Sababu ya tatizo la Tumbo kujaa gesi na jinsi ya kujitibu
Date: April 15, 2022
Author: SW - Melkisedeck Shine
Tatizo la tumbo kujaa gesi husababishwa na kumeza chakula pamoja na gesi inayotolewa katika vyakula mbalimbali tunavokula ambayo hujaa tumboni na kwenye utumbo mdogo. Hali hii husababisha tumbo kujaa au kuvimba na mtu hutoa gesi hiyo kwa njia ya ushuzi na kubeua.
Nini husababisha.
Tatizo ili mara nyingi husababishwa na huambatana na mambo yafuatayo:
1. Kula vyakula vyenye mafuta mengi ambayo huchelewesha tumbo kufunguka kwa ajili ya usagaji wa chakula.
2. Kunywa vinywaji vyenye Carbonates, cola na kula vyakula vyenye gesi kama maharage, bigiji, vitunguu, kabichi n.k
3. Msongo wa mawazo na hasira.
4. Kula haraka haraka na kula unaongea.
5. Uvutaji wa Sigara
6. Magonjwa na maambukizi katika mfumo wa chakula asa kwenye tumbo na utumbo ambayo huzuia kusagwa na kufyonzwa kwa chakula.
Jinsi ya kujitibu.
· Kunywa chai ya tangawizi au karafuu itasaidia kupunguza gesi.
· Unaweza kunywa glasi moja ya juisi ya Limao baada ya kula.
· Tafuna mbegu za maboga zinasaidia kulainisha mfumo wa chakula
· Lalia ubavu wa kushoto na pumua kwa kasi ili kupunguza gesi tumboni.
· Kunja miguu na ikalie uku ukinyoosha mikono na kuinamia mbele itasaidia.
· kuongeza kasi ya mfumo wa chakula kufanya kazi na kuondoa gesi.
· Fanya mazoezi mepesi ya kutembea na kuruka ruka.
· Kula na tafuna chakula taratibu na epuka vyakula vyenye gesi na mafuta mengi,.
· Nenda hospitali kama tatizo ili linaambatana na kuharisha, kutapika, maumivu makali ya tumbo, kinyesi chenye rangi tofauti au damu na maumivu ya kifua.
Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.
Related Posts
Nyonyo Mbarika (Castor)
Mnyony(KiSwahili) Erand (KiHindi) Kastorka(KiRusi) ni mmea wa jamii ...
Read More
Vyakula hivyo ni;
- Maharage
- Nyanya
- Samaki
- Mboga za majani zenye...
Read More
Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinaz...
Read More
Unaweza kutumia Lozi na maziwa kutibu shinikizo la chini la damu kama ifuatavyo;
- Lowek...
Read More
NI muujiza! Pengine hivyo ndivyo yeyote anaweza kusema pindi akisikia kwa mara ya kwanza juu ya n...
Read More
Mwili wa binadamu unafanya mambo
mengi ya kibaiolojia ambayo mara
nyingi ni vigumu kuya...
Read More
Mchanganyiko wa mdalasini na asali unasaidia katika mambo ya aiana tofauti tofauti kama ifutavto:...
Read More
Ili uweze kuwa na siku nzuri basi unashauriwa kuanza siku yako kwa kutumia mchanganyiko wa maji y...
Read More
Wakati wa ujauzito ni kipindi cha kubadili mambo mengi katika mfumo wa maisha wa mjamzito. Mjamzi...
Read More
Unapotokwa na damu puani fanya yafuatayo;
1. Simama wima na inamisha kichwa kwa mbele, kusim...
Read More
Zifutazo ni faida zitokanazo na ulaji wa tende;
1. Tende huongeza nguvu kutokana na kuwa na sukari ...
Read More
Tafadhali chukua walau dk 2 kusoma hii:
1. Chukulia ni muda wa saa 1:25 jion unarudi nyumba...
Read More
No comments yet. Be the first to share your thoughts!