Updated at: 2024-05-25 17:54:11 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kama umesoma st Kayumba utakuwa una aidia na hayaโฆ
1.Unaenda shule umechelewa unakuta mwalim anakamata wachelewaj unaamua urudi nyumbani 2.unachukua kimbegu cha ubuyu unasugua sakafuni af unamuunguza mwenzio 3.mkiruhusiwa tu unakimbia unataka uwe wa kwanza kwenye njia yenu y kurudia nyumban 4.MTU akikukera unamfungia shule (mnapigana baada ya kufunga shule) 5.MTU akikunyima kitu chake unamwambia "Ahaa eeh utaona sa nne" 6.wadada wembamba ndo wanaongoza kwa kusuta wenzao 7.ukiibiwa daftar jipya unalia kuliko hata uliloandika 8.unajaza mapeni kwenye mkebe(compass) na mengine hayaandiki 9.vifaa vingine kwenye mkebe hujawahi hata kuvitumia mfano bikari labda utolee mwiba๐ 10.hakuna habari nzur kama kuambiwa Leo hamna shule mwalim haupo 11.habari mbaya zaidi n kurud nyumban kutoka shule una njaa af unaambiwa chakula mgeni kaja tumempa 12.mtoto wa mwalim utamgundua tu kwanzia sweta begi na viatu vyake 13.usiombee umpige mtoto wa mwalim utataman uache shule 14.unatengeneza kifutio cha ndala af unatishia eti kinafuta hadi peni๐ 15.ukaguzi na huna ufagio.. unaomba chelewa kwa watu af unaongeza kijiti katikati 16.siku ukienda na ufagio wanakagua maji, ukienda na naji wanakagua kuni au mbolea๐ ๐ Dah shule zetu hizi kiboko!!
Updated at: 2024-05-25 16:54:13 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kuoa vijijini raha sana Hata ukiulizwa unafanya kazi gani ukiwaambia mimi ni admin basi daaaah wanaona wewe ni bonge la boss๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐
Cha kufanya msichana akikukimbia halafu atake kukurudia
Updated at: 2024-05-25 17:05:23 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
โฆโฆโฆ Kama msichana atakutupa kwa sababu huna pesa, na baadaye unapopata pesa akarudi tena kuomba msamahaโฆ Ndugu yanguโฆ.. Msameheโฆ. Mpe ahadi ya ndoa, mwambie utamuoaโฆ. iambie familia yake unataka kufanya ukarabati wa nyumba yaoโฆโฆ Ondoa paa lote la nyumba yao halafu TOWEKAโฆ..
Binti:ย Niletee chipsi kuku, soseji, mayai manne ya kukaangwa pembeni, baga, piza, coke take away baridi, mkate wa moto kwenye ile bekari ya wapemba na maji ya kunywa ya kiimanjaro.
Jamaa:Umesahau viti, meza, masufuria, sahani na beseni na vijiko.
Angalia kilichotokea baada ya dogo kupewa ada na kuitumia kubeti
Updated at: 2024-05-25 17:10:08 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Dogo kampigia simu baba yake; DOGO: Baba katika zile shilingi laki mbili ulizonipa nikalipe ada nimetumia shilingi alfu 30 kubeti BABA : Unasema nini we mpumbavu mshenzi mkubwa? Nimekukanya mara ngapi kuhusu kubeti? DOGO : Lakini baba BABA : Lakini baba nini ngoja urudi utaona ntakachofanya. DOGO : Nilitaka kukwambia kuwa nimeshinda shilingi milioni 3 BABA : Ndio hayo ninayosema wewe mpumbavu sana kwanini hukutumia laki nzima kubeti? Si ungepata pesa nyingi zaidi? Ngoja urudi niwataarifu ndugu zako kuhusu uulivyo na akili za kuamua haraka mwanangu mpenziโฆ