Tafuta

Unatafutwa na marafiki zako wa zamani Bado wanakupenda sana ndio maana wanakutafuta

👉SOMA ZAIDI HAPA...

👉 UFUGAJI BORA NA RAHISI WA KUKU WA KIENYEJI👇✔

Utangulizi

Kuna usemi fulani unatumiwa na watu wengi sana, unasema; “kazi ndio msingi wa maendeleo ya mtu yeyote” .Hata mimi
nakubaliana na usemi huu kwani ni kweli kabisa kazi ndio msingi wa hatua yoyote ya maendeleo ya mtu yeyote chini ya msingi
mkuu ambao ni Mungu. Kinyume chake, asiyefanya kazi (ya kuajiriwa/kujiajiri) basi atabaki kuwa maskini na mtu wa shida ya
kipato, mahusiano mabaya na wanadamu wenzako, kuwa tegemezi nk. Kwa kuwa tunatamani sana kutoka katika kongwa hili la
umasikini wa kipato na hali mbaya ya maisha, tunalazimika kufanya jukumu letu kuu la kumuomba sana Mungu ili atuwezeshe
kujua na kufahamu mbinu mbalimbali kisha kujifunza na kufahamu kwa makini tena kwa njia rahisi mno za kututoa katika hali hii ya
umaskini uliokithiri.

Ikumbukwe kwamba, kujifunza kwa msisimko tu bila ya kuyaingiza mambo hayo uliyojifunza katika mazoezi na vitendo vya
makusudi maishani mwetu ni wazi kwamba hayatatusaidia, bali yatabaki vichwani mwetu kama hadithi tu zaalfulelaulela na maisha
ya kubahatisha maarufu kama akadabraakadabra. Hivyo tumuombe sana Mungu wetu ili mafundisho haya yaweze kubadili maisha
yetu kwa uchumi bora na endelevu ili tuweze kupata kipato na kurudishia Mungu zaka na sadaka badala ya kukaa kulalamika kuwa
hatuna cha mkurudishia muumba wetu YEHOVA.

Kama ilivyo chunvi ya dunia, ufugaji pia huhitaji upendo, uvumilivu, karama, utu na maombi ya dhati ambayo yatazaa namna nzuri
ya kuipenda kwa dhati ya moyo wako kazi hii ya ufugaji. Vinginevyo utabakia kuwa mtu wa kujaribu na kuishia kushindwa kila
mara. Kama ilivyo kanuni ya maendeleo yoyote yale, ufugaji wa kuku pia huhitaji; Ubunifu, utundu wa akili, kujaribu bila kukata
tamaa, kugundua, kujifunza, kufanyia kazi mawazo yaa wengine, kusoma vitabu na majarida mbalimbali yahusuyo kazi
yako, kujishughulisha nk. Hata ukifundishwa darasani huwezi kufundishwa vyote na mwalimu wako, vingine itakubidi utafute
mahali pengine kwa ubunifu mkubwa, ugunduzi na mambo mengine mengi ili ufanikishe lengo la kupata elimu bora ya kile
unachokitaka. Hii huhusisha akili yako vema katika kujifunza kutoka kwa watu au vitu vingine nk. Lakini mafanikio zaidi yatapatikana pale utakapokuwa katika utendaji zaidi.

UFUGAJI WA KUKU WATANO (5) WA KIENYEJI UPATE KUKU MIA MBILI (200) KWA MIEZI SITA (6) TU!

(Kuku 200 x 5,000 = 1,000,000)
Unaweza ukaniona kama mimi ni kichaa na ninaye ota ndoto za mchana ambazo hazina mafanikio wala tija maana nadharia hii
inaweza isiwaingie vizuri watu vichwani mwao. Watu wengi wamekuwa wakisema na kushauri hata kushauriwa hata na wale
wasiofaa. Ninaamini wengi wetu hawapendi kuamini kile wanachoambiwa hadi pale watakapoona kwa macho yao ndipo waamini
(akina Tomaso). Sikia nikuambie! kama huamini haraka kitu chochote hebu usimkatishe tamaa yule aliyekwambia habari hizo za
kukatisha tamaa, badala yake jaribu kupeleleza na kufuatatilia hatua kwa hatua tena kwa makini maelezo uliyopewa, kisha yaweke
katika utendaji (tenda/fanya) kwa ufanisi kisha subiri matokeo. Baada ya kupata matokeo sasa unaweza kwenda mbele kidogo
ukauliza/kusoma/kujifunza zaidi ili kuona kama kuna mahali umekosea au hukuzingatia kanuni na maelekezo uliyopewa. Baada ya
kupata maelezo ya ziada hebu rudia kufanya tena kwa kuboresha kupitia maelekezo ya awali na hayo mapya uliyopata yote kwa
pamoja ili upime matokeo yake. Hapo sasa utakuwa upo kwenye haki ya kuamini au kutoamini kwamba jambo hilo ni kweli au siyo
kweli na siyo kutaa tu kwa ubishi usiokuwa na maana yeyote. Kwa kufanya hivi hakika utapiga hatua mbele katika kuboresha
maisha yako ya sasa na ya baadae. Ila ukifanikiwa usije ukamkufuru Mungu aliyekuwezesha.

Hebu anza na kuku Watano (5) tu Majike wenye Rika/Umri mmoja (au wanaokaribiana). Watunze vizuri kwa kuwapatia chakula
kilicho na mchanganyiko kamili wa viini lishe vinavyotakiwa katika mwili wa kuku, yaani; wanga, protini, calcium, chumvichumvi,
madini joto nk (kama nilivyoeleza hapa chini). Wawekee na Jogoo mmoja mzuri wa kienyeji/kizungu/chotara (kama nilivyoeleza
hapa chini juu ya uchaguzi wa majogoo).

Wanapoanza kutaga watayarishie mahali pazuri/Kiota kizuri cha kutagia na kuatamia kwa kuwajengea viota ndani ya banda.
Hakikisha mahali hapo hapavuji wala hapapati unyevunyevu wala joto kali sana. Hakikisha mahali hapo pana usalama wa kutosha
(mahali wanyama hatari kama vicheche, pakashume, nyoka nk hawawezi kufika).
Kuku wakiendelea kutaga na sasa ukaona wanakaribia kuatamia,Anza kuchagua aina ya mayai unayotaka kuku wako walalie. Hii
inamaanisha kuwa; ukichagua mayai makubwamakubwa hayo yanakuwa na vifaranga majogoo na mayai madogomadogo
mara nyingi huwa ni ya vifaranga majike. Acha kuwawekea mayai ya mviringokama mpira!
Hakikisha kuku wote wanasubiriana ili walalie/waatamie kwa pamoja.
Weka mayai 12 hadi 15 kwa kila kiota cha kuku 1 kulingana na umbo la kuku wako. Kuku anaweza kutaga hadi mayai 30 kwa kila
msimu wa kutaga unapofika. Unaweza kutumia mayai machache kati ya 30 kwa kumuatamishia kuku wako huku mayai mengine
yakisubiri awamu ya pili ya kuatamiwa.Kwa mfano ukiwawekea kuku wako hao watano, Kuku 5 x Mayai 12 = Mayai 60.
Kwa kawaida kuku huatamia/hulalia mayai kwa siku 19 hadi 21/24 tu hadi anapototoa vifaranga. Hakikisha unawawekea kuku
walioatamia chakula chenye viini lishe vya kutosha na maji mengi karibu na viota vyao ili wakitoka kwenye viota vyao wale chakula
mara moja na kunywa maji kisha warudi haraka kwenye mayai yao. Hii itasaidia kuangua mayai yote 12/15 bila kuharibu yai hata
moja. Au hata yakiharikbika basi hayataharibika mengi kama ukiacha kuwawekea chakula waende kufukuzana na panzi na vyakula
majalalani huko nje na kuchelewa kurudi kwenye mayaiyao.
Wakati ukisubiria siku hizo 21/24 anza kujenga kibanda kidogo ndani ya banda kubwa ulilojenga awali au jikoni au andaa boksi
kubwa na gumu kwaajili ya kutunzia vifaranga watakaoanguliwa ndani ya siku 21/24 zijazo.

Baada ya kuku hao 5 kuangua vifaranga wako 60 hapo ndipo kazi kubwa ya kulea vifaranga inapoanza. Elewa kuwa ili upate
mafanikio haraka hakikisha kuwa kazi ya kulea vifaranga inakuwa yako na siyo ya kuku! Kwanza,Unatakiwa kuondoa na kuchoma
moto/kufukia mabaki yote ya mayai na kuboresha usafi wa banda lote ili kuepusha magonjwa kama vile kuharisha, viroboto, papasi
nk. Hapo unaweza kuwatoa vifaranga wako wote 60 mmojammoja kadri wanavyoanguliwa hadi kufikia kifaranga wa mwisho,
yaani Yule wa 60 na kuwaweka katika kibanda kidogo/boksi ulichokijenga na kuwawekea mayai mengine mama zao (yale 15/18
kati ya 30 uliyoyabakiza) ili waatamie tena kwa siku 21 hadi 24 zingine. Unapotoa kifaranga kutoka kwa kuku aliyeatamia humfanya
kuku Yule ashindwe kutoka kwenye mayai maana hana mtoto wa kulea.
Akimaliza kuangua mayai yote na ukamuwekea mengine ni rahisi kwake kuendelea kuatamia maana atasubiri kupata vifaranga na
ndipo atajikuta amelalia kwa siku 21 zingine bila wasiwasi. Kwa kufanya hivyo utakuwa tayari umejipatiavifaranga/kuku zaidi
ya 100 ndani ya wiki 7 tu! Sasa Unatakiwa kuwajali sana kuku hawa wanaolalia kwa mara ya pili kwa kuwapa chakula cha
kutosha, maji, majani ya makongwe, mchicha, mchunga nk ili wapate vitamini na madini mengine muhimu kwa afya zao. Fanya
hivyo hata watakapokuwa wametotoa na ukawanyang’anya vifaranga. Hii itawasaidia ili wasinyonyoke sana manyoya maana kuku
wengi hunyonyoka manyoya wanapoatamia. Kwa kufanya hivi, kuku wako watakaa kwa wiki 2 hadi 3 bila vifaranga na kisha
wataanza kutaga tena na kuatamiakama mwanzo.
Vifaranga wako hakikisha unawatengenezea chumba chao kido ndani ya banda kubwa/jikoni, kisha wawekee chanzo chochote
cha joto kama vile; taa ya chemli/jiko la mkaa/vizinga vya moto nk ili wasiathiriwe na baridi hasa wakati wa usiku. Umakini
mkubwa sana unatakiwa hapa! Hakikisha unakuwa makini wakati wa usiku ili kuongeza na kupunguza joto ndani ya kibanda cha
vifaranga maana wakati huu maranyingi joto hupungua na ubaridi huongezeka na hivyo unaweza kuua vifaranga wako.

NAMNA YA KULEA VIFARANGA.

Katika ulezi wa vifaranga kama kuku utawanyang’anya vifaranga vyao utatakiwa kuwajengea banda dogo (ndani ya banda
kubwa/uzio) ili uwawekee chanzo cha joto kama taa/jiko la mkaa (kama ni sehemu/majira ya baridi). Kamautatumia jiko la mkaa
unatakiwa kuacha kwanza hadi mkaa mweusi uwake wote ndipo uweke bandani maana mkaa ukitoa moshi unaweza kuathiri
vifaranga vyako. Angalia namna ya kuweka jiko lako la mkaa juu kidogo ili vifaranga wasiungue. Hakikisha taa yako haitoi moshi
sana na haivujishi mafuta. Pia uwe na akiba ya mafuta ya taa ya kutosha. Usiweke mafuta mengi kwenye taa maana inaweza
kulipuka ikakuletea hasara. Vifaranga wasizidi 50 kwa boksi 1.Hakikisha umewasha taa/jiko lako ndani ya boksi saa tatu au zaidi
kabla ya kuwaweka vifaranga ili chumba/boksi lipate joto kabla ya vifaranga kuwasili. Njia hizi zinahitaji uangalifu wa hali ya juu
sana kwani kuhatarisha/kuua vifaranga ni kuhatarisha maendeleo yako. Kama utaamua kutumia umeme pia ni vizuri zaidi maana
inapunguza hatari zaidi.
Kwa hiyoa njia zote tatu unaweza kutumia jedwali lifuatalo ili kuweza kumeneji joto la kibanda cha vifaranga;

1) UMRI WA
KKUKU/VIFARANGA

2) JOTO NDANI YA BOX/KIBANDA CHA KULELEA
VIFARANGA

3) JOTO NDANI YA
CHUMBA/BANDA

1) (2) (3)
Wiki 1 33-35oc 30-32oc
Wiki 2 30-33oc 27-29oc
Wiki 3 27-31c 24-26oc
Wiki 4 24-29oc 21-23oc
Wiki 5 26-27oc 22-23oc

Baada ya wiki ya 4/5 pasua box/watoe kwenye banda la kulelea ili walelewe kwa joto la kawaida la banda/chumba.
Kwa kawaida joto hupimwa kwa kipimajoto (thermometer), lakini kama huna kipimo hiki, njia rahisi ni kuwaangalia kulingana na tabia zifuatazo; Kama vifaranga wamejikusanya sehemu moja basi joto ni kidogo bandani mwao, au kama wanaenda mbali
na chanzo cha joto huku wanatanua mabawa yao na wakihema harakaharaka basi joto ni kali/limezidi kiwango. Pale
watakapo tawanyika vizuri ndani ya boksi/kibanda cha kulelea huku wanakula na kunywa maji vizuri basi joto ni la wasta
na ndilo linalofaa. Kama unatumia njia ya Boksi, basi unatikiwa kulipanua kulingana na ukuaji na mahitaji ya vifaranga vyako.
Vifaranga wako wape chakula cha vifaranga cha kutosha, maji safi na salama, majani mabichi ambayo hufungwa kwa
kuning’inizwa kwa kamba,na CHANJO za minyoo nk ili wapate vitamin, madini na protini itakiwayo na kuzuia tabia ya kudonoana ili
wakue vizuri.
Hakikisha kuwa chumba chao ni kisafi na hakina unyevunyevu wakati wote. Unyevunyevu husababisha ugonjwa wa baridi na
hufanya vifaranga wajikunyate na kutetemeka na wanaweza kufa ghafla!
Inashauriwa kuwa siyo salama kufuga aina nyingine ya ndege kama vile njiwa, bata, bata mzinga nk kwa kuwachanganya na kuku
maana kila aina ya ndege wanamagonjwa yao. Hivyo kuwachanganya kutakufanya ushindwe namna ya kuwatibu wanapopatwa na
ugonjwa. Pia chawa wa njiwa huleta ugonjwa wa Ndui hasa kuku wanapoangua vifaranga wao. Hapa ugonjwa unaweza kufyeka
vifaranga wako wote 60/100 kama utafuata ushauri wangu!
Baada ya wiki 2 hadi 3 baada ya kuwanyang’anya vifaranga kuku wako wataanza tena kutaga mayai. Wakiatamia wote 5 Kama
utaimarisha huduma kwao na kwa vifaranga/kuku wale 100 tayari utakuwa una kuku 105 au zaidi. Kuku wale 5 wa mwanzo
wakiatamia tena kwa siku 21 hadi 48 (kama utafuata mfumo ule wa mwanzo wa kuaatamishia mara 2) utajipatia vifaranga
wengine 100 tena na hivyo kuwa na kuku zaidi ya 200 ndani ya miezi 5/6 tu!Ukiwahudumia vifaranga wale wa mwanzo 100
vizuri kwa miezi 3 na nusu nao wataanza kutaga kama mama zao. kwahiyo, Chukulia walalie majike 5 wa mwanzo na majike 50
waliopatikana baada ya uzao wa kwanza kwa miezi ile 3 ya mwanzo utakuwa na mitetea 55. Wote wakiatamia na watoe vifaranga
10 kila mmoja kwa siku zilezile 21 hadi 46, tayari utakuwa na vifaranga 550! Sasa jumlisha na wale 150 waliobakia kati ya kuku
200 na wote wakakua vizuri utapata kuku na vifaranga zaidi ya 700! Jumlisha na 550 watakaototolewa na mama zao wale 5 wa kwanza na wale 50 wa uzao wa 1 na 2 kwa mara ya 2 si tayari utakuwa na kuku zaidi ya 1,200 ndani ya miezi 6 hadi 8 tu? Hivyo
utajikuta unao kuku zaidi ya 1,000!
Kati ya kuku 1,000 ukisema utoe kuku 800 wa kuuza na ukiwauza kwa bei ya Tsh. 4,000 kwa kila kuku 1 tayari utakuwa na Jumla
ya Tsh. 3,200,000/= ambazo unaweza kufanya mtaji wa mambo mengine au kuboresha mradi wako zaidi. Unafikiri hapo hujaanza
kufikia lengo la kuku 1 akuletee shilingi Milioni 1? Ukiendelea hivi inamaana kuku 1 atakuzalishia zaidi ya hapo.

BANDA LA KUKU.

Unatakiwa kuwa na banda bora la kufugia kuku ambalo litaweza kutunza kuku ili wasiweze kupatwa na madhara mbalimbali kama
vile; kuliwa/kujeruhiwa na wanyama wakali, kuchukuliwa na wezi nk. Lakini banda bora pia litawasaidia kuku kuhimili mabadiliko
mbalimbali ya hali ya hewa yanayoweza kujitokeza.
Sehemu ambayo inafaa kwa ujenzi wa banda bora ni ile ambayo inaweza kufikika kwa urahisi, iwe na mwanga wa kutosha, isiwe
na upepo mkali na isiyoruhusu maji kusimama au kuingia ndani.
Banda ni vema likawa la ukuta/mbao/mabanzi.matete/mianzi imara ili lishikilie paa vizuri lisianguke. Kuta hizi zaweza kujengwa
kwa matofali ya saruji/matope/kuchomwa/mabanzi/mbao nk. Katika kuezeka waweza kutumia mabati/vigae/nyasi. Banda ni vema
likawa kubwa kulingana na kiasi cha kuku na umri walionao. Kitu cha kuzingatia ni kwamba banda liwe na hewa ya kutosha.
Kuku wanaofugwa ndani ni vema wakatengenezewa uzio mpana (angalau Mita 8x10) ili wapate mahali wanapoweza kuota jua,
kupumzikia/kupunga hewa na kufanya mazoezi (wawekee kamba/bembea/ngazi ndani ya banda). Hakikisha kuwa banda ni imara
na hawatoki nje ya banda na kwenda mbali ili uweze kuwawekea chakula cha kutosha na maji na hata wale wanaotaga/kuatamia
wapate chakula na kurudi haraka.
Banda likiwa kubwa na bora litapunguza magonjwa kwani litakuwa na hewa ya kutosha ambayo itasaidia kupunguza joto na
unyevunyevu usio wa lazima bandani mwako. Hii itasaidia uingizaji oksijeni ya kutosha na kupunguza hewa chafu zenye madhara kwa kuku. Pia litasaidia namna ya kufanya usafi kwa urahisi na kupunguza vumbi ambalo linaweza kusababisha kikohozi kwa kuku
wako. Ni vema banda lisipungue Mita 3 kwenda juu.

Mambo muhimu ndani ya Banda la kuku

1. Mambo muhimu ndani ya Banda.
1. Sakafu nzuri (iliyotengenezwa kwa saruji/udongo ili isituamishe maji. Isiwe na nyufa ili iweze kusafishwa kwa urahisi.
2. Hakikisha kuwa banda linakuwa na Viota (vitagio) vizuri kwaajili ya kutagia. Viota viwe na urefu wa Sentimita 30 na upana sentimita
30 na kina sentimita 35. Sehemu ya mbele izibwe kwa sentimita 10 tu chini. Sehemu zote hizo zizibwe kwa ubao. Kama kuku wako
ni wakubwa unaweza kuongeza upana, urefu na kina kiasi cha kutosha mfano, Upana na Urefu 35cm, kina 55cm nk. Hakikisha
kiota/kitagio kinakuwa na giza kiasi maana kuku hupenda kutaga mahala pa giza kidogo/palipojificha. Giza litasaidia kuku asiweze
kula mayai au asiweze kudonoana na kuku wengine. Kiota pia kinatakiwa kiwe mahali ambapo ni rahisi kwa kuku kuingia na
kutoka, pia iwe ni rahisi kusafisa.
Ndani ya kiota kuwekwe majani makavu/maranda ya mbao laini na kinyunyize dawa ya unga ya kuzuia viroboto/utitiri kabla ya
kuweka nyasi.
AIDHA, ni vizuri sana kuwawekea kuku wanaoatamia mayai wakati wa usiku maana ukimuwekea wakati wa mchana anaweza
kuyaacha.
Kuku anayetarajiwa kuatamia ni vema akachunguzwa kama anao utitiri/viroboto/chawa kwenye manyoya yake. Wadudu hawa
humkosesha raha kuku anayeatamia na wengi huacha mayai na kukimbia/wasitulie kwenye viota vyao. Hali inapelekea kuanguliwa
kwa vifaranga wachache. Unaweza kumuona mtaalam wa mifugo kwa ushauri zaidi.
1. Banda liwe na vichanja maana kuku hupenda kulala juu ya vichanja maana nao ni ndege.
2. Vyombo safi na vizuri kwaajili ya chakula na maji.
3. Walazie majani makavu/maranda ya mbao/makapi ya mazao sakafuni kwa banda zima.

UCHAGUZI NA UHIFADHI WA MAYAI.

Mayai huharibika kwa urahisi sana yasipo tayarishwa na kutunzwa vizuri kwa uangalifu. Matayarisho huanzia bandani hadi ndani
kwa kufanya yafuatayo;
o Hakikisha viota vyote ni safi wakati wote.
o Chakula kiwe ni cha kuimarisha gamba la yai na vyakula vingine.
o Vyombo vya kukusanyia mayai viewe safi na imara.
o Kusanya mayai mara2 hadi 3 kwa siku ili kuepuka mayai kuvunjwa/kuliwa/kuchafuka kwa mayai mengi na kupoa haraka.
o Ondoa mayai yaliyo na nyufa na maganda yasiyo imara.
o Safisha mayai mara baada ya kukusanya na kabla ya kuweka kwenye chombo cha kuhifadhia saa 12-24. Mayai yanaweza
kuoshwa kwa maji ya uvuguvugu (nyuzijoto 35oc) na kusugua taratibu kwa mkono ili kuondoa uchafu (kama upo). Lakini
unashauriwa kusugua kwa mkono bila maji ili kusafisha maana maji hupunguza ubora wa yai na maranyingi yai huharibika haraka.
o Weka katika vyombo visafi kwa kuelekeza sehemu ya yai iliyo pana iwe juu na sehemu nyembamba iwe chini, beba kwa uangalifu.
o Hifadhi mayai katika sehemu ya baridi nyuzijoto10 hadi 16 za sentigredi.
o Mayai yapangwe kwa daraja kwa kufuata ukubwa na rangi ili kuvutia wateja na kuongeza bei. Pia unaweza kuweka kwa kufuata
muda unapoyaokota kutoka bandani. Weka lebo yenye tarehe ili usichanganye wakati wa kuwaatamishia kuku wako/kuuza.
Kuchagua mayai ya kuatamishia kuku kwaajili ya kuangua vifaranga.
Mayai yanayofaa kwa kuatamiwa na kuanguliwa ni vema yawe na ukubwa wa wastani, yasiwe na ufa/nyufa, yasiwe ya mviringo
kama mpira, yasiwe na uchafu wowote juu ya gamba lake, yasiwe yametengwa kwa zaidi ya wiki 1 (siku 7).

🙉🙉🙉Usisahau kushare posti hii kuhusu (UFUGAJI BORA NA RAHISI WA KUKU WA KIENYEJI).👍 Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasome💯✔

Marafiki zako wa zamani utawakuta hapa sasa Bado wanakupenda sana na wanakungoja kwa hamu kubwa

👉SOMA ZAIDI HAPA...

tafuta-rafiki.gif

.