Tafuta

Tazama ni marafiki wangapi wanaokutafuta Wengi wanaweza wakawa wanakutafuta lakini hujui

πŸ‘‰SOMA ZAIDI HAPA...

πŸ‘‰ NDOA NA MIMBA KATIKA UMRI MDOGOπŸ‘‡βœ”

NDOA NA MIMBA KATIKA UMRI MDOGO

Zipo sababu nyingi na ushahidi mwingi wa kisayansi, unaonyesha kuwa, ndoa na mimba katika umri mdogo wa msichana chini ya umri wa miaka 18 ni hatari kwa afya na mstakabali wa maisha yake na mtoto wake.Wasichana wengi wakati huu licha ya kuanza kupevuka wanakuwa hawajakomaa kiakili na uwezo wao ni duni katika maamuzi juu ya kufaa kwa mtu atakayekuwa mwenzi sahihi wa maisha.
Kimwili pia wasichana katika umri huu wanakuwa hawajawa tayari kuyakabili majukumu ya uzazi na unyumba, nyonga za wasichana wanaoendelea kukuwa mara nyingi huwa changa na finyu kiasi kwamba husababisha matatizo mengi ya uzazi wakati wa kujifungua kwa njia ya kawaida.
Wasichana wengi huchelewa kujifungua au huchukuwa saa nyingi za uchungu kabla ya kujifungua, hali hii inaweza kusababisha kifo cha mama au mtoto au wote wawili kama matibabu ya dharura ya upasuaji kwa ajili ya uzazi hayakufanyika. Idadi kubwa ya akina mama wanaojifungua kwa njia ya upasuji ni wale walio na umri mdogo.
Wasichana wanaopata ujauzito na kujifungua katika umri mdogo wengi wao pia hupata tatizo la fisitula - Vescovaginal fistula (VVF) au Rectovaginal fistula (RVF). Fisitula husababisha msichana kutokwa na haja ndogo au kubwa bila kujizuia. Haja kubwa pia inaweza kumtoka msichana kwa kupitia tupu ya mbele. Tatizo la fistula huharibu sana afya ya mwili na hisia za msichana.
Tatizo jingine linaloambatana na mimba katika umri mdogo ni pamoja na kutokwa na damu nyingi pale mimba inapoharibika au wakati wa kujifungua. Wasichana wengi hukabiliwa na tatizo hili ikiwa ni pamoja na kupata uambukizo wa bakteria katika njia ya kizazi pamoja na kupata kifafa cha mimba.
Wasichana wadogo mara nyingi huzaa watoto wenye uzito pungufu au njiti, watoto namna hii hukabiliwa na na hatari pamoja na changamoto nyingi za kiafya katika umri wao chini ya miaka mitano. Watoto wengi hupata matatizo ya mtindio wa ubongo na taahira ya akili. Wasichana wengi wanaozaa katika umri mdogo hupata hali ya aibu na hisia ya kudharauliwa mambo ambayo huongeza mzigo kwa wote mama na mtoto.
Wasichana wanao olewa au kupata mimba za utotoni hupeteza fursa na haki ya elimu. Wengi wao hufukuzwa shuleni au wazazi wao hupoteza imani kwao kiasi kwamba, husita kuwaendeleza kimaisha hata baada ya kujifungua, hali hii hufungua mlango kwa msichana kuingia katika umaskini na kuzaa ovyo bila mpangilio. Mzigo huongezeka pale msichana anapolea watoto peke yake kama hakubahatika kuolewa au kama ataachika baada ya kuolewa.
Wasichana wanaoolewa kutokanan na kukosa uwezo wa kukabili matakwa ya unyumba na majukumu yake, wengi hukabiliwa na unyanyasaji, ukatili pamoja na udhalilishaji wa kijinsia ndani ya ndoa. Wengi hupata vipigo vinavyo wasababishia ulemavu wa maisha au vifo.Wengi hutukanwa na kubezwa.Wengi hulazimishwa kuolewa na watu wenye umri mkubwa bila hata kupima damu kwa ajili ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI kabla ya ndoa.
Hali hii huwafanya wasichana wanaoolewa katika umri mdogo kukabiliwa na hatari ya kuambukizwa virusi vya UKIMWI na wengi huwa wajane kabla ya kuwa watu wazima. Wale wanaoachika huwa na uwezekana mkubwa wa kuachika tena pale wanapoolewa kwa mara nyingine. Hii hutokana na athari za kisaikolojia zinazowajengea wasichana hawa doa la kitabia katika jamii na kuwafanya wasione umuhimu wa kudumisha mahusiano ya ndoa kutokana na uzoefu mbaya walioupata katika ndoa za awali.

Mimba zisizotarajiwa na zisizotakiwa

Mara nyingi wasichana wadogo hawana elimu ya kutosha kuhusu muda wa vipindi ambavyo wanaweza kupata ujauzito. Wengi hujiona kuwa ni wajanja kiasi cha kutokupata madhila ya mimba lakini husahau kuwa ndege mjanja hunaswa na tundu bovu. Wengi wao pia kutokana na sababu mbalimbali za kibinafsi na za kijamii, hawapati fursa za kutumia huduma za afya ya uzazi wa mpango.
Wasichana wengi wanaojihusisha na ngono kabla ya ndoa hupata mimba zisizopangwa, zisizotakiwa na zisizotarajiwa. Jambo hili huleta mzigo mkubwa wa kihisia kwa msichana hasa pale anapokuwa mwanafunzi. Wasichana wengi wanaojikuta katika hali hii hufikiria kutoa mimba kama njia pekee ya ufumbuzi wa tatizo. Wengi hutoa mimba katika mazingira hatarishi na kwa njia zisizozingatia afya na usalama. Hii hutokana na ukweli kuwa, utoaji mimba ni kosa la kisheria na kimaadili katika nchi nyingi.
Wasichana wanaopata mimba hutangaza hadharani kuwa wao ni washiriki wa ngono hatarishi ambayo inaweza kumsababishia mtu maambukizi ya virusi vya UKIMWI na magonjwa mengine hatari. Hivyo basi kutoa mimba hakumhakikishii msichana usalama maana wakati wa ngono zembe anaweza kupata maambukizi ya virusi vya UKIMWI pia ambavyo huwa havitoki kwa njia ya kutoa mimba.
Utoaji mimba hata hivyo huambatana na hatari nyingi kwa afya na maisha kwa ujumla wake. Utoaji mimba unaweza kusababisha hali ya kutokwa na damu nyingi kiasi cha kupoteza maisha, kutoboa mfuko wa mji wa mimba, uambukizo hatari wa mji wa mimba, ugumba, matatizo ya kisaikolojia na migogoro ya kisheria.
Kutoa mimba pia huambatana na matumizi ya rasilimali za mtu binafsi na zile za umma kwa namna ambayo huchangia kuongezeka kwa umaskini. Gharama za kuhudumia msichana aliyepata athari za utoaji mimba ni kubwa na huduma hizi hutumia muda na rasilimali nyingine ambazo zingetumika kuhudumia wangonjwa wengine.

Watoto wanaozaliwa na watoto wenzao
Wasichana wengi wanaopata watoto katika umri mdogo, hukabiliwa na tatizo la kulea watoto peke yao kwa vile wengi huwa hawajaolewa. Na hata kama wataolewa, wengi huachika mapema. Wengi wao hawana maandalizi kwa ajili ya ndoa na majukumu ya kutunza watoto.Watoto wengi wa akina mama hawa hupata matatizo ya kihisia hasa pale wasipowaona baba zao pale nyumbani kama ilivyo kwa watoto wenzao. Jambo hili huwasababishia athari ziambatanazo na huzuni, fedheha, msongo wa mawazo, kuumwa mara kwa mara, kutofanya vizuri katika masomo yao, kukosa usingizi mara kwa mara na kukosa mapenzi ya baba.
Watoto wa kiume huathiriwa zaidi na hali hii kuliko watoto wa kike. Mtoto wa kiume hupenda kujifunza majukumu ya ubaba kwa kuiga yale baba yake anayoyafanya. Watoto wasiopata mfano mzuri wa kuiga toka kwa wazazi mara nyingi huchagua kuiga mambo mabaya kama vile uhalifu, uhuni na matumizi ya dawa za kulevya kama mbadala wa mambo sahihi waliyotakiwa kuyaiga kwa wazazi wao.
Wengi wa watoto waliozaliwa na kulelewa na akina mama wenye umri mdogo hukabiliwa na hatari nyingi na tabia zao hudhoofika. Wengi huwa wavivu, hukosa nidhamu na kukosa heshima hasa kwa wanawake. Watoto wa kike wanaozaliwa na akina mama wenye umri mdogo wao mara nyingi nao huzaa katika umri mdogo kama mama zao.
Watoto hawa mara nyingi hupenda kuwa na mahusiano na wanaume kama mbadala wa baba zao lakini pia wanaweza kuchukia wanaume na kutoona umuhimu wa kuolewa kwa namna ya kujiheshimu.Wengi wa watoto hawa hujenga chuki dhidi ya wazazi wao kutokana na kutotimiziwa mahitaji yao kama watoto wanaozaliwa na kulelewa ndani ya ndoa zenye upendo amani na utulivu.

Jinsi ya kuepuka mimba na ndoa za utotoni

o Kugunga (kujinyima ngono ili kupata afya na usalama) kabla ya ndoa, ndiyo njia salama na yenye uhakika zaidi kuliko njia nyingine yeyote inayomsaidia msichana kuepuka na kuzuia mimba za utotoni. Njia hii ilitumiwa na wasichana wengi wa vizazi vilivyopita na kuwaletea mafanikio mengi tena makubwa.
o Wasichana ni lazima wawe na stadi za maisha zinazowawezesha kufanya maamuzi bora na sahihi, wajiamini na kuachana na ngono hadi watakapokuwa wamekomaa kwa ajili ya kukabiliana na majukumu ya unyumba. Balehe ya wasichana hufananishwa na kukomaa kwa tunda ambalo halijaiva tayari kwa kuliwa. Balehe ni maandalizi ya awali ya kuwa mwanamke.
o Ni haki ya msingi ya mwanamke kufanya ngono ndani ya ndoa yake katika kipindi chote cha maisha yake. Hivyo hakuna haja ya wasichana kuwa na haraka, kila jambo lina wakati wake, kuna wakati wa tunda kupevuka lakini likiendelea kuwa bichi na kunawakati tunda hukomaa na kuiva tayari kwa kuliwa bila kuleta madhara.
o Ingawa kuachana na ngono kabisa ni jambo zito kwa wasichana wengi wa kizazi kipya kutokana na shinikizo la utandawazi, lakini bado inawezekana. Kinachohitajika ni kuwa na sababu za msingi za kuacha na kusubiri pamoja na kujizoeza kusema hapana. Kwa wasichana wengi ni vigumu kukabiliana na msukumo wa marika wao wa kuwa na maamuzi yanayotofautiana na wasichana wengine wengi, lakini ni muhumu kufanya maamuzi ya kibinafsi yatakayo kufaidia wewe mwenyewe.
o Ipo haja ya kuwajulisha wenzako msimamo wako hata kama utaonekana mshamba. Ni bora kuwa mshamba ukiwa salama kuliko kuwa jogoo wa mjini bila manyoa wakati wa baridi. Msichana anatakiwa kutumia kichwa chake badala ya vichwa vya wasichana wengine, ni busara kukumbuka kuwa, msingi wa maisha mazuri ya kesho hujengwa leo.
o Mungu ameweka uwezo ndani ya kila msichana wa kuamua kwa uhuru ili apate mtoto kwa wakati ufaao. Kinachotakiwa ni kuwa na msimamo na uelewa wa umuhimu wa kupata mimba kwa wakati unaofaa na salama.

 

πŸ™‰πŸ™‰πŸ™‰Usisahau kushare posti hii kuhusu (NDOA NA MIMBA KATIKA UMRI MDOGO).πŸ‘ Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasomeπŸ’―βœ”

Kutana na marafiki zako wa enzi hizo hapa Wewe ni miongoni mwa rafiki yao wa kipekee sana

πŸ‘‰SOMA ZAIDI HAPA...

Slide3-mliopoteana.GIF

.