Tafuta

Kutana na marafiki zako wa enzi hizo hapa Wewe ni miongoni mwa rafiki yao wa kipekee sana

πŸ‘‰SOMA ZAIDI HAPA...

πŸ‘‰ Tohara ya Mwanaume kwa Ajili ya Kukinga Maambukizo ya VVUπŸ‘‡βœ”

Ukataji wa ngozi ya mbele ya uume (ngozi
inayofunika kichwa cha uume), ni moja ya
njia za zamani sana za upasuaji katika
historia ya mwanadamu.

Manufaa ya Tohara
kwa Mwanaume

Hupunguza hatari/uwezekano wa kupata
maambukizo ya VVU kwa kiasi cha asilimia
60.

Hupunguza hatari ya kupata baadhi ya
maambukizo yanayofanywa kwa njia ya kufanya
ngono kama vile: matutuko (herpes)
na kaswende.

Inaweza kukukinga na saratani ya uume.

Kinga ya matatizo kadhaa ya afya ya uume
na govi mfano uvimbe, uchungu, kutoka
makovu na kuvimba kwa kichwa cha uume,
kubana kwa govi na kusinyaa kwa nyuma
kwa govi.

Usafi wa uume kwa urahisi.

Inakubalika kisayansi na kitamaduni.

Madhara Yanayoweza
Kutokea Wakati wa Tohara

Tohara ya mwanaume imethibitika kuwa ni
salama na yenye mafanikio inapofanywa katika
mazingira rasmi ya utoaji tiba.

Kama shughuli yoyote ya upasuaji, matatizo
yanaweza kutokea baada ya operesheni hii.

Matatizo/Madhara yanayoweza kutokea ni
pamoja na maumivu, kutokwa na damu na
uambukizo katika kidonda.

Hata hivyo, matatizo haya huisha haraka kwa
kupata tiba za ziada.

Tohara ya Mwanaume na VVU

Sababu za kibayolojia kwa kinga hii inayotolewa
ni pamoja na:

Kupungua sana kwa msuguano na
govi.

Kuwepo kwa mrundikano wa seli
ambazo huvutia VVU.

Tohara ya mwanaume huimarisha
ngozi ya kichwa cha uume.

Tohara ya mwanaume hupunguza
urahisi wa kupata maambukizo
yanayoenezwa kwa njia ya ngono.

Baadhi ya Visa-Asili na
Dhana Potofu Kuhusu
Tohara ya Wanaume

  • Tohara ya wanaume ni kinga kamilifu dhidi ya VVU – si kweli
  • Hutakuwa na uwezo wa kusimamisha uume – si kweli
  • Hupunguza nguvu za kiume – si kweli
  • Huongeza nguvu za kiume – si kweli
  • Tohara ya wanaume inasababisha utasa – si kweli
  • Ni wahudumu wa kiume tu ndio wanaoweza kufanya tohara

ya wanaume kwa uhakika – si kweli

  • Tohara kwa wanaume hupunguza raha ya ngono – si kweli
  • Watu wazima huchukua muda mrefu kupona vidonda vya

tohara – huwachukua wiki 6 tu.

Hatua za Utaratibu
wa Tohara

Tohara itafanywa katika chumba maalumu cha kufanyia operesheni
chenye vifaa safi.

Uume wako na eneo zima la kinena litasafishwa kikamilifu
kabla ya kufanyiwa tohara.

Utapewa sindano yenye dawa ya ganzi ili usihisi maumivu
wakati wa kufanyiwa tohara.

Mchakato mzima wa kufanyiwa tohara utachukua kati ya
dakika 30 na saa moja.

Uume wako uliotahiriwa utafungwa kwa kutumia bandeji.

Utakuwa na muda wa dakika 30 za kupumzika ambapo
kwao utapewa unasihi kwa mara nyingine kuhusu jinsi unavyopaswa
kuhudumia jeraha lako na kuchunguza dalili zozote
za hatari.

Utaruhusiwa kwenda nyumbani na kupewa ahadi ya kurudi
tena ndani ya masaa 24 – 48.

Baada ya Tohara

Usifanye kazi ngumu kwa muda wa siku 4 baada ya tohara.
Eneo lililofanyiwa tohara liwe kavu kwa siku 3 baada ya
kufanyiwa tohara. Epuka kutumia dawa za kuulia vijidudu.
Safisha kwa maji salama na laini eneo la jeraha kwa uangalifu.
Usifungue bendeji mpaka utakaporudi kituo cha afya.
Uvimbe mdogomdogo na kutojisikia vizuri ni hali ya kawaida.
Uume unaweza ukawa na uwezo mkubwa wa hisia
katika wiki chache za mwanzo baada ya tohara. Hili ni
jambo la kawaida na hupungua baada ya muda.
Kuongezeka kwa maumivu, wekundu, kuvimba, kutokwa
damu au uchafu katika eneo la tohara, ni dalili za hatari.
Wahi kwenye kituo cha afya mara moja.

Baada ya Tohara

Kidonda huonekana kupona baada ya siku 7, lakini
jeraha hupona kipindi cha wiki 6.
Uponyaji kabisa huchukua muda mrefu hadi miezi 6.
Unashauriwa kutumia kondomu kwa miezi mingine
6 baada ya tohara ili kuendelea kulinda
jeraha linalopona.
Kufanya ngono na kupiga punyeto hakuruhusiwi
kwa muda usiopungua wiki sita za mwanzo.
Kurudi kwa mara ya kwanza__ Saa 24 – 48.
Kurudi kwa mara ya pili_ Siku 7.
Kurudi kwa mara ya tatu
Wiki 4.

Mambo mengine muhimu
ya kufahamu…

Mwanaume ana jukumu
gani katika uzazi
wa mpango?

Uzazi wa mpango ni sehemu muhimu ya afya ya uzazi
kwa mwanaume.
Kwa kufuata uzazi wa mpango wewe na mwenzi wako
mwaweza kupanga wakati muafaka wa kupata mtoto
pia ukubwa wa familia yenu.
Mwanaume anaweza pia anatakiwa kushiriki na mwenzi
wake kuamua njia salama na muafaka ya uzazi wa
mpango.
Njia za kisasa za uzazi wa majira zinamhusu mwanaume
pia. Baba aweza kutumia Kondom. Kondomu zinafaa
kwa wanandoa na hata walio nje ya ndoa. Zinaweza
kukulinda wewe na mpenzi wako kutokana na magonjwa
ya ngono na mimba isiyopangiliwa.
Wanaume wanaoamua kufunga uzazi wanaweza kutumia
njia ya operesheni ndogo.

Je? Mwanaume ana nafasi
gani wakati wa ujauzito na
hata uzazi?

Msaidie mwenzako kwa:
Kupata ushauri na upimaji wa VVU pamoja. Kumbuka
dawa za ART huzuia maambukizi toka kwa mama kwenda
kwa mtoto.
Kumkumbusha mwenzako kutumia virutubisho na dawa
alizopewa pia muimize kurudi siku ya tarehe yake.
Kufanya maandalizi ya mtoto ikiwa ni pamoja na kutenga
fedha za usafiri, matibabu na mahitaji mengine yawezayo
kutokea.
Kumuhimiza na kumuunga mkono akajifungulie kwenye
kituo cha afya.

πŸ™‰πŸ™‰πŸ™‰Usisahau kushare posti hii kuhusu (Tohara ya Mwanaume kwa Ajili ya Kukinga Maambukizo ya VVU).πŸ‘ Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasomeπŸ’―βœ”

Mtafute ndugu yako usiyewahi kumuona hapa Na yeye anakutafuta sana hapa

πŸ‘‰SOMA ZAIDI HAPA...

Slide3-mliopoteana.GIF

.