salama (ubaya hulipwa kwa ubaya, ipo siku ubaya wako kwa wengine utakurejea kama sio kuwarejea watu wa kizazi chako)


3. Usichukue maamuzi kabla ya kutafiti ukweli (pengine wapo wanadamu wanaopenda kuonekana wao wema kwa kuumiza wengine). Mtuhumu mtu lakini mpe muda wa kumsikiliza, usimshambulie mtu kwa maneno makali bila kuujua ukweli, ukijua ukweli nafsi inaweza kukusuta.


4. Mchukulie kila mwanadamu ni mkosaji (tambua kuwa hata wewe unawakosea sana wengine na wanakuvumilia. Hivyo usiwe mwepesi wa kuwaadhibu wenzio kwa ubaya).


5. Usipande mbegu ya chuki na ubaya katika jamii unayoishi ukadhani itakuacha salama (chuki hukua kama mti utambaao, ukiipanda ndani ya jamii yako, haitatoka kwako na inaweza kutafuna kizazi chako ukajutia.


6. Tambua kuwa yule unayeishi nae ni mwanadamu kama wewe, mpe heshima na mwonyeshee upendo hata kama huoni anafanana nawe. Maisha ni duara huenda ulikuwa kama yeye au atakuja kuwa kama wewe baadae.


6. Usiwe muongeaji ovyo ovyo na usiye na subira. Kuongea sana kunapoteza busara.


7. Jiepushe na maisha ya kusukumwa na wengine kufanya jambo usilojua manufaa yake. Jifunze kujitegemea kiakili. Sio kila unayemdhania rafiki moyoni mwake yupo pamoja nawe, na ukashirikiana nae, wengi wa marafiki zetu hututumia sana kuliko tunavyoweza kuwatumia wao.


8. Usipende sana kugombana na watu kwa njia ya maongezi yanayodumu kama vile, ujumbe wa maandishi, mawasiliano ya simu au ujumbe wa maneno (SMS). Kumbuka kuwa maneno yanaishi kuliko ugomvi au uadui, ipo siku yatakurudi na utajiona mpumbavu na kukosa pa kujificha. Jifunze kusubiri.


9.Usifumbue mdomo wako kutamka ubaya au kunyanyua kidole chako kuandika ubaya juu ya mwenzio bila kujiuliza mara mbili moyoni mwako hatima ya unachokitoa kwa mwingine.


10. Jishushe na jifunze kusikiliza wengine wakati wa mazungumzo ili uweze kujifunza kabla ya kukurupuka kujibu, usikivu ni kipimo cha busara, mtu anayekurupuka kujibu jibu kila anachosikia hawezi kuwa kiongozi, Mume au Mke mwema kwani mara nyingi atapotoka tu.


10. Usitunze hasira nyingi moyoni kwani hasira hukaa kifuani mwa mpumbavu. Jitahidi pia kuepuka kuwa na hasira mara kwa mara na zisizo na maana. Elewa kuwa hasira zisizo maana hukupunguzia maisha na kukupa maumivu wewe mwenyewe kuliko yule uliyemfanyia hasira, utakufa kwa magonjwa kabla ya wakati ufaao.


11. Thamani yako inategenezwa na watu wengine, wewe kama ni mtoto, mheshimu sana mzazi wako na kama umeoa au kuolewa, heshimu wazazi na familia ya mke au mumeo kwa kuwa bila wao, usingekuwa hivyo ulivyo leo unajivunia ndoa njema, kwa kuwa yupo mtu alimzaa huyo mwenzio. Mheshimu kwa lolote liwe jema au baya, utalipwa kwa wakati ufaao.


13. Usijibizane na mtu usiyemjua au ambaye hawezi kukupunguzia kitu katika maisha yako. Tambua kuwa unapunguza sehemu kubwa ya maisha yako kwa kutafuta magomvi na mtu wa mbali nawe.


14. Kumbuka asili yako, kumbuka upo hapo kwa kuwa kuna mahali ulitoka, maisha yanabadilika, usidharau pale ulipokuwa zamani kwa kuwa ndipo palipokufanya leo uwe hapo.


15. Subiri, sikiliza, elekeza, vumilia. Elewa sio kila mtu ana uelewa kama wako. Jitahidi kuwa mvumilivu katika kila jambo, usiinuke kuwafokea au kuwakaripia wengine kwa jambo ambalo pengine nao wanahitaji muda kueleweshwa ili walifanye vyema. Kumbuka sana, kuna wakati nawe ulikuwa huelewi kabisa lakini wapo wenzio walikuvumilia, wakakuelekeza njia njema, kufokea wengine mara kwa mara sio njia njema ya kuwafundisha bali ni kuwaweka mbali nawe.


Kumbuka: Ishi kwa kumpendeza Mungu.






Yafahamu Mambo Mbalimbali kuhusiana na Wanawake kwa Ku-Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE




Kitabu hiki kina topiki Zifuatazo;
1. Mambo anayohitaji mwanamke kutoka kwa Mwanaume
2. Mambo yanayowavutia wanawake kutoka kwa wanaume
3. Mambo wanayoyapenda wanawake wakati wa kufanya mapenzi
4. Dalili za mwanamke kicheche
5. Maswali ya kujiuliza kama mwanamke anakupenda kwa dhati au anakudanganya
6. Tabia za mwanamke anayekupenda lakini hawezi kusema
7. Ishara za mwanamke aliyevutiwa na wewe
8. Dalili za mwanamke anayeelekea kukukubali
9. Mambo ambayo mwanamke hawezi kukwambia
10. Njia za kudumisha na kuamsha mapenzi na mwanamke





Kitabu hiki ni Soft copy [pdf] kwa hiyo unaweza kusoma moja kwa moja kirahisi kabisa hata kwenye simu yako. Utatumiwa Kopi ya kitabu hiki kwenye email yako na utaweza kukihifadhi na kusoma wakati wowote utakaotaka.





[products columns="2" ids="30827"]


AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Jinsi ya Kuomba Msichana Awe Rafiki Yako

Jinsi ya Kuomba Msichana Awe Rafiki Yako

Kuomba msichana awe rafiki yako si jambo rahisi kama inavyoweza kuonekana kwa wengi. Hata hivyo, ... Read More

Jinsi ya Kuweka Mazoea ya Upendo na Shukrani katika Familia: Kuleta Furaha na Ukarimu

Jinsi ya Kuweka Mazoea ya Upendo na Shukrani katika Familia: Kuleta Furaha na Ukarimu

Kuweka mazoea ya upendo na shukrani katika familia ni muhimu sana, kwani huleta furaha na urafiki... Read More

Jinsi ya Kudumisha Umoja na Kuishi kwa Amani katika Familia

Jinsi ya Kudumisha Umoja na Kuishi kwa Amani katika Familia

Jinsi ya Kudumisha Umoja na Kuishi kwa Amani katika Familia

Kuishi katika familia yenye um... Read More

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu mipango ya likizo na mapumziko ya familia

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu mipango ya likizo na mapumziko ya familia

Wapendwa, hakuna jambo zuri kama kufanya mipango ya likizo na mapumziko ya familia pamoja na mpen... Read More

Jinsi ya Kuelewa na kushughulikia tofauti za kisiasa na misimamo na mpenzi wako

Jinsi ya Kuelewa na kushughulikia tofauti za kisiasa na misimamo na mpenzi wako

Kumekuwa na misimamo na tofauti za kisiasa miongoni mwa wapenzi wengi duniani kote. Inaweza kuwa ... Read More

Kuimarisha Uhusiano kupitia Mazoezi ya Kimwili: Kufanya Mapenzi kama Njia ya Kujenga Ushirikiano

Kuimarisha Uhusiano kupitia Mazoezi ya Kimwili: Kufanya Mapenzi kama Njia ya Kujenga Ushirikiano

  1. Kufanya mazoezi pamoja na mwenzi wako ni njia bora ya kuimarisha uhusiano wenu na kuongeza ... Read More
Jinsi ya Kuweka Malengo ya Ndoa na mke wako

Jinsi ya Kuweka Malengo ya Ndoa na mke wako

Kuweka malengo ya ndoa na mke wako ni hatua muhimu katika kujenga msingi imara na kufikia furaha na ... Read More
Muda wa Kufanya Kufanya Mapenzi

Muda wa Kufanya Kufanya Mapenzi

Muda wa Kufanya Kufanya Mapenzi

Wapenzi wote duniani wana nia ya kufanikiwa katika mapenzi... Read More

Kuweka Mazingira ya Kufurahisha na Amani katika Familia Yako

Kuweka Mazingira ya Kufurahisha na Amani katika Familia Yako

  1. Kujenga mahusiano mazuri ya familia ni jambo muhimu katika kuhakikisha kuwa kila mtu an... Read More

Kujenga Mazoea ya Kuonyeshana Upendo na Kuthamini katika Familia Yako

Kujenga Mazoea ya Kuonyeshana Upendo na Kuthamini katika Familia Yako

Karibu katika makala yetu kuhusu "Kujenga Mazoea ya Kuonyeshana Upendo na Kuthamini katika F... Read More

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kuishi na kukabiliana na msongo wa kazi

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kuishi na kukabiliana na msongo wa kazi

Kila siku, tunakutana na changamoto nyingi kazini, na hii inaweza kuwa ngumu sana kwa wapenzi wan... Read More

Kuhamasisha Ushirikiano wa Kielimu na Kuweka Mipango ya Elimu katika Familia

Kuhamasisha Ushirikiano wa Kielimu na Kuweka Mipango ya Elimu katika Familia

Kuhamasisha Ushirikiano wa Kielimu na Kuweka Mipango ya Elimu katika Familia

Elimu ni muhi... Read More