Tafuta

👉 # Njia za kuzuia mimba na kupanga uzazi👇✔

Mbinu za homoni

Njia ya uzuwiaji mimba inayotumikisha homoni kwa kubadilisha rutuba (upevu) kwa kuzuia yai kusitotoka,
kuzuia chembechembe za kiume na kubadili njia ya uterasi. Ni yenye manufaa makubwa ila yanaweza
kuwa na mazara. Hizo mbinu hazikingi mtu zidi ya magonjwa yanayoambukiza kupitia zinaa (ngono).

Mchanganyiko wa vidonge vya kuzuia mimba

Kiidonge cha kuzuia mimba kilicho mchanganiko wa progestogeni na oestrogeni na kikitumiwa kila siku.
• Inaweza kufanya hedhi kuwa nyepesi zaidi, ya kawaida zaidi na bila maumivu mengi.
• Inaweza kuleta madhara kama vile maumivu ya kichwa, kichefuchefu, maziwa kupoteza hali yake ya
kawaida na kuongeza uzito, hata kubadili kwa aina ya vidonge uweza kusaidia kwa matatizo kama haya.
• Inaweza kutoa kinga ya muda mrefu dhidi ya ovari na kansa ya mkojo

Pete ya njia ya uke (NuvaRing)

Pete nyepesi ya plastiki inayoingizwa ndani ya uke na utoa kiwango kidogo cha oestrogeni na progestogeni
kwenyi mkondo wa damu. Inatiwa hapo kwa mda wa wiki tatu na utolewa kwa wiki moja.
• inaweza kuleta madhara madogomadogo zidi ya vidonge kwani uatoa kiwango kidogo cha hormoni
• madhara yanayoambatana na kuharisha na kutapika yanaepukwa kwani hormone hazipitii tumboni
Mbinu zifwatazo utumia hormoni za progestogeni tu na ni njia ingine bora kwa wamama wasioweza
kutumia oestrogeni, wakiwemo pia wakinamama wanaonyonyesha.

Njia dharura ya uzuiaji wa mimba (EC)

Kidonge cha progestogeni kinachotumiwa baada ya tendo la ngono haramu.
• inapashwa kunywiwa haraka iwezekanavyo baada ya tendo la ngono haramu kwa mafaa zaidi
• inaweza kuwa ya mafaa ikiwa imenywiwa kwenyi kipindi cha siku tano cha tendo la ngono haramu
• inapatikana kwenyi kaunta ya duka la dawa, kliniki ya SHine SA na baadhi ya hospitali

Progestogeni-kidonge tu

Kidonge cha progestogeni kinachotumiwa kila siku.
• inapashwa tumiwa kila siku na kwa wakati unaofaa
• inaweza sababisha madhara, ikiwemo hedhi isiokuwa yakawaida, kuongeza uzito, kuwa mchovu na
kuotwa na chunusi mwilini.

Njia ya uzuwiaji mimba ya kudungwa: Depo Ralovera ao Provera

Sindano ya progestogeni inayodungwa kwa kawaida kila wiki 12.
• hedhi kila mara usimama kunapokuwa matumizi ya mbinu hii
• inaweza kusababisha madhara, ikiwemo hedhi isiokuwa ya kawaida, kuongeza uzito, kuwa mchovu na
kuotwa na chunusi mwilini, na hayo yote yanapashwa kuvumiliwa hadi mwisho wa kudungwa
• inaweza kusababisha kurudi nyuma kwa mda hedhi ya kawaida na rutuba (upevu) kiisha kumaliza
kudungwa

Njia ya uzuwiaji mimba ya kupandikizwa: Implanon

Progestogeni ya kupandikizwa kwenye pande ya juu ya mkono inafaa kwa kipindi cha myezi mitatu.
• hedhi ubadilika na damu inaweza kugeuka nyepesi zaidi, nzito, utoka nyakati zisizotarajiwa ao usimama
pia
• inaweza kusababisha madhara, ikiwemo ongezeko la uzito, uchovu na kuotwa na chunusi mwilini
• pandikizo uweza kutolewa kwa wakati wowote
• wakati pandikizo linatolewa hedhi na rutuba (upevu) hurudi kuwa ya kawaida mara moja
• pandikizo uingizwa na utolewa na bahadhi ya waganga(GPs), wanajikolojia (kupitia uhamisho) na
wadaktari wa SHine SA chini ya utumiaji wa anestezia mahali panapolengwa

Chombo kinachoingizwa ndani ya uterasi (IUD): Mirena

Chombo hiki utiwa ndani ya uterasi na utoa kiwango kidogo cha progestogeni. Inafaa kwa kipindi cha
miaka mitano.
• ingawa kunaweza kuwa hedhi isio ya kawaida na/ao yenyekutoka kwa matoni mwanzoni, chombo
ufanya damu kuwa nyepesi zaidi na uweza kusimamisha haya yote
• kuna hatari ndogo kwa maana kiwango cha hormoni ni kidogo na utumika ndani ya uterasi
• hasara ya maambukizo ni ndogo, kutoboka kwa uterasi, kutikisika ao kufukuzwa kwa chombo
• inaingizwa na bahadhi ya waganga (GPs), wanajikolojia (kupitia uhamisho) na wadaktari wa SHine SA

Mbinu zingine

Vyombo vinavyoingizwa ndani ya uterasi IUD): Multiload and Copper T

Chombo kinatiwa ndani ya uterasi. Kinahathiri maendeleo ya chembechembe za kiume na kuzuia
upandikizaji wa yai.
• Shaba nyekundu (Copper T) inafaa kwa kipindi cha myaka mitano na Multiloadi ufaa vilevile kwa kipindi
cha myaka mitano.
• hedhi inaweza kuwa nzito na maumivu zaidi
• hakuna hormoni, kwa hiyo hakuna mazara yanayoambatana na hormoni
• inaingizwa na bahadhi ya waganga (GPs), wanajikolojia (kupitia uhamisho) na wadaktari wa SHine SA

Mpira (condom)

Ala nyembamba ya mpira unaovikwa kwenyi uume unaosimama kabla ya tendo la ngono ili kuzuia mimba.
Mpira pia upunguza hasara ya uambukizaji wa magonjwa ya zinaa.
• Ni maafaa zaidi inapotumiwa ikiwa na mafuta yake kwa kuzuia msuguano na kupasuka
• Inapatikana kwenye maduka yote, duka za madawa, vyombo vya kuuzia vipatikanavyo kwenye vyoo vya
watu wote, na kliniki ya SHine SA

Kiwambo

Chepeo ya mpira wa kubana yenye hali nzuri inayotiwa juu ya mlango wa uzazi na inaweza kutumiwa
pamoja na dawa iitwayo spermicide.
• inapashwa kuchomekwa kabla ya tendo la ngono na kuziacha hapo kwa muda wa karibuni saa sita
mbele ya tendo.
• Inaingizwa kawaida kwenye kliniki ya SHine SA au na bahadhi ya wa daktari (GPs)

Mpango wa uzazi wa kawaida

Mbinu za kucheki kutaga kwa mayai

Mbinu hizi utegemea kwa kuchagua kutenda ngono kwenyi vipindi vya mwezi ambapo akinamama hana
rutuba kwa kuepuka mimba.
• akinamama anaitaji kucheki duru yake mwenyewe
• mbinu hizi zinajumuisha ushirikiano na elimu kwa wapenzi wote

Kusimama kwa hedhi kwenyi kipindi cha kunyonyesha

Kwenye kipindi cha kunyonyesha, mabadiliko za hormoni usimamisha hedhi na kutagwa kwa mayai kwenyi
mwili wa mama. Hii inafaa tu ikiwa kama mama ataendelea kunyonyesha kwa kawaida mchana na usiku (bila
kumlisha mtoto chakula cha aina yoyote), hawezi kupata hedhi kabla ya mtoto kuwa na umri wa myezi sita.
Akina mama wanaonyonyesha wanaweza pia fikiria utumiaji wa mbinu nyingi ziliomo ndani ya maandishi
haya kwa kupunguza hasara za mimba. Ujadiliane na mganga wa familia yako (GP) ao daktari wa Shine SA.

Utowaji (hakuruhusiwi)

Utowaji ni kuondoa uume kwenye uke baada ya kumwaga shahawa (cumming).
Hii sio ya kutumainia kwa maana shahawa inaweza kuwa imefika kwenyi kichwa cha uume.

Mbinu za kudumu

Uzuizaji wa uzazi: kufunga uzazi kwa wanaume

Upasuaji kwa kufunga njia inayochukua shahawa kutoka kwenyi mapumbu, ili shahawa zisiweze kufika
kwenye kichwa cha uume.
• utaratibu ufanyiwa kabla ya kudungwa anestezia ya mahali panapolengwa ao ya mwili mzima
• Unastahili kumuona daktari wako (GP) kwa uamisho kwa mpasuaji
• mafaa yake siyo ya nyakati ile ile, inaomba karibuni umwagaji 20 wa shahawa kabla ya mafaa yake
kujitambulisha
• inafikiriwa kuwa ya kudumu

Uzuizaji wa uzazi: kwa wanawake

Huu ni utaratibu unaoziba njia kwa kuzuia shahawa kukaribia yai. Huu unaweza kutekelezwa kupitia njia
mbili. Usafishaji wa tyubu ni utaratibu ambao njia zinafungwa mara nyingi kwa kutumia kudira ao pete,
kupitia kudungwa anestezia ya mwili mzima. Essure ni utaratibu wa kuingiza kamani nyepesi kwenyi tyubu,
na anestezia ikidugwa hapo panapolengwa.
• Unastahili kumuona GP wako kwa kupata uamisho kwenda kwa jenikolojia
• Uzuizaji wa uzazi kupitia tyubu hutumika hasa kwa kupasua, alakini manufaa yake ni ya palepale
• Essure haigeuki na hudumu myezi mitatu kabla ya kuleta manufaa

Rejea

Site Web www.shinesa.org.au

🙉🙉🙉Usisahau kushare posti hii kuhusu (# Njia za kuzuia mimba na kupanga uzazi).👍 Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasome💯✔

Marafiki zako mliopotezana wako hapa Wapo kukutafuta wewe uliyepotezana

👉SOMA ZAIDI HAPA...

tafuta-ndugu.gif

.