Kwa ajili ya Baba Mtakatifu wetu ..(N); Bwana, umpe moyo wako wa uchungaji mwema
Kwa ajili ya makardinali na maaskofu wakuu; Uwape moyo wa kichungaji ee Bwana
Kwa ajili ya mapadre wa majimbo; Uwajaze na Roho wako ee Bwana
Kwa ajili ya mapadre watawa; Wakamilishe katika wito wao ee Bwana
Kwa ajili ya mapadre walioko hatarini; Uwaokoe ee Bwana
Updated at: 2024-05-27 07:13:38 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Kwa ajili ya Baba Mtakatifu wetu ..(N); Bwana, umpe moyo wako wa uchungaji mwema Kwa ajili ya makardinali na maaskofu wakuu; Uwape moyo wa kichungaji ee Bwana Kwa ajili ya mapadre wa majimbo; Uwajaze na Roho wako ee Bwana Kwa ajili ya mapadre watawa; Wakamilishe katika wito wao ee Bwana Kwa ajili ya mapadre walioko hatarini; Uwaokoe ee Bwana Kwa ajili ya mapadre wenye udhaifu; Uwatie nguvu ee Bwana Kwa ajili ya mapadre wenye hofu; Uwape amani ee Bwana Kwa ajili ya mapadre waliokata tamaa; Uwavuvie upya ee Bwana Kwa ajili ya mapadre wakaao upweke; Uwasindikize ee Bwana Kwa ajili ya mapadre wamisionari; Uwalinde ee Bwana Kwa ajili ya mapadre wanaohubiri; Uwaangazie ee Bwana Kwa ajili ya mapadre na watawa waliokufa; Uwafikishe kwenye utukufu wako ee Bwana Kwa ajili ya mapadre wote; Wajalie hekima na ufahamu wako ee Bwana Kwa ajili ya mapadre wote; Uwajalie elimu na shauri lako Kwa ajili ya mapadre wako; wajalie wakuheshimu na wakuogope Kwa ajili ya mapadre wote; Wajalie subira na upendo Kwa ajili ya mapadre wote; wajalie utii na upole Kwa ajili ya mapadre wote; uwajalie hamu kuu ya kuokoa roho za watu Kwa ajili ya mapadre wote; wape fadhila za imani, matumaini na mapendo Kwa ajili ya mapadre wote; Wajalie upendo mkuu kwa Ekaristi Tunakuomba uwajalie mapadre wote; Waheshimu uhai na hadhi ya mtu ee Bwana Tunakuomba uwajalie mapadre wote nguvu na bidii katika kazi zao ee Bwana Tunakuomba uwajalie mapadre wote amani katika mahangaiko yao ee Bwana Tunakuomba uwajalie mapadre wote upendo mkuu kwa Utatu Mtakatifu ee Bwana Tunakuomba uwajalie mapadre wote upendo mkuu kwa Bikira Maria ee Bwana Uwajalie mapadre wote wawe mwanga wa Kristo ee Bwana Uwajalie mapadre wote, wawe chumvi kwa ulimwengu ee Bwana Uwajalie mapadre wote, wajizoeze kujitoa sadaka na kujinyima ee Bwana Uwajalie mapadre wote, wawe watakatifu kimwili, kiakili na kiroho ee Bwana Uwajalie mapadre wote wawe watu wa sala ee Bwana Uwajalie mapadre wote wawe kioo cha imani kwako ee Bwana Uwajalie mapadre wote wajali sana wongofu wetu ee Bwana Uwajalie mapadre wote wawe waaminifu kwa wito wao wa kikuhani ee Bwana Uwajalie mapadre wote, ili mikono yao ibariki na kuponya ee Bwana Uwajalie mapadre wote wawake moto wa mapendo yako ee Bwana Uwajalie mapadre wote hatua zao zote ziwe kwa ajili ya utukufu wa Mungu ee Bwana Uwajalie mapadre wote wajazwe na Roho Mtakatifu na uwajalie karama zake kwa wingi ee Bwana.
Tuombe. Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, usikie sala tunazokutolea kwa ajili ya mapadre wetu. Uwajalie wafahamu waziwazi kazi uliyowaitia kuifanya, uwape neema zote wanazohitaji ili waitikie wito wako kwa ushujaa, kwa upendo, na majitoleo yenye udumifu katika mapenzi yako matakatifu. Amina.
Ee Yosef mwenye heri, tunakimbilia kwako, katika masumbuko yetu, na kishaomba shime ya Mchumba wako Mtakatifu, tunaomba pia kwa matumaini usimamizi wako. Kwa ajili ya mapendo uliyompenda nayo Bikira Mtakatifu, Mzazi wa Mungu, na kwa ajili ya tunza ya Baba, uliyomtunza nayo Mtoto Yesu, tunakuomba sana, utuangalie kwa wema, sisi tuliokuwa fungu lake Yesu Kristo, tuliokombolewa kwa damu yake, utusimamie katika masumbuko yetu, kwa enzi na shime yako.
Updated at: 2024-05-27 07:14:10 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Ee Yosef mwenye heri, tunakimbilia kwako, katika masumbuko yetu, na kishaomba shime ya Mchumba wako Mtakatifu, tunaomba pia kwa matumaini usimamizi wako. Kwa ajili ya mapendo uliyompenda nayo Bikira Mtakatifu, Mzazi wa Mungu, na kwa ajili ya tunza ya Baba, uliyomtunza nayo Mtoto Yesu, tunakuomba sana, utuangalie kwa wema, sisi tuliokuwa fungu lake Yesu Kristo, tuliokombolewa kwa damu yake, utusimamie katika masumbuko yetu, kwa enzi na shime yako. Ee Mlinzi amini wa Jamaa Takatifu, uwakinge watoto wateule wa Yesu Kristo, ee Baba uliyetupenda mno, utuepusha na kilema chochote cha madanganyo na upotevu. Ee kinga yetu mwezaji,utusimamie huko juu mbinguni ulipo, tunaposhindana na wenye nguvu wakaao gizani. Kama vile siku za kale ukamwokoa Mtoto Yesu katika hatari ya kuuawa, na leo hivi, ulikinge Kanisa Takatifu la Mungu katika mitego ya adui, na katika shida yote, mtunze daima kila mmoja wetu, tupate mfano wako, tusaidie kwa msaada wako, kukaa na utakatifu maisha, kufa kifo chema, na kupokelewa mbinguni makao ya raha milele. Amina
Salamu Maria Umejaa neema Bwana yu nawe Umebarikiwa kuliko wanawake wote Na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa Maria Mtakatifu Mama wa Mungu Utuombee sisi wakosefu Sasa, na saa ya kufa kwetu. Amina.
Updated at: 2024-05-27 07:13:39 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Salamu Maria Umejaa neema Bwana yu nawe Umebarikiwa kuliko wanawake wote Na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa Maria Mtakatifu Mama wa Mungu Utuombee sisi wakosefu Sasa, na saa ya kufa kwetu. Amina.
Nakusikitikia sana Mama Mtakatifu Maria kwa sababu ya ukiwa wako mkuu. Uchungu wako ulikuwa mkubwa sana ulipotazama mateso na kifo cha Mwana wako mpenzi. Muda ule uliweza kutuliz kidogo kwa sababu ya kumwona angali hai. Lakini je, baada ya kufa na kumzika? Sasa wewe ni mkiwa mkubwa mno!
Updated at: 2024-05-27 07:14:14 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Nakusikitikia sana Mama Mtakatifu Maria kwa sababu ya ukiwa wako mkuu. Uchungu wako ulikuwa mkubwa sana ulipotazama mateso na kifo cha Mwana wako mpenzi. Muda ule uliweza kutuliz kidogo kwa sababu ya kumwona angali hai. Lakini je, baada ya kufa na kumzika? Sasa wewe ni mkiwa mkubwa mno! Uh, ukiwa wa pekee, uniombee mimi ninayempoteza mara nyingi kwa dhambi zangu. Unijalie nisimpoteze tena Yesu wangu kwa ubaya wa uvivu wangu, bali nimtumikie kiaminifu duniani hapa ili nimwone na kumfurahia milele mbinguni. Amina.
Ee Baba yetu Mungu mkuu,umenilinda usiku huu. Nakushukuru kwa moyo, ee Baba,Mwana na Roho. Nilinde tena siku hii,niache dhambi nikutii.Naomba sana Baba wee, baraka yako nipokee. Bikira safi, Ee Maria nisipotee nisimamie. Mlinzi mkuu malaika wee kwa Mungu wetu niombee,nitake nitende mema tu na mwisho nije kwako juu.Amina.
Updated at: 2024-05-27 07:14:06 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Kwa jina la Baba…..
Ee Baba yetu Mungu mkuu,umenilinda usiku huu.
Nakushukuru kwa moyo, ee Baba,Mwana na Roho.
Nilinde tena siku hii,niache dhambi nikutii.Naomba sana Baba wee, baraka yako nipokee.
Bikira safi, Ee Maria nisipotee nisimamie.
Mlinzi mkuu malaika wee kwa Mungu wetu niombee,nitake nitende mema tu na mwisho nije kwako juu.Amina.
NIA NJEMA.
Kumueshimu Mungu wangu,namtolea roho yangu.
Nifanye kazi nipumzike ,amri zake tu nishike.
Wazo,neno,tendo lote namtolea Mungu pote Roho,Mwili chote changu.
Pendo na uzima wangu.
Mungu wangu nitampenda wala dhambi sitatenda.
Jina lako nasifia,utakalo hutimia kwa utii navumili.
Teso na matata pia,nipe Bwana neema zako, niongeze sifa yako.Amina.
SALA YA MATOLEO.
Ee Yesu kwa mikono ya Bikira Maria,na kwa maungano na sadaka yako kuu.
Ninakutolea sala,matendo,masumbuko na furaha zangu zote za leo.
Ee Yesu ufalme wako utufikie.Amina.
BABA YETU.
Baba yetu uliye mbinguni,jina lako litukuzwe.
Ufalme wako ufike.Utakalo lifanyike duniani kama mbinguni.
Utupe leo mkate wetu wa kila siku.Utusamehe makosa yetu,kama tunavyo wasamehe na sisi waliyo tukosea.
Usitutie katika kishawishi,lakini utuopoe maovuni.Amina.
SALAMU MARIA.
Salamu Maria,umejaa neema Bwana yu nawe,umebarikiwa kuliko wanawake wote,na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa.
Maria mtakatifu Mama wa Mungu,utuombee sisi wakosefu sasa na saa ya kufa kwetu.Amina.
KANUNI YA IMANI.
Nasadiki kwa Mungu,Baba Mwenyezi,muumba mbingu na dunia.
Na kwa Yesu Kristu Mwanaye wa pekee,Bwana wetu aliyetungwa kwa Roho Mtakatifu,akazaliwa na Bikira Maria,akateswa kwa mamlaka ya ponsyo Pilato,akasulibiwa, akafa,akazikwa,akashukia kuzimu siku ya tatu akafufuka katika wafu, akapaa mbinguni amekaa kuume kwa Mungu Baba Mwenyezi,toka huko atakuja kuwahukumu wazima na wafu.
Nasadiki kwa Roho Mtakatifu,kanisa takatifu katoliki ushirika wa Watakatifu,maondoleo ya dhambi,ufufuko wa miili na uzima wa milele.Amina.
AMRI ZA MUNGU.
1.Ndimi Bwana Mungu wako,usiabudu miungu wengine.
2.Usilitaje bure jina la Mungu wako.
3.Shika kitakatifu siku ya Mungu.
4.Waheshimu Baba na Mama upate miaka mingi na heri duniani.
5.Usiue.
6.Usizini.
7.Usiibe.
8.Usiseme uwongo.
9.Usitamani mwanamke asiye mke wako.
10.Usitamani mali ya mtu mwingine.
AMRI ZA KANISA.
1.Hudhuria misa takatifu domonica na sikukuu zilizo amuliwa.
2.Funga siku ya jumatano ya majivu,usile nyama siku ya Ijumaa kuuu.
3.Ungama dhambi zako walau mara moja kwa mwaka.
4.Pokea Ekarist takatifu hasa wakati wa Pasaka
5.Saidia kanisa katoliki kwa zaka.
6.Shika sheria katoliki za ndoa.
SALA YA IMANI.
Mungu wangu,nasadiki maneno yote linayo sadiki na kufundisha kanisa katoliki la Roma kwani ndiwe uliye fumbuliwa hayo,wala hudanganyiki na wala hudanganyi.Amina.
SALA YA MATUMAINI.
Mungu wangu,natumaini kwako nitapewa kwa njia ya Yesu Kristu,neema zako duniani na utukufu mbinguni.Kwani ndiwe uliyeagana hayo nasi nawe mwamini.Amina.
SALA YA MAPENDO.
Mungu wangu,nakupenda zaidi ya chochote, kwani ndiwe mwema ndiwe mwenye kupendeza.
Nampenda na jirani yangu kama nafisi yangu kwa ajiri yako.Amina.
SALA YA KUTUBU.
Mungu wangu,nimetubu sana dhambi zangu kwani ndiwe mwema,ndiwe mwenye kupendeza wachukizwa na dhambi.
Basi sitaki kukosa tena nitafanya kitubio,naomba neema yako nipate kurudi.Amina.
SALA KWA MALAIKA MLINZI.
Malaika mlinzi wangu,unilinde katika hatari zote za Roho na za Mwili.Amina.
MALAIKA WA BWANA.
K.Malaika wa Bwana alimpasha habari Maria.
W.Naye akapata mimba kwa Roho mtakatifu.
Salamu Maria…..
K.Ndimi mtumishi wa Bwana.
W.Nitendewe ulivyo nena.
Salamu Maria…..
K. Neno la Mungu akatwaa Mwili.
W. Akakaa kwetu.
Salamu Maria….
K. Utuombee Mzazi Mtakatifu wa Mungu.
W. Tujaliwe ahadi za Kristu.
Tuombe.
Tunakuomba Ee Bwana utie neema yako mioyoni mwetu ili sisi tuliyojuwa kwa maelezo ya malaika kwamba, Kristu mwanao amejifanya mtu kwa mateso na msalaba wake.
Tufikishwe kwenye utukufu wa ufufuko.
Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu Bwana wetu.Amina.
ATUKUZWE BABA.
Atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu,kama mwanzo na sasa na siku zote na milele.Amina.
K. Moyo Mtakatifu wa Yesu
W.Utuhurumie.
K. Moyo safi wa Bikira Maria.
W. Utuombee.
K. Mtakatifu Yosefu.
W. Utuombee.
K. Watakatifu somo wa majina yetu.
W. Mtuombee.
K.Watakatifu wote wa Mungu.
W.Mtuombee.
Kwa jina la Baba…..
(Sala iliyotungwa na Mtk. Aloisi) Bibi yangu mtukufu Maria, nakuwekea amana ya roho yangu na mwili wangu, nikikuomba uipokee amana yangu, kuitunzia ulinzi mwema ulinzi bora, ninakuaminia na kila neno langu, matumaini na kitulizo na kisongo chote, na masumbuko na uzima na ukomo
Updated at: 2024-05-27 07:13:48 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
(Sala iliyotungwa na Mtk. Aloisi) Bibi yangu mtukufu Maria, nakuwekea amana ya roho yangu na mwili wangu, nikikuomba uipokee amana yangu, kuitunzia ulinzi mwema ulinzi bora, ninakuaminia na kila neno langu, matumaini na kitulizo na kisongo chote, na masumbuko na uzima na ukomo wa uzima wangu: nitakayo ndiyo unifanyizie kwa maombezi na stahili zako, ili mambo yangu yote yapate kuongoka, yakiwa na kufuata mapenzi yako, pamoja na mapenzi ya Mwanao. Amina.
Updated at: 2024-05-27 07:13:37 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
KUMBUKA
Kumbuka ee Bikira mwenye rehema, haijasikika kamwe kwamba ulimwacha mtu aliyekimbilia ulinzi wako, akiomba msaada wako, akitaka umwombe.
Nami kwa matumaini hayo, nakukimbilia ee mama, mkuu wa mabikira, ninakuja kwako, ninasimama mbele yako, nikilalamika mimi mkosefu ewe mama wa neno la mungu, usiyakatae maneno yangu, mbali uyasikilize kwa wema na unitimizie Amina.
Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina.
SALA YA KUSHUKURU
Tunakushukuru, ee Mungu, kwa mapaji uliyotujalia leo. Amina.
Baba yetu …
Salamu Maria …
Updated at: 2024-05-27 07:14:07 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina.
SALA YA KUSHUKURU
Tunakushukuru, ee Mungu, kwa mapaji uliyotujalia leo. Amina.
Baba yetu …
Salamu Maria …
SALA YA IMANI
Mungu wangu, nasadiki maneno yote. Linayosadiki na linayofundisha Kanisa Katoliki la Roma. Kwani ndiwe uliyetufumbulia hayo. Wala hudanganyiki, wala hudanganyi. Amina.
SALA YA MATUMAINI
Mungu wangu, natumaini kwako, nitapewa kwa njia ya Yesu Kristo. Neema zako hapa duniani, na utukufu mbinguni. Kwani ndiwe uliye agana hayo nasi, nawe mwamini. Amina.
SALA YA MAPENDO
Mungu wangu, nakupenda zaidi ya chochote. Kwani ndiwe mwema, ndiwe mwenye kupendeza. Nampenda na jirani yangu, kama nafsi yangu, kwa ajili yako. Amina.
KUTUBU DHAMBI
Tuwaze katika moyo wetu makosa ya leo tuliyomkosea Mungu kwa mawazo, kwa maneno, kwa vitendo na kwa kutotimiza wajibu. (Husubiri kidogo ).
Nakuungamia Mungu Mwenyezi, nanyi ndugu zangu, kwani nimekosa mno, kwa mawazo, kwa maneno, kwa vitendo, na kwa kutotimiza wajibu. Nimekosa mimi, nimekosa mimi, nimekosa sana. Ndiyo maana nakuomba Maria mwenye heri, Bikira daima, Malaika na Watakatifu wote, nanyi ndugu zangu, niombeeni kwa Bwana Mungu wetu. Mungu Mwenyezi atuhurumie, atusamehe dhambi zetu, atufikishe kwenye uzima wa milele. Amina.
SALA YA KUWAOMBEA WATU
Ee Mungu, nawaombea watu wa nchi hii, wapate kusikia maneno yako na kukupenda wewe Bwana Mungu wetu.
SALA KWA MALAIKA MLINZI
Malaika mlinzi wangu, unilinde katika hatari zote za roho na za mwili. Amina.
MALAIKA WA BWANA
(kipindi kisicho cha Pasaka) Malaika wa Bwana alimpasha habari Maria. Naye akapata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Salamu, Maria,….. Ndimi mtumishi wa Bwana. Nitendewe ulivyonena. Salamu, Maria…. Neno la Mungu akatwaa mwili. Akakaa kwetu. Salamu, Maria…. Utuombee, Mzazi mtakatifu wa Mungu. Tujaliwe ahadi za Kristu. Tuombe: Tunakuomba, Ee Bwana, utie neema yako mioyoni mwetu, ili sisi tuliojua kwa maelezo ya Malaika kwamba Mwanao amejifanya Mtu kwa mateso na msalaba wake tufikishwe kwenye utukufu wa ufufuko. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu Bwana wetu. AMINA.
AU;
MALKIA WA MBINGU (kipindi cha Pasaka)
Malkia wa mbingu, furahi, aleluya. Kwani uliyestahili kumchukua, Aleluya. Amefufuka alivyosema, Aleluya. Utuombee kwa Mungu, Aleluya. Furahi shangilia, ee Bikira Maria, Alaluya. Kwani hakika Bwana amefufuka Aleluya. Tuombe. Ee Mungu, uliyependa kuifurahisha dunia kwa kufufuka kwake Bwana wetu Yesu Kristu, Mwanao, fanyiza, twakuomba, kwa ajili ya Bikira Maria, tupate nasi furaha za uzima wa milele. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu Bwana wetu. Amina.
ATUKUZWE (mara tatu) Atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu. Kama mwanzo na sasa na siku zote na milele. Amina.
KUJIKABIDHI
Enyi Yesu, Maria na Yosefu nawatolea moyo na roho na uzima wangu! Enyi Yesu, Maria na Yosefu mnijilie saa ya kufa kwangu! Enyi Yesu, Maria na Yosefu mnijalie nife mikononi mwenu!
(Rehema ya siku 300).
WIMBO:
Kwa heri Yesu mpenzi mwema, Naenda usiudhike mno. Nakushukuru, nakupenda, Kwa hizo nyimbo za mwisho. Asubuhi nitarudi. Yesu kwa heri.
Kwa heri Mama mtakatifu, Sasa napita pumzika. Asante kwa moyo na nguvu, Leo umeniombea. Asubuhi nitarudi. Mama kwa heri.
Kwa heri Yosefu mnyenyekevu, Kazi zatimilizika. Kama mchana, leo usiku, Nisimamie salama. Asubuhi nitarudi. Yosefu kwa heri.
Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina.
KUOMBA ULINZI WA USIKU
Mungu wangu naenda kulala naomba malaika 14, waende nami, wawili juu, wawili chini, wawili upande wa kuume, wawili upande wa kushoto, wawili wanifunike, wawili waniamshe, wawili wanipeleke juu mbinguni. Mimi mtoto mdogo, roho yangu ni ndogo, haina nafasi kwa mtu yoyote ila kwa Yesu pekee. Amina.
Anza kusali Rozari kwa kuibusu miguu ya Bwana Yesu katika taswira (picha) yake Msalabani kisha fanya Ishara ya Msalaba ukiwa unasema “Kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, Amina”.
Updated at: 2024-05-27 07:14:15 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Mwongozo wa namna ya Kusali Rozari Takatifu ya Mama Bikira Maria
Anza kusali Rozari kwa kuibusu miguu ya Bwana Yesu katika taswira (picha) yake Msalabani kisha fanya Ishara ya Msalaba ukiwa unasema “Kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, Amina”.
Taja kwa ufupi nia za Rozari hii. Tangaza nia hizo kwa sauti kama mnasali wengi kwa pamoja, Mfano, “Tusali kuombea amani katika nchi yetu na ulimwenguni kote, na tuunganishe nia hizo na nia zetu sisi wenyewe, nk).
Baada ya Sala ya Nasadiki pamoja na ya Baba Yetu, tunamwomba Mungu (Utatu Mtakatifu) fadhila za Imani, Matumaini na Mapendo, zikiambatana na Salamu Maria tatu.
Mojawapo ya maneno yafuatayo huweza kutumika: “Mungu Baba utuongezee Imani. Salamu Maria, …… Mungu Mwana utuongezee matumaini, Salamu Maria, …… Mungu Roho Mtakatifu washa nyoyo zetu kwa mapendo yako, Salamu Maria, …..”
Au;
“Utuongezee Imani ee Bwana, Salamu Maria,…. Utuongezee matumaini ee Bwana, Salamu Maria,…. Uwashe nyoyo zetu kwa mapendo yako ee Bwana, Salamu Maria, …..” Au; “Salamu e uliyechaguliwa na Mungu Baba, Salamu Maria,….. Salamu e Mama wa Mungu Mwana, Salamu Maria,….. Salamu e Mchumba wa Mungu Roho Mtakatifu, Salamu Maria,……” Atukuzwe Baba, na Mwana na Roho Mtakatifu, kama mwanzo na sasa na siku zote, na milele, Amina.
Ee Yesu wangu, utusamehe dhambi zetu, utuepushe na moto wa milele, ongoza roho zote mbinguni, hasa za wale wanaohitaji huruma yako zaidi. Tuwasifu milele, Yesu, Maria na Yosef.
Kisha endelea na sala zinazofuata kama mpangilio unavyoonyesha hapo juu.
Kila baada ya Tendo moja na makumi ya Salamu Maria…, “Atukuzwe..”, “Ee Yesu wangu…” na “Tuwasifu milele…” kama muda unatosha wimbo ufaao wa Bikira Maria uimbwe (kama muda ni mfupi basi angalau ubeti mmoja mmoja uimbwe kila baada ya makumi hayo). Baada ya Wimbo, Tendo linalofuata litangazwe kwa sauti pamoja na tafakari fupi au ombi linaloambatana na Tendo husika kama inavyoonyeshwa hapa chini.
MATENDO YA ROZARI TAKATIFU
MATENDO YA FURAHA (Jumatatu na Jumamosi)
Tendo la kwanza; Malaika Gabrieli anampasha habari Maria kuwa atakuwa Mama wa Mungu. Tumwombe Mungu atujalie unyenyekevu.
Tendo la pili; Maria Mtakatifu anakwenda kumtembelea Elizabeti. Tumwombe Mungu atujalie mapendo ya jirani.
Tendo la tatu; Yesu anazaliwa Betlehemu. Tumwombe Mungu atujalie moyo wa ufukara
Tendo la nne; Yesu anatolewa hekaluni. Tumwombe Mungu atujalie usafi wa moyo.
Tendo la tano; Maria anamkuta Yesu hekaluni. Tumwombe Mungu atujalie kuwatii wakubwa wetu.
MATENDO YA UCHUNGU (Jumanne na Ijumaa)
Tendo la kwanza; Yesu anatoka jasho la damu kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie sikitiko la dhambi.
Tendo la pili; Yesu anapigwa kwa mijeledi kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie kuacha dhambi za uchafu.
Tendo la tatu; Yesu anatiwa miiba kichwani kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie kushinda kiburi.
Tendo la nne; Yesu anachukua Msalaba kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie kuvumilia taabu.
Tendo la tano; Yesu anakufa Msalabani. Tumwombe Mungu atujalie kuwapenda Yesu na Maria.
MATENDO YA UTUKUFU (Jumatano na Jumapili)
Tendo la kwanza; Yesu anafufuka. Tumwombe Mungu atujalie kugeuka watakatifu.
Tendo la pili; Yesu anapaa mbinguni. Tumwombe Mungu atujalie kwenda mbinguni.
Tendo la tatu; Roho Mtakatifu anawashukia Mitume. Tumwombe Mungu atujalie bidii katika dini yetu.
Tendo la nne; Bikira Maria anapalizwa mbinguni. Tumwombe Mungu atujalie kufa vizuri.
Tendo la tano; Bikira Maria anawekwa Malkia mbinguni. Tumwombe Mungu atujalie kudumu katika njia njema.
MATENDO YA MWANGA (Alhamisi)
Tendo la kwanza; Yesu anabatizwa Mto Jordani. Tumwombe Mungu atujalie uaminifu kwa ahadi zetu za ubatizo.
Tendo la pili; Yesu anageuza maji kuwa divai huko Kana. Tumwombe Mungu atujalie kuukoleza ulimwengu kwa chachu ya enjili.
Tendo la tatu; Yesu anatangaza Ufalme wa Mungu. Tumwombe Mungu atujalie kupokea Ufalme wake kwa toba ya kweli.
Tendo la nne; Yesu anageuka sura. Tumwombe Mungu atujalie neema ya kuung’arisha ulimwengu kwa uso wa Yesu.
Tendo la tano; Yesu anaweka Sakramenti ya Ekaristia. Tumwombe Mungu atujalie neema ya kujitoa sadaka kwa ajili ya wengine.
LITANIA YA BIKIRA MARIA
Bwana utuhurumie
Bwana utuhurumie
Kristo utuhurumie
Bwana utuhurumie
Bwana utuhurumie
Kristo utusikie
Kristo utusikilize
Mungu Baba wa Mbinguni,…… Utuhurumie
Mungu Mwana Mkombozi wa dunia ……… Utuhurumie
Mungu Roho Mtakatifu …….. Utuhurumie
Utatu Mtakatifu Mungu Mmoja …….. Utuhurumie
Maria Mtakatifu ………. utuombee
Mzazi Mtakatifu wa Mungu …….. utuombee
Bikira Mtakatifu Mkuu wa Mabikira …….. utuombee
Mama wa Kristo ……… utuombee
Mama wa Neema ya Mungu ………….. utuombee
Mama Mtakatifu sana ……… utuombee
Mama mwenye usafi wa Moyo ……….. utuombee
Mama mwenye ubikira ……….. utuombee
Mama usiye na doa ……….. utuombee
Mama mpendelevu ………. utuombee
Mama mstajabivu ………. utuombee
Mama wa Muumba ………. utuombee
Mama wa Mkombozi ………….. utuombee
Mama wa Kanisa……….. utuombee
Bikira mwenye utaratibu ………….. utuombee
Bikira mwenye heshima ………….. utuombee
Bikira mwenye sifa ………….. utuombee
Bikira mwenye uwezo ………….. utuombee
Bikra mweye huruma ………….. utuombee
Bikra mwaminifu………….. utuombee
Kioo cha haki ………….. utuombee
Kikao cha hekima ………….. utuombee
Sababu ya furaha yetu ………….. utuombee
Chombo cha neema ………….. utuombee
Chombo cha kuheshimiwa ………….. utuombee
Chombo bora cha ibada ………….. utuombee
Waridi lenye fumbo ………….. utuombee
Mnara wa Daudi ………….. utuombee
Mnara wa pembe ………….. utuombee
Nyumba ya dhahabu ………….. utuombee
Sanduku la Agano ………….. utuombee
Mlango wa Mbingu ………….. utuombee
Nyota ya asubuhi ………….. utuombee
Afya ya wagonjwa ………….. utuombee
Kimbilio la wakosefu ………….. utuombee
Mtuliza wenye huzuni ………….. utuombee
Msaada wa waKristo ………….. utuombee
Malkia wa Malaika ………….. utuombee
Malkia wa Mababu ………….. utuombee
Malkia wa Manabii ………….. utuombee
Malkia wa Mitume ………….. utuombee
Malkia wa Mashahidi ………….. utuombee
Malkia wa Waungama dini ………….. utuombee
Malkia wa Mabikira ………….. utuombee
Malkia wa Watakatifu wote ………….. utuombee
Malkia uliyepalizwa Mbinguni ………….. utuombee
Malkia wa Rozari takatifu ………….. utuombee
Malkia wa amani ………….. utuombee
Mwanakodoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia,…………..Utusamehe ee Bwana.
Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia,…………..Utusikilize ee Bwana
Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia,…………..Utuhurumie.
Utuombee, Mzazi Mtakatifu wa Mungu,…………..Tujaliwe ahadi za Kristo.
Tuombe
Ee Bwana Mungu, utujalie sisi watumishi wako afya ya roho na mwili siku zote; na kwa maombezi matukufu ya Maria Mtakaatifu Bikira daima, tuopolewe na mashaka ya saa, tupate na furaha za milele. Kwa Kristo Bwana wetu, Amina.