Updated at: 2024-05-25 10:23:14 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Mchele - 1 kilo
Kuku - 1
Vitunguu - 3
Viazi/mbatata - 5
Jira/bizari ya pilau nzima - 3 vijiko vya supu
Mdalasini - 1 kijiti
Pilipili manga - 1 kijiko cha supu
Hiliki - 3 chembe
Karafuu - 5 chembe
Kitunguu saumu(thomu/galic) kilosagwa - 3 vijiko vya supu
Tangawizi mbichi ilosagwa - 3 vijiko vya supu
Mafuta ya kupikia - ½ kikombe
Chumvi - kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Baada ya kumsafisha kuku na kumkatakata, mchemshe kwa chumvi na ndimu, kijiko kimoja cha kitunguu thomu/somu na tangawizi yote.. Menya viazi, katakata vipande vya kiasi. Katakata vitunguu maji kisha kaanga kwa mafuta katika sufuria ya kupikia pilau. Tia bizari zote isipokuwa hiliki. Saga hiliki kisha tia pamoja na kitunguu thomu/somu ukaange kidogo. Mimina kuku na supu yake ikichemka kisha tia mchele na viazi. Koroga kisha acha katika moto mdogomdogo wali uwive kama kawaida ya kupika pilau.
Updated at: 2024-05-25 10:23:14 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Vipimo Vya Wali
Mchele wa Basmati/Pishori - 1 kilo moja
Vitunguu maji - 3
Karoti - 2
Siagi - 3 vijiko vya supu
Kidonge cha supu (stock) - 1 kimoja
Chumvi - kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Ósha mchele uroweke kama saa moja au mbili Katakata vitunguu vipande vidogodogo (chopped) weka kando. Kwaruza karoti (grate) weka kando. Tia siagi katika sufuria ya kupikia wali, weka katika moto iyayuke Kaanga vitunguu hadi vigeuke rangi kiasi tu. Tia maji kiasi ya kupikia wali, changanya na kidonge cha supu. Yakichemka tia mchele, koroga, funika uweke moto mdogo mdogo. Kabla ya maji kukauka tia karoti changanya wali kisha funika uive kama unavyopika pilau.
Vipimo Vya Kuku Wa Kukaanga
Kuku alokatwakatwa - 1
Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi ilosagwa - 2 vijiko vya supu
Bizari ya mchanganyiko/garam masala - kijiko cha supu
Mtindi/Yoghurt - 1 kijiko cha supu
Ndimu - 1
Chumvi - kiasi
Mafuta ya kukaangia - kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Ukishamuosha kuku, mchuje atoke maji yote. Changanya viungo vyote katika kibakuli kidogo. Changanya pamoja na kuku kisha acha akolee viungo (marinate) kwa muda wa masaa mawili takriban. Weka mafuta katika karai na kaanga kuku, akiwiva yu tayari kuliwa na wali.
Updated at: 2024-05-25 10:34:52 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Viamba upishi
Maziwa ya unga 2 vikombe
Sukari 3 vikombe
Maji 3 vikombe
Unga wa ngano ½ kikombe
Mafuta ½ kikombe
Iliki kiasi
Jinsi ya kuandaa na kupika
Paka sinia mafuta kabla ya kupika labania Katika sufuria chemsha maji na sukari pamoja na iliki mpaka inate vizuri Kisha mimina mafuta koroga Halafu mimina unga wa ngano na ukoroge haraka haraka Kisha tia unga wa maziwa, endelea kukoroga usiwe na madonge mpaka uwe rangi ya browni isiokoleza. Kisha mimina mchanganyiko kweye sinia uliyoipaka mafuta, iwache ipoe na kata kata upendavo na itakuwa tayari.
Updated at: 2024-05-25 10:34:41 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
MAHITAJI
Maziwa ya unga - 2 vikombe
Sukari - 3 vikombe
Maji - 3 vikombe
Unga wa ngano - ½ kikombe
Mafuta - ½ kikombe
Iliki - kiasi
MAPISHI
Paka sinia mafuta kabla ya kupika labania Katika sufuria chemsha maji na sukari pamoja na iliki mpaka inate vizuri Kisha mimina mafuta koroga Halafu mimina unga wa ngano na ukoroge haraka haraka Kisha tia unga wa maziwa, endelea kukoroga usiwe na madonge mpaka uwe rangi ya browni isiokoleza. Kisha mimina mchanganyiko kweye sinia uliyoipaka mafuta, iwache ipoe na kata kata upendavo na itakuwa tayari.
Updated at: 2024-05-25 10:37:35 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Mchele - 3 vikombe
Samaki Nguru (king fish) - 5 vipande
Vitunguu - 2
Nyanya/tungule - 4
Mafuta - 3 vijiko vya supu
Tui la nazi zito - 2 vikombe
Pilipili mbichi - 5-7
Kitunguu saumu(thomu/galic) - 7-9 chembe
Kotmiri - 1 msongo (bunch)
Bizari ya samaki - 1 kijiko cha chai
Ndimu - 2-3
Chumvi - kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Osha samaki, kata vipande kiasi weka kando. Katakata kitunguu na nyanya vipande vidogo vidogo sana (crush) . Katakata kotmiri weka kando. Saga pamoja, pilipili mbichi, kitunguu thomu, ndimu na chumvi. Changanya pamoja na bizari ya samaki kisha paka katika vipande vya samaki acha kidogo vikolee. Weka mafuta katika sufuria au karai, kaanga vitunguu kidogo tu kisha tia nyanya/tungule endelea kukaanga hadi vilainike na kupondeka. Tia kikombe kimoja na nusu cha tui la nazi, kisha tia vipande vya samaki na masala yake, acha mchuzi uchemke samaki aive. Ongeza chumvi, ndimu, pilipili ikihitajika. Ongezea tui lilobakia acha motoni kwa daika chache tu. Epua mwagia kotmiri mchuzi ukiwa tayari.
Pika wali wa maji/mweupe kama kawaida utolee na mchuzi.
Updated at: 2024-05-25 10:23:06 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
VIAMBAUPISHI
Unga wa ngano - magi 2 (vikombe vikubwa)
Hamira kijiko 1 cha chai
Sukari Vijiko 2 vya supu
Maziwa ¾ Magi
Siagi Vijiko 2 vya supu
Mafuta ya kukaangia kiasi
VIAMBAUPISHI:SHIRA
Sukari ¾ Kikombe
Maji ¾ Kikombe
Illiki ya unga kiasi
Zafarani kiasi
JINSI YA KUPIKA
Katika bakuli, changanya vipimo vyote pamoja na ukande unga usiwe mgumu wala laini sana uwe kiasi. Kisha fanya donge moja na iache pahali penye joto mpaka iimuke. Halafu weka mafuta ya kukaangia kwenye moto. Sukuma donge hadi liwe duara sio nyembamba sana, kisha katakata kama maandazi. Mafuta ya kisha pata moto choma mittai hukuunazigeuza hadi ziwive na kugeuka rangi. Katika sufuria tia vipimo vya shira na iache ichemke isiwe nzito sana. Mimina mitai kwenye shira na uzipepete, kisha weka kwenye sahani na zitakuwa tayari kwa kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:34:45 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Soda ni kiburudisho ambacho si muhimu sana kwa afya.
Aina nyingi za soda zina kafeini ambayo huzuia usharabu (ufyonzwaji) wa madini ya chuma mwilini hasa yatokanayo na vyakula vya mimea Hata hivyo soda zinaweza kutumika kwa kiasi kidogo kama kiburudisho, ila tunapotaka ubora zaidi wa afya zetu inafaa kupunguza matumizi ya soda na badala yake kutumia vinywaji vyenye virutubishi muhimu kama vile maji ya matunda, maziwa, madafu au asusa kama vile matunda, karanga na aina mbalimbali za mboga mfano karoti.
Hii inasaidia pia kutumia fedha kidogo tuliyo nayo kwa vyakula muhimu, hasa ukizingatia badala ya soda moja unaweza kupata mayai matatu au nusu lita hadi lita moja ya maziwa.
Updated at: 2024-05-25 10:23:05 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Mayai yaliochemshwa 4 Nyama ya kusaga robo kilo Kitunguu swaum Tangawizi Limao Chumvi Pilipili Breadcrambs Carry powder Binzari nyembamba ya unga Yai moja bichi Mafuta
Matayarisho
Marinate nyama na pilipili, kitunguu swaum, tangawizi, limao, chumvi, carry powder, binzari nyembamba na breadcrambs pamoja. Kisha vunja yai moja bichi kwenye kibakuli na ulikoroge kisha tia kwenye mchanganyiko wa nyama.Gawanisha matonge manne kwa ajili ya kuzungushia kwenye mayai .Chemsha mayai kwa muda wa dakika 20. Yakisha iva acha yapoe na kisha yamenye maganda na uyaweke pembeni. Baada ya hapo chukua yai moja lililochemshwa na ulizungushie donge moja la mchanganyiko wa nyama. fanya hivyo kwa mayai yote yaliobakia. Baada ya hapo paka mafuta kwa nje ya hizo eggchop na kisha paka mafuta kwenye sinia la kuokea na uziokee kwenye oven kwa moto wa kawaida, kwa muda wa dakika 20.Na eggchop zako zitakuwa tayari kwa kuliwa
Updated at: 2024-05-25 10:37:44 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Mchele (rice vikombe 2 na 1/2) Vitunguu (onion 2) Nyanya ya kopo (tin tomato kopo 1) Tangawizi (ginger paste kijiko 1 cha chakula) Kitunguu swaum (garlic paste kijiko 1 cha chakula) Paprika (kijiko 1 na 1/2 cha cha chai) Pilipil (scotch bonnet pepper 1) Curry powder (kijiko 1 cha chai) Maggi cubes 3(unaweza kutumia yenye ladha ya chicken, beef au vegetable. Inategemea unasevu na mchuzi wa aina gani) Chumvi (salt) Mafuta (vegetable oil)
Matayarisho
Loweka mchele kwa muda wa dakika 10.Katakata vitunguu kisha weka pembeni, saga pamoja nyanya ya kopo,pilipili, tangawizi na kitunguu swaum kisha weka pembeni. Baada ya hapo kaanga vitunguu vikiiva tia curry powder, maggi cubes, chumvi na paprika na uchanganye vizuri. Kisha tia mchanganyiko wa nyanya na uupike mpaka uive. Baada ya hapo tia mchele na maji na uupike mpaka ukaribie kuiva kisha ugeuze na umalizie kwa kutia njegere na umalizie kuupika mpaka uive. baada ya hapo utakuwa tayari kuseviwa na mboga yoyote kama kuku, nyama, samaki au assorted meat (Mchanganyiko wa utumbo, makongoro na nyama), Hapo mimi nili-save na mchuzi wa kuku wa kienyeji.