Ufugaji Kware

By, Melkisedeck Shine.

Kware ni jamii ya ndege ambao kwa sasa wanafugwa majumbani na wanaotaga mayai kama kuku ama bata na kwa wingi sana. Ndege hawa ni wadogo 280gm - 300gm, wana rangi ya brown, nyeusi au hata nyeupe yenye miraba na madoa ya rangi ya udongo au kijivu. Manyoya yao pia yana rangi ya brown au nyeupe na yenye madoa yanayovutia.

Kutaga na kuatamia kwa Kware

Kware dume humpanda jike kwa muda kidogo, Hapo jike anakuwa tayari kutaga na hutaga mayai 290 hadi 310 kwa mwaka (hii hulingana na lishe nzuri atakayopatiwa).

Mayai ya Kware huatamiwa kwa siku 18 na huanza kuanguliwa vifaranga kwa muda wa siku 2, kuanzia siku ya 18 na hadi 20.

Njia bora ya kutotolesha mayai ya Kware ni kwa kutumia incubator ambapo mayai huatamiwa kwa wingi ndani ya siku 18.

Utunzaji wa vifaranga vya kware na chakula

Utunzaji wa vifaranga vya kware Siku 1 – 7

Vifaranga wapatiwe chakula “STARTER PELLET” na maji masafi ya kutosha. Siku ya 1 wawekee ‘GLUCOSE’ kwenye maji, Packet moja kwa lita 20 za maji, na siku ya pili hadi ya tano wawekee Amin Total kwenye maji, Wape maji pekee siku ya sita na siku ya saba wapatie chanjo ya Newcastle. Utawapatia joto kwa njia ya umeme kwa ‘BULB’ mbili (2) za 200watts kwa kila vifaranga 300, ama unaweza kuweka taa ya ‘Energy Server’ pamoja na jiko la mkaa uliofunikwa na majivu ambao utakidhi kuwapatia joto sawia kwa masaa 24 kwa siku 7. (Majivu yanasaidia moto kukaa kwa muda mrefu)

Banda/box lako liwe la ukubwa wa 1.5m x 1.5m (au eneo la ukubwa huo ndani mwa banda kubwa la kufugia kuku) lazima uzingatie usalama wa vifaranga dhidi ya panya, paka au vicheche. Unatakiwa kuweka magazeti au mabox chini kwenye sakafu yatakayosaidia usafi. Kwa week ya kwanza chakula kitawekwa chini na tunashauri utumie chakula cha pellet ili kusaidia vifaranga wasiteleze na kuathiri miguu. NOTE: Weka gololi au mawe kwenye drinkers zako ili kuzuia vifaranga wasizame ndani ya (drinkers) maji na kufa.

Utunzaji wa vifaranga vya kware Siku 8-14

Vifaranga wataendelea kupewa chakula “STARTER PELLET” na maji safi. Wataendelea kuhitaji ‘mwanga’ wa kutosha muda wote na joto la wastani bulb 2 za watts 100 au moja ya watts 200

Utunzaji wa vifaranga vya kware Siku 15-21

Uhitaji wa joto utapungua, ila ni kipindi ambacho wanakula chakula zaidi kwa ajili ya kukua. Ni vizuri waendelee kupata taa ili kupata mwangaza utakayowawezesha kula mchana na usiku.

Utunzaji wa vifaranga vya kware Siku 21 na Kuendelea

Kware wako hawatahitaji joto tena wawekee taa tu za energy server kipindi cha usiku, wape chakula na maji ya kutosha zaidi kwa ajili ya kukua.

UTAGAJI WA KWARE

WIKI YA SITA

Wiki ya sita kuelekea ya saba Kware wako wataanza kutaga mayai kila siku, kwa wastani Kware mmoja hutaga mayai 300 kwa mwaka.

Magonjwa ya Kware

Kware ni ndege wenye kinga kubwa na ni vigumu sana kushambuliwa na magonjwa kama kuku na mara wanapougua ni rahisi sana kutibika. Magonjwa yanayoweza kuwapata Kware ni typhoid, mafua na kuharisha .

Tiba za asili za kware

Waweza kuwatibu vifaranga au Kware wako kwa kutumia njia ya asili ambayo pia ni rahisi, gharama nafuu na bora zaidi kuliko kutumia madawa yaliyochanganywa na kemikali na yenye gharama.

Vifuatazo ni vitu vya asili vinavyotumika kutibu magonjwa mbali mbali kwa Kware na yanayopatikana kwa wingi katika maeneo ya mfugaji. Madawa haya hutumika kwa kiwango cha wastani na hayana kipimo maalum kwani hata ukiyazidisha hayana madhara.

Mwarobaini na Aloe Vera:

Madawa haya hutumika kutibu kuharisha damu pamoja na mafua kwa vifaranga vya Kware. Chukua kiasi kidogo cha mwarubaini kisha twanga vizuri kupata maji maji. Kamua maji yale, kisha weka katika maji uliyoandaa kuwanywesha vifaranga wako. Kata vipande vidogovidogo vya aloe vera (jani moja laweza kutosha) na tia katika maji yaliyochanganywa na mwarobaini, kisha wapatie vifaranga wanywe (Aloe Vera itaendelea kujikamua yenyewe ikiwa ndani ya maji huku vifaranga wakiendele kunywa).

Kitunguu swaumu:

Hii hutumika kukinga na kutibu vifaranga vya kware wanaosumbuliwa na kuharisha damu. Unachukua kitunguu swaumu na kuondoa maganda ya nje kisha kusafisha na kukata vipande vidogo sana, na kuwawekea kama chakula. Vifaranga wanapenda sana vitunguu hivyo na watakula kwa kasi kama chakula lakini ni tiba tayari. Unaweza kuwapatia kila siku hadi watakapo pona.

Maziwa:

Maziwa yanayotokana na ng’ombe pia hutumika kutibu ugonjwa wa kuhara pamoja na kuwapa nguvu Kware waliolegea. Mnyweshwe maziwa hayo Kware anayeumwa bila kuyachemsha na umnyweshe maziwa ya kutosha kiasi cha kushiba. Unamnywesha mara tatu kwa siku. Hakikisha maziwa unayotumia yanatoka kwa ng’ombe wanaotibiwa kila mara.

Angalizo

Siyo lazima Kware waugue ndipo uwapatie tiba hizi. Hakikisha unawapa tiba kabla hata hawajaugua hivyo utawakinga na magonjwa hayo. Waweza kuchanganya madawa hayo yote kwa wakati mmoja kwani hayana madhara.

Endapo madawa ya asili hayapatikani katika eneo la mfugaji basi waweza kuwatibu Kware kwa madawa yafuatayo ambapo vipimo huelezwa moja kwa moja kwa maandishi katika madawa hayo au kuelezwa na muuzaji pale utakaponunulia; Amprolium kwa ugonjwa wa kuharisha damu (Coccidiosis), Fluban,Coridix au Doxyco kutibu mafua (Coryza) na Esb3,Trisulmycine au Trimazine hutumika kwa homa ya matumbo (Typhoid).

Chanjo Ya kware

Siku ya 7 lazima vifaranga wapatiwe chanjo ya “kideri/mdondo”
(respiratory & digestive diseases) kwa dawa inayoitwa ‘newcastle’. Chanzo cha maambukizi ni maji na chakula kilichochafuliwa na kinyesi na pia husababishwa na virusi kwa njia ya hewa.

Siku ya 14 lazima wapewe chanjo ya “gumboro”. Chanzo cha
maambukizi ni maji na chakula kilichochafuliwa na kinyesi na pia husababishwa na virusi kwa njia ya hewa.

Siku ya 21 lazima warudie chanjo ya “Newcastle (aina ya IBDL)”. Chanzo cha maambukizi ni maji na chakula kilichochafuliwa na kinyesi na pia husababishwa na virusi kwa njia ya hewa.

Siku ya 35 lazima wapate chanjo ya “Ndui”.

Soko la kware

Mayai ya Kware ni bidhaa adimu sana hapa nchini kwa kuwa ni wafugaji wachache waliojikita katika ufugaji huu, Ufuatao ni muhtasari wa wastani wa bei ya bidhaa za Kware sokoni

1. Trei ya (mayai 30) ya KWALE inauzwa shilingi 30,000 .
2. Kifaranga wa Kware wa siku moja anauzwa shilingi 2500 – 3000
3. Kware wa week 4 (mwezi mmoja) anauzwa kwa shilingi 10,000– 12,000
4. Kware aliyeanza kutotoa (week 6) huuzwa shillingi 20,000 – 25,000
5. Kware kwa aliyekomaa kwa ajili ya kitoweo huuzwa kwa shilingi 25,000
6. DROPING za Kware huuzwa kwa shilingi 10,000 kwa 50kg kwa wafugaji wa samaki

Soko la KWALE liko juu sana kwa mayai na nyama. KWALE pia hutofautiana bei kwa jike na dume.


Marafiki-wa-enzi.GIF

Endelea kusoma makala hizi zifuatazo;

a.gif Kilimo cha Mgagani

Mgagani (Cleome gynandra) au Spider plant kwa kingereza, ni mmea wa asili ya Afrika unaostawi vizuri kwa kumwagiliwa hapa afrika ya mashariki wakati wa joto. Pia huchumwa mashambani ikiwa imeota yenyewe zao hili hushambiliwa na magonjwa na wadudu mara chache. Majani na Matawi machanga yana virutubisho kuliko Sukuma wiki na kabichi. Mahitaji yake yanaongezeka kwenye miji midogo na mikubwa kila siku… soma zaidi

a.gif UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

Wanaume Wengi Hapa Duniani Huamini Kuwa, Mwanaume Hasa Ni Yule Anayeweza Kufanya Tendo Hilo Kwa Muda Mrefu Na Mara Nyingi Ndio Maana Vijana Wengi Utawasikia Wakijisifu Kuwa, Mpenzi Wake Hakulala Usiku Mzima Kutokana Na Dozi Ya Maana Aliyompa Na Ukimuuliza Mtu Wa Namna Hii Atakwambia Kuwa Alikwenda Mizunguko Sita Usiku Mzima… soma zaidi

a.gif Tofauti kati ya mwanamme anayetaka kukuoa na anayetaka kukuchezea na kukupotezea muda

Mwanaume Ambaye Ana Malengo Ya Kuoa Hubadilika Kitabia. Muda Mwingi Hutaka Kuonekana Mtu Mzima Mwenye Sifa Nzuri. Hatakuwa Mtu Wa Kulewa Kupita Kiasi Na Kutapanya Mali Na Wanawake Wengine. Tabia Zake Mbaya Za Zamani Ataziacha.. soma zaidi

[Kitendawili Kwako] 👉Nilikwenda nikichoma nikarudi nikichoma

[Chemsha Bongo Kwako] 👉Je, hii familia ina watoto wangapi?

Slide2-utotoni.GIF

a.gif Magonjwa ya zinaa yanavyoenea

Magonjwa ya zinaa husababishwa na vijidudu vya magonjwa na huambukizwa kwa kukutana kimwili na mtu mwenye vijidudu hivyo.
Katika Tanzania magonjwa haya yameenea sana haswa kwa vijana.. Hivyo kama una wasiwasi wewe au mpenzi uliyekutana naye kimwili kuwa na ugonjwa kama huo, muhimu mwende kupimwa. Magonjwa hayo yasipotibiwa kikamilifu yanaweza kuleta madhara makubwa. Magonjwa ya zinaa mara nyingi yanasababisha ugumba… soma zaidi

a.gif Faida za mafuta ya nazi kiafya kwenye mwili

Wakati mafuta ya nazi yakiwa yamemeng’enywa na mwili huhamasisha uundwaji wa nguvu mpya za ubongo zijulikanazo kama ‘ketones’… soma zaidi

a.gif Kwa nini Albino hawapewi kazi kwa mtazamo kwamba hawawezi kazi?

Watu wengi katika jamii hawana uelewa unaotosheleza kuhusu
ulemavu wa ngozi na ulemavu wa macho wa Albino.
Hii ndiyo sababu mara nyingi jamii inawatenga ikiamini kuwa
inawalinda ili wasipatwe na madhara ya ziada. Wanaweza
vilevile kuwatenga hata kwa kuwazuia kufanya kazi ambazo
wanazimudu bila sababu za msingi au bila kusikiliza maoni yao.
Watu wanapaswa kuzingatia mapungufu walio nayo Albino na
kuwapa kazi kwa kuzingatia uwezo walionao. Kwa mfano kufanya
kazi katika jua kwa muda mrefu ni jambo lisilofaa au kumtaka
Albino asome kwa muda mrefu inaweza kumshinda. Ni muhimu
pia kwa mtu anayeishi na ualbino kujielewa, kujitambua na.. soma zaidi

a.gif Je, ukinywa pombe unaongeza damu?

Si kweli.
Pombe haiongezi damu, vitamini wala nguvu. Ukweli ni kwamba unywaji pombe kupita kiasi huvuruga ufyonzaji wa vitamini na madini kutoka kwenye chakula kuingia mwilini… soma zaidi

a.gif UNYONYESHAJI BORA WA MAZIWA YA MAMA

• Maziwa ya mama pekee ndio chakula na kinywaji cha mtoto bora zaidi kwa watoto kwa miezi sita ya kwanza.
• Ni jambo la muhimu sana kunyonyesha watoto wachanga kwa muda wa miezi minne na uendelee kunyonyesha hadi mtoto atakapofikisha mwaka mmoja na kuendelea… soma zaidi

[Msemo wa Leo] 👉Kushindwa jambo sio Makosa

[Hadithi Nzuri] 👉Kisa cha kusisimua cha mama mjane

FURSA.PNG

Fursa Ya Kazi Na Ajira Yenye Malipo Mazuri

Au soma zaidi hapa

.

UJUMBE-ZA-USIKU-KWA-NDUGU.JPG
mtu.gif

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.