Nyumba ya kulelea Vifaranga

By, Melkisedeck Shine.

Ukipenda kujenga nyumba ya vifaranga itafaa ufi kirie yafuatayo:-
a Nyumba ya vifaranga iwe karibu na nyumba yako mwenyewe ili uweze kuwakagua
vifaranga wako mara kwa mara.
b) Ijengwe hatua 20 au zaidi mbali na nyumba ya kuku wakubwa, hii ni kinga mojawapo
ya kupunguza hatari ya maambukizi ya magonjwa.

c) Nyumba ya vifaranga isiruhusu ubaridi au unyevu au wanyama waharibifu kuingia.
Lakini nyumba iingize hewa na mwanga wa kutosha kila wakati.
d) Nyumba iwe na eneo la kutosha ili vifaranga wapate nafasi ya kutembea kutafuta
chakula na maji bila kubanana.
e) Ijengwe kwenye sehemu isiyoelekea upepo unaotoka kwenye nyumba ya kuku
wakubwa. Tahadhari hii husaidia vifaranga kuepukana na magonjwa yanayoenezwa
na upepo.

Ukubwa wa Nyumba

Eneo:

Vifaranga hawahitaji eneo kubwa katika muda wa majuma 4 ya kwanza. Nafasi
inayohitajiwa kwa kukadiria ni meta za eneo 1 kwa kila vifaranga 16. Kwa mfano nyumba
yenye meta 10 za mraba inatosha kulea vifaranga 160 hadi umri wa majuma 4. Vipimo
vya nyumba yenye eneo kama hili inaweza kuwa na hatua 5 kwa hatua 4 au hatua 3 kwa
3.25. Utajenga kutegemea na eneo ulilonalo. Baada ya majuma 4 ya umri ongeza nafasi na
uwape vifaranga eneo la kuwatosha.

Sakafu:

Sakafu nzuri katika nyumba ya vifaranga ikiwezekana inafaa ijengwe na simenti
iliochanganywa na zege. Ili kupunguza gharama, unaweza kutumia vifaa vya ujenzi
vinavyopatikana kirahisi katika eneo lako vitumikavyo kusiriba sakafu kama udongo wa
kichuguu au unaweza kulainisha kinyesi cha ng’ombe kwa maji na kusiriba eneo lote la
sakafu.

Ukuta:

Ingefaa kuta za nyumba za kulea vifaranga za matofali, udongo, mabati au debe.
Kuta za matofari na udongo zipigwe lipu ili kurahisisha usafi shaji wa nyumba au umwagiaji
wa dawa. Urefu wa kuta uwe tangu meta 1.8 – 2.4 (futi 6-8). Sehemu ya kutoka chini ya meta
0.9 – 1.2 (futi 3 – 4) izibwe na ukuta wa tofali au udongo na sehemu ya juu iliyobakia yenye
meta 0.9 – 1.2 (futi) 3-4) ijengwe kwa wavu wa chuma au fi to.

Mbao:

Nguzo za miti au mbao zilowekwe dawa ya mbao kama vile “Dudu killer” au oili chafu
ili kuzuia kuoza. Ukitumia miti ni vizuri uondoe magome ambayo yanaweza kuweka vimelea
na wadudu.

Madirisha:

Unaweza kutumia maboksi, mikeka ya magunia, mapazia ya magunia ni rahisi na
yanaweza kuwekwa kwa kupigiliwa misumari kwenye dari na upande wa chini pazia ipigiliwe
misumari kwenye ubao ili ininginie.Unaweza kukunja mapazia/magunia ili uingize hewa na
mwanga wa kutosha katika nyumba ya vifaranga.

Paa:

Mjengo wa paa uwe unaoweza kuwapatia vifaranga hewa ya kutosha hivyo paa liwe na
tundu la kutoa nje hewa yenye joto. Kwa kadri utakavyoweza, unaweza kutumia madebe,
mabati, makuti au nyasi n.k. kuezeka nyumba ya vifaranga. Sehemu ya paa ikianza kuvuja
iezekwe bila kuchelewa.

Vyombo kwenye nyumba ya vifaranga

Kuna vyombo vingi pia njia nyingi zinazotumika katika kulea vifaranga kutegemeana na hali
halisi ya mfugaji. Mfugaji kijijini anaweza kutumia vyombo vifuatavyo:

1. Vitalu

Vifaranga hutunzwa ndani ya kitalu
kilichotengenezwa kwa mbao au karatasi
ngumu zinazotumika kujengea dari.
Au katika mazingira ya kijijini unaweza
kutengeneza wigo wa mduara kwa
magunia. Upana wake uwiane na wingi wa
vifaranga ulionao na kina chake kama mita
moja. Ukuta wake uwe na tabaka mbili za
magunia hayo zilizoachana kwa nafasi
ya inchi tatu au nne. Katikati ya nafasi
hiyo jaza maranda ya mbao au pumba za
mpunga. Tayari utakuwa umepata kitalu
cha kulelea vifaranga.

Ndani ya kitalu weka taa ya chemli ya kutoa joto linalohitajika kwa vifaranga.

2. Taa ya chemli (taa ya mkono)

Kutegemeana na hali ya hewa taa moja ya chemli inaweza kulea vifaranga 50 au zaidi.
Hakikisha kuwa unayo akiba ya mafuta ya taa ya kutosha, vioo, utambi n.k. Taa moja
hutumia debe moja la mafuta ya taa kwa muda wa siku 16 hadi 20. Unashauriwa uweke
mafuta kwenye taa asubuhi na kukagua jioni kama yanatosha kwa sababu taa ikizimika
usiku utapata hasara ya vifo kwa vifaranga kujikusanya na kukosa hewa .Weka mafuta ya
kutosha lakini usijaze taa. Joto la taa za chemli hurekebisha kwa kupandisha au kushusha
utambi pia kuongeza au kupunguza idadi ya taa.

3. Jiko la Mkaa

Jiko la mkaa linaweza kutumika badala ya taa kwa ajili ya kuwapa vifaranga joto. Unapotumia
jiko la mkaa ni hakikisha kwamba mkaa unaotumia hautoi moshi na chumba kinapitisha
hewa safi na ya kutosha. Pia jiko liwekwe juu ya matofaili ili kuzuia vifaranga wasiliguse.

4. Mwamvuli

Mfugaji akimudu anaweza kutengeneza mwamvuli wa kuning’inia juu ya kitalu cha kulea
vifaranga kwa kutumia makaratasi magumu ya “hardboard”. Mwamvuli unasaidia kupunguza
upotevu wa joto na hivyo kupunguza matumizi ya mafuta ya taa. Kwenye mwamvuli wa
duara toboa tundu moja ili kupitisha hewa yenye joto. Angalia mviringo wa mwamvuli wako
uwiane na ukubwa wa kitalu chako. Ili kuwapa vifaranga uhuru wa kufuata au kuepuka joto.
Ni lazima mwamvuli uwekwe juu ya matofali na kila juma inabidi uinuliwe juu kiasi cha cm 5
(inchi 2, kufuatana na hali ya hewa.

5. Vyombo vya chakula (Vihori)

Ili vifaranga wakue vizuri vyombo vya
chakula lazima viwafae. Vipimo pamoja na
idadi ya vyombo vya chakula ni vya muhimu
viwatosheleze. Chombo chenye urefu wa (futi
3 x inch 3) kinatosha vifaranga 100. Ukitumia
mbao kutengeneza vyombo vya chakula
unashauriwa mbao ziwe unene wa cm 1/25
(inchi ½). Pia, unaweza kutumia sahani za
kawaida unazotumia nyumbani kuwawekea
vifaranga chakula.
Chombo cha kulishia vifaranga

6. Vyombo vya maji:

Chombo chochote chenye kina kifupi kinafaa kwa
kuwayweshea kuku ila budi kiinuliwe ili vifaranga wasiweze
kuingiza takataka za chini kwenye maji. Pia kama ni cha wazi
maji yawekewe changarawe safi kabisa ili kuzuia vifaranga
wasiloane maji. Au tumia sahani na makopokama ifuatavyo.
Toboa sentimita tatu kutoka kwenye mdomo wa kopo, jaza
maji katika kopo halafu lifunike kwa sahani na ligeuze.
Kinywesheo cha vifarangaUJUMBE-MSAMAHA-35JHF32.JPG

Endelea kusoma makala hizi zifuatazo;

a.gif Upendo wa Yesu

.. soma zaidi

a.gif Madhara ya soda

Soda ni kiburudisho ambacho si muhimu sana kwa afya… soma zaidi

a.gif Madhara ya kula yai bichi

Yai bichi linaweza kuwa na vijidudu viitwavyo kwa kitaalamu “SALMONELLA” vinavyoweza kusababisha tumbo kuuma, kichefuchefu na pia kuharisha.
Vijidudu ya “Salmonella” vinaweza kusababisha madhara makubwa kwa watoto, wazee na wale wenye hali dhaifu ya kimwili kama wagonjwa wa UKIMWI… soma zaidi

[Kitendawili Kwako] 👉Bibi anakung'uta matandiko

[Kichekesho Kwako] 👉Duh! Huyu kazidi sasa

Slide2-utotoni.GIF

a.gif UNATAFUTA NDOTO ZAKO AU MAPENZI YA MUNGU?

Watu husema, na hata wahubiri pia nao husema, ‘Fuata ndoto zako!’ Lakini Yesu alisema, ‘Nifuate mimi’. Ikiwa utafuata ndoto zako, unajifurahisha mwenyewe tu. Lakini ikiwa utamfuata Yesu, atampendeza yeye. Kama utafuata ndoto zako, basi unajitumikia wewe mwenyewe. Ukimfuata Yesu, utamtumikia yeye na kanisa lake. Kama utafuatisha ndoto zako, unajitengenezea njia yako mwenyewe. Kama utamfuata Yesu, yeye ndiye atakayekuandalia njia.
Kuwaambia wakristo kwamba wanapaswa ‘kufuata ndoto zao’ ama ‘kuwa na ndoto ama maono ya maisha yao yajayo’ ni kuwaongoza katika njia isiyokuwa sahihi na kuwadanganya. Hao wanaofundisha mafundisho hayo watawajibika mbele za Mungu kwa kuwadanganya waamini. Hao wanaopokea mawazo ya namna hiyo kwenye mioyo yao nao pia wanawajibika kwa kupokea kitu ambacho hakifundishwi katika biblia na ni kinyume na mafundisho ya Biblia… soma zaidi

a.gif Jinsi ya kupika Pilau Ya Nyama Ya Ng'ombe Na Nyanya

Mchele (Basmati) 3 vikombe

Nyama ya ngo’mbe 1 kg

Pilipili boga 1 kubwa

Nyanya 2 kubwa

Vitunguu maji 2 vikubwa

Kitunguu saumu(thomu/galic) iliyosagwa 1 kijiko cha supu

Tangawizi 1 kijiko cha chai

Ndimu 1

Mafuta ya kupikia ½ kikombe

Mdalasini ½ kijiko cha chai

Binzari nyembamba 1 kijiko cha chai

Pilipili manga ½ Kijiko cha chai

Hiliki ½ Kijiko cha chai.. soma zaidi

a.gif Tofauti kati ya mwanamme anayetaka kukuoa na anayetaka kukuchezea na kukupotezea muda

Mwanaume Ambaye Ana Malengo Ya Kuoa Hubadilika Kitabia. Muda Mwingi Hutaka Kuonekana Mtu Mzima Mwenye Sifa Nzuri. Hatakuwa Mtu Wa Kulewa Kupita Kiasi Na Kutapanya Mali Na Wanawake Wengine. Tabia Zake Mbaya Za Zamani Ataziacha.. soma zaidi

a.gif MADHARA YA SHISHA

Yafuatayo ni madhara ya shisha;.. soma zaidi

a.gif Jinsi ya kutibu chunusi kwa kutumia tango

Tango ni tunda na ni mboga pia na ni chanzo kizuri cha potasiamu na vitamini nyingi ambazo zina kazi mhimu katika ngozi yako na huifanya ngozi ngozi ionekane laini na yenye kupendeza… soma zaidi

[Msemo wa Leo] 👉Ushauri kwa mtu

FURSA.PNG

Fursa Ya Kazi Na Ajira Yenye Malipo Mazuri

Au soma zaidi hapa

.

ml.gif
UJUMBE-WA-ZA-JIONI-KWA-NDUGU.JPG

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.