Tatizo la maumivu wakati na baada ya kufanya mapenzi
Date: April 15, 2022
Author: SW - Melkisedeck Shine
Wakati wa kufanya tendo la ndoa wapo baadhi ya watu hupatwa na maumivu wakati au baada ya kushiriki tendo, Maumivu haya yaweza kuwa;- Wakati tu uume unaingia,
Unapoingiza kitu chochote hata kidole, Wakati uume ukiwa ndani na Maumivu ya kupita (throbbing pain) yanayodumu masaa kadhaa baada ya tendo.
Sababu za maumivu
Sababu zaweza kuwa za kimwili (physical) au za kisaikolojia.
Sababu za kimwili baadhi ni kama;
Kutokua na ute wa kutosha kwa ajili ya kulainisha uke kutokana na kukosa maandalizi ya kutosha, kupungua kwa homoni baada ya ukomo wa hedhi, kujifungua au kunyonyesha, baadhi ya dawa za magonjwa ya akili, presha na uzazi wa mpango.
Ajali au upasuaji maeneo ya nyonga, ukeketaji na kuongezewa njia wakati wa kujifungua. Pia matibabu ya kutumia mionzi eneo la nyonga.
Tatizo la mishipa ya uke kusinyaa yenyewe (Vaginismus).
Tatizo la uumbaji linalopelekea mtu kuzaliwa wakati uke haujatengenezwa vizuri mfano “vaginal agenesis na imperforate hymen.”
Magonjwa ya kizazi kama “endometriosis, PID,fibroids.”
Sababu za kisaikolojia;
Msongo wa mawazo, wasiwasi, sonona, matatizo ya mahusiano, woga wa mimba, historia ya kuumizwa kimapenzi (sexual abuse) siku za nyuma.
Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.
Related Posts
Kwa ajili afya ya mama na mtoto ni muhimu sana, mwanamke anatakiwa apate chakula bora kilicho na ...
Read More
Ugonjwa wa dengue ni tishio la ugonjwa hatari linaongezeka siku hadi siku. Dengue ni ugonjwa unao...
Read More
Ni mhimu kula mlo kamili kila siku. Kula lishe duni kunaweza kupelekea kuzalishwa kwa damu isiyo ...
Read More
Unapopita maeneo mengi ya mijini na pembezoni wa miji utakutana na wafanyabiashara wa miwa wanaou...
Read More
Uyoga una vitamini na aina nyingi na madini. Virutubisho vilivyothibitishwa kuwemo kwenye uyoga n...
Read More
Ni kazi ngumu kidogo kuacha uvutaji wa sigara. Uvutaji ni tishio kwa maisha yetu. Yawezekana hufa...
Read More
Unaweza kutumia Lozi na maziwa kutibu shinikizo la chini la damu kama ifuatavyo;
- Lowek...
Read More
Kutumia mtindi na asali ni moja ya dawa rahisi zaidi za kutibu chunusi.
Unahitaji:
...
Read More
Yafuatayo ni magonjwa na njia za kujitibu kwa kutumia matunda
KUTUBU KIUNGULIA
Aliy...
Read More
☘☘piga chini kitambi☘☘
Mahitaji
🌹Tikiti🍉 1
🌹Tangawizi kid...
Read More
Kumekuwepo na tatizo la vifo vya ghafla sana tena kwa watu ambao wana afya njema na hii inatokana...
Read More
Asilimia kubwa tunapenda kutumia karoti katika kuunga katika mboga ya nyama na si kuila karoti ka...
Read More
No comments yet. Be the first to share your thoughts!