Mtakatifu Yuda Tadei,/ Mtume Mtakatifu,/ mtumishi mwaminifu na rafiki wa Yesu./ Jina la yule msaliti aliyemwuza Yesu/ limewafanya wengi wakusahau./ Walakini Kanisa zima linakuheshimu/ na kukuomba kama Msaidizi katika mashaka makubwa,/ na katika mambo yasiyo na matumaini tena.
Updated at: 2024-05-27 07:14:17 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Mtakatifu Yuda Tadei,/ Mtume Mtakatifu,/ mtumishi mwaminifu na rafiki wa Yesu./ Jina la yule msaliti aliyemwuza Yesu/ limewafanya wengi wakusahau./ Walakini Kanisa zima linakuheshimu/ na kukuomba kama Msaidizi katika mashaka makubwa,/ na katika mambo yasiyo na matumaini tena./
Uniombee mimi mnyonge./ Ninaomba utumie uwezo ule uliojaliwa/ wa kuleta upesi msaada kwa watu walioukosa./ Unisaidie sasa katika mahitaji yangu,/ ili nipate kitulizo na msaada wa mbinguni/ katika lazima zangu,/ masumbuko na mateso,/ hasa/ (taja shida yako)./ Pia ili niweze kumsifu Mungu nawe na wateule wote milele./
Mtakatifu Yuda Tadei,/ utuombee,/ na uwaombee watu wote wanaokuheshimu na kukuomba msaada./
Moyo Mtakatifu wa Yesu,/ Rafiki mpenzi wa Yuda Tadei,/ nakutumainia./
(Mwisho Sali: Baba yetu (x3), Salamu Maria (x3) na Atukuzwe(x3).
Salamu Maria Umejaa neema Bwana yu nawe Umebarikiwa kuliko wanawake wote Na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa Maria Mtakatifu Mama wa Mungu Utuombee sisi wakosefu Sasa, na saa ya kufa kwetu. Amina.
Updated at: 2024-05-27 07:13:39 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Salamu Maria Umejaa neema Bwana yu nawe Umebarikiwa kuliko wanawake wote Na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa Maria Mtakatifu Mama wa Mungu Utuombee sisi wakosefu Sasa, na saa ya kufa kwetu. Amina.
Ee Mama mbarikiwa na Bikira mwenye uchungu, Malkia wa Mashahidi, uliyesimama chini ya msalaba na uliyemtazama Mwana wako akifa, unitazame kwa huruma ya kimama ninayekusikitikia. Kwa sababu ya upanga uliochoma moyo wako, kwa mateso ya maisha yako nakuomba uniangalie kwa wema ukasikilize maombi yangu.
Updated at: 2024-05-27 07:13:57 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Ee Mama mbarikiwa na Bikira mwenye uchungu, Malkia wa Mashahidi, uliyesimama chini ya msalaba na uliyemtazama Mwana wako akifa, unitazame kwa huruma ya kimama ninayekusikitikia. Kwa sababu ya upanga uliochoma moyo wako, kwa mateso ya maisha yako nakuomba uniangalie kwa wema ukasikilize maombi yangu. Nakuomba, ee Mama, uniombee daima kwa Mwana wako, najua hawezi kukuvyima wewe kitu chochote. Basi, ufanye, Moyo wa Mwanao ukubali kunijalia ombi langu hili …………………(taja ombi lako). Maana nitamkimbilia nani katika mahitaji na misiba yangu isipokuwa kwako, ee Mama wa huruma? Wewe hasa unaweza kutusaidia sisi tulio bado katika bonde la machozi kwa sababu ulishiriki mateso ya Mwanao kutukomboa. Umtolee Yesu tone moja la Damu yake takatifu. Umkumbushe ya kuwa wewe ni matumaini, furaha na maisha yetu ukanipatie jambo ninalokuomba kwa Yesu Kristo, bwana wetu. Amina.
Bwana utuhurumie Bwana utuhurumie Kristo utuhurumie Kristo utuhurumie Bwana utuhurumie Bwana utuhurumie Kristo utusikie Kristo utusikilize Baba wa mbinguni Mungu Utuhurumie Mwana, Mkombozi wa dunia Mungu Utuhurumie Roho Mtakatifu Mungu Utuhurumie
Updated at: 2024-05-27 07:14:15 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Bwana utuhurumie Bwana utuhurumie Kristo utuhurumie Kristo utuhurumie Bwana utuhurumie Bwana utuhurumie Kristo utusikie Kristo utusikilize Baba wa mbinguni Mungu Utuhurumie Mwana, Mkombozi wa dunia Mungu Utuhurumie Roho Mtakatifu Mungu Utuhurumie Utatu Mtakatifu Mungu mmoja Utuhurumie Moyo wa Yesu Mwana wa Baba wa Milele Utuhurumie Moyo wa Yesu uliotungwa na Roho Mtakatifu mwilini mwa Mama Bikira Maria Utuhurumie Moyo wa Yesu ulioungana na Neno wa Mungu Utuhurumie Moyo wa Yesu ulio na utukufu pasipo mfano Utuhurumie Moyo wa Yesu, hekalu takatifu la Mungu Utuhurumie Moyo wa Yesu, hema la Yule aliye juu Utuhurumie Moyo wa Yesu tanuru lenye kuwaka mapendo Utuhurumie Moyo wa Yesu, nyumba ya Mungu na mlango wa Mbingu Utuhurumie Moyo wa Yesu, tanuru yenye kuwaka mapendo Utuhurumie Moyo wa Yesu, chombo cha haki na upendo Utuhurumie Moyo wa Yesu, unaojaa upendo na wema Utuhurumie Moyo wa Yesu, kilindi cha fadhila zote Utuhurumie Moyo wa Yesu, unaostahili sifa zote Utuhurumie Moyo wa Yesu, unaotawala mioyo yote Utuhurumie Moyo wa Yesu, zinamokaa hazina za hekima na elimu Utuhurumie Moyo wa Yesu, uliopendelewa na Mungu Baba Utuhurumie Moyo wa Yesu, uliotuenezea maziada yake Utuhurumie Moyo wa Yesu, mtamaniwa wa vilima vya milele Utuhurumie Moyo wa Yesu, wenye uvumilivu na huruma nyingi Utuhurumie Moyo wa Yesu, tajiri kwa wote wenye kukuomba Utuhurumie Moyo wa Yesu, chemchemi ya uzima na utakatifu Utuhurumie Moyo wa Yesu, malipo kwa dhambi zetu Utuhurumie Moyo wa Yesu, ulioshibishwa matusi Utuhurumie Moyo wa Yesu, uliovunjika kwa sababu ya ubaya wetu Utuhurumie Moyo wa Yesu, uliotii mpaka kufa Utuhurumie Moyo wa Yesu, uliochomwa kwa mkuki Utuhurumie Moyo wa Yesu, chemchemi ya faraja zote Utuhurumie Moyo wa Yesu, uzima na ufufuo wetu Utuhurumie Moyo wa Yesu, amani na upatanisho wetu Utuhurumie Moyo wa Yesu, sadaka ya wakosefu Utuhurumie Moyo wa Yesu, unamokaa wokovu wao wenye kukutumaini Utuhurumie Moyo wa Yesu, matumaini yao wenye kuzimia kwako Utuhurumie Moyo wa Yesu, sababu ya furaha ya watakatifu wote Utuhurumie Mwanakondoo wa Mungu, uondoaye dhambi za dunia Utusamehe Bwana Mwanakondoo wa Mungu, uondoaye dhambi za dunia Utusikilize Bwana Mwanakondoo wa Mungu, uondoaye dhambi za dunia Utuhurumie
Kiongozi: Yesu mwenye Moyo mpole na mnyenyekevu, Wote: Ufanye mioyo yetu ifanane na Moyo wako
TUOMBE: (W) Ee Mungu Mwenyezi milele, uuangalie Moyo wa mwanao mpendelevu, pia na heshima na malipo aliyokutolea kwa ajili ya wenye dhambi, uridhike, uwaondolee wenye kuomba toba kwako kwa njia ya huyo Mwanao Yesu Kristo anayeishi na kutawala nawe pamoja na Roho Mtakatifu, Mungu milele. Amina.
SALA YA KUMWOMBA MT. YOSEFU MSAADA (SALA KUU KWA MTAKATIFU YOSEFU)
Ee Mt. Yosefu mwenye heri, tunakimbilia kwako katika masumbuko yetu, na kisha omba shime ya Mchumba wako Mtakatifu, tunaomba pia kwa matumaini usimamizi wako. Kwa ajili ya mapendo uliyompenda Bikira Mtakatifu Mzazi wa Mungu, na kwa ajili ya kumtunza Mtoto Yesu, twakuomba sana, utuangalie kwa wema sie tuliokuwa fungu lake Yesu Kristu, tukakombolewa kwa damu yake. Tusimamie katika masumbuko yetu kwa enzi na shime yako.
Updated at: 2024-05-27 07:13:44 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Ee Mt. Yosefu mwenye heri, tunakimbilia kwako katika masumbuko yetu, na kisha omba shime ya Mchumba wako Mtakatifu, tunaomba pia kwa matumaini usimamizi wako. Kwa ajili ya mapendo uliyompenda Bikira Mtakatifu Mzazi wa Mungu, na kwa ajili ya kumtunza Mtoto Yesu, twakuomba sana, utuangalie kwa wema sie tuliokuwa fungu lake Yesu Kristu, tukakombolewa kwa damu yake. Tusimamie katika masumbuko yetu kwa enzi na shime yako.
Ee Mlinzi amini wa jamaa takatifu, uwakinge watoto wateule wa Yesu Kristu. Ee Baba uliyetupenda mno tuepushe na kilema chochote cha madanganyo na upotevu. Ee kinga yetu mwezaji, utusimamie huko juu mbinguni ulipo, tunaposhindana na wenye nguvu wakaao gizani. Kama vile siku za kale ukamwopoa Mtoto Yesu katika hatari ya kuuawa, na leo hivi likinge Kanisa Takatifu la Mungu katika mitego ya adui, na katika shida yote; mtunze daima kila mmoja wetu, tufwate mfano wako, ili tupate na msaada wako, kukaa na utakatifu maisha, kufa kifo chema, na kupata mbinguni makao ya raha milele. Amina.
Ewe Mtakatifu Yuda Tadei,/ mtume mtukufu na shahidi wa Kristo,/ umesifika pote kwa wepesi wako wa kutoa misaada/ kwa wanaokukimbilia katika matatizo yao mazito./ Pia ni mwombezi wa waliopondeka moyo./
Updated at: 2024-05-27 07:14:23 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Ewe Mtakatifu Yuda Tadei,/ mtume mtukufu na shahidi wa Kristo,/ umesifika pote kwa wepesi wako wa kutoa misaada/ kwa wanaokukimbilia katika matatizo yao mazito./ Pia ni mwombezi wa waliopondeka moyo./
Mimi ni mmoja wa hao./ Nakujia na moyo uliojaa shida na matatizo./ Nakusihi kwa moyo wote/ unisaidie kwa maombezi yako yenye nguvu/ kufikia utatuzi unaofaa kadiri ya mapenzi ya Mungu./ Maisha yangu yamejaa misalaba,/ siku kwa siku matatizo hayapungui./ Moyo wangu umekuwa bahari ya siki chungu sana./ Mapito yangu nayaona yamejaa miiba mikali./ Roho yangu imezama katika dimbwi la machozi na kite./ Nafsi yangu imezingirwa na giza nene./ Ghasia na kukatishwa tamaa ya kuishi/ hunyemelea roho yangu./ Maongozi ya Mungu na imani naviona vinanitoka kidogo kwa kidogo./
Nikielemewa na mawazo kama hayo/ najikuta sina nguvu za kuishi,/ na maisha kwangu ni msalaba mzito/ ninaouogopa hata kuunyakua./ Wewe unaweza kabisa kunitoa katika balaa hili./ Sitaacha kukusihi/ hadi hapo utakaponisaidia/ au kunijulisha mapenzi ya Mungu kwangu./ Natangulia kutoa shukrani kwa jibu liwalo lote.
Mama Mtakatifu, Mama wa Mungu na Malkia wa Mashahidi, leo nakuchagua Wewe uwe mfano wangu, mkingaji na mteteaji wangu. Naweka roho fukara katika moyo wako uliotobolewa na panga nyingi za mateso. Unipokee mimi niwe mtumishi wako wa pekee na mshiriki wa mateso yako. Nijalie nguvu niwe daima karibu na msalaba ule alikosulibiwa Yesu. Nakutolea nafsi yangu na mali yangu yote.
Updated at: 2024-05-27 07:14:20 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Mama Mtakatifu, Mama wa Mungu na Malkia wa Mashahidi, leo nakuchagua Wewe uwe mfano wangu, mkingaji na mteteaji wangu. Naweka roho fukara katika moyo wako uliotobolewa na panga nyingi za mateso. Unipokee mimi niwe mtumishi wako wa pekee na mshiriki wa mateso yako. Nijalie nguvu niwe daima karibu na msalaba ule alikosulibiwa Yesu. Nakutolea nafsi yangu na mali yangu yote. Pokea kila tendo langu jema ukalisindikize kwa Mwanao, Mama, nifanye nistahili kuitwa mtumishi wa Maria, Simama karibu yangu katika matendo yangu yote ili yafanwe kwa sifa ya Mungu. Ulivyosimama karibu kabisa ya Mwanao alipokufa msalabani uwe karibu nami saa ya kufa kwangu. Nijalie niweze kutaja jina lako na la Mwana wako nikisema: “Yesu, Maria na Yosef mnisaidie saa ya kufa kwangu. Yesu, maria na Yosef, naomba nife kwa amani kati yenu!” . Amina.
Ee Baba yetu Mungu Mkuu, Umenilinda usiku huu, Ninakushukuru kwa moyo, Ee Baba, Mwana na Roho, Nilinde tena siku hii, Niache dhambi nikutii, Naomba sana Baba wee, Baraka yako nipokee, Bikira safi ee Maria, Nisipotee unisimamie, Mlinzi Mkuu Malaika wee, Kwa Mungu wetu niombee, Nitake nitende mema tu, Na mwisho nije kwake juu, Amina.
Updated at: 2024-05-27 07:14:19 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Ee Baba yetu Mungu Mkuu, Umenilinda usiku huu, Ninakushukuru kwa moyo, Ee Baba, Mwana na Roho, Nilinde tena siku hii, Niache dhambi nikutii, Naomba sana Baba wee, Baraka yako nipokee, Bikira safi ee Maria, Nisipotee unisimamie, Mlinzi Mkuu Malaika wee, Kwa Mungu wetu niombee, Nitake nitende mema tu, Na mwisho nije kwake juu, Amina.
Tuusifu Utatu Mtakatifu wa Mungu Mwenyezi, Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, milele na milele, Amina.
Ee Utatu Mtakatifu wa Mwenyezi Mungu, Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, nasadiki kuwa upo hapa na mahali pote. Ee Mungu wangu, umeniumba, umenikomboa, umenifanya mkristo, umenizidishia neema zako hapa duniani, umenitayarishia makao yangu mbinguni, umenijalia na siku hii nikutumikie.
Updated at: 2024-05-27 07:13:53 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Tuusifu Utatu Mtakatifu wa Mungu Mwenyezi, Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, milele na milele, Amina.
Ee Utatu Mtakatifu wa Mwenyezi Mungu, Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, nasadiki kuwa upo hapa na mahali pote. Ee Mungu wangu, umeniumba, umenikomboa, umenifanya mkristo, umenizidishia neema zako hapa duniani, umenitayarishia makao yangu mbinguni, umenijalia na siku hii nikutumikie. Ee Mungu wangu! Nakuabudu, nakushukuru, nakuomba toba, nakupenda! Ee Mungu wangu, nakutolea roho yangu, na mawazo, na maneno, na kazi, na furaha, na mateso yangu: uyapokee unipe neema yako nisikutende leo dhambi!