SIMU YA MKONONI NA AFYA YA MSICHANA

Mpendwa Msomaji, baada ya kukuandalia makala inayopendwa kuhusu; Namna ya kupika Vitumbua, sasa nimekuandalia makala hii kuhusu;

SIMU YA MKONONI NA AFYA YA MSICHANA.

Endelea kefurahia makala nzuri kila siku unapotembelea tovuti hii.

USIKOSE HIIπŸ‘‰ Mtafute ndugu yako mliopotezana

SIMU YA MKONONI NA AFYA YA MSICHANA

By, Melkisedeck Shine.

SIMU YA MKONONI NA AFYA YA MSICHANA

Simu za mkononi leo zimekuwa kama sehemu ya maisha ya kila mwanadamu katika mabara yote duniani. Imefikia mahali simu zimesababisha urahibu kiasi kwamba mtu asipokuwa na simu anakuwa kama amepungukiwa na kiungo muhimu cha mwili wake. Kama simu ya mkononi (cell phone) itatumika vizuri kwa malengo na kwa wakati unaofaa, ni chombo kizuri na cha uhakika kwa mawasiliano ya haraka, kujifunza mambo mapya, kukuza uchumi na mambo mengine ya maana na hilo halina ubishi wala mjadala.
Tatizo la simu za mkononi linakuja pale tunapoanza kuangalia athari za mionzi inayopenya mwilini kama matokeo ya matumizi ya simu hizi na athari nyingine za kiafya zitokanazo na matumizi ya muda mrefu ya simu pamoja na athari za kijamii zinazotokana na matumizi mabaya ya simu.
Matumizi ya simu za mkononi yana hatari nyingi za kijamii na kiafya kwa watoto na vijana walio chini ya umri wa miaka 20. Inashauriwa kuwa ni bora kwa vijana hawa kuepuka matumizi ya simu za mkononi au watumie mara chache sana tena kwa muda mfupi na pale inapokuwa hakuna njia mbadala ya mawasiliano. Matumizi makubwa ya simu za mkononi yanaingilia utendaji wa ubongo wa vijana wadogo. Huathiri uwezo wa kufikiri sawasawa na kuwa makini lakini pia inasemekana kuwa, matumizi makubwa ya simu hizi katika umri mdogo, yanaongeza uwezekano wa kupata kansa ya damu kutokana na mionzi.
Vijana wanaotumia simu za mkononi kwa muda mrefu hukabiliwa na msongo, kukosa utulivu wa kiakili, hali ya kupata uchovu wa mwili na hali ya kutokupata usingizi vizuri. Wengi hawazimi simu zao wanapokwenda kulala usiku na wengine hulala nazo kitandani karibu kabisa na kichwa, jambo ambalo huharibu mtiririko wa usingizi wakati akili inapohitaji kupumzika.
Jumbe na miito mingi ya wasichana huwa inahusiana na mambo ya kimapenzi ambayo huchochea akili kufikiria ngono kwa nguvu kutokana na ukweli kuwa wakati wa balehe, tamaa za ngono huwa na nguvu kubwa. Simu zenye mtandao pia huwaingiza vijana wengi katika mtego wa kuangalia picha za ngono zinazochochea tamaa ya ngono haramu na hatarishi.
Akili za watoto, ikiwa ni pamoja na wasichana hudhurika kirahisi kwa mionzi na athari zake kuchukua muda mrefu hata baada ya matumizi ya simu kwa muda mfupi. Mionzi ya simu hupenya katika fuvu la watoto kwa nguvu zaidi kuliko watu wazima waliokomaa. Uwezo wa kiakili wa vijana ambao unatazamiwa kuwa utapungua wafikapo katika umri wa kustaafu kazi (miaka 60), hupunguzwa na mionzi ya simu. Wafikapo miaka 30 tu ya umri wao, vijana wanao tumia sana simu za mkononi, huwa sawa na wazee wa miaka 60 katika uwezo wa kiakili.
Tafiti kadhaa huonyesha vijana wenye umri wa miaka 20 wakiendesha gari huku wanaonge kwa simu uwezo wao wakiakili wa kufanya maamuzi huchelewa sawa na ule wa wazee wa miaka 70. Umakini wao hugawanyika katika kuangalia usalama na kutafakari maana ya ujumbe na jinsi ya kujibu. Mionzi pia huvuruga uwezo wa ubongo wa kufanya maamuzi kwa haraka. Mara nyingi matokeo ya jambo hili huwa ni ajali za barabarani, zinazo sababisha madhara makubwa ya kiafya na ulemavu au vifo.
Upo ushahidi pia unaoonyesha kuwa kutumia simu kwa muda mrefu husababisha maumivu ya kichwa na hisia ya ganzi katika ngozi ya kichwa. Mionzi ya simu za mkononi pia hupunguza uzalishwaji wa kichocheo cha melatonin mwilini ambacho ni muhimu kwa utendaji mzuri wa ubongo na kinga dhidi ya saratani ya matiti. Wasichana wanaotumia simu za mkononi kwa muda mrefu, wanakabiliwa na uwezekano mkubwa wa kupata saratani ya matiti na ugonjwa wa ubongo (Alzheimer’s disease) mapema au baadaye sana katika kipindi chote cha maisha yao yaliyobaki. Hii inatokana na uwezo mkubwa wa seli za vijana kuitikia nguvu za mionzi. Hali huwa mbaya zaidi kama simu inatoa mionzi zaidi ya kipimo cha SAR (Specific Absorption Rate) Wart 2/kg.
Tatizo jingine la kiafya kutokana na simu ni ugonjwa wa masikio kuunguruma muda wote (Tinnitus) hasa kwa wasichana wanaosikiliza muziki kwa kutumia simu zao au kupokea miito ya simu yenye makelele kupitia vipokeleo vya sauti vinavyobandikwa masikioni (ear phone).
Athari nyingine za matumizi ya simu ya mkononi kwa msichana ni athari za kijamii. Wasichana wengi wamekuwa walengwa na wahanga wa ngono hatarishi kutokana na matumizi mabaya ya simu za mkononi. Wasichana wengi wanaomiliki simu, kutokana na umri wao, wanashindwa kutumia simu hizi kwa ajili ya mawasiliano yenye kuleta faida na matokeo yake huwa ni kujitumbukiza katika hatari nyingi za kimaisha. Siku hizi simu ya mkononi ndicho chombo kinachotumiwa na wasichana wengi kufanya mawasiliano ya haraka na wale wanaowaita wapenzi wao na kurahisisha mipango ya kukutana na kutimiza matakwa yao.

Matumizi ya simu ya mkononi yanahitaji gharama za kuiendesha na hili huwafanya wasichana wengi wasiokuwa na ajira kutafuta njia mbadala ya kupata fedha kwa ajili ya kugharamia simu zao. Njia ambayo wasichana wengi huitumia kupata fedha za kugharamia simu zao ni kupata fedha kutoka kwa wale wanaowasiliana nao. Wasichana wengi wamepoteza heshima, utu na uhuru wao kwa vile wamegeuka kuwa ombaomba wa vocha za simu.
Wavulana wengi hutumia udhaifu huu wa kiuchumi wa wasichana kuwarubuni na kuwaingiza katika mitengo yao inayohatarisha afya na usalama wa wasichana hawa. Ni jambo la busara pia kukumbuka kuwa pesa zinazotumiwa kiholela ili kugharamia mawasiliano yasiyokuwa na tija katika maisha ni upotezaji wa rasilimali muhimu ambazo zingetumika kwa ajili ya kupunguza umaskini na kuboresha maisha kwa kugharamia mahitaji muhimu na ya lazima. Miongoni mwa makampuni yanayoongoza kwa kupata faida kubwa duniani ni pamoja na makampuni ya simu za mkononi.
Wasichana imewapasa kuelewa matumizi salama na yenye tija ya simu za mkononi ili kuepuka hatari na athari hasi zinazotokana na matumizi yasiyofaa na athari za kiafya za chombo hiki cha mawasiliano. Simu za mkononi zimekuwa chanzo kikubwa cha kuharibu tabia na maisha ya wasichana wengi leo hivyo ni jambo la busara kwa msichana yeyote kutathimini faida na hasara za matumizi ya simu katika maendeleo yake katika masomo na maisha kwa ujumla.

 

Unaweza kusoma makala mpya nzuri kila unapotembelea website hii wakati wowote. Baada ya kusoma makala hii kuhusu; SIMU YA MKONONI NA AFYA YA MSICHANA, sasa endelea kusoma makala hizi nyingine nzuri nilizokuandalia;

Usipitwe na Nafasi za kazi kwa leo

<<Bofya HAPA kujua zaidi>>

.

KADI-SHUKRANI-MZAZI.JPG
Ndugu.gif