Kichekesho%20Kipya Usikose 📕Kitabu cha Mbinu za Kilimo Bora Cha Mboga🌿🍅 kwa punguzo kutoka Tsh 7000/= hadi Tsh 1500/= kwa leo tuu!.
👉<<Bofya hapa Kuoda>> Kizuri

.

👉 NGONO KABLA YA NDOA KWA MSICHANA

NGONO KABLA YA NDOA

Siku hizi ngono kabla ya ndoa hutazamwa na vijana wengi kama jambo la kawaida.Vijana wa kike na wa kiume hawahisi hatia yoyote ya kuwa na uhusiano wa kingono katika umri mdogo. Kwa kufanya hivi vijana hupoteza mwelekeo kwa kuishi kiholela bila ya kuwa na mwongozo unaongoza maisha yenye mafanikio sasa na baadaye. Uwezo, fursa na bahati ya vijana kwa ajili ya maisha bora hupotea bure. Vijana hufikiria kuwa ngono ndilo jibu na ufumbuzi wa hali ngumu wanayokabiliana nayo wakati wa balehe na kupevuka. Wengi wao hupungukiwa uwezo wa kutabili nini kitatokea baadaye kama matokeo ya ngono kabla ya ndoa.
Wasichana wanaojiingiza katika mahusiano ya kingono kabla ya ndoa na katika umri mdogo huweka rehani uaminifu, afya na uvumilivu wao wa hisia kuhusu mahusiano ya kingono wakati watakapo ingia ndani ya ndoa hapo baadaye.Vijana wengi hawaelewi kuwa ngono haramu huzaa wivu, tuhuma mbaya na majanga ya kijamii. Hufanya mwenzi kumfikiria msichana kuwa ana udhaifu wa kimaadili na hali hii hutia alama katika hisia za mwenzi kuhusu hali ya uaminifu wa mwenzake hasa pale anapokuwa mbali naye.
Tafiti kadha wa kadha huonyesha kuwa wasichana wasiothamini umuhimu wa kujitunza, kujilinda na kubakia waaminifu kabla ya ndoa, wana uwezekano mara dufu wa kufanya ngono nje ya ndoa baada ya kuolewa ikilinganishwa na wale wanaojitunza na kuanza ngono ndani ya ndoa. Uzoefu pia unaonyesha kuwa wasichana wengi wanaoanza ngono kabla ya ndoa, maisha yao ya baadae huwa magumu kutokana na kuacha masomo au kuzaa hovyo ovyo bila mpangilio. Wengi hujikuta wakizaa na wanaume wengi tofautitofauti na kusababisha malezi ya watoto kuwa magumu.
Wasichana wengi hufikiri kuwa ngono kabla ya ndoa ndio njia pekee ya kujenga na kudumisha uhusiano wa kimapenzi na wavulana. Hii si kweli na huenda msichana na mvulana wanaotamaniana kingono hutazamana kwa mitazamo inayotofautiana kabisa mara baada ya tendo la ngono. Ni vigumu kutabiri nini kitatokea baada ya mvulana kutosheleza tamaa yake ya ngono kwa mara ya kwanza.
Huenda mvulana akamwona msichana havutii tena kimahaba na kumchukia sana. Huenda msichana pia akapata athari za kisaikolojia na kupata hisia za kunyanyaswa kijinsia au kutumiwa kama chombo cha kustarehesha wanaume kingono. Na huenda akajichukia kwa udhaifu na kujirahisisha aliko onesha. Hii mara nyingi hutokea pale msichana anapokataliwa na mvulana baada ya kupata mimba.
Mbali na athari za kisaikolojia na kijamii, ngono katika umri mdogo kabla ya ndoa pia inazo hatari za kiafya katika mwili wa msichana. Tishio kubwa kwa wasichana ni maambukizi ya magonjwa kama vile virusi vya UKIMWI, kansa ya mlango wa mji wa mimba na magonjwa mbalimbali yaambukizayo kwa njia ya ngono.

Mikono.JPG

Magonjwa yanayohusiana na tendo la ngono

Magonjwa ya ngono ni maambukizi yanayosambazwa kwa njia ya tendo la ngono au kujamiiana. Magonjwa haya kwa karne nyingi yamejulikana kama nyororo la maangamizi au bomu la kibaiolojia. Hii ni kutokana na ukweli kuwa ukiona mgonjwa mmoja mwenye tatizo la ugonjwa wa kuambukiza kwa njia ya ngono basi ni muhimu kutambua kuwa kuna mtu mwingine nyuma yake ambaye ana tatizo hilo pia.
Kwa kawaida wasichana huwa katika hatari kubwa zaidi ya kupata magonjwa ya ngono kama watajiingiza katika vitendo vya kujamiiana. Sababu kubwa zinazowaweka katika hatari ni ile hali ya kushindwa kuamua namna ya kufanya ngono kwa tahadhari, maumbile ya kike kama mpokeaji na kutokukomaa kwa shingo ya mji wa mimba nazo ni sababu zingine zinazoongeza hatari.
Magonjwa mengi ya ngono husababishwa na bakteria, virusi, kuvu (fungus), protozoa na parasaiti. Magonjwa yasababishwayo na bakteri ni kama vile kisonono, mitoki (Granuloma inguinale na Chancroid), kaswende na klamydia. Magonjwa kama vile malengelenge (Herpes simplex), molluscum contageosum, viotea (warts), virusi vya UKIMWI na saratani ya mlango wa kizazi (HPV infection) haya hutokana na virusi. Magonjwa yasababishwayo na kuvu ni kama vile kandidiasisi ambayo huambatana na muwasho sehemu za siri. Magonjwa yaletwayo na protozoa kama vile Trikomoniasisi pia husababisha muwasho sehemu za siri na hutokwa kwa majimaji machafu yenye harufu mbaya hasa kwa wanawake. Upele na chawa wanaokuwa kwenye nywele za kinenani haya pia ni magonjwa ya ngono yanayosababishwa na parasaiti.
Dalili za magonjwa ya ngono hujitokeza kwa njia na dalili nyingi. Wakati mwingine magonjwa haya hayatokezi dalili zozote na pia mgonjwa anaweza kupata maambukizo ya magonjwa mawili au zaidi kwa wakati mmoja anapotenda tendo la ngono. Hatari kubwa zaidi inayoambatana na magonjwa haya ni kutokuwepo kwa dawa zinazotibu baadhi ya magonjwa haya kama vile UKIMWI.

Tafuta%20marafiki

Athari za magonjwa ya ngono kwa wasichana

Wasichana wengi wanaojihusisha na maswala ya ngono katika umri mdogo wanakabiliwa na ongezeko la uwezekano wa kupata saratani ya mlango wa mji wa mimba (cervical cancer). Shingo ya mlango wa mji wa mimba ambayo haijakomaa inapokutana na misukosuko ya ngono hudhoofika na kupoteza nguvu za kukabiliana na mashambulizi ya virus vya Human Papilloma – (HPV) ambao husababisha saratani hiyo mapema au baadaye sana.
Virusi hawa huambukiza kwa njia ya kujamiiana na wanaume hata kama mwanaume atakuwa amevaa kondomu wakati wa kufanya tendo la ngono na msichana. Saratani hii ni tatizo kubwa la kiafya linaloongoza kwa vifo vya wanawake vitokanavyo na ugonjwa wa saratani katika nchi zinazoendelea. Saratani hii kwa kawaida huwapata wanawake wengi ambao huanza kufanya tendo la kujamiiana katika umri mdogo, miaka michache baada ya kuvunja ungo.
Wasichana na wanawake wenye wapenzi wengi, au wenye wapenzi wa kiume ambao wana mtandao mkubwa wa wapenzi wengine wengi, huwa katika hatari kubwa ya kupata maambukizi ya virusi wanaosababisha ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi.
Kwa bahati mbaya sana wasichana wengi hupata maambukizi ya virusi hawa kwa kufanya ngono kwa mara ya kwanza, hata kama ni mara moja tu. Tatizo jingine kuhusiana na maambukizi ya virusi hawa ni kwamba, msichana anaweza kuishi na virusi hawa bila habari kwa miaka 10 hadi 15 hivi ndipo madhara yake yanapojitokeza kwa wazi.
Tatizo jingine linalowakabili wasichana wadogo wanaoendekeza ngono ni ugumba wakati watakapo hitaji kuzaa. Magonjwa mengi ya ngono hushambulia mirija ya uzazi na kusababisha mirija hiyo izibe. Mirija ya uzazi inapoziba, hushindwa kupitisha mayai kwa ajili ya kutunga mimba pale msichana atakapohitaji kupata watoto hapo baadaye.
Magonjwa ya ngono kwa wasichana pia husababisha maumivu makali na kuugua hasa pale tumbo la chini linaposhambuliwa. Msichana hupata ugonjwa wa mwanamimba yaani uambukizo katika mji wa mimba na wakati mwingine katika njia ya mkojo. Hii pia huambatana na maumivu makali wakati wa kukojoa.
Magonjwa mengine katika kundi hili la magonjwa mengi mbalimbali, husababisha madhara makubwa na ya muda mrefu. Kaswende inaweza kusababisha ugonjwa wa moyo na akili hasa pale msichana anapochelewa kupata matibabu sahihi. Magonjwa haya pia yanaweza kukaa mwilini kwa muda mrefu bila kuonyesha dalili huku yakiendelea kudhuru afya ya msichana.

Mikono.JPG

Jinsi ya kujikinga dhidi ya magonjwa haya

Njia bora na ya uhakika zaidi kwa wasichana kujikinga dhidi ya maambukizo ya magonjwa ya ngono ni kuachana na ngono katika umri mdogo na kabla ya ndoa. Uelewa juu ya magonjwa haya pia ni njia inayosaidia katika mapambano.
Kwa wasichana ambao hawajaanza kujamiiana na wanaume, wanaweza kupewa chanjo ya kuzuia maambukizi ya virusi wanaosababisha ugonjwa wa saratani ya mlango wa mji wa mimba ambayo ni salama. Chanjo hii haiwasaidii wasichana ambao tayari wamekwishaanza tabia ya kujamiiana na wanaume katika umri mdogo kwa vile mara nyingi huwa wamekwisha pata maambukizi.
Njia pekee inayosaidia wasichana ambao wamekwishaanza kujihatarisha kwa kufanya ngono mapema, ni kufanyiwa uchunguzi wa kitabibu katika vituo vya tiba za kisayansi ili kuona kuwa viashiria vya awali vya saratani vimeanza kujitokeza au la.
Uchunguzi huu hufanyika kwa kutumia kipimo cha mpako wa asidi ya Acetic na kuangalia - Viasual Inspection with Acetic Acid (VIA). Kama itagundulika kuwa msichana tayari amekwisha athirika kwa virusi hawa, atapatiwa matibabu kabla hajachelewa. Saratani ya mlango wa mji wa mimba inazuilika na kutibiwa kabisa iwapo itagunduliwa na kutibiwa mapema.
Tabia ya kuchangia nguo za kuvaa au taulo za kujifutia maji baada ya kuoga pia ikiepukwa, inasaidia kwa kiasi kikubwa katika kinga ya magonjwa haya. Magonjwa kama kaswende, kisonono, upele na mengine yanaweza kuambukizwa kwa urahisi kupitia njia hii ya kuchangia nguo, mavazi ya aina nyingine au matandiko.
Njia nyingine ya muhimu ni ile ya kuepuka vishawishi kutoka kwa wavulana na wanaume wasiojiheshimu. Vishawishi vya pesa, simu za mkononi, lifti za magari, vyakula kama viazi vya kukaanga maarufu kama chips na nyama ya kuku, mara nyingi hutumika kuwanasa wasichana wengi hasa wale wenye tamaa mbaya ya vitu na wenye uroho wa vyakula. Wengi husahau umuhimu wa maisha na masomo na huangalia vishawishi kama mafanikio, badala ya mtego yenye hatari kwa afya zao na maendeleo yao.
Kumbuka kuwa mazoea mabaya yakisitawishwa ni vigumu sana kuyaacha. Jitihada kubwa sana zinahitajika ili kuepuka mtego huu wa kufanya mapenzi na ngono katika umri mdogo. Jitahidi kwa kadri ya uwezo na nguvu zako zote za kimwili, kiroho na kiakili kupambana na hisia hasi kuelekea ngono hata kama ni vigumu, kwani huo ndio uamuzi sahihi na salama.
Jaza mawazo na hisia njema katika akili yako kila siku na kuepuka jambo lolote linalokupeleka katika mtego wa kuwazia mapenzi ya mahaba na ngono.Tamaa ya ngono inaweza kutawaliwa kwa mafanikio, kwani Mungu ameweka uwezo mkubwa ndani ya akili za wasichana ili waweze kujitawala. Na ushahidi wa jambo hili ni mwingi sana katika jamii za mataifa mbalimbali katika historia.
Epuka hadithi na liwaya za mahaba, magazeti ya udaku yanayosifia ngono, vipindi vya luninga (Televisheni) vinavyopamba mambo ya mapenzi na ngono kiufundi ili kuwavutia vijana. Epuka mitandao ya wavuti pamoja na mikanda ya video inayoonyesha picha za ngono na miziki inayochochea mapenzi na ngono. Nijambo la busara pia kuwaepuka marafiki pamoja na vijana wa rika lako wasiokuwa na maadili mema.
Wasichana wengi huondoa hofu na kujidanganya kuwa wanaweza kuonyeshana mapenzi na wavulana kwa kukumbatiana, kubusiana, kunyonyana ndimi na kushikanashikana sehemu za siri bila kufanya ngono. Hilo ni jambo la hatari, ni mbegu nzuri ambayo baada ya muda mfupi itazaa matunda ya ngono hatarishi.
Matendo hayo huamusha na kuchochea kwa nguvu sana hisia, tamaa mbaya na hamu kali ya ngono kwa wasichana na wavulana ambayo itawasumbua sana na baada ya muda mfupi sana watatumbukia ghafla katika mtego wa ngono hatarishi. Kanuni ya usalama ni kuepuka kuchezacheza na mambo ya hatari. Epuka kuchezacheza na bunduki yenye magazini iliyojaa risasi, kwani ni rahisi kufyatuka na kusababisha maafa makubwa.

Tafuta%20marafiki

Kondomu- Je ni kinga madhubuti?

Kondomu ni mpira unaovaliwa kwenye tupu ya mbele ya mwanaume au katika tupu ya mbele ya mwanamke wakati wa tendo la kujamiiana kwa lengo la kupanga uzazi au kusaidia kupunguza uwezekano wa kupata maambukizo ya magonjwa ya ngono. Kutokana na malighafi zinazotumika katika utengenezaji wa kondomu, kimsingi kondomu zinaweza kugawanywa katika makundi makuu matatu. Kuna kondomu zinazotengenezwa kwa mpira, kondomu zinazotengenezwa kwa plastiki laini na zile zinazotengenezwa kutokana na vibofu au matumbo ya wanyama.
Kondomu za mpira na zile za prastiki zina uwezo kwa kiwango fulani wa kuzuia maambukizi ya virusi vya UKIMWI na magonjwa ya ngono kama zitatumika vizuri na kwa usahihi. Kondomu zitokanazo na matumbo ya wanyama ni mahususi kwa ajili ya kupanga uzazi. Kondomu hizi hazina uwezo mkubwa wa kudhibiti maambukizi ya virusi vya UKIMWI.
Yapo magonjwa mengine ya ngono ambayo yanaweza kuambukizwa hata kama kondomu imevaliwa wakati wa kujamiiana. Magonjwa haya huambukiza kupita sehemu ambazo hazijafunikwa na kondomu pale zinapogusana na majimaji yanayotoka sehemu za siri hasa pale mmojawapo wa wahusika anapokuwa na michubuko itokanayo na kunyoa nywele za kinenani kwa wembe au jeraha. Mifano mizuri ya magonjwa haya ni kaswende na maambukizi ya virusi vinavyosababisha saratani ya mlango wa kizazi (Human Papilloma Virus)
Kondomu pia inaweza kupasuka au kuvulika wakati wa tendo la kujamiina ikiwa haikuvaliwa kwa usahihi. Wanawake wanaonyoa nywele za kinenani kwa wembe pia wanaweza kusababisha kutoboka kwa kondomu hasa pale nywele zinapoanza kuota tena. Nywele zinazoota huwa zina ncha kali na ngumu kiasi cha kuhatarisha usalama wa kondomu. Kondomu pia huwa dhaifu pale inapotumika kabla uke haujalainika vizuri wakati wa tendo la kujamiiana au pale muda wa matumizi ya kondomu unapokuwa umepita (expired).
Msichana asidanganyike wala asijidanganye mwenyewe kuwa matumizi ya kondomu yatamkinga na athari za magonjwa yote ya ngono. Ingawa kondomu ina uwezo kiasi fulani wa kupunguza maambukizi bado haiwezi kumkinga mtu yeyote kwa asilimia mia moja [100%]. Katika utafiti mmoja iligundulika kuwa kondomu ina uwezo wa kupunguza hatari ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI (VVU) kwa takribani asilimia 69 pekee. Hii ina maana kuwa kondomu inashindwa kuzuia maambukizi ya VVU kwa kati ya 15-31% [21].
Kondomu zingine zinazotumika wakati wa kujamiiana, hasa katika sehemu za vijijini, huwa zimekwisha poteza kiwango cha ubora kutokana na matunzo duni. Hivyo zinaweza kupasuka au kuchanika wakati wa tendo la ngono. Kwa vile wasichana wengi hawana uelewa wa kutosha juu ya matumizi sahihi ya kondomu, tatizo linaweza kuwa kubwa zaidi katika kundi hili. Hali hii kwa hahika husababisha kondomu kupoteza sifa ya kuitwa kinga madhubuti.

Wazo la ngono salama

Usalama wa ngono hautokani na kutumia kondomu. Tendo la ngono kabla na nje ya ndoa halikubaliki kimaadili bila kujali kuwa kondomu imetumiwa au la. Hivyo basi kufanya ngono huatarisha afya ya msichana yeyote anayejihusisha na ngono kabla ya ndoa na katika umri mdogo. Hatari za kisaikolojia haziepukiki kwani kondomu haiwezi kuzuia athari hizi za kihisia zitokanazo na kuvunja kanuni za kimaadili katika jamii.Kondomu haina uwezo wa kumkinga mtu dhidi ya huzuni na hisia za hatia anazopata mtu kutokana na kufanya kitendo kisichokubalika kimaadili.
Ngono itakuwa salama pale tu itakapozingatia makusudi yake ya awali, yaani ndoa, ambayo kimsingi ni mkataba wa kisheria unaounganisha watu wazima wawili, mtu mke na mtu mume kwa hiyari yao ili waambatane kwa maisha yao yote yaliyobaki kama mume na mke kwa kuzingatia majukumu ya unyumba. Ngono yoyote inayofanyika nje ya ndoa au kabla ya ndoa haiwezi kuwa ngono salama, ni ngono inayohatarisha afya ya mwili, akili na roho za wahusika wa jinsia zote mbili.
Ngono hatarishi ni ile inayosababisha maumivu ya kimwili, kiafya na kisaikolojia mapema sana au baadaye sana. Ngono ya namna hii inawezekana ikasababisha maambukizo ya magonjwa ya ngono au kuwaingiza wahusika katika migogoro ya kisheria na kimaadili, ni ngono ambayo haizingatii umri sahihi, wakati sahihi, mahali sahihi, malengo sahihi na nia sahihi. Ni ngono inayofananishwa na mtoto njiti ambaye anazaliwa kabla ya wakati wake na kabla hajakomaa. Ngono hatarishi inaweza kusababisha mimba za utotoni, zisizotakiwa na zile zisizotarajiwa.
Ngono salama lazima izingatie matakwa ya sheria, maadili, haki za binadamu, ustaarabu na taratibu za jamii. Ngono salama inampatia uhakika kila mhusika kuwa yuko salama, inaleta hali ya matumaini ya kweli, burudiko la moyo la kudumu na kuondoa wasiwasi, woga, sonona na aibu.
Ngono salama huleta uponyaji dhidi ya msongo wa mawazo na kutia nguvu ya misuli. Kamwe haiwezi kuwa chanzo cha msongo, sononeko la moyo na majuto.Ngono salama inatokana na uhalali wake, upendo wa dhati na inazingatia ustawi wa elimu, afya, uchumi na maendeleo ya wahusika wote wawili sasa na baadaye. Msichana yeyote kabla hajaingia katika maswala ya ngono inampasa kujiuliza maswali yafuatayo:-
• Je? Umri wangu unaniweka katika hali ya usalama nitakapofanya ngono?
• Lengo na uamuzi wangu wa kufanya ngono je ni sahihi?
• Ni matokeo gani chanya au hasi yanayoweza kutokea nitakapofanya ngono katika umri nilionao?
• Je najua kwa hakika kuwa kondomu haiwezi kufanya ngono kuwa salama?
• Je nimeamua mwenyewe kwa dhati au nimeshinikizwa kufanya ngono?
• Je nina taarifa za kutosha na sahihi kuhusu ngono zinazoniwezesha kufanya maamuzi sahihi na yenye manufaaa?
Imewapasa wasichana kutambua kuwa kiumbe mwenye hatari zaidi duniani kwa maisha na usalama wa afya ya msichana, ni mwanaume mwenye tamaa ya ngono haramu na isiyokuwa salama.

Mikono.JPG

Kujidhibiti dhidi ya ngono hatarishi

Kutokana na utandawazi, maendeleo ya sayansi na teknolojia na ongezeko la uhuru wa vyombo vya habari, mashambulizi na ushawishi wa jamii kujihusisha na ngono vimeongezeka maradufu kiasi kwamba wasichana na vijana wasiokuwa na taarifa sahihi na msingi imara wa kimaadili wanashindwa kusema ‘ hapana’ kwa urahisi zaidi dhidi ya ngono kabla ya ndoa. Ili vijana waweze kukabiliana na mivuto potofu inayohatarisha afya, vijana hasa wasichana imewapasa kuchagua maisha na kukataa kubanwa kwa kujenga nidhamu binafsi kwa ajili ya mafanikio yao ya sasa na baadaye.
Watangazaji na mashabiki wa ngono haramu na hatarishi wanaweza kuchapisha picha na matangazo yao ya kusisimua lakini hawawezi kutulazimisha kuziangalia au kuzinunua. Watunzi wa muziki wanaosifia ngono haramu kwa nyimbo na vyombo vilivyopangiliwa vizuri wanaweza kutunga nyimbo nyingi sana lakini hawawezi kutulazimisha kuzisikiliza au kuziangalia picha zao.
Kila mtu Mungu amemuumba na kumpa uwezo wa kujidhibiti ndani yake. Kinachohitajika ni kuufanyia mazoezi uwezo huo kila siku ili uweze kuongezeka zaidi. Imetupasa kuchukua hatua na kubeba jukumu la kujidhibiti wenyewe dhidi ya chochote kinachotuvuta ili kututumbukiza katika shimo la ngono hatarishi na tabia zingine zisizofaa. Hatuna sababu za msingi za kutufanya tushindwe kuwajibika kikamilifu na kutafuta visingizio vya kuhalalisha udhaifu wetu wa kimaadili.
Tuamue wenyewe yale tunayoyataka kusikiliza, kuona, kugusa, kuonja, kusoma na tutakayoyawaza. Na yote hayo yalenge kutoa mchango kwa ajili ya mafanikio ya kweli na ustawi wetu wa mwili, akili, moyo na roho. Tafakari yetu ya kila siku maishani isivuke mipaka ya mambo yale yanayofaa.
Kujidhibiti ni kuweka utashi wa tabia njema katika vitendo na kuishughulisha akili kwa mawazo chanya. Utashi huzaa vitendo, vitendo huzaa tabia, hivyo basi tabia yoyote ile iwe mbaya ama njema ni mjukuu wa utashi. Imetupasa kuwa wenye busara na kuepuka mabaya ili tusijeumia kama wajinga. Huu ndio ushauri wa mwenye hekima Mheshimiwa Suleimani Daudi, mfalme wa Israel ya kale [22]. Waswahili husema kuwa ‘kata pua uunge wajihi’ maana ya usemi huu wenye hekima za wahenga wetu ni kwamba kupata mambo mema si kazi rahisi, kunahitaji kujitoa mhanga na uvumilivu.

Faida za kiafya za ubikira na kugunga

Bikira ni msichana au mwanamke ambaye tangu kuzaliwa kwake amejitunza na kujilinda kimaadili dhidi ya mahusiano ya kingono kabla ya ndoa. Kinachoamua hali ya ubikira wa msichana au mwanamke ni ile hali ya dhamira na nia yake ya ndani ya moyo ya kujiheshimu na kuheshimu maadili ya mila, utamaduni na dini dhidi ya ngono haramu.
Ubikira ni uamuzi mugumu lakini salama kwa msichana binafsi na jamii kwa ujumla. Mila hii ya kale zaidi imetoa ulinzi na faida nyingi kwa vizazi vilivyopita. Ingawa katika ulimwengu wa leo wasichana bikira ni watu adimu, lakini ukweli ni kwamba wapo wasichana waaminifu wachache wanaodumisha mila hii yenye manufaa makubwa katika nyanja zote za kiafya.
Kupoteza ubikira kunaweza kuonekana kama jambo jepesi lakini adha na athari zake kwa afya ya mwili, akili, roho na jamii ni kubwa kuliko msichana anavyoweza kufikiria. Msichana anayedhibiti tupu yake ya mbele pekee ili isiingiliwe kwa kujamiiana na mwanaume, huku akiruhusu sehemu zingine za mwili wake kwa hiyari zitumike kwa kusudi la kutimiza tamaa ya ngono aidha na mwanaume au mwanamke mwenzake kabla ya ndoa, hupoteza ubikira wake.
Hali kadhalika, ni busara kukumbuka kuwa, ngono yoyote bila ridhaa ya mwanamwali au mwanamke (mfano kubakwa) haiwezi kumwondolea ubikira wake kwani ubikira ni swala la kimaadili. Ni usafi wa dhamira na mawazo dhidi ya ngono haramu.
Kwa kutambua umuhimu wa ubikira katika afya ya msichana na taifa, serikali ya Marekani (USA), hutumia mabilioni ya dola za kimarekani ili kufundisha wasichana juu ya kugunga na kuhifadhi ubikira wao. Tokea mwaka 1996 hadi 2008 serikali hiyo ilitumia USD 1.5 billion, na mwaka 2008 pekee dola za kimarekani million 50 zilitengwa kwa kazi hiyo [23]
Ukweli ni kwamba ubikira na kugunga huleta faida nyingi za kiafya kwa msichana mwenyewe na kwa jamii.Baadhi ya faida za ubikira na kugunga kwa wasichana ni pamoja na :-
• Kujikinga dhidi ya magonjwa mengi yanayotokana na kujamiiana ambako ni hatarishi na haramu, magonjwa hayo ni kama vile magonjwa ya ngono, uambukizo wa virusi vya UKIMWI na UKIMWI wenyewe, kansa ya shingo ya mlango wa kizazi na ugumba.
• Hupunguza uwezekano wa msichana kupata magonjwa ya akili. Anakuwa na utulivu wa mawazo unaompa fursa ya kushughulika na mambo muhimu ya maisha kama masomo na kazi kwa namna bora zaidi.
• Hudumisha afya ya kijamii ya msichana kwa vile mtindo wake wa maisha ya ubikira unaendana na matakwa ya jamii.
• Mahusiano ya msichana bikira na familia yake mara nyingi huwa bora.
• Wasichana wanofanya bidii kutunza ubikira wao hupata uwezo mkubwa wa kudumisha mahusiano yenye uaminifu katika ndoa zao pindi wanapoolewa na hii husaidia kupunguza uwezokano wa ndoa kuvunjika.
• Msichana anyedumisha mila hii ya ubikira safi huwa na uwezo mkubwa wa kuwajengea watoto wake maadili mema kuhusiana na ngono.
• Humwepusha msichana na hatari zinazotokana na mimba zisizotakiwa na zisizotarajiwa katika umri mdogo.
• Humsaidia msichana kuepuka migogoro ya kisheria na migongano ya kifamilia, hivyo ubikira ni siraha nzuri inayosaidia katika ulinzi wa amani na usalama.
• Ubikira huongeza thamani ya msichana au mwanamke katika jamii yake. Hii huongeza hali ya kujiamini na uchangamfu wa moyo unaodumisha afya ya mwili na akili.
• Huongeza uwezo wa msichana wa kusimamia vizuri mambo yenye faida na tija kwake binafsi, familia na jamii kwa ujumla. Huongeza uwezo wa kujiamini pia katika utetezi wa haki za msingi za binadamu.

Toaujumbe.JPG

📚Msomaji wangu mpendwa, leo nimekuandalia 📖 📕Kitabu cha Mbinu za Kilimo Bora Cha Mboga🌿🍅 ambacho nakupa kwa bei ya punguzo kutoka Tsh 7000/= hadi Tsh 1500/= kwa leo tuu! <<Bofya hapa Kuoda>>👈

🙉🙉🙉Usisahau kushare posti hii kuhusu; NGONO KABLA YA NDOA KWA MSICHANA.💯✔ Share facebook, twitter n.k bila kusahau WhatsApp!👍


🐼 Endelea kusoma kuhusu;-🙉

happy-dog-smiley-emoticon.gif

.

vichekesho.jpg
Kwa punguzo kutoka Tsh 6500/= hadi Tsh 1500/= kwa leo tuu!.
Jipatie 📕Kitabu cha Vichekesho Vikuu Vikali 300+✔ kwa Tsh 1500/= tuu.
jua%20zaidi%2C%20dont%20delete

.

MBINU-YA-KILIMO-BORA-CHA-MBOGA.jpg
Kwa punguzo kutoka Tsh 7000/= hadi Tsh 1500/= kwa leo tuu!.
Jipatie 📕Kitabu cha Mbinu za Kilimo Bora Cha Mboga🌿🍅 kwa Tsh 1500/= tuu.
jua%20zaidi%2C%20dont%20delete

.

📰 Posti nyingine👇

📌 Mambo ya kufanya mwezi Disemba

✍🏽MAMBO YA KUFANYA MWEZI HUU WA DECEMBA

👋soma zaidi kuhusu👉Mambo ya kufanya mwezi Disemba

📌 Elimu Kuhusu Madawa ya Kulevya, Mambo ya Msingi kujua Kuhusu dawa za Kulevya

Madawa ya kulevya ni aina ya madawa au vilevi ambapo mtumiaji akishatumia mfumo wa mwili na akili yake hubadilika. Mtumiaji huweza kudhoofika kimwili au kupata madhara ya kiakili na baadhi huweza hata KUFA.

👋soma zaidi kuhusu👉Elimu Kuhusu Madawa ya Kulevya, Mambo ya Msingi kujua Kuhusu dawa za Kulevya

📌 Unafikiri nini kilifuata??

DOGO: Mama Jana Baba Alikuja Na Mwanamke Na
Akaanza Kumtoa Nguo Huku Akimuita Beib…
BABA: Kwa Hasira Ebu Wacha Kuongea Na Chakula Mdomoni Wewe Mpumbavu Sana Khaa!!!
MAMA: Eti Nini Hebu Endelea Mwanangu Alafu
Wakafanya Nini Hawa Nguruwe… DOGO: Wakanza Kufanya Kama Vile Mlifanya Na Anko nassoro Wakati Baba Alikua Safari Za
kikazi…
MAMA: Kwa Hasira Babako Amesema Uwache
Kuongea Na Chakula Mdomoni We Kweli
Mpumbavu sana…

👋soma zaidi kuhusu👉Unafikiri nini kilifuata??

📌 KAMA WEWE UNGEENDELEA KURUSHA VOKO?

Siku moja katika pitapita zangu nikakutana na mtoto mmoja mkali baraa yaani ni mzuri sanaaaa, moyo ukanituma nimuimbishe mtoto akakubali kwamba nitafute siku tukae tuongee vizuri akasema nimpe namba yangu ya simu.
Ebwana si akatoa simu hiyo inauzwa laki sita mimi hapa nina kisimu cha tochi tena nimefunga na rababendi
Je, wewe ungeendelea kumtajia namba zako!!!

👋soma zaidi kuhusu👉KAMA WEWE UNGEENDELEA KURUSHA VOKO?

📌 Tofauti kati ya mwanamke na mwanamme

UTOFAUTI KATI YA MWANAMKE NA MWANAUME
1. Kwenye mshituko; mwanaume hushituka halafu huangalia nini kimemshitua, mwanamke hushituka halafu huzimia hivyo ataambiwa na mwanaume kilichomshitua😂😂
2. Kwenye kupenda; mwanaume huanza kutamani alafu hupenda, mwanamke huanza kupenda moja kwa moja bila kumjua vizuri huyo ampendae😂😂😂
3.Kwenye kusaidia; mwanaume hutoa msaada alafu uhuzunika, mwanamke huuzunika badae ndo anakumbuka km msaada unahitajika😂😂😂
4.Kwenye maamuzi; mwanaume hufikiri ndipo hutenda, mwanamke hutenda halafu hufikiri😂😂😂
5.Kwenye kudanganya; Mwanaume hudanganya ili kumlinda mwanamke, mwanamke hudanganya ili kumkomoa mwanaume😂😂😂
6.Kwenye ugomvi; wanaume hupigana halafu hueshimiana, wanawake hupiga mikelele alafu kila mmoja hurud kwake, kexho tena😂😂😂
7.Kwenye ndoa; mwanaume hutafuta maixha ndipo huoa, mwanamke huolewa ndipo atafute maisha😂😂😂
8.Kwenye kukata tamaa; mwanaume hukata tamaa mapema ili jambo lisimsumbue, mwanamke hajui kukata tamaa hadi aumizwe😂😂😂
9.Kwenye kula;Mwanaume hushiba alafu huanza madoido, mwanamke huanza na madoido alafu badae hujilaumu hakushiba😂😂
10.Kwenye siri; Mwanaume hutunza siri hasa za aibu, mwanamke humueleza shoga yake badae hugombana nae baada ya kumrudia mwenyewe kwa siku 2 tu😂😂😂
Hizi ni baadhi tu ya sifa tofauti kati ya mwanaume na mwanamke….. VIVA GENTLEMEN👊🏽👊

👋soma zaidi kuhusu👉Tofauti kati ya mwanamke na mwanamme

📌 Ushauri wang katika maisha

Kuna baadhi ya LEVEL huwezi kufika…Kuna MAFANIKIO huwezi kuyafikia…Kuna HELA huwezi kuzipata…Kama umezungukwa na watu BASIC…
Kuanzia asubuhi mpaka jioni wanaongelea WATU TU….Fulani kamegwa na yule……halafu yule naniliu saivi anatembea na yule ex wa nanii……Asubuhi mpaka jioni DISCUSSING PEOPLE…Hawa ndio watu BASIC…Hata siku 1 hawatakupa Ushauri kuhusu HOW TO REACH SOMEWHERE…NEVER
Na ukionekana unaanza kufanya vitu EPIC watakugeuka kwamba UNARINGA..UNAJISIKIA..UMEWATENGA…UNAJIDAI UNA HELA…and lots of negatives thoughts..
Pengine ulipaswa kuwa mbaaalii kibiashara lakini HUWEZI coz umezungukwa n Mbaazi tupu…BASIC PEOPLE…Ukiwaambia umesikia Kiwanja kinauzwa Kigamboni wanakwambia Kigamboni watu wanatapeliwa kuna mradi wa Joji Bushi…Ukiwambia unataka kujiunga GNLD wanakwambia UNALIWA HELA…Unaamini unaacha!…Nataka kufanya Kitu flani WANAKUKATISHA TAMAA
Unahitaji kuzungukwa na watu wenye POSITIVE ENERGY ambao ukiwambia unataka kwenda Mbinguni kwa kupitia Mkuranga wanakuchangia Nauli…ukisema naacha kazi watu ohh utakula nini..utaishije…Mji Mgumu huu..Wenzio wanatafuta kazi we unaacha ur losing it…WHO SAID??…NEGATIVE PEOPLE WILL BRING U DOWN….Ukitaka Kupaa kaa karibu na ndege…We unataka kupaa unakuwa rafiki wa Nyangumi…UNAZAMISHWA SASA HIVI!!
Positive people wakiona umefanya jambo wanauliza HOW DO WE ACHIEVE THIS na sio FULANI ALIWAHIFANYA HII AKAFELI..
Ikikusaidia Chukua..
ISOLATE ALL NEGATIVE PEOPLE AROUND YOU kama unataka kufikia Malengo Makubwa

👋soma zaidi kuhusu👉Ushauri wang katika maisha

📌 Wakaka hili lenu sasa!

Wakaka acheni ujinga, ukitaka dem wa peke yako mgharamie nakwambia wanawake asilimia kubwa hukumbuka fadhila za mtu anayemgharamikia kuliko wanaume zao, usidanganyike hakuna mwanamke asiyependa kuhongwa, kuna wanawake natural hawawezi kuomba, ila anakua anataka ujiongeze, sasa kama ww ni wale ambao akikwambia "baby kifurushi kimekata" unajibu "basi mumy pls ukiweka nicheki" umekwisha, anakueleza shida zake unasema "mpnz vumilia nakuombea upate kazi" kaka umeisha, ujue ulivokata simu umefatiwa na bonge la msonyo ka sio tusi, yani ww kama ni wale wa baby mwezi huu mambo yangu hayako sawa, nakuapia unagongewa, unamuona dem wako kasuka, kapendeza na hana kazi umekazana byb umependeza, we fala ujue mume mwenzio kaweka nguvu. so anapokua anatoa calendar za kukuona tulizana, service inakua kwa anayehudumia….hakuna dem wa siku hizi anayetaka kuambiwa nakupenda jumapili mpaka jumapili we mhonge tu uone heshima. foward kwa wakaka wote, inauma ila ndo ukweli.

👋soma zaidi kuhusu👉Wakaka hili lenu sasa!

📌 Jiamini na Amini unaweza

*AMINI UNA AKILI YENYE UWEZO MKUBWA WA KUBUNI WAZO LA KUWEZA KUKUSAIDIA KUFANIKIWA KIMAISHA.*

👋soma zaidi kuhusu👉Jiamini na Amini unaweza

📌 Ungekua wewe ni mwalimu ungemshauri nini huyu mwanafunzi?

Mwalimu aliingia darasani na kuwauliza wanafunzi juu ya ndoto zao za baadae.

👋soma zaidi kuhusu👉Ungekua wewe ni mwalimu ungemshauri nini huyu mwanafunzi?
dancing-guy-smiley-emoticon.gif

📓 Posti za sasa👇

A Huu mchezo hautaki makeup

mama mwenye nyumba anajipodoa anashinda saloon kujipodoa lakini house girl hata mafuta usoni hapaki lakini akipita na khanga yake moja tuu nyumba inatetemeka😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂 huu mchezo hautaki mekapu

👋soma zaidi kuhusu👉Huu mchezo hautaki makeup

A Angalia alichokifanya huyu mtu baada ya kuokota wallet ya thamani

Jamaa aliokota wallet, alipofika nyumbani akapiga simu kwenye radio station "naitwa Juma nimepiga simu kutangaza kuwa nimeokota wallet ndani ina laki7, ATM card na karatasi yenye PIN ya ATM card na kijimfuko cha dhahabu" Mtangazaji akasema, kwa hiyo ungependa kumrudishia mwenyewe kama anakusikiliza? Jamaa akajibu; hapana, ninaomba kumuombea dedication wimbo wa R.Kelly usemao "U SAVED ME" umfikie popote alipo!!

👋soma zaidi kuhusu👉Angalia alichokifanya huyu mtu baada ya kuokota wallet ya thamani

A Je, nikijamiiana na mtu mwenye virusi vya UKIMWI bila kutumia kondomu, nitapata virusi vya UKIMWI na UKIMWI?

Uwezekano wa kuambukizwa na Virusi vya UKIMWI na UKIMWI ukijamii ana na mtu mwenye virusi vya UKIMWI bila kutumia kondomu ni mkubwa.
Mpaka leo, kondomu ni njia pekee ya kuzuia kuambukizwaVirusi vya UKIMWI na UKIMWI wakati wa kujamii ana. Kama kondomu i inatumiwa i ipasavyo na kila unapojamii ana na mtu mwenye virusi vya UKIMWI, uwezekano wa kuambukizwa ni mdogo sana. Kutumia kondomu ipasavyo i i ina maana kutumia kondomu mpya, kuivaa vizuri uumeni na kuitoa kabla ya uume kulegea.

👋soma zaidi kuhusu👉Je, nikijamiiana na mtu mwenye virusi vya UKIMWI bila kutumia kondomu, nitapata virusi vya UKIMWI na UKIMWI?

A Chezea mgeni ww.!!!

Hata kama ni Mgeni this is too much.
Mwenyeji: Karibu mgeni karibu ukae,utapenda chai au soda?
Mgeni: Nipe nianze na soda wakati chai inachemka.
Mwenyeji: Utakunywa fanta au sprite?
Mgeni: Nipe fanta wakati sprite inapoa.
Mwenyeji: Utakunywa na keki au mkate?
Mgeni: Nipe keki mkate nitanywea chai ikishachemka.
Mwenyeji: Utapendelea ndiz au machungwa,
Mgeni: Nipe machungwa ndizi ntakula na wali
mchana.
Chezea mgeni ww.!!!

👋soma zaidi kuhusu👉Chezea mgeni ww.!!!

A Hizi hapa, Aina 10 za ndoa usizozijua

Inatokana na kufumaniwa na Binti wa watu.
Ndoa hii huwa Haina mahari. Hii huvunjika
mwaka mmoja tu,baada ya wanandoa kugundua
hawakuwa wakipendana!

👋soma zaidi kuhusu👉Hizi hapa, Aina 10 za ndoa usizozijua

A Sheria gani zimetungwa kuhusu ukeketaji?

Serikali zote na mashirika ya kimataifa wameweka mdhamana
na kukubali kulinda haki za binadamu. Tanzania imetia saini ya
mapatano na mikataba ya kimataifa inayohakikisha kuwa kila
mtu ana haki kwa afya na haki ya kuwa huru kutokunyanyaswa
kwa mfano katika Azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za
Binadamu.
Maazimio mengine yaliyoboreshwa ili kulinda haki za wanawake na
watoto,15 ni kama lile Azimio la Kuondoa Ubaguzi kwa Wanawake
na Azimio la Haki za Mtoto. Maazimio haya yanaeleza wazi kuwa
ukeketaji ni desturi mbaya na ni kinyume na haki za binadamu,
kinyume cha haki za mtoto na kinyume cha haki za afya kwa
wanawake. Na zaidi nchi nyingi za kiafrika wamepitisha sheria
kupiga marufuku ukeketaji.16 Hapa Tanzania, Bunge limepitisha
sheria maalumu ya Makosa ya Kujamiiana ya mwaka 1998 ambayo
inakataza ukeketaji kwa wasichana na wanawake vijana chini ya
miaka 18. Pia kuna sera17 ambayo inaelezea jamii kuondoa mila na
desturi kama vile ukeketaji kwa kuwa zina madhara kwa vijana.
Hivyo kama wewe ni msichana chini ya miaka 18 ni kosa la jinai
kufanyiwa tohara na pia ni kosa kwa mangariba kujishughulisha
na ukeketaji wa wanawake.

👋soma zaidi kuhusu👉Sheria gani zimetungwa kuhusu ukeketaji?

A Angalia huyu dogo alivyoingizwa mjini

Ndio nilikuwa nimeshuka kwenye basi la SAI BABA pale Ubungo, nina Begi kubwa Mgongoni na begi Dogo la Lap Top mkononi, sura inatazama Mbele Very Serious kama nipo kwenye Gwaride la Uhuru!..Mabega juu yanafanya Cheers na Mawingu!, natembea kwa madoido…..leo nimetoka Likizo Moshi,

👋soma zaidi kuhusu👉Angalia huyu dogo alivyoingizwa mjini

A Je, pombe inaweza kusababisha uitegemee?

Ndiyo, Kama nikotini, pombe huweza kukufanya mwenye busara
iwapo utakunywa, na ujiwekee kiwango maalumu cha kuinywa.
Mtu aliyetawaliwa na pombe anapotaka kuacha kunywa atakuwa
na dalili za upweke kama kutetemeka na wasiwasi.

👋soma zaidi kuhusu👉Je, pombe inaweza kusababisha uitegemee?

A Angalia huyu jamaa anavyojiona msomi, huyu kamuotea, hapa amekwama

USIJIONE MJUAJI SAAAA…NA.
Jamaa kamaliza chuo anarudi nyumbani kwa wazee, kufika
nyumbani. kwa furaha waliopata wazazi, mama aliamua
kurosti kuku WAWILI(2) kwa ajili yao.
Mezani jamaa akataka kuwadhihirishia kuwa yeye ni msomi,
akawaambia "hawa kuku unaona wako wawili ila kwa kutumia
sheria za arthematic na geometric kuna kuku watatu mezani"
mama"hee embu tuoneshe mwanangu"
jamaa akachukua kuku ya kwanza akainua juu "ngapi?"
wazazi"moja" akainua wa pili "ngapi?" wazazi "mbili"
akawarudisha akisema"wazee wangu nadhani japo shule
hamkwenda ila mnajua moja+mbili=tatu so tuna kuku watatu
mezani"
baba"mmh kweli mwanangu umesoma. SASA TUFANYE IVI
MIMI NACHUKUA KUKU MOJA NA MAMA YAKO WA PILI WE
UTAKULA UYO WA TATU ULIYOSEMA"

👋soma zaidi kuhusu👉Angalia huyu jamaa anavyojiona msomi, huyu kamuotea, hapa amekwama

A Je, kuna madhara gani usipooga baada ya kujamiiana?

Hakuna madhara yoyote ya msingi anayopata mtu asipooga baada ya kujamiiana. Isipokuwa kwa ajili ya kutunza usafi, mnashauriwa kunawa via vya uzazi mara baada ya tendo la kujamii ana.

👋soma zaidi kuhusu👉Je, kuna madhara gani usipooga baada ya kujamiiana?

A Je, ni kweli kwamba uvutaji wa bangi hukufanya uwe na nguvu?

Si kweli kabisa! Baada ya kuvuta bangi mtu hujiona kama jasiri sana na mwenye nguvu. Lakini madhara ya bangi ni kinyume na matarajio ya mtumiaji kwani mishipa husinyaa na ubongo hushindwa kufanya kazi zake vyema na kutoa uamuzi usio sahihi wa utendaji sahihi wa kazi za mwili.

👋soma zaidi kuhusu👉Je, ni kweli kwamba uvutaji wa bangi hukufanya uwe na nguvu?

A Kwa nini hairuhususiwi kuotesha au kuvuta bangi, iwapo kupanda na kuvuta tumbaku kunaruhusiwa?

Sheria ya Tanzania inaeleza dawa zilizo halali na zisizo halali.
Tumbaku imekubalika na jamii kwa muda mrefu, na ni katika
miaka kama hamsini iliyopita ndipo madhara yatakanayo na
nikotini iliyomo kwenye tumbaku yalipoanza kukubalika. Hata
hivyo, hadi sasa tumbaku ni halali, lakini ni bangi kwa upande
mwingine si halali kisheria Tanzania.
Kwa hivyo, kutokana na kwamba nikotini kwenye sigara
ina madhara, basi serikali ilichukua hatua ya kuanza
kuwatahadhadharisha wavutaji na kuwazuia vijana kuvuta sigara.
Kuna sheria mpya Tanzania ambayo inawalazimisha
watengenezaji wa bidhaa za tumbaku kuandika tahadhari
ya afya kwenye bidhaa wanazotengeneza na kuuza. Kuanzia
mwaka 2000 bidhaa za tumbaku zote zililazimika kuwa na onyo
kwamba “Uvutuaji wa sigara ni hatari kwa afya yako.”

👋soma zaidi kuhusu👉Kwa nini hairuhususiwi kuotesha au kuvuta bangi, iwapo kupanda na kuvuta tumbaku kunaruhusiwa?
pink-kitty-purring-hug-smiley-emoticon.gif

Majarida na vitabu kutoka Ackyshine eBook Shop

MBINU-YA-KILIMO-BORA-CHA-MBOGA.jpg
Kwa punguzo kutoka Tsh 7000/= hadi Tsh 1500/= kwa leo tuu!.
Jipatie 📕Kitabu cha Mbinu za Kilimo Bora Cha Mboga🌿🍅 kwa Tsh 1500/= tuu.
jua%20zaidi%2C%20dont%20delete

vichekesho.jpg
Kwa punguzo kutoka Tsh 6500/= hadi Tsh 1500/= kwa leo tuu!.
Jipatie 📕Kitabu cha Vichekesho Vikuu Vikali 300+✔ kwa Tsh 1500/= tuu.
jua%20zaidi%2C%20dont%20delete

.

happy-times-smiley-emoticon.gif
happy-times-smiley-emoticon.gif