Njia za Kuzuia Mimba

By, Melkisedeck Shine.

Njia za uzazi wa mpango zinatofautiana sana na zinaweza kugawanywa katika makundi mengi:

Vizuizi

(hizi huzuia mbegu kulifikia yai): Kuna mpira wa kiume (kondomu ya kiume), yaani mfuko wa mpira uliozibwa upande moja. Unavishwa kwenye uume uliosimama kabla ya kuingia ukeni. Pia kuna mpira wa kike (kondomu ya kike), yaani mpira unaoingizwa ukeni kabla ya kujamiiana.

Vidonge vya kuzuia mimba:

Lazima mwanamke anywe vidonge hivi kila siku hata kama hajamiiani.

Njia nyingine za kuzuia mimba kwa muda mrefu

. Njia hizi hazihitaji maandalizi maalum, ili kuzuia mimba, kabla ya kujamiiana na pia mwanamke hahitaji kukumbuka kufanya chochote kila siku. Kati ya njia hizi ni pamoja na sindano anazopewa mwanamke kila baada ya miezi mitatu. Pili, kuna vipandikizi, yaani vijiti vyembamba vya plastiki vinavyowekwa kwenye sehemu ya juu ya mkono wa mama kwa njia ya upasuaji mdogo. Vijiti vina kichocheo kinachozuia kupevuka kwa yai. Pia, kuna kitanzi ambacho ni kitu kidogo kilichotengenezwa kwa aina maalum ya plastiki. Kwa ufupi kinaitwa IUD. Huwekwa kwa utaalamu ndani ya mfuko wa uzazi. Sindano, vipandikizi na vitanzi lazima viwekwe na mtaalamu mwenye ujuzi kwenye kituo cha afya chenye vifaa vya kutosha. Kwa vile dawa za kuzuia mimba kwa muda mrefu zinaingiliana na mzunguko wa kawaida wa hedhi kwa kiasi, athari zake ni kubwa kuliko kutumia vidonge.

Kwa mwanaume na mwanamke kuna njia ya kudumu ya kufunga kizazi kwa njia ya upasuaji

. Kwa mwanaume mirija inayopitisha mbegu hukatwa na kufungwa, ili kuzuia mbegu zisitoke. Akijamiiana, anaweza kumwaga shahawa, lakini ndani ya shahawa hakuna mbegu. Kama mwanaume amefunga kizazi uume utadinda kama kawaida na kufikia mshindo atamwaga maji ya shahawa ambayo hayatakuwa na mbegu. Kwa mwanamke mirija ya kupitisha mayai hukatwa na kufungwa, ili kuzuia mayai kufika kwenye mfuko wa uzazi. Baada ya upasuaji huu, mama ataendelea na hedhi kama mwanzo, lakini yai halitaweza kukutana na mbegu za kiume tena.

Vilevile kuna njia nyingine mbalimbali ambazo hazina uhusiano na matumizi ya dawa au vizuizi vya mimba. Njia hizi hazina uhakika mkubwa wa kutopata mimba. Mara nyingine mama anatumia ishara mbalimbali, au tarehe kujua lini anaweza kupata mimba, ili kuepuka kujamiiana katika kipindi hicho. Kumwaga mbegu za kiume nje ya uke, au kutegemea kwamba mimba hazishiki wakati wa kunyonyesha ni njia nyingine za asili zinazotumiwa. Kumbuka kwamba njia hizi hutumika sana, lakini si njia salama sana za kuzuia mimba wala kuambukizwa na magonjwa ya zinaa.
Ni muhimu kukumbuka kwamba njia ya uzazi wa mpango inaweza kufaa kwa mtu huyu na isifae kwa mtu mwingine. Kwa hiyo, ni vizuri kila mtu aliyeamua kupanga uzazi apate ushauri kwenye kliniki kuhusu njia inayomfaa zaidi


MPENZI-MLO-MWEMA-34NG.JPG

Endelea kusoma makala hizi zifuatazo;

a.gif mapenzi salama

Mapenzi salama ni yale yanayofanyika bila wasiwasi wa kupata mimba zisizotarajiwa, magonjwa ya zinaa pamoja na maambukizi ya virusi vya UKIMWI. Mapenzi salama yanaweza kuwa ni vitendo vya kumaliza hamu bila uume kuingizwa ukeni. Ngono ya kuingiza uume ukeni inaweza kuwa ngono salama kama tahadhari husika zinatumika.
Vitendo vya kumaliza hamu bila kujamiiana ni kupiga busu, kukumbatia, kunyonyana ndimi, kushikana mikono na kupiga punyeto. Matendo haya yote ni salama kabisa kuhusiana na mimba zisizotarajiwa na maambukizi ya virusi vya UKIMWI.
Ili kuhakikisha mnafanya mapenzi salama wakati mnahusisha mwingiliano kati ya uume na uke, lazima mchukue tahadhari. Tahadhari mojawapo ni uaminifu katika mapenzi, kwa maana wewe uwe mwaminifu na yeye awe mwaminifu. Lakini pia inabidi muwe na uhakika kwamba wote wawili hamjaambukizwa magonjwa wakati mnapojamiiana kwa mara ya kwanza. Tahadhari nyingine ni kutumia kondomu. Kondomu inazuia mimba pamoja na magonjwa ya zinaa. Kuwa mwaminifu pekee yake haitoshi kama mmoja wenu au wote wawili mliwahi kujihusisha na uhusiano wa kimapenzi ambao haukuwa salama. Kama kweli mnataka kuwa upande wa uhakika wote ni vyema kwenda kupima Virusi vya Ukimwi kwa hiari… soma zaidi

a.gif Je, kama mwanamke na mwanaume wanapata watoto wa jinsia moja tu, ni kosa la nani?

Hakuna mwenye kosa, kwa sababu jinsia ya mtoto i inategemea na bahati na hamna uwezekano wa kupanga kuzaa aina fulani ya mtoto. Tulivyoona juu ni mwanaume ndiye aliye na aina mbili za mbegu. Aina moja husababisha kutokea mtoto wa kike na aina nyingine mtoto wa kiume. Mwanaume hana uwezo wa kuhakikisha achangie aina ya mbegu gani. Kwa hiyo, hata kama ni mwanaume anayeyakinisha jinsia ya mtoto, hana kosa, kwa sababu hana uwezo wa kuamua achangie mbegu ya aina gani… soma zaidi

a.gif Inakuwaje mtoto anakuwa wa kike au wa kiume?

Mwili wa mwanaume unatengeneza aina mbili za mbegu. Kuna mbegu zinazokua kuwa mtoto wa kiume na kuna mbegu zinazokua kuwa mtoto wa kike. Ile mbegu inayofika kwenye yai kwanza, inarutubisha yai na ni wakati uleule, jinsia ya mtoto i inatokea. Uwezekano wa kumpata mtoto wa kike au wa kiume unafanana, na hii ni kweli katika nchi zote duniani… soma zaidi

[Chemsha Bongo Kwako] 👉Je, hii familia ina watoto wangapi?

tafuta-rafiki.gif

a.gif Faida ya kupanda maharagwe katikati ya kabichi

Maharagwe yanapandwa kwenye kabichi yanafanya kazi zifuatazo;.. soma zaidi

a.gif Mahitaji na jinsi ya kupika uji wa ulezi kwa ajili ya watoto, wagonjwa na mtu yoyote

Uji wa ulezi ni kati ya vyakula vyenye nguvu na vinavyopendekezwa kutumiwa hasa kwa wagonjwa na watoto. Uji wa ulezi unapikwa hivi.. soma zaidi

a.gif Jinsi ya kupika Biryani ya mbogamboga

Biriani ni miongoni mwa vyakula ambavyo ni nadra sana kupikwa katika familia nyingi tofauti na vyakula vingine. Inawezekana ni kutokana na watu wengi kutoelewa namna ya kuoika chakula hiki kutokana na kuhitaji viungo vingi ambavyo huwapa usumbufu wapishi.
Kuna aina mbalimbali za upishi wa biriani ambapo mara nyingi hutofautiana kutokana na viungo vinavyotumika katika upishi.
Biriani la mbogamboga ni miongoni mwa aina hizo za upishi. Chakula hiki kinaweza kuliwa na kila mtu hususan wale wasiotumia nyama wala samaki… soma zaidi

a.gif Namna nzuri ya kuhudumia nywele zako za asili kirahisi

Kwa wale ambao tuna nywele asilia (natural hair), tayari tunafahamu changamoto kadhaa tunazokumbana nazo. Kwa wale mnaofikiria kuanza kuwa na nywele asilia, karibuni sana tuendelee kujuzana namna ya kutunza nywele zetu kama tulivyopewa na Mungu… soma zaidi

a.gif Ujumbe kwa wakina dada

Wasichana 2 waliwasili kwenye Kikao huku wamevaa nguo ambazo zilikuwa zikionyesha miili yao… soma zaidi

[Picha Nzuri] 👉Eti mapenzi ndo hivi?

[Jarida la Bure] 👉Jarida la kilimo bora cha kabichi

Usipitwe na Nafasi za kazi kwa leo

<<Bofya HAPA kujua zaidi>>

.

nn.gif
KADI-SALAMU-USIKU-MZAZI.JPG

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.