Sidebar with Floating Button
AckySHINE SMS💌💕
AckyShine

Ugumu wa maisha huanzia akilini mwako

Featured Image

Ebu fikiria Dada anayechoma mahindi maeneo ya Manzese Darajani kuanzia saa 12 jioni mpaka SAA 2 usiku, kwa siku moja anauwezo wa kuchoma mahindi .50. Kila hindi moja ananunua shambani kwa shilingi 100/- Na Anauza kwa sh.600/-

Hiyo ina maana mahindi 50 ananunua kwa shilingi 5000/- akichoma na kuuza anapata sh.30,000/-. Akitoa pesa ya mtaji (5000/- ya mahindi na 1500/- ya mkaa) anabakiwa na sh.23,500/- kwa siku.

Hivyo kwa mwezi huyu mchoma mahindi atakuwa ameingiza kiasi cha sh.705,000/-

Mwalimu mwenye Degree anayeanza kazi analipwa 584,000/- akikatwa kodi pamoja na makato mengene ya mifuko ya jamii anabakiwa na sh.425,000/.

Tofauti ya Mwalimu wa degree na Muuza mahindi ni kuwa Mwalimu kaajiriwa, muuza mahindi kajiajiri. Mwalimu anafanya kazi masaa 9 kwa siku, muuza mahindi anafanya kazi masaa matatu kwa siku (saa 12 jioni hadi 2 usiku). Mwalimu anatumia muda wake wa ziada kusahihisha mitihani na homework, mchoma mahindi anatumia muda wake wa ziada kutafuta fursa nyingine za kupata hela.

Uoga wako ndio umaskini wako.
KAMA HUNA FURAHA NA UNACHOKIFANYA BADILI MTAZAMO NA SIKUSHAURI UKAUZE MAHINDI NO HUO NI MF. KAMA SWALA NI KIPATO TU BASI KUNA FURSA NYINGI SANA KIPINDI HIKI NA WAWEZA BILA HATA YA KUWA NA MTAJI CHA MSINGI NI WEWE KUAMUA KUWAONA WATAALAMU WAKUSHAURI NI NINI CHA KUFANYA.

mafanikio yanaanza nawewe

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Kukataliwa ni mtaji

Kukataliwa ni mtaji

Hakuna mtu duniani ambaye hajawahi kukutana na hali ya kukataliwa. Yaani kukataliwa katika hali y... Read More

MAFANIKIO YA MAISHA SIO ELIMU TU, UTHUBUTU, KUJIAMINI NA UJASIRI WA MAAMUZI

MAFANIKIO YA MAISHA SIO ELIMU TU, UTHUBUTU, KUJIAMINI NA UJASIRI WA MAAMUZI

✍🏽Ukichunguza katika jamii, utabaini kuwa sehemu kubwa ya matajiri ni ... Read More

JINSI YA KUTENGENEZA BATIKI

JINSI YA KUTENGENEZA BATIKI

Batiki inatengenezwa kama ifuatavyo

MAHITAJI:

1.Vibanio vyenye urembo mbalimbali.Read More

Usiyoyajua kuhusu pesa haya hapa

Usiyoyajua kuhusu pesa haya hapa

Habari za Leo Rafiki yangu wa Muhimu sana. Ni furaha yangu kujua unaendelea vyema sana na majukum... Read More

Siri 39 za kuwa Milionea, Jinsi ya kupata pesa na kuwa tajiri

Siri 39 za kuwa Milionea, Jinsi ya kupata pesa na kuwa tajiri

1. Tafuta fursa kila kona. 2. Tumia kipaji chako. 3. Kuwa na nidhamu katika fedha - matumizi mazuri ... Read More
Ilinde ndoto yako

Ilinde ndoto yako