Huu ndio mlolongo wa michepuko kuwahi kutokea kati ya mke, mume mwanafunzi na boss
BOSS anamwambia sekretari wake: Wiki hii tutaenda wote Serena Hotel kwenye mkutano fanya mipango yote.
SEKRETARI (anamuaga mumewe): Tunaenda na bosi Serena hotel kwenye mkutano for 1 week.
MUME (anampigia mpango wa kando): Mambo safi, wife anaenda kikazi Serena, jitayarishe tujipe raha for 1 week
(Mpango wa kando) anamwambia mwanafunzi wake wa tution: wiki hii nina kazi fulani hakuna tution mpaka week ijayo.
Updated at: 2023-04-29 22:53:20 (2 years ago by Melkisedeck Leon Shine)
BOSS anamwambia sekretari wake: Wiki hii tutaenda wote Serena Hotel kwenye mkutano fanya mipango yote. SEKRETARI (anamuaga mumewe): Tunaenda na bosi Serena hotel kwenye mkutano for 1 week. MUME (anampigia mpango wa kando): Mambo safi, wife anaenda kikazi Serena, jitayarishe tujipe raha for 1 week (Mpango wa kando) anamwambia mwanafunzi wake wa tution: wiki hii nina kazi fulani hakuna tution mpaka week ijayo. MWANAFUNZI anampigia simu sugar daddy wake ambaye ndo (BOSS): Dear hakuna tution wiki hii nakuja kwako…..
BOSS anamwambia sekretari wake: Siendi Serena tena coz mjukuu wangu atanitembelea. SEKRETARI: Mume wangu hatuendi Serena MUME (anampigia Mpango): dah! mpenzi, huyu mke wangu haendi tena. Shit! So hadi next time plz Mpango wa kando a.k.a teacher (anampigia mwanafunzi): Darasa kama kawaida sorry for the earlier message. MWANAFUNZI: darling tution inaendelea kumbe, so nakuja wiki ijayo!! BOSS: Sekretari sorry jitayarishe ile safari ya Serena iko palepale……
Angalia kilichojiri katika semina ya wanandoa kuhusu upendo
Updated at: 2024-05-25 18:00:09 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kulikuwa na semina ya wanawake kuhusu namna ya kuishi kwa upendo katika ndoa. Mwalimu aliwauliza ni wangapi wanawapenda waume zao? Wote wakanyoosha mikono kama ishara ya kuwa wanawapenda waume zao. Mwalimu akauliza tena, “Ni lini mara ya mwisho umemwambia mumeo “Nakupenda Mpenzi”?
Majibu yalikuwa kama ifuatavyo: Wengine wakisema Asubuhi ya leo, Wengine jana, Wengine wiki iliyopita Wengine mwezi uliopita Na wengine wakasema hawakumbuki! Mwalimu aliwapa kazi kila mwanasemina achukue simu yake na kumtumia mume wake meseji yenye neno “NAKUPENDA MPENZI” Baada ya meseji kwenda aliwaamuru kubadilishana simu kila mtu na jirani yake. Kila mwanasemina aliambiwa kusoma meseji za majibu kwenye simu aliyoshika
Simu ya 1 – “Samahani, nani mwenzangu”! Simu ya 2 – “Samahani, wrong number”! Simu ya 3 – “Si nimekuambia usinitumie messages kwenye namba hii”! Simu ya 4 – “Mh! leo mvua itanyesha”! Simu ya 5 – “Nikija tutaongea zaidi”! Simu ya 6 – “……Imedhibitishwa umepokea Tsh300,000 kutoka kwa ……”! Simu ya 7 – “Me too”! Simu ya 6 – “Huu ujumbe ndio ulikuwa unamtumia huyo hawara yako ee, leo utanikoma”!