Sidebar with Floating Button
AckySHINE SMSπŸ’ŒπŸ’•
☰
AckyShine

Kisa cha kusisimua: Funzo kwa mabinti

Featured Image

Kijana maskini na mwenye maisha duni alimpenda msichana mmoja
Baada ya kutumia muda mwingi kumfikiria msichana huyo,
Siku moja akaamua kumwita na kumwambia ukweli ya kwamba amempenda na angehitaji kumuoa.

Msichana kwa nyodo na jeuri akasema "sikiliza tena unisikilize kwa makini wewe maskini mshahara wako unaopokea kwa mwezi hautoshi hata kwa matumizi yangu ya siku moja sasa utawezaje kunitunza mm!

Kwaufupi mm sio levo zako hivyo basi sahau kabisa kuhusu kunipata mimi
Nenda katafute maskini mwenzio atakae endana na maisha yako,
Mwisho akamwangalia kwa dharau na kisha akaenda zake.

Kwanzia siku ile kijana hakubahatika tena kumuona msichana yule lkn kwakuwa alimpenda basi hakuweza kumsahau kirahisi rahisi siku zilienda na miezi ikasonga,
Miaka 10 baadae wawili hawa walikuja kukutana katika supermarket moja hivi mjini

Kijana alipomwona msichana alitabasamu lakin kabla hajasema chochote msichana kama kawaida yake kwa dharau akasema "we maskin upo! hivi na ww unaingiaga supermarket eh!

Akaongeza huku akisema walau sasahivi nakuona umependeza inaonekana boss wako kakuongeza mshahara
ila kwa kifupi naomba nikwambie sasahivi nimeshaolewa mume wangu anafanya kazi kwenye kampuni moja hivi ya mtu binafsi kampuni maarufu sana na mshahara wa mume wangu ni shilingi milioni moja na laki mbili kwa mwezi na malupulupu mengine kibao,
Unafikiri ww na umaskini wako kuna siku utakuja kufikia kiwango cha mshahara anachopokea mume wangu!

Macho ya kijana yalitokwa na machozi kwa kuona msichana hajabadilika na anaendelea kuwa na maneno ya kejeri na dharau.

Mara hii mume wa yule dada akaingia ktk supermarket
Ile kumuona yule kijana mume akasema "ooh! Kiongozi upo hapa! Leo imekuwa bahati umekutana na mke wangu!" Kisha akamgeukia mke wake na kusema "mke wangu huyu ndo boss wangu

Na unajua nn mke wangu usishangae kumuona boss wangu anakuja kununua vitu mwenyewe hapa supermarket ukweli ni kwamba boss wangu hana mke, anasema alisha wahi kumpenda msichana mmoja lakini hakufanikiwa kumpata na amekuwa na ndoto ya kuja kukutana tena na msichana huyo ndio maana mpaka sasa bado hajaoa.

Akaendelea kusema hebu fikiria ni bahati kiasi gani alikuwa nayo msichana huyo kama angekubali kuolewa na boss wangu leo hii siangekuwa
maisha!

Muda wote msichana alikuwa kimya hajui hata ajibu nn kwa dharau alizomuonyesha kijana tangu mwanzo.


UJUMBE WANGU
Kwenye maisha mambo huweza kubadilika kama vile upepo unavoweza kubadili mwelekeo kulingana na masaa Hivyo basi usimdharau na kumbeza mtu yeyote kwa sababu ya hali aliyonayo,
Maana kila mtu anafungu lake alilopangiwa na Mungu,

Lakini pia kumbuka hakuna ajuaye kesho
Wakati mwingine mtu unayemdharau leo ndiye huyohuyo ambaye kesho utasimulia mafanikio yake.

Kwako unayesoma ujumbe huu nakuombea Mungu akakufungulie milango ya baraka na kuyapa thamani maisha yako ili pale ulipozomewa ukashangiliwe na wale wote waliokudharau punde wakapate kukupigia magoti kwa uweza wa Mungu.

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

Director J (User) on May 15, 2025

Good story πŸ’ͺ

Related Posts

Kukabiliana na Mazoea ya Kukosa Mshikamano katika Familia: Kuunda Nafasi ya Kusaidiana

Kukabiliana na Mazoea ya Kukosa Mshikamano katika Familia: Kuunda Nafasi ya Kusaidiana

  1. Familia ni kitovu cha mahusiano ya kijamii. Hivyo basi, ni muhimu kuhakikisha kuwa kuna... Read More

Ushawishi wa Teknolojia katika Kufanya Mapenzi: Changamoto na Fursa za Zama za Kidijitali

Ushawishi wa Teknolojia katika Kufanya Mapenzi: Changamoto na Fursa za Zama za Kidijitali

  1. Teknolojia imebadilisha jinsi watu wanavyofanya mapenzi. Kwa sasa, kuna zana nyingi za ... Read More

Njia za Kuimarisha Ushirikiano wa Kijamii na Kuwa na Urafiki katika Familia

Njia za Kuimarisha Ushirikiano wa Kijamii na Kuwa na Urafiki katika Familia

Ushirikiano wa kijamii ni jambo muhimu sana katika maisha yetu. Ni muhimu kwa sababu inatupa furs... Read More

Angalia binadamu walivyo

Angalia binadamu walivyo

Angalia Binadamu walivyo!,

"Ukitafuta sana anakuita MCHAWI,"

Ukifanikiwa sio BURE,Read More

Mbinu Bora za Kuimarisha Ushirikiano wa Kifedha Ndani ya Familia

```html

Jinsi ya Kuimarisha Ushirikiano wa Kifedha Ndani ya Familia: Kukuza Ustawi na Uthabiti w... Read More

Kuweka Kipaumbele cha Kujifunza na Kukua Pamoja ili Kuwa na Amani na Furaha katika Familia

Kuweka Kipaumbele cha Kujifunza na Kukua Pamoja ili Kuwa na Amani na Furaha katika Familia

Kuweka kipaumbele cha kujifunza na kukua pamoja ni muhimu sana katika familia ili kufikia amani n... Read More

Jinsi ya Kupenda na Kuunga Mkono Watoto Walemavu: Kuunda Mazingira ya Ukuaji na Furaha

Jinsi ya Kupenda na Kuunga Mkono Watoto Walemavu: Kuunda Mazingira ya Ukuaji na Furaha

Siku zote, kama wazazi au watunzi wa watoto, tunapaswa kujifunza jinsi ya kupenda na kuunga mkono... Read More

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya mazingira na uhifadhi wa asili

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya mazingira na uhifadhi wa asili

Jinsi ya Kuwasiliana na Mpenzi Wako Kuhusu Masuala ya Mazingira na Uhifadhi wa Asili

Kumek... Read More

Njia za Kuimarisha Ushirikiano wa Kijamii na Familia katika Mahusiano

Njia za Kuimarisha Ushirikiano wa Kijamii na Familia katika Mahusiano

Kuimarisha ushirikiano wa kijamii na familia ni muhimu sana katika kuendeleza mahusiano yenye fur... Read More

Jinsi ya Kujenga Heshima na Uthamani katika Ndoa na mke wako

Jinsi ya Kujenga Heshima na Uthamani katika Ndoa na mke wako

Kujenga heshima na uthamani katika ndoa na mke wako ni muhimu sana kwa ustawi wa uhusiano wenu. Hapa... Read More
Njia za Kupunguza Mazoea ya Kukosa Uwiano katika Familia: Kuweka Nafasi ya Mazungumzo na Ushiriki

Njia za Kupunguza Mazoea ya Kukosa Uwiano katika Familia: Kuweka Nafasi ya Mazungumzo na Ushiriki

Familia ni kitovu cha maisha yetu, lakini kuna wakati tunakosa uwiano na kuwa na mazoea ambayo ya... Read More

Kuunda Mazingira ya Ushirikiano na Kuhamasisha Kujali katika Familia Yako

Kuunda Mazingira ya Ushirikiano na Kuhamasisha Kujali katika Familia Yako

Kuunda mazingira ya ushirikiano na kuhamasisha kujali katika familia ni jambo muhimu ambalo linap... Read More