Sidebar with Floating Button
AckySHINE SMS💌💕
AckyShine

Jinsi ya kumlisha n'gombe anayekamuliwa atoe maziwa mengi

Featured Image
Ng’ombe wa maziwa wanahitaji virutubisho zaidi ili kuweza kuzalisha maziwa kwa wingi hasa katika kipindi cha miezi 3-4 ya mwanzo baada ya kuzaa, wakati ambao uzalishaji wa maziwa unakuwa juu.

Malisho ya ng'ombe wa maziwa ni lazima yawe na uwiano sahihi wa viungo. Mifugo inahitaji chakula kitakachowapa nguvu, protini, madini, na vitamin ili kujenga miili yao, kuzalisha maziwa, na kuzaliana.

Kulisha ng’ombe wa maziwa kwa kutumia aina yoyote ya malisho haitoshi kukuhakikishia ng’ombe anakuwa na afya nzuri na kutoa maziwa ya kutosha. Kama ilivyo kwa mifugo mingine kama kuku na hata binadamu, ng’ombe anahitaji
mlo bora yaani kamili.

Vyakula vinavyohitajika kwa ng'ombe wa maziwa


Malisho ya kijani (Majani)


Huu ni mlo mkuu kwa ng'ombe wa maziwa. Mlo ni muhimu na wenye virutubisho. Lakini malisho bora ya kijani ni yale yanayoweza kumpatia ng’ombe wa maziwa virutubisho muhimu vinavyohitajika.

Malisho ya kijani yanatakiwa yawe ya kijani kibichi na machanga, hii ina maana kuwa, majani ya malisho ni lazima yakatwe na kuhifadhiwa yakiwa bado machanga na kabla ya kuchanua. Hii ina maana kuwa mimea ambayo imepoteza rangi yake halisi ya kijani inaweza tu kuwasaidia mifugo kuishi lakini haina virutubisho muhimu vya kuwapa mifugo nguvu, madini, protini na haiwezi kusaidia katika uzalishaji wa maziwa.

Malisho yenye viwango vya chini vya virutubisho yanatakiwa yaongezewe kwa chakula cha ziada chenye virutubisho vya kutosha kitakachoziba pengo la virutubisho vilivyokosekana.

Vyakula vya kutia nguvu


Kwa kawaida aina zote za majani ni chanzo kizuri cha vyakula vya kutia nguvu kwa mifugo, kama tuu tu yatalishwa yakiwa bado machanga.

Mfano wa Majani yaliyo maarufu kwa malisho ni matete, ukoka, majani ya tembo, seteria na Guatemala. Majani ya mahindi au mtama ni chakula kizuri sana kwa kuwapa nguvu mifugo.

Vyakula vingine vinaweza kutokana na aina zote za nafaka, punje za ngano, au molasesi.

Vyakula hivi vya kutia nguvu vinatakiwa vilishwe kwa kiasi kidogo.

Vyakula vya Protini


Mimea michanga ina kiasi kikubwa cha protini kuliko mimea iliyokomaa. Mahindi machanga pamoja na majani ya viazi vitamu ni mahususi kwa protini.

Mikunde ina protini nyingi zaidi kuliko nyasi. Mfano, mabaki ya majani ya maharage, njegere, desmodium na lusina. Majani yanayotokana na mimea kama lusina, calliandra au sesbania ina kiwango kikubwa cha protini pia.

Aina nyingine ya vyakula vyenye protini ni mashudu ya pamba, mashudu yaalizeti na soya.

Ng’ombe wa maziwa wasilishwe kwa kutumia aina zote za jamii ya mikunde kwa zaidi ya asilimia 30 ya uwiano wa mchanganyiko wa malisho ili kuepuka matatizo ya kiafya.

Madini


Ng'ombe wa maziwa wanahitaji madini ya ziada. Madini Ni lazima yapatikane muda wote, mfano kama jiwe la chumvi au kama chumvi ya unga ya kuweka kwenye (chakula) pumba.

Wanyama wanaokuwa, wenye mimba, na ng’ombe anaenyonyesha wanahitaji kiasi kikubwa cha madini, mfano calcium na phosphorous kwa kuwa madini mengi yanatoka kwenye maziwa.

Madini yanaweza kupatikana katika Mimea ya jamii ya mikunde na mengineyo isipokuwa nyasi. Mimea hii inatoa kiasi kikubwa cha calcium na madini mengineyo.

Chakula cha ziada (mf. Pumba)


Ng'ombe wa maziwa anapewa cha kula cha ziada mfano pumba. Pumba inahitajika kwa ng'ombe lakini kwa kiasi kidogo. Pumba aina ya Dairy meal ina kiwango kikubwa sana cha madini. Lakini ina madhara kwa mifugo endapo wanyama watalishwa kwa kiwango kikubwa.

Malisho yanayotokana na majani au nyasi kavu ni lazima yabakie kuwa chakula kikuu kwa mifugo. Haishauriwi kulisha zaidi ya kilo 6 za pumba kwa siku kwa ng’ombe mwenye kilo 450.

Ni lazima wapewe kwa kiwango kidogo sana, ambacho si zaidi ya Kilo 2 kwa mara moja na kichanganywe na majani. Kuongeza kiwango cha pumba kabla na wakati wa kunyonyesha/kukamuliwa, kisizidi kiasi cha kilo 2 kwa wiki ili tumbo la mnyama lizoee.
AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Siri ya kilimo cha nyanya kwa faida

Siri ya kilimo cha nyanya kwa faida

NYANYA HASA KWENYE OPEN SPACE CHANGAMOTO NI NYINGI, HASA WADUDU, KAMA SASA ... Read More

Namna ya kutunza kuku na kuwakinga na magonjwa

Namna ya kutunza kuku na kuwakinga na magonjwa

1. Zingatia chanjo muhimu kwa kuku ili kuzuia magonjwa kama utakavyoshauriwa na mtaalamu wa mifugo. ... Read More
Mambo Ya Kuzingatia Kuongeza Utagaji Wa Kuku

Mambo Ya Kuzingatia Kuongeza Utagaji Wa Kuku

Inafahamika kuku kutaga mayai mengi hutokana na aina ya mbegu ya kuku, ila jua kwamba hata aina y... Read More

Kilimo kizuri cha pilipili hoho

Kilimo kizuri cha pilipili hoho

Pilipili hoho ni zao la jamii ya pilipili isiyo kali, tunda lake ni nene ki... Read More

Ufugaji wa nguruwe na faida zake

Ufugaji wa nguruwe na faida zake

Na, Patrick Tungu

Kware au Read More

Jinsi ya kufanya nyuki waingie kwenye mzinga mpya

Jinsi ya kufanya nyuki waingie kwenye mzinga mpya

Ukitaka kuwavutia na kuingiza nyiki kwenye mzinga unatakiwa kufanya yafuatayo;

  1. Tafuta ... Read More
Mchanganuo wa Tsh 300,000/= kwa uzalishaji wa kuku wa kienyeji kwa faida

Mchanganuo wa Tsh 300,000/= kwa uzalishaji wa kuku wa kienyeji kwa faida

Hapa tuta hitaji kuku 11 tu wakubwa wanao taga yani majike 10 na Jogoo 1 tu. Kwa kutumia kuku hao... Read More

Mambo muhimu ya kuzingatia kwenye ufugaji wa nyuki wa asali

Mambo muhimu ya kuzingatia kwenye ufugaji wa nyuki wa asali

Mtaalamu wa nyuki

Unapohitaji unahitaji kufuga nyuki ni lazima uwe na uelewa wa m... Read More
Mbinu za kuzuia magonjwa kwa kuku

Mbinu za kuzuia magonjwa kwa kuku

Mbinu hizo ni hizi zifuatazo;

Read More

Jinsi ya kutunza nyumba ya kuku ili kuzuia magonjwa

Jinsi ya kutunza nyumba ya kuku ili kuzuia magonjwa

1. Nyumba ya kuku iwe safi na kavu muda wote kuzuia ueneaji na kuzaliana kwa vijidudu vya magonjwa ... Read More
Jinsi ya kulima vizuri vitunguu twaumu (swaumu)

Jinsi ya kulima vizuri vitunguu twaumu (swaumu)

Vitunguu twaumu viungo vinavyopendwa na watu wengi hasa kwa harufu yake nzuri Kwenye chakula na u... Read More