Nikitafuta rafiki kwa nia ya kuoana (mchumba), je ni sifa gani niangalie kwa msichana/mvulana?

By, Melkisedeck Shine.

afya-mapishi-na-lishe.png

Nikitafuta rafiki kwa nia ya kuoana (mchumba), je ni sifa gani niangalie kwa msichana/mvulana?

Kuchagua mchumba ni moja ya maamuzi ambayo kijana anahitaji kuyafanya kwa uangalifu mkubwa sana. Kwa sababu huyo ndiye atakayekuwa mwenzi wake wa maisha. Katika kuchagua mchumba kila mtu ana mawazo yake kuhusiana na kilicho muhimu kuzingatiwa. Mara nyingi mhemuko una nguvu zaidi kuliko uamuzi wa kimantiki

Hata hivyo, vifuatavyo ni kati ya vigezo ambavyo vinaweza kuangaliwa:

โ€ข Chagua mtu anayekuheshimu wewe na wengine; Chagua mtu unayemwamini;
โ€ข Chagua mtu ambaye unaweza kuongea, kujadiliana, na kuhojiana naye kwa uwazi bila kugombana;
โ€ข Chagua mtu mwenye umri unaokaribiana na wa kwako;
โ€ข Chagua mtu anayependelea vile unavyopendelea;
โ€ข Chagua mtu ambaye ataelewa matatizo yako na yuko tayari kukusaidia kuyatatua; na
โ€ข Chagua mtu mwenye afya nzuri.

Hii inamaanisha pia kumpata mtu ambaye kabla ya kuanza kujaamiana naye, atakuwa tayari kwenda kupima kwa hiari kujua hali yake ya VVU na pia kuwa tayari kutumia kinga kwa maana ya kondomu hadi hapo mtakapojua hali zenu.

Wafahamishe wazazi wako mtu uliyemchagua kama mchumba na mtambulishe kwao i ili wamfahamu na yeye awafahamu wazazi wako. Wakati huohuo na wewe jaribu kuwafahamu wazazi wake. Usifanye uchumba wa haraka. Pata muda wa kutosha kumwelewa rafiki yako.


Endelea kusoma makala hizi zifuatazo;

a.gif Kufahamu tabia ya rafiki yako wa kike/kiume kabla ya kuoana hata kama anaishi mbali

Unaweza kufanya uchunguzi wa kutosha kuhusu tabia, muono na imani ya rafiki yako hata kama mnaishi mbalimbali. Unaweza kumuuliza maswali kuhusu mahali anapoishi na familia yake kwa ujumla. Jaribu kufanya mawasiliano ya karibu zaidi ili uweze kumdadisi, na yeye aweze kujieleza mwenyewe kwa undani zaidi kuhusu yeye mwenyewe… soma zaidi

a.gif Nifanye nini ili kuepuka kubakwa na mpenzi/ rafiki?

Kuna baadhi ya vidokezo ambavyo vinaweza kukusaidia:
1. Usikae faragha na mwenzi wako kabla hujawa tayari na kumwamini. Ongozana na marafiki wengine hasa mwanzoni mwa urafiki wenu. Msitoke tu nyie wawili hadi hapo utakapojisikia kuwa umemjua kiasi cha kumwelewa na kumwamini. Pia jiepushe kukaa sehemu za faragha naye… soma zaidi

a.gif Kulambana sehemu za siri ni salama kiafya? Je, tendo hili ni la kawaida?

Si rahisi kusema ni kitendo kipi kilicho cha kawaida na kisicho cha kawaida. Kulamba ni jambo linalofanyika.. soma zaidi

[Msemo wa Leo] ๐Ÿ‘‰Maisha ya ujana

[Jarida la Bure] ๐Ÿ‘‰Picha Kali Za Kuchekesha

[Hadithi Nzuri] ๐Ÿ‘‰Jinsi mke alivyotoboa siri ya Mmme wake

[SMS kwa Umpendaye] ๐Ÿ‘‰Meseji ya pongezi kwa mpenzi wako

a.gif Jinsi ya kutengeneza Pilau Ya Kuku

Mchele wa basmati - 3 vikombe.. soma zaidi

a.gif Jinsi ya kulima vizuri zao la kabichi

Kichwa cha kabichi kinapofunga vizuri, hutumika kama chakula na huvunwa baada ya kufunga na kukomaa vizuri. Kwa kawaida kabichi hupandwa kwa msimu mmoja, lakini iwapo itakuzwa kwa ajili ya kutoa mbegu hukuzwa zaidi ya msimu mmoja. Endapo inalimwa sehemu yenye maji ya kutosha, inaweza kulimwa msimu wote wa mwaka. Soko lake ni la uhakika katika kipindi chote na ni muhimu kwa afya. Pia, linaweza kutumika kama malisho ya mifugo
Mizizi: Mizizi ya kabichi hutawanyika ardhini vizuri. Kwa kawaida, huenda chini kiasi cha sentimita ishirini (20 sm), na hujitawanya kwa kiasi cha sentimita sabini na tano (75sm).
Shina: Shina la mmea wa kabichi huwa na rangi ya kijani au zambarau. Hii hutegemeana na aina ya kabichi, na kwa kawaida ni fupi… soma zaidi

a.gif Uhusiano uliopo kati ya pesa na muda

Bila shaka upo uhusiano mkubwa kati ya pesa na muda…. soma zaidi

a.gif Namna ya kupika Vitumbua

Vitumbua ni aina ya vitafunwa vya chai ambavyo hutengenezwa kwa kutumia unga wa mchele. Kiasili vitumbua ni chakula ambacho hupendelewa sana na watu wa pwani. Na mara nyingi wamekuwa wakipika kwa kuchanganya na nazi ili kuvifanya view na ladha nzuri zaidi.. soma zaidi

a.gif Jinsi ya kutunza udongo

Uelewa wa maisha ya mimea husaidia kwa kiasi kikubwa kwa hatua ya kuchukua kuilisha mimea hiyo… soma zaidi

picha-kali.png

.

afya-mapishi-na-lishe.png
KADI-SALAMU-JIONI-MZAZI.JPG
afya-mapishi-na-lishe.png

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.