Updated at: 2024-05-25 17:45:54 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
High school Flashback!! . Watchman : Amkeni muende morning preps. Allan : Mimi ni mgonjwa. Watchman : Unaumwa na nini hiyo? Allan : Bionomial Nomenclature. Watchman : Eeh, lala tu kijana. Hiyo kitu ni mbaya. Imeuwa watu South Africa. 😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
Baada ya kuulizwa nani anapenda kwenda peponi, haya ndiyo yalikua majibu ya wanafunzi
Wanafunzi waliulizwa na mwalimu nani angependa kwenda peponi? Wote wakanyosha ila mmoja tu alipokwenda nyumbani akamuelezea mamake, mamake akamuuliza je wewe ulinyosha mtoto hapana mama yule mama akamuuliza kwanini.
Updated at: 2023-04-29 14:10:46 (2 years ago by Melkisedeck Leon Shine)
Wanafunzi waliulizwa na mwalimu nani angependa kwenda peponi? Wote wakanyosha ila mmoja tu alipokwenda nyumbani akamuelezea mamake, mamake akamuuliza je wewe ulinyosha mtoto hapana mama yule mama akamuuliza kwanini.
mtoto kwa sababu mama uliniambia nikitoka shule nije moja kwa moja mpaka nyumbani nisiende kokote
Updated at: 2024-05-25 17:53:39 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Darasa lolote lile (hasa vyuoni) lazima liwe na wanafunzi wafuatao: 1. Mrembo wa darasa. 2. Playboy/playgirl. Hawezi kutembea na msichana/mvulana mmoja mara mbili. 3. Group ya marafiki watatu. Kila mara wako pamoja. 4. Mtu mwenye maswali ya kuudhi/kukera. 5. Msongolist kimeo. Huyu huwa anasoma sana bt hana bahati ya kufanya vizuri. Yani msuli tembo, bt matokeo sisimizi.
6. Mlafi. Huyu huwa hakatai offer. 7. Mtoro wa kudumu. Haji darasani hata km hana sababu. 8. Mchelewaji wa kudumu. Anakuja kipindi kiko katikati au kinakaribia kuisha. 9. Miss/Mr.Misifa. kila mara ataeleza the way nyumbani kwao walivyo matajiri. 10. Less talkative bt kiwembe. Jamaa mkimya bt unakuta ametembea na karibu wasichana 15 hapo class. 11. Handsome boy ambaye hana mpango na wanawake. 12.Chips addicted. Hawa wanaweza kula chips asubuhi mchana na jioni. Jumatatu hadi jumatatu. 13. Back benchers. Hawa huwa watundu sana na ni watu wa jokes. Huwa hawajibu swali, but wanasubiri wakati wa kushangilia waongeze bezi. 14. Wambea. Hawapitwi na kitu darasani na washazoea kufeli. 15. Mchungaji/Mtumishi wa Mungu, 16. Waimbaji/Wasanii, 17.Walevi 18.Mabishoo. 19. Team popo. Hawa wewe na hela wasiwe na hela wanakesha club, 20.Mwenye aibu kusimama mbele za watu. Wakati wa Presentation anakimbilia kusimama nyuma ya wenzie, 21. Viherehere. Hawa mara nyingi hutokea kupendwa sana na waalimu. 22. Wanaosoma ili kushindana kwny GPA. 23. Kupe. Huyu boom likitoka atawaganda wenzie hadi ziishe, halafu yeye anaanza kula zake alone. 24. Wise man/woman. Huyu huwa ni mtu anayeaminika na kila mtu darasani. Hutumika sn kushauri pale mambo yanapoenda mrama. Mara nyingi huwa ni mtu mzima. 25.mpenda supu" yeye hata ya nyani atakunywa tu. 26.Fix man. Huyu atakuomba jero, akafuatilie dili la milioni kumi town, kumbe hana hela ya chai. 27. Photocopy machine. Huyu ukimuonesha majibu kwny mtihani anaweza kucopy hadi jina lako. 💥Usposema wewe uko namba ngapi mwngine atakusema😜😜😅😅😅😅😅
Updated at: 2024-05-25 16:53:24 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
HAHAHAHAHAAAAAA DUH TAMAA MBAYA
Muokota makopo katika uokotaji wake wa makopo akaona chupa ambayo ndani kuna ki2, alipoifungua likatoka jitu la ajabu. Huku akitetemeka lile jitu likamwambia kijana asante sana kwa kuniokoa omba vi2 viwili sasa hivi. Kijana kwa hofu akaomba pesa za kumiliki magari na majumba ya kifahari. Ghafla fuko la hela na pete ya bahati vikadondoka. Akaambiwa ombi la pili,akasema nibadilishe niwe kivutio ili nipendwe sana nakina dada Hapohapo akageuzwa akawa chipsi yai.!!😂🤣🤣🤣
Alichofanya mke baada ya mme wake kupenda kumchunga sana
Alifanya hivi; Siku ya kwanza
MUME: Halooo vipi mke wangu salama weye?. MKE: Salama tu MUME: Uko wapi? MKE: Jamani si niko nyumbani MUME: Mhh kama kweli uko nyumbani washa blender nisikie…..mke akawasha blender MKE: Umesikia? MUME: Okay haya mi natoka kazini naja
Updated at: 2023-04-29 22:53:52 (2 years ago by Melkisedeck Leon Shine)
Alifanya hivi; Siku ya kwanza
MUME: Halooo vipi mke wangu salama weye?. MKE: Salama tu MUME: Uko wapi? MKE: Jamani si niko nyumbani MUME: Mhh kama kweli uko nyumbani washa blender nisikie…..mke akawasha blender MKE: Umesikia? MUME: Okay haya mi natoka kazini naja
Siku ya pili MUME: Vipi mko salama huko? MKE: Tupo kama ulivyotuacha MUME: kwani uko wapi? MKE: Niko nyumbani napika MUME: Washa brender kama kweli uko nyumbani Mke akawasha blender MKE: Umesikia? MUME: Poa ntarudi baada ya masaa mawili
Siku sita baadae mume akaamua kurudi bila kumtaarifu mkewe alipofika home kamkuta mdada wa kazi yuko peke yake. MUME: We mama yako yuko wapi? MDADA: Sijui ameondoka na blender toka asubuhi
Updated at: 2024-05-25 17:59:43 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Badala yakupika PILAU tutapika TAMBI kwenye Xmas maana tutakua tumeokoa sh.15,000/= Vitunguu swaumu 2000, Vitunguu maji 1000, hiliki 1000, Magome 1000, Michele wa 2000, Soda 3000, Nyama 5000 . Fedha hizi zitatumika kununua mfuko wa cement ili tuanze kujaza kibubu cha ujenzi wa nyumba badala ya kupanga. Karibuni saana maji ya kunywa tumechemsha ndoo nzima.