Updated at: 2024-05-25 10:37:42 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Maini (Cow liver) 1/4 kilo Vitunguu (chopped onion) 2 Nyanya (chopped tomato) 1 Kitunguu swaum/tangawizi (ginger /garlic paste) 1 kijiko cha chai Mafuta ya kupikia Chumvi Coriander Curry powder 1 kijiko cha chai Limao (lemon) 1/4 Pilipili (scotch bonnet ) 1
Matayarisho
Safisha maini na ukate vipande vidogovidogo na uweke pembeni. Baada ya hapo kaanga vitunguu kidogo(visiwe vya brown) kisha tia ginger/ garlic paste,carry powder kaanga kidogo kisha tia nyanya. Kaanga nyanya mpaka zitoe mafuta kisha tia chumvi, pilipili na vimaji kidogo. Acha vichemke kidogo kisha tia maini na uyapike mpaka yaive. Malizia kwa kukamulia limao na kutia coriander kisha ipua na hapo yatakuwa tayari kwa kuliwa.
Jinsi ya kutengeneza biskuti za Matunda Makavu Na Cornflakes
Updated at: 2024-05-25 10:23:08 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
VIAMBAUPISHI
Unga - 4 Vikombe
Sukari - 1 Kikombe
Baking powder 1 kijiko cha chai mfuto
Siagi - 454 gms
Mayai - 2
Matunda makavu (tende, zabibu, lozi) - 1 Kikombe
Vanilla - 2 Vijiko vya chai
Cornflakes - ½ kikombe
JINSI YA KUANDAA
Changanya sukari na siagi katika mashine ya keki (cake mixer) mpaka iwe laini (creamy) Tia yai moja moja huku unachanganya mpaka iwe laini kama sufi. (fluffy) Tia unga, baking powder, matunda makavu, changanya na mwiko. Chota mchanganyiko wa biskuti kwa mkono kama (kiasi cha kijiko kimoja cha supu) fanya duara na uchovye katika cornflakes iliyopondwa kwa mkono (crushed) Zipange katika treya ya kupikia na zipike (bake) katika moto wa 375°F kwa muda wa kiasi dakika 15 huku unazitazama tazama.
Updated at: 2024-05-25 10:22:58 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Unga wa ngano (plain flour 1/2 of kilo) Siagi (butter vijiko 2 vya chakula) Yai (egg 1) Chumvi (1/2 ya kijiko cha chai) Hiliki (ground cardamon 1/4 ya kijiko cha chai) Maji ya uvuguvugu (warm water) Mafuta (vegetable oil)
Matayarisho
Weka unga wa ngano katika bakuli la kukandia, kisha tia chumvi na hiliki na uchanganye kwanza, baada ya hapo tia siagi na uichanganye vizuri na unga mpaka ipotee. Baada ya hapo tia tena yai na uchanganye vizuri. Mchanganyiko ukishachanganyika vizuri sasa unaweza kutia maji ya uvuguvugu kidogo, kidogo huku ukiwa unauchanganya ili kupata donge. Baada ya hapo anza kukanda hilo donge mpaka mabuje yote yapotee na unga uwe mlaini, ambapo itakuchukua kama dakika 15. Baada ya hapo tawanyisha unga katika madonge ya wastani (yasiwe makubwa sana au madogo sana) Ukimaliza hapo, andaa kibao cha kusukumia chapati kwa kukitia unga kidogo ili chapati isinatie kwenye kibao. Sukuma donge moja la chapati mpaka liwe flat na kisha weka kijiko kimoja cha mafuta na usambaze. ukisha maliza ikunje (roll). Fanya hivyo kwa madonge yote yaliyobakia. Baada ya hapo andaa chuma cha kuchomea (fry-pan) katika moto wa wastani. Kisha anza kusukuma chapati (ni vizuri ukaanza na zile ulizozikunja mwanzo ili kuzipa nafasi zile za mwisho ziweze kulainika) ukiwa unasukuma hakikisha zinakuwa flat (na zisiwe nene sana au nyembamba sana) Ukishamaliza hapo tia kwenye chuma cha kuchomea. Acha iive upande mmoja then igeuze upande wa pili. Tia mafuta ama kijiko kimoja kikubwa upande wa chini wa chapati na uanze kuukandamiza kwa juu uku ukiwa unaizungusha. fanya hivyo uku ukiwa unaigeuza kuiangalia kwa chini ili isiungue. ikishakuwa ya brown, geuza upande wa pili na urudie hivyohiyvo mpaka chapati iive. Rudia hii process kwa chapati zote zilizobakia.
Siri ya chapati kuwa laini ni kutia siagi au mafuta ya kutosha kipindi unazikanda na pia kuzikanda mpaka unga uwe laini.
Updated at: 2024-05-25 10:37:44 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Mchele (Basmati rice) 1 kilo Vitunguu (chopped onion) 2 vikubwa Garlic powder 1/2 kijiko cha chai Njegere (peas) 1 kikombe Turmaric 1/2 kijiko cha chai Coriander powder 1/2 kijiko cha chai Cumin seeds 1/2 kijiko cha chai Mafuta ya kupikia 2 vijiko vya chakula Chumvi kiasi
Matayarisho
Osha kisha loweka mchele kwa muda wa dakika 5 na kisha uchuje maji na uweke pembeni. Baada ya hapo kaanga vitunguu mpaka viwe vya brown na kisha tia spices zote.Zikaange kwa muda wa dakika 3 kisha tia mchele na uchanganye vizuri na spice.Ukaange mchele pamoja na spice uku ukiwa unageuzageuza kwa muda wa dakika 5. Baada ya hapo tia maji ya moto(kiasi ya kuivisha wali) na chumvi kisha ufunike. Upike mpaka uive kisha malizia kwa kutia njegere na uchanganye vizuri baada ya dakika 2 uipue utakuwa tayari kwa kuliwa.Unaweza kuula kwa mboga yoyote uipendayo
Mapishi ya Muhogo Na Mbatata Za Nazi Kwa Nyama Ngombe
Updated at: 2024-05-25 10:37:34 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Vipimo - Mahitaji Ya Nyama
Nyama ya n’gombe ya mifupa - 3 lb
Tangawizi mbichi ilosagwa - 1 kijiko cha supu
Kitunguu thomu - 1 kijiko cha supu
Bizari ya pilau/jira/uzile (cumin) - 1 kijiko cha supu
Ndimu - 1
Kitunguu kilokatwakatwa (chopped) - 1 cha wastan
Pilipili mbichi - 3 Zilizosagwa
Chumvi - Kiasi
Vipimo - Muhogo Na Mbatata/Viazi
Muhogo menya na ukate vipande pande - 2
Mbatata/Viazi menya ukate vipande vikubwa kiasi - 5 kiasi
Tui la nazi zito - 1 gilasi
Nyanya ilokatwakatwa au kusagwa - 1
Kitunguu kilokatwakatwa (chopped) - 1 kiasi
Bizari ya mchuzi - kiasi
Chumvi - kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Osha nyama kisha weka katika pressure cooker au sufuria. Tia viungo vyote vya nyama uchanganye vizuri, kisha ikorogekoroge mpaka maji yake yakaribie kukauka. Usifunike. Tia maji kiasi ya kuivisha nyama na kubakisha supu yake kiasi ya kuivisha muhogo na mbatata. Muda wa kuivisha nyama inategemea nyama yenyewe na kama unatumia pressure cooker ni takriban dakika 35-40. Ikiwa sufuria ya kawaida utakuwa unaikoroga. Mimina ndani ya supu, muhogo, mbatata, nyanya, kitunguu, bizari ya mchuzi, chumvi. Acha ichemke uive muhogo na viazi. Tia tui la nazi, changanya vizuri acha kwenye moto dakika chache tu. Epua ikiwa tayari. Tolea na achari.
Jinsi ya kupika Biskuti Za Kopa Za Kunyunyuziwa Sukari Za Rangi
Updated at: 2024-05-25 10:34:43 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
MAHITAJI
Unga vikombe 2 ¼
Siagi 250g
Sukari kukaribia kikombe ½ (au takriban vijiko 10 vya kulia)
Baking powder ½ kijiko cha chai
Ute wa yai 1
Vanilla 1 kijiko cha chai
Sukari Ya Kunyunyizia na rangi mbali mbali.
MATAYARISHO
Kagawa sukari katika vibakuli utie rangi mbali mbali uweke kando. Changanya siagi na sukari katika mashine ya kusagia keki upige mpaka ilainike iwe nyororo. Tia ute wa yai vanilla uhanganye vizuri. Tia unga na baking powder kidogo kidogo uchanganye upate donge. Sukuma donge ukate kwa kibati cha shepu ya kopa. Pakaza siagi katika treya ya kupikia kwenye oveni upange biskuti Nyunyizia sukari za rangi rangi kisha pika katika oven moto mdogo wa baina 180 – 190 deg F kwa takriban robo saa. Epua zikiwa tayari.