Tafuta

Kutana na wale mliosoma pamoja Bado wanakumbukia urafiki wa Kishule shule

πŸ‘‰SOMA ZAIDI HAPA...

πŸ‘‰ MSONGO WA MAWAZO NA MFADHAIKO WA AKILI KWA MSICHANAπŸ‘‡βœ”

MSONGO WA MAWAZO NA MFADHAIKO WA AKILI

Wasichana pia kama ilivyo kwa watu wengine, hukabiliwa na msongo wa mawazo na mfadhaiko wa akili. Msongo na mfadhaiko ni sehemu ya maisha na siyo rahisi kuvikwepa. Msongo wa mawazo ni mwitikio wa akili na mwili ili kukabiliana na hali ya hatari au hali ngumu..
Kwa kawaida msongo wa mawazo na mfadhaiko wa akili hutokana na tafsiri hasi ya akili ya mtu kwa jambo lolote linapompata au analowazia kuwa litampata. Kwa wasichana wa kizazi kipya vyanzo vya msongo na mfadhaiko wa akili vinaongezeka.
Wanafunzi wanaposhinikizwa sana kufaulu masomo hutumia muda mwingi kukaza sana fikra zao juu ya kazi za shule na kukosa usingizi wa kutosha. Mlundikano wa masomo mengi na kazi nyigi za kimasomo kama maandalizi ya wanafunzi kufaulu mitihani na kujitayarisha kwa ajili ya kupata kazi katika ulimwengu usio na ajira za kutosha, huongeza shinikizo, msongo na mfadhaiko kwa wasichana.
Wingi wa kazi za nyumbani au shuleni baada ya saa za masomo pia huongeza msongo kwa wasichana. Tatizo huwa kubwa zaidi pale msichana anapojiingiza katika maswala ya kimapenzi na mashindano ya kimaisha yasiyofaa. Urafiki usiofaa pia ni chanzo kingine cha msongo kwa wasichana.Upo wakati ambapo wasichana hutendewa vibaya au kufikiri kuwa wanatendewa vibaya na wapendwa wao kama vile wazazi, waalimu, ndugu, marafiki au wanafunzi wenzao. Hali hii pia huleta msongo, lakini pia upo wakati ambao wasichana wenyewe pia hulaumiwa kwa kuwakwaza wengine. Jambo hil pia huleta msongo na mfadhaiko wa kiakili hasa pale uhusiano wa kijamii unapokuwa mbaya.
Hali kama hiyo inapojitokeza msamaha huwa njia bora ya kutibu msongo. Kusamehe na kuomba msamaha huondoa maumivu ya kihisia, hasira na chuki. Msamaha ni mzuri kwa vile huwasaidia wote wanaohusika kuwa katika hali bora. Anayesamehe na anayesamehewa wote hurejesha afya ya kihisia.
Wasichana hawakabiliwi na msongo pamoja na mfadhaiko wa akili kwa ajili ya mambo yanayowanyima furaha pekee, bali pia yale yanayowafurahisha yanaweza kuzalishwa msongo na mfadhaiko. Jambo la muhimu kuelewa kuhusiana na shinikizo, msongo na mfadhaiko ni jinsi ya kukabiliana na maisha kwa mtazamo chanya.
Inatupasa kupata muda wa kupumzisha akili zetu na miili yetu. Mzigo hata kama ni mwepesi unaweza kukulemea kama utaubeba kwa muda mrefu bila kupumzika. Mapumziko na kupata usingizi wa kutosha, husaidia sana katika kukabiliana na athari za msongo. Mazoezi ya mwili pia ni dawa ya asili ya kupunguza msongo.
Msongo kwa wasichana usipodhibitiwa ili kubakia katika kiwango cha wastani, hutokeza matatizo ya kiafya. Inakadiliwa kuwa kati ya 75-80% ya magonjwa ya binadamu yanatokana na mashinikizo ya maisha kama vile woga, vitisho, mashaka, usumbufu nk.
Kwa wasichana wengi msongo wa mawazo na mfadhaiko hutokeza magonjwa kama vile maumivu ya kichwa, kutapika, kukosa usingizi, sonona, kusahausahau, kuchokachoka, kiherehere cha moyo na mapigo ya moyo kuongezeka. Msongo pia unaweza kusababisha ugonjwa wa β€˜hysteria’ na shinikizo la damu. Vidonda vya tumbo pia vinaweza kutokea kama mfadhaiko utadumu kwa siku nyingi.
Wasichana wengi hushindwa kupata damu ya hedhi kwa mpangilio mzuri kila mwezi kutokana na msongo. Msongo wa mawazo na kufadhaika pia hupunguza kinga ya mwili na kuufanya mwili wa msichana kupata magonjwa kwa urahisi.
Ili kujipunguzia mashinikizo na misongo ya kimaisha, msichana anayethamini afya yake lazima aepuke mambo mengi yasiyokuwa ya muhimu na kuwa na malengo yenye manufaa. Ni busara atumie muda wake, nguvu zake na rasilimali zake vizuri kwa ajili ya kufikia malengo bora.
Ni vizuri kukumbuka kuwa furaha na maisha bora havitokani na kupata vitu vya gharama kubwa, pesa nyingi, elimu nzuri, madaraka makubwa, umaarufu na urembo. Ingawa vyote hivyo ni vitu vizuri na vya muhimu lakini sio vitu pekee vinavyoamua furaha na ubora wa maisha, kwa sababu hiyo msichana hana haja ya kupata shinikizo kutokana na vitu hivi kiasi cha kufadhaika kiakili na kudhuru afya yake.

Ugonjwa wa hysteria

Hysteria ni ugonjwa unaotokana na tatizo la afya ya akili. Kihistoria ugonjwa huu ulianza zamani hata kabla ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo. Jina la ugonjwa huu lilitokana na mawazo ya madaktari wa zamani wa kigiriki waliokuwa wanafikiria kwamba, chanzo cha ugonjwa huu ni matatizo katika mfuko au mji wa mimba wa mwanamke, ambao kwa kigiriki unaitwa β€˜hystera’. Hivyo basi madaktari hao waliuita ugonjwa huu kwa jina la β€˜Hysterikos’.
Madaktari wa kigiriki walidhani kuwa huu ni ugonjwa unaowapata wanawake pekee. Hii ilitokana na idadi kubwa ya wagonjwa wa tatizo hili kuwa wanawake, na hata pale wanaume walipokuwa na dalili za tatizo la hysteria ilidhaniwa kuwa wana tatizo jingine kwa vile hawakuwa na mfuko au mji wa mimba.
Dhana ya madaktari wa kipindi hicho juu ya ugonjwa huu ilikuwa kwamba mfuko wa kizazi (mji wa mimba) unabana na kukauka kutokana na kutokufanya ngono kwa muda mrefu au kuzidiwa na hamu ya ngono. Matibabu ya enzi hizo yalihusisha kumtekenya mwanamke katika sehemu zake za siri ili apate kumaliza hamu ya ngono, lakini matibabu hayo yalikuwa hayatowi matokeo ya uponaji yaliyotarajiwa.
Dhana hii ya ugonjwa wa hysteria ingawa ni ya kale sana lakini inaonekana kusadikiwa na watu wengi hata leo. Hata hivyo, sayansi ya tiba ya binadamu imethibitisha kuwa hysteria ni ugonjwa wa akili unaotokana na msongo mkali wa kihisia, ni tatizo la afya ya saikolojia. Tatizo hili hutokea pale mtu anapopata msongo wa kihisia maishani zaidi ya vile alivyojiandaa au anavyoweza kukabiliana nao.
Mara nyingi msongo huu hutokanan na hisia au mgogoro wa kifikra, kutokuwa na uhakika wa usalama katika siku za usoni, kutengwa kijamii au kutosikilizwa kwa upendo.Tamaa kali ya kutaka kupendwa kuliko kawaida isipotimizwa, pia huleta tatizo hili pale mgonjwa anapoona kuwa ndani ya moyo wake hakuna akiba yoyote ya kupendwa.
Hysteria huibuka pale sehemu ya akili ndani ya ubongo inapojitahidi bila mafanikio kumlinda muhusika dhidi ya fikra na hisia zinazomsonga. Wakati mwingine hisia na fikra hutokana na matatizo ya kawaida lakini akili huyakuza sana na mhusika akajiona hawezi kuyakabili, hafai na hathaminiwi. Mgonjwa anaweza kujilaumu na kupata hisia za kupoteza ulinzi au kupata kumbukumbu isiyonyamazishwa ya tukio la kinyama alilotendewa.
Watu wanaopata ugonjwa wa hysteria huwa na matatizo ya kihisia ambayo mara nyingi hawapendi kuyazungumzia na kwa sababu hiyo matatizo ya kihisia huwalemea sana. Ingawa watu wa jinsia zote, wakubwa kwa wadogo, hupata tatizo hili lakini wagonjwa wengi ni wanawake hasa wasichana walio kati ya umri wa miaka 12 na18 huathirika zaidi.
Ugonjwa huu unaweza kumpata mtu mmoja pekee lakini pia unaweza kusambaa kwa wengine katika kundi la watu wanaokabiliwa na msongo wa kisaikolojia unaofanana (mass hysteria or hysterical contagion). Kichocheo cha hali hii huwa ni imani ya kuwa na tatizo au kupata uambukizo kutoka kwa mgonjwa wa kwanza.
Hysteria inayosambaa huanza na mtu mmoja na anapoonyesha dalili, wengine nao huanza kujenga hofu na hisia za kuathirika baada ya kuona mwenzao. Athari hizi katika kundi hutegemea jinsi mtu anavyo tafasri dalili anazoziona na uwezo wake wa kudhibiti msongo. Mara nyingi dalili za hysteria inayosambaa hazionyeshi chanzo bayana na hazitafasiriki sawasawa lakini zinaenea kwa haraka miongoni mwa walioona mgonjwa wa kwanza aliyepata tatizo.
Hofu huongezeka zaidi na tatizo husambaa zaidi pale linapoanza kuhusishwa na imani za kishirikina au mambo ya kimizimu, kupagawa na majini au pepo wabaya. Hofu huzidi pale timu ya wataalamu wa uchunguzi wa vyanzo vya magonjwa wanaposhindwa kubaini chanzo bayana cha tatizo.
Hysteria ingawa ni shida ya afya ya akili lakini pia hudhuru mwili kwa kiwango kikubwa. Hofu, woga na wasiwasi husababisha mapigo ya moyo wa mgonjwa kwenda harakaharaka, kutapika, kupata kichefuchefu, mwili kuishiwa nguvu, maumivu ya kichwa, miguu kufa ganzi, kushindwa kutembea, kupiga makelele au kucheka sana bila sababu za msingi au kupata degedege.
Wagonjwa wengine hupoteza hamu ya chakula, kutopata choo kabisa au kuharisha na wengine hutokwa jasho jingi, kutetemeka, kupumua kwa shida au kushindwa kupumua vizuri kiasi kwamba hewa chafu ya ukaa haitolewi mwilini kwa kiwango cha kutosha. Na hii husababisha kutokea kwa dalili nyingi za mgonjwa mwenye tatizo la hysteria.
Wagonjwa wenye tatizo hili pamoja na mambo mengine wanahitaji zaidi kuonyeshwa upendo wa dhati, kujengewa hisia zitakazowahakikishia usalama, kuaminiwa na kuwaondolea chanzo cha tatizo. Wengi hupata nafuu kutokana na uangalizi wa karibu, upendo wa dhati na dawa za usingizi.

πŸ™‰πŸ™‰πŸ™‰Usisahau kushare posti hii kuhusu (MSONGO WA MAWAZO NA MFADHAIKO WA AKILI KWA MSICHANA).πŸ‘ Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasomeπŸ’―βœ”

Slide1-mabest-skull.PNG

.