UFUGAJI WA KUKU

By, Melkisedeck Shine.

familia-mapenzi-na-mahusiano.png

UFUGAJI WA KUKU

NJIA MBALIMBALI ZA UFUGAJI WA KUKU.

Kuna njia kuu mbili za ufugaji wa kuku.

1. Ufugaji Huria

Aina hii ya ufugaji, kuku huachiwa huru wajitafutie chakula na maji wao wenyewe. Utaratibu huu hutumika zaidi kufugia kuku wa
kienyeji ambapo mfugaji hupata hasara na pengine hupata faida kidogo maana kuku hukosa uangalizi na hawapewi chakula cha
ziada.

Faida.

o Haina gharama kubwa za ufugaji.
o Kuku hupata mazoezi ya kutosha.

Hasara.

o Huharibu mazingira maana hula nafaka, mazao nk.
o Ni rahisi kuambukizwa na kusambaza magonjwa.
o Ni rahisi kuathiriwa na hali mbaya ya hewa, watu na wanyama wakali kama paka, vicheche, mwewe, kipanga, nyoka nk.
o Ni rahisi kutaga mayai porini/vichakani na hivyo mayai/kuku mwenyewe kupotea.
o Ukuaji wake ni hafifu/uliodhorota.
o Kuna uwezekano wa kuhamia nyumba nyingine/kwa jirani kwa urahisi.

1. Ufugaji wa ndani ya Uzio/Banda.

Hufanyika katika sehemu iliyozungushiwa uzio/ndani ya uzio maalum ambapo kunakuwa kuna utaratibu wa kuku kupewa chakula
na maji kwa urahisi. Ndani ya uzio huwekwa banda zuri, bora na imara ambalo huruhusu kuku kuingia na kutoka
wanapopumzika/kulala/kutaga mayai. Ufugaji huu hutumika zaidi kwa kuku wa kigeni na kuku chotara na hata wa kienyeji pia.

Faida.

o Gharama ya ufugaji wake ni kubwa.
o Faida yake ni kubwa hasa ukufuga kibiashara.
o Ni rahisi kuelewa kiwango cha utagaji na utotoaji wa kuku wako.
o Ni rahisi kufahamu kuku wazuri wa kuatamiashia mayai na kulea kwa faida ya haraka.
o Siyo rahisi kuku kuathiriwa na wezi/wanyama/vicheche/mwewe/hali mbaya ya hewa.
o Siyo rahisi kuambukizwa magonjwa mbalimbali kutoka nje.
o Ni rahisi kutibu na kujua maendeleo ya kuku wako kwa urahisi.
o Wanakuwa na usalama wa uhakika.
o Faida zake ni nyingi kuliko ufugaji huria.

Hasara

o Gharama za mwanzo za ujenzi wa banda, uzio na vifaa vya chakula na maji ni kubwa kiasi. Hivyo zinahitaji mtaji.
o Njia hii inahitaji eneo kubwa na huru.
o Ni rahisi kuambukizana ugonjwa kama itatokea.
o Ufugaji huu unahitaji utaalam na umakini wa kutosha

UCHAGUZI WA KUKU.

Chagua kuku wenye sifa zifuatazo;

o Wenye kukua haraka,
o Wenye uwezo wa kustahimili magonjwa,
o Wanaotaga mayai mengi,
o Wawe na uwezo wa kuatamia na kuangua vifaranga wengi na kuwalea (jike/mtetea).

Ni vema sana kutumia majogoo chotara au majogoo wa kienyeji wale wakubwa, warefu, wenye kucha fupi. Chagua wenye
maumbile mazuri, uzito wa wastani na wawe wenye rangi za kuvutia kisha uwachanganye na majike/mitetea yenye umbo zuri,
uzito mzuri na rangi nzuri ili kupata kuku chotara wanaokua haraka na wenye uzito mzuri kwaajili ya biashara nk. Kama huna kuku
wenye sifa hizo basi ni bora sana ukanunua kutoka mahali pengine.
Wakati wa kuatamia ni vema kuku mmoja apewe/awekewe mayai 12 hadi 15 kwenye kiota chake mwenyewe na siyo
kuwachanganya kama wakati wa kutaga maayai. Kama wametotoa kuku 2 au zaidi kwa wakati mmoja ni vema aangaliwe kuku
mwenye uwezo wa kulea vifaranga ili aachiwe vifaranga vyote (kama utashindwa kuwatengenezea boksi/kibanda cha vifaranga
kama nilivyoshauri hapo juu) na kuku wengine watengwe na vifaranga ili waanze kulishwa vizuri na kuchanganywa na majogoo,
hapa wataanza kutaga baada ya wiki 2 hivi.
MUHIMU: Ni vema sana kutofautisha makundi ya kuku kulingana na umri wao ili kupunguza kuku kudonoana/kuumizana.

NAMNA BORA YAKULISHA NA KUNYWESHA KUKU.

1. MAJI.

Maji ni muhimu sana kwa kuku wawapo bandani. Wape maji ya kutosha kila wakati unapoona yanapungua/kuisha ili waendelee
kuyeyusha chakula wanachokula Nna kupunguza joto mwilini. Kuku 1 anaweza kunywa hadi robo lita ya maji kwa siku. Kwa hiyo
utawawekea kulingana na wingi wao. Pata chombo kizuri ili uwaningโ€™inizie juu kidogo kutoka usawa wa ardhi. Hii itasaidia
kupunguza uchafuzi wa maji na magonjwa yanayoenezwa kwa njia ya maji.

ZINGATIA= hakikisha kuwa maji ni safi na salama.

1. CHAKULA.

Ni vema kutafuta vifaa vizuri kwaajili ya kuwawekea chakula. Tafuta vyombo ambavyo utaweza kuningโ€™iniza/tundika juu
kidogo kutoka chini kulingana na umri wa kuku. Hii itasadia sana kupunguza uwezekano wa kutosambaa kwa magonjwa hasa yale
yanayoenezwa kupitia viatu tunvyo vaa tunapoingia bandani. Pia itasaidi sana kupunguza chakula kinacho mwagika chini wakati
kuku wanapokula.
Kwa mfugaji yeyote wa kuku anapaswa kuelewa kuwa chakula cha kuku ni ghali. Hivyo ni vema kufuata taratibu vizuri katika
ulishaji na kutengeneza/kununua vyombo ambavyo kuku hataweza kumwaga chakula. Kumbuka kwamba kama vyombo siyo vizuri
basi vitamwaga chakula kingi na hivyo kukuletea hasara.
Ili kuweza kupata mazao mazuri yenye faida, ni vema ununue chakula cha kuku madukani au utengeneze wewe mwenyewe kama
nitakavyoeleza hapa chini ili uwape kuku wako chakula chenye viini lishe vyote muhimu kwa kuzingatia umri wa kuku ulionao. Kwa
vifaranga, unaweza kuwawekea chakula chini kwenye magazeti/mifuniko ya ndoo/sahani. Baada ya siku 10 unaweza kuwawekea
kwenye chombo maalum.

1. Namna ya kuandaa chakula cha kuku.

Vyakula vya kuku vinapaswa kuwa na aina/viini lishe muhimu kama vile Protini, Wanga, madini na Vitamini.
Vyakula hivyo vimegawanyika kama ifuatavyo;
o Vyakula vya kujenga mwili ni; Jamii ya kunde,samaki, dagaa,mashudu ya ufuta/alizeti/pamba,
o Vyakula vya kulinda mwili ili usipatwe na maradhi ni; Mafuta ya samaki na majani mabichi kama vile; kabichi, mchicha,majani ya
mpapai na nyasi mbichi.
o Vyakula vinavyojenga mwili/mifupa ni kama vile; Aina za madini, chokaa, chumvi na mifupa iliyosagwa.

o Vyakula vilivyotajwa vinaweza kumkuza vizuri kuku hadi uuzwaji/kuliwa kwake. Surghum Larrymeal huzuia kudonoana, huboresha
kiini cha yai na kuongeza mayai. Changanya kg 1 kwa kg 50 za pumba.
Ukosefu wa madini kama fosforasi na kalsiam husababisha matege, vidole kukunjamana, kufyatuka kwa misuli ya magoti, kuwa
kilema na kupofuka macho kwa kuku.
Mfugaji wa kuku anaweza kununua vyakula hivi kwenye maduka ya pembejeo za kilimo/mifugo. Na kama huwezi unaweza
kujitengenezea wewe mwenyewe kwa kukusanya mahitaji muhimu ya viinilishe kama ifuatavyo hapa chini;

Kuchanganya%20chakula%20cha%20kuku.PNG
iuuy.PNG

NB. Kabla ya kufanya kazi hii unaweza ukamuona mtaalam wa mifugo kwa ushauri zaidi kama utaona ni muhimu.


Endelea kusoma makala hizi zifuatazo;

a.gif UFUGAJI BORA NA RAHISI WA KUKU WA KIENYEJI

Kuna usemi fulani unatumiwa na watu wengi sana, unasema; โ€œkazi ndio msingi wa maendeleo ya mtu yeyoteโ€ .Hata mimi
nakubaliana na usemi huu kwani ni kweli kabisa kazi ndio msingi wa hatua yoyote ya maendeleo ya mtu yeyote chini ya msingi
mkuu ambao ni Mungu. Kinyume chake, asiyefanya kazi (ya kuajiriwa/kujiajiri) basi atabaki kuwa maskini na mtu wa shida ya
kipato, mahusiano mabaya na wanadamu wenzako, kuwa tegemezi nk… soma zaidi

a.gif UPENDO WA MUNGU

Upendo wa Mungu hauna mipaka, Soma makala Hizi Zifuatazo;.. soma zaidi

a.gif Jinsi ya kuimarisha ndoa zetu

Ndoa ni makubaliano kati ya watu wawili wenye jinsia mbili tofauti kuishi pamoja kama mume na mke… soma zaidi

[Msemo wa Leo] ๐Ÿ‘‰Uzuri na ubora

[Jarida la Bure] ๐Ÿ‘‰Jarida la kilimo bora cha HOHO

[Hadithi Nzuri] ๐Ÿ‘‰Kisa kilichombadilisha mume tabia

[SMS kwa Umpendaye] ๐Ÿ‘‰SMS ya kumuomba umpendaye akukubalie

a.gif Ujumbe kwa Mke Mtarajiwa

Mke wangu mtarajiwa, najua uko sehemu
salamanukivuta muda na jamaa mwingine kabla
hatujaoana. Lakini kabla sijakuweka ndani Ninayo
machache ya kukueleza….. soma zaidi

a.gif Je, kuna madhara gani kama mtu anakaa muda mrefu bila kujamiiana?

Ukweli ni kwamba hakuna madhara yoyote ya kiafya iwapo utakaa muda mrefu bila ya kujamiiana. Viungo vya uzazi havidhuriki wala sehemu nyingine yoyote katika mwili wako. Mwanamke na mwanaume wakianza kujamiiana baada ya kukaa muda mrefu watapata raha na starehe kama kawaida… soma zaidi

a.gif Kwa nini watu wanakuwa wagomvi na wakali wanapokuwa wamelewa?

Madhara ya pombe husababisha watu walioolewa kugombana.
Kutokana na ushawishi wa pombe watu hupoteza tabia zao
za kawaida na kuona vigumu kuhimili mihemko na kushindwa
kufanya maamumzi katika hali hiyo. Matokeo yake, mlevi
huyachukulia tofauti mazingira na maneno. Watu waliolewa hukasirishwa haraka na vitu ambavyo wangevipuuza kama
wasingekuwa wamelewa. Mara nyingi huwapiga watu wakati
wangetatua hali hiyo kwa njia tofauti kama wasingelewa.
Kama jambo hili litatokea miongoni mwa rafiki zako au familia,
jaribu kuwa mbali na uepuke ulevi. Usijaribu kujadiliana na mtu
aliyelewa kwa sababu kwa vyovyote hatakuelewa… soma zaidi

a.gif Mapishi ya Pilau ya nyama ya ng'ombe na kachumbari

Mchele (rice vikombe 3)
Nyama ya ng'ombe (beef 1/2 kilo)
Viazi mbatata (potato 3)
Vitunguu maji (onions 3)
Kitunguu swaum (garlic cloves 4)
Tangawizi iliyosagwa (ginger kiasi)
Hiliki nzima (cardamon 4)
Karafuu (clove 4)
Pilipili mtama (blackpepper 4)
Amdalasini (cirnamon stick 1)
Binzari nyembamba nzima(cumin seeds 1/2 ya kijiko cha chai)
Binzari nyembamba ya kusaga (ground cumin 1 kijiko cha chai)
Chumvi (salt)
Mafuta (vegetable oil)
Nyanya (fresh tomato 3)
Limao (lemon 1)
Pilipili (chilli 1)
Hoho (green pepper).. soma zaidi

a.gif USHAURI WANGU ANZA KUAJIRIWA KAMA MUWEKEZAJI TU ILI UJIAJIRI NA KUAJIRI WENGINE

Kwa lugha nyepesi ni kwamba ukiajiriwa maana yake umeshindwa kujitegemea kwa ujuzi wako (yaani hujui ufanyie nini) hivyo umeona uukabidhi ujuzi wako kwa wenye "akili na uwezo" wa kuupangia matumizi ya huo ujuzi wako… soma zaidi

vichekesho-bomba-vya-siku.png

.

familia-mapenzi-na-mahusiano.png
UJUMBE-WA-MSAMAHA-KWA-NDUGU.JPG
afya-mapishi-na-lishe.png

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.