Updated at: 2024-05-25 17:17:44 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Jamaa alikuwa kwenye daladala pembeni kuna dada mrembo kakaa. Kamlia timing kwa muda kisha halafu akamuuliza "Samahani dada unaitwa Google?". Dada: "hapana, kwanini umedhani naitwa hivyo?". Jamaa: "Una kila kitu nnachokitafuta "π πππππππππ
Dokta: Mama tumemchunguza mumeo kwa makini sana, jopo lote la madaktari tumekubaliana mumeo anahitaji mapumziko japo ya mwezi. Sasa tafadhali chukua hivi vidonge vya usingizi vitasaidia sana.
Updated at: 2024-05-25 18:04:24 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Dokta: Mama tumemchunguza mumeo kwa makini sana, jopo lote la madaktari tumekubaliana mumeo anahitaji mapumziko japo ya mwezi. Sasa tafadhali chukua hivi vidonge vya usingizi vitasaidia sana.
Mama: Asanteni sana, sasa niwe nampa mara ngapi?
Dokta: Unatakiwa wewe uwe unakunywa vidonge hivi kutwa mara tatu kwa mwezi mzima, mumeo atapona.
Jambazi mmoja aliingia kanisani na bunduki akapiga risasi juu ya bati akasema "asiyempenda YESU atoke nje" wakatoka wote ispokuwa Mchungaji na Wazee wawili.
Updated at: 2024-05-25 18:07:09 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Jambazi mmoja aliingia kanisani na bunduki akapiga risasi juu ya bati akasema "asiyempenda YESU atoke nje" wakatoka wote ispokuwa Mchungaji na Wazee wawili.
Jambazi likamwambia Mchungaji "unaweza kuendelea na ibada, nilikuwa nakuondolea wanafiki", Mchungaji akasema "ungewaacha kwanza nichukue sadakaβ¦!
Updated at: 2024-05-25 17:58:59 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Duh! Sikubali bora mbavu zituume wote!
Watalii wana dharau sana bana, Mtalii alikodi boti akazunguka nayo kwenye mto Rufiji kuangalia mandhari, akamuuliza kijana anayeongoza boti, "Do you know Biology, Psychology and Anthropology?" Kijana akajibu "NO," Mtalii akamwambia "nothing you know under the sun? You are useless, and u'll die with your illiteracy!" baada ya muda boti ikaanza kuzama, kijana akamwambia mtalii "Do you know kuogelealogy and kusepalogy from mambalogy? Mtalii akajibu huku ametoa macho "No" kijana akamwambia "You will kufalogy and mambalogy wil eat your matakology because of your bad-mdomology..ππππππ
Kilichotokea baada ya polisi wa kibongo kukutana na mwizi mzungu
POLISI KAKAMATA MZUNGU 'yestaday I saw u at ze maize shop..(jana nilikuona dukani kwa muhindi) when u saw me u started 2 six six.(uliponiona ulianza ku-sitasita) u ran n decided 2 plant a car.
Updated at: 2024-05-25 18:03:14 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
POLISI KAKAMATA MZUNGU 'yestaday I saw u at ze maize shop..(jana nilikuona dukani kwa muhindi) when u saw me u started 2 six six.(uliponiona ulianza ku-sitasita) u ran n decided 2 plant a car.(ulikimbia na ukaamua kupanda gari) zen u pot-cry me through ze window.(kisha ukanichungulia dirishani) now sleep down n snake well b4 I cut u a millet.(sasa lala chini kisha nyooka vizuri kabla sijakukata mtama) Chezea lugha wewe..!!!
Updated at: 2024-05-25 17:08:18 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Sitasahau mwaka ule ambapo nilipeleka barua ya maombi yangu ya kazi kwenye kampuni moja maarufu. Wakati nasubiri majibu siku moja nikaenda kwa mama ntilie kununua maandazi akanifungia vizuri, kufika nyumbani hamu yote ya maandazi iliniishia pale nilipogundua karatasi iliyofungiwa maandazi ni barua yangu ya kuombea kaziππ