Sidebar with Floating Button
AckySHINE SMS💌💕
AckyShine

SALA YA MTAKATIFU INYASI

Featured Image

Roho ya Kristo unitakase
Mwili wa Kristo uniokoe
Damu ya Kristo unifurahishe
Maji ya ubavu wake Kristo yanioshe
Mateso ya Kristo nguvu yanizidishie
Ee Yesu mwema unisikilize

85 Comments

SALA KWA MTAKATIFU MIKAELI MALAIKA MKUU

Featured Image

Mtakatifu Mikaeli Malaika Mkuu, utulinde katika vita, uwe kinga yetu katika maovu na maoteo ya shetani, Mungu amtiishe, tunaomba sana, nawe Mkuu wa Majeshi ya Mbinguni kwa nguvu ya Mungu uwaangushe motoni shetani na pepo wabaya wengine wote, wanaozunguka duniani, ili kuzipoteza roho za watu. Amina.

88 Comments

SALA ZA IBADA KWA BIKIRA MARIA WA MATESO

Featured Image

ROZARI YA MATESO SABA YA BIKIRA MARIA

Tumia Rozari ya Mateso Saba ya Bikira Maria iliyo na mafungu 7 yaani mateso 7 yenye Salamu Maria saba kwa kila teso.

TESO LA KWANZA

Mzee Simeoni aliagua kuwa Moyo wa Mama Maria utachomwa kwa upanga.
Tuombe neema ya kuvumilia mateso.
Mama wa mateso utuombee.

83 Comments

SALA YA BWANA: SALA YA BABA YETU

Featured Image

Baba yetu uliye mbinguni
Jina lako litukuzwe
Ufalme wako ufike
Utakalo lifanyike
Duniani kama mbinguni
Utupe leo mkate wetu wa kila siku
Utusamehe makosa yetu
Kama tunavyowasamehe
Na sisi waliotukosea
Usitutie katika kishawishi
Lakini utuopoe maovuni.
Amina.

83 Comments

SALA YA IMANI

Featured Image

Mungu wangu, nasadiki maneno yote linalosadiki na linalofundisha kanisa katoliki la Roma; Kwani ndiwe uliyefundisha hayo, wala hudanganyiki, wala hudanganyi. Amina

84 Comments

Kumbuka ee Bikira Mwenye Rehema

Featured Image
83 Comments

SALA KWA MAMA WA UCHUNGU KUOMBA NEEMA YA PEKEE

Featured Image

Ee Mama mbarikiwa na Bikira mwenye uchungu, Malkia wa Mashahidi, uliyesimama chini ya msalaba na uliyemtazama Mwana wako akifa, unitazame kwa huruma ya kimama ninayekusikitikia. Kwa sababu ya upanga uliochoma moyo wako, kwa mateso ya maisha yako nakuomba uniangalie kwa wema ukasikilize maombi yangu. 

83 Comments

Sala ya Saa Tisa

Featured Image

✝⌚✝

Sala ya saa tisa🙏🏾

Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. A mina

Yesu, ulikufa, lakini chanzo cha uhai kilitoka kwa ajili ya watu, na bahari ya huruma ilifunguka kwa ajili ya ulimwengu mzima. Ee chemchemi ya Uhai, huruma ya Mungu isiyo na mwisho, ikafunika ulimwengu mzima na ukajimwaga mwenyewe juu yetu.

83 Comments

Novena ya Siku tisa kwa Mtakatifu Agustino wa Hippo: Sala zote na Litania

Featured Image
Pamoja na Mtakatifu Augustino tunasema “ Umetuumba kwa ajili yako ee Bwana, kwani ni wewe peke yako ndie Mungu wetu, na nyoyo zetu hazitapumzika, hadi tupumzike ndani mwako.”
83 Comments

SALA YA KUTUBU

Featured Image

Mungu wangu ninatubu sana, niliyokosa kwako, kwani ndiwe mwema, ndiwe mwenye kupendeza, wachukizwa na dhambi, basi sitaki kukosa tena, nitafanya kitubio, naomba neema yako nipate kurudi wkako. Amina.

84 Comments