Tafuta

.

πŸ‘‰ Wakati wa makuzi, ni mabadiliko gani yanatokea kwenye miili ya wasichana?πŸ‘‡βœ”

Kuna mabadiliko mengi ya kimwili ambayo yanatokea kwa msichana wakati anaingia utu uzima. Baadhi ya mabadiliko hayo ni kama yafuatayo:

Mabadiliko ya mwili

  1. Kuongezeka urefu na kupanuka mwili haswa nyonga na matiti kuanza kukua;
  2. Ngozi yako i taanza kuwa na mafuta mengi, unaweza pia kuota chunusi usoni;
  3. Kuota nywele sehemu za siri (mavuzi) na makwapani; na
  4. Kupata damu ya hedhi (kuvunja ungo).

Mabadiliko ya hisia

  1. Kuanza kuwa na muhemko wa kutaka kujamii ana na wakati mwingine mwili wako unaweza kusisimka ukimwona mvulana anayekuvutia;
  2. Mihemuko ya kupenda wanaume huongezeka na wewe kupenda kujipamba i li kuwa na mwonekano wa kupendeza; na
  3. Kuanza kujiamini, kutotaka kulazimishwa kufanya baadhi ya vitu na wewe kutaka kuonekana kama mtu mzima anayeweza kufanya maamuzi pekee yake.

Mabadiliko haya ni jambo la kawaida kwa msichana balehe. Kumbuka, kila msichana anapitia mabadiliko haya katika nyakati tofauti na ukali / nguvu tofauti.

πŸ™‰πŸ™‰πŸ™‰Usisahau kushare posti hii kuhusu (Wakati wa makuzi, ni mabadiliko gani yanatokea kwenye miili ya wasichana?).πŸ‘ Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasomeπŸ’―βœ”

Slide2-utotoni.GIF

.