Tafuta

Hapa unaweza kuwakuta marafiki zako wa zamani Wanakupenda sana na wanakungoja uwatafute

πŸ‘‰SOMA ZAIDI HAPA...

πŸ‘‰ VIPIMO VYA MSINGI VYA KUHAKIKI UBORA WA MAZIWAπŸ‘‡βœ”

Kuna vipimo vine vya ubora wa maziwa, kama ifuatavyo

1. Kipimo cha Kuangalia na Kunusa

2. Kipimo cha Kuchemsha

3. Kipimo cha Alkoholi

4. Kipimo cha Laktomita

Kwa kawaida wakati wa kupima ubora, kiasi kidogo cha maziwa (sampuli) kutoka kwenye kila chombo hupimwa. Maziwa ambayo sampuli yake haikufikia kiwango kinachotakiwa hukataliwa na ni hasara kwa mfugaji. kwa hiyo, ni muhimu kushughulikia na kuhifadhi maziwa kwa kuzingatia kanuni za usafi. Vipimo hivi hufanyika kila wakati maziwa yanapofikishwa katika vituo vya kukusanyia maziwa ili kuhakikisha maziwa bora pekee ndiyo yanayopokelewa. Utaratibu huu wa upimaji maziwa kama unavyofafanuliwa hapo chini utakusaidia kuelewa na kukubali matokeo ya upimaji.

Kipimo cha Kuangalia na Kunusa

. Kipimo hiki ni cha haraka na rahisi kufanyika ili kutambua maziwa yasiyo bora. Kipimo hiki hakihitaji kifaa chochote, ila mpimaji anatakiwa kuwa na uzoefu na uwezo wa kuona na kunusa. Iwapo ubora wa maziwa hauwezi kuthibitishwa kwa kipimo hiki, inabidi vipimo vingine bora zaidi vitumike. Kipimo hiki hufanyika awali kupima ubora wa maziwa kwa kuangalia rangi, mwonekano na harufu.

Hatua za Upimaji

1. Funua chombo chenye maziwa
2. Nusa mara unapofunua na gundua aina ya harufu iliyomo. Maziwa yenye harufu ya kuchachuka au harufu nyingine yoyote isiyo ya kawaida kama vile rangi au mafuta ya hayana ubora.
3. Angalia rangi ya maziwa. Iwapo yana tofauti na rangi ya kawaida ya maziwa, inaashiria ugonjwa wa kuvimba kiwele (wekundu ni damu, njano ni usaha).
4. Angalia kama kuna uchafu ambao huashiria kuwa maziwa hayakukamuliwa na kutunzwa katika hali ya usafi.
5. Gusa chombo cha maziwa kwa kuangalia joto la maziwa. Hii inaashiria kujua muda uliotumika tangu maziwa yalipokamuliwa (kama hayajapozwa).

Matokeo

Mwonekano na harufu isiyo ya kawaida unaoweza kusababisha maziwa kukataliwa ni kama vifuatavyo:

1. Aina ya chakula au harufu ya mazingira (maziwa yanavuta harufu) ya ukamuaji au utunzaji
2. Ng’ombe wanaokaribia kukaushwa
3. Harufu ya bakteria
4. Harufu ya kemikali au rangi isiyo ya kawaida
5. Kuchachuka kupita kiasi

Sababu za kujitenga kwa mafuta kwenye maziwa:

1. Maziwa ambayo yalipozwa na kisha yakatikiswa sana wakati wa kuyasafirisha
2. Kuongeza vitu vingine (yanaweza pia kuonyesha chenga au taka chini ya chombo chenye maziwa)
3. Kuchemsha, kama mafuta yameganda

Kipimo cha kuchemsha

Kinasaidia kugundua maziwa yaliyokaa muda mrefu baada ya kukamuliwa bila kupozwa na hivyo kuanza kuganda, au dang’a ambayo kawaida yana protini nyingi. Maziwa kama hayo hayawezi kustahimili joto wakati wa kuchemsha, hivyo kipimo kitaonyesha matokeo mazuri kwenye maziwa yanayoanza kuganda. Kipimo hiki ni cha haraka na rahisi.

Hatua za upimaji/kufuata/kuzingatia na Matokeo ya kipimo cha kuchemsha

1. Kwa sekunde chache chemsha kiasi kidogo cha maziwa kwenye kijiko au chombo chochote kinachofaa
2. Angalia haraka kama yanaganda
3. Maziwa yatakataliwa kama yataganda, yatakuwa na vibonge au chengachenga.

Kipimo cha Alkoholi

Alkoholi maalum inayotumika inaitwa β€˜ethanoli’. Kipimo hiki ni makini zaidi kwa kutambua maziwa yaliyoanza kuganda na yaliyojaribiwa kwa vipimo hivyo vingine vya awali. Pia kipimo hiki hutambua maziwa yaliyokaa muda mrefu bila kupozwa, dang’a au maziwa kutoka kwenye ng’ombe mwenye ugonjwa wa kuvimba kiwele. Kwa kuwa hiki kipimo ni makini zaidi, maziwa yanayopita kipimo hiki yanaweza kuhifadhiwa kwa saa mbili kabla hayajaharibika.

Hatua za upimaji/kufuata/kuzingatia na Matokeo ya kipimo cha alkoholi

1. Tumia bomba la sindano kunyonya kiasi kinacholingana cha maziwa na alkoholi yenye kiwango cha asilimia 70 kisha tia katika neli ya majaribio au testityubu (test tube) au glasi nyeupe (kama kikombe maalum kinachochutumika kuwapa dawa watoto).
2. Changanya na kutikisa ml. 2 za maziwa na ml. 2 za alkoholi kisha angalia kama maziwa yataganda.
3. Iwapo maziwa yataganda, yasipokelewe.

Kipimo cha Lactomita

Kipimo hiki kinatumika kugundua kama maziwa yameongezwa maji au vitu vingine. Kuchanganya kitu chochote na maziwa husababisha kuingiza bakteria ambao huharibu maziwa mapema.
Kipimo cha laktomita kinatumika kwa sababu maziwa yenye 1.026 – 1.032g/ml ni mazito zaidi kuliko maji yenye 1.00g/ml. Kwa hiyo maziwa yakiongezwa maji au vitu vingine, uzito unapungua (kama yamewekwa maji) au unaongezeka (kama yamewekwa vitu vingine vizito). Kama maziwa yameongezwa mafuta (krimu) uzito unapungua. Kifaa kinachotumika kupima uzito wa maziwa kinaitwa laktomita. Laktomita nyingi huanzia kwenye β€œ0” ikiwa na maana ya uzito wenye 1.000g/ml mpaka β€œ40” ikiwa na maana ya uzito wenye 1.040g/ml.

Hatua za upimaji/kufuata/kuzingatia

1. Baada ya kukamua acha maziwa kwa angalau dakika 30 ili yafikie joto la kawaida mathalan, nyuzijoto 20 Sentigredi (20Β°C)..
2. Koroga sampuli ya maziwa kisha mimina taratibu kwenye silinda ya kupima yenye ujazo wa ml 200 au chombo chenye kina kirefu kama laktomita.
3. Laktomita taratibu ndani ya maziwa.
3. Soma namba ya Zamisha laktomita usawa wa maziwa.

Ikiwa joto la maziwa ni tofauti na lile la laktomita (20Β°C), Unaweza kurekebisha kama ifuatavyo:

1. Kwa kila nyuzijoto ya maziwa inayozidi joto la laktomita, ongeza digrii 0.2 (Β°L) katika kipimo kilichopatikana cha laktomita.
2. Kwa kila nyuzijoto ya maziwa inayopungua joto la laktomita, punguza digrii 0.2 (Β°L) katika kipimo kilichopatikana cha laktomita.
3. Angalizo: masahihisho haya hufanyika kwenye vipimo vya laktomita (k.m. 29 badala ya uzito halisi wa 1.029g/ml).

πŸ™‰πŸ™‰πŸ™‰Usisahau kushare posti hii kuhusu (VIPIMO VYA MSINGI VYA KUHAKIKI UBORA WA MAZIWA).πŸ‘ Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasomeπŸ’―βœ”

Marafiki zako mliopotezana wako hapa Wapo kukutafuta wewe uliyepotezana

πŸ‘‰SOMA ZAIDI HAPA...

nn.gif

.