.

mtu.gif

๐Ÿ‘‰ Uzalishaji lishe kwa ngโ€™ombe wa maziwa kiasili na kwa gharama nafuu๐Ÿ‘‡โœ”

images-13.jpeg

Imehaririwa na; Melkisedeck Leon Shine. Tarehe 27 Nov 2015 23:58. [Legal & Authority]


Uzalishaji lishe kwa ngโ€™ombe wa maziwa kiasili na kwa gharama nafuu

Lishe bora: Ngโ€™ombe hawezi kulaumiwa kwa kushindwa kufanya urutubishaji. Ukosefu wa lishe sahihi husababisha ngโ€™ombe kuwa dhaifu na pia husababisha kutokea kwa magonjwa ambayo huweza kuathiri mfumo wa uzazi.

Kupungua kwa ulaji wa vyakula vya kutia nguvu huathiri joto na hatimae kupunguza uwezo wa uzalishaji kwa ngโ€™ombe. Hii ina maana, lishe hafifu kwa ngโ€™ombe wa maziwa husababisha ngโ€™ombe kutokupata joto kwa wakati uliotarajiwa kwa sababu miili yao haipo katika hali nzuri ya kubeba mimba. Ngโ€™ombe lazima alishwe mlo kamili unaojumuisha wanga, protini, madini na vitamini.

Utafiti unaonesha kwamba ngโ€™ombe aliyeathirika kutokana na utapiamlo, baada ya mwili wake kujijenga kwa upya na kuwa katika hali ya kawaida, huweza kujirudia katika hali ya uzalishaji na akashika mimba kwa haraka sana hata kuliko ngโ€™ombe aliyekuwa akipata mlo kamili kwa wakati wote.

Uzalishaji wa lishe

Ngโ€™ombe anayelishwa nyasi tu hawezi kufikia kiwango kizuri cha uzalishaji maziwa hivyo anahitaji kupatiwa lishe ya ziada. Virutubisho vya ziada kama vile dairy meal inakadiriwa kugharimu asilimia 20% zaidi ya gharama ya jumla ya uzalishaji wa maziwa, hivyo kupunguza faida kwa mfugaji.

Kuongeza virutubisho vinavyochochea uzalishaji wa maziwa kwa kutumia lishe ya asili inayopatikana kwenye mazingira ya mfugaji na yenye gharama nafuu husaidia wafugaji kupata maziwa mengi kwa gharama ya chini. Ili virutubisho vya ziada kuwa na manufaa kwa ngโ€™ombe ni lazima uwepo uwiano wa upatikanaji wa nishati, protini na madini.

Vyanzo vya wanga: Mahindi, makapi ya ngano, molasesi, pumba ya mahindi, na pumba ya ngano.

Vyanzo vya protini: Nyasi, mbegu za pamba, soya, mbegu za alizeti, majani ya sesbania, majani ya kaliandra, na dagaa.

Vyanzo vya madini: Kalishamu, fosifeti, mawe ya chokaa, pamoja na madini ya premix.

Namna ya kuchanganya virutubisho vya uzalishaji wa maziwa

1. Uzalishaji wa kawaida

Kufanya mchanganyiko wa kilo 100;

โ€ข Kilo 75 ya lishe ya wanga

โ€ข Kilo 23 ya lishe ya protini

โ€ข Kilo 2 za madini

Kwa mfano;

โ€ข Kilo 57 za mahindi

โ€ข Kilo 18 za makapi ya ngano

โ€ข Kilo 17 za lusina

โ€ข Kilo 6 za soya

โ€ข Kilo 2 za fosifeti

2. Uzalishaji wa maziwa kwa kiwango cha juu

Kufanya mchanganyiko wa Kilo 100;

โ€ข Kilo 68 za lishe ya wanga

โ€ข Kilo 30 za lishe ya protini

โ€ข Kilo 2 za lishe ya madini

Kwa mfano;

โ€ข Kilo 50 za mahindi

โ€ข Kilo 16 za makapi ya ngano

โ€ข Kilo 2 za molasesi

โ€ข Kilo 14 za mbegu za pamba

โ€ข Kilo 12 za lusina

โ€ข Kilo 4 za dagaa

Faida za mchanganyiko unaotengenezwa kiasili

โ€ข Una ubora sawa na lishe zinazouzwa.

โ€ข Gharama yake ni ndogo ukilinganisha na lishe ya kununua.

โ€ข Hukubalika kwa ngโ€™ombe.

โ€ข Ni rahisi kutunza na kutengeneza.

Usisahau kushare posti hii Kwenye Mitandao ya Kijamii

[NZURI HII๐Ÿ‘‰] SOMA-VICHEKESHO-KWA-MHENGA

misaadas.gif

.

.

.

Melkisedeck%20Shine.gif

Mimi ni Melkisedeck Shine Mmiliki, Mwandishi /Mhariri.Soma%20Zaidi.gif

.

Wasiliana nami;

Kwa maoni, ushauri, nyongeza na hata salamu

Jina lako
Mawasiliano
Andika namba yako ya simu
Mahali unapotoka
Email
Ujumbe wako
Uwe Huru. Ujumbe huu ni siri yangu na wewe.

ABOUT AUTHOR | LEGAL GUIDELINES | CONSULT ME


HAPPY-MOMENTS.jpg

"Maisha ya ujana ni kufanya mema au mabaya, kushinda au kushindwa. Uzee ni majuto ya ujana.."