MSICHANA NA UPUNGUFU WA KINGA MWILINI

By, Melkisedeck Shine.

Afya ya mwili wa binadamu hutegemea kiwango cha kinga mwilini. Kinga ya mwili husaidia mwili kupambana na vimelea hatari vinavyo sababisha magonjwa. Mwili wa binadamu unaweza kupungukiwa na kinga yake kutokana na sababu mbalimbali.
Kutokana na ujio wa virusi vya UKIMWI mwanzoni mwa miaka ya 1980, sababu ya vyanzo vya upungufu wa kinga mwilini vinaweza kugawanyika katika makundi makuu mawili yaani upungufu wa kinga mwilini kutokana na maambukizo ya virisi vya UKIMWI na upungufu wa kinga mwilini bila maambukizi ya virusi vya UKIMWI.

Virusi vya UKIMWI (VVU)

VVU husababisha upungufu wa kinga ya mwili wa binadamu kutokana na mashambulizi yake dhidi ya chembe chembe nyeupe za damu na ‘tissue’ zingine zinazohusika na kinga ya mwili. Kwa kawaida chembechembe nyeupe zinazoshambuliwa VVU ni chembechembe saidizi za T (Helper T Cells – CD4+) na chembechembe aina ya B (B–Cells) pamoja na mfumo wa monocyte/ macrophage. UKIMWI ni upungufu wa kinga mwilini unaosababishwa na virusi vya UKIMWI (VVU).
Upungufu huu wa kinga ya mwili husababisha mwili kushambuliwa na magonjwa mengi ambayo hutokeza mkusanyiko wa dalili za magonjwa mbalimbali kwa mtu aliyeathirika kwa virusi hivyo. Kimsingi kuna aina kuu mbili za virusi vya UKIMWI – VVU 1(HIV 1) na VVU 2(HIV 2). Msichana au mtu mwingine anaweza kupata uambukizo wa aina zote hizi kupitia njia zifuatazo:
Njia ya ngono hatarishi: Ngono haramu na isiyo salama au ngono halali kisheria lakini isiyo salama kulingana na kanuni na taratibu za jamii, inafaa kujulikana kama ngono hatarishi. Ngono isiyo salama ni ile inayotendeka bila tahadhari dhidi ya maambukizi ya magonjwa na mimba zisizotakiwa, hivyo huhatarisha usalama na afya ya wahusika na watu wengine katika jamii.
Kugusana na damu au majimaji ya mwili yenye VVU: Hii inaweza kuwa kwa njia ya kuongezewa damu, kuchangia nyembe, sindano, miswaki au vifaa vya kutogea masiko nk.
Maambukizo kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto: Baadhi ya wasichana hupata maambukizi ya virusi vya UKIMWI kutoka kwa mama zao wakati wa ujauzito, wakati wa kuzaliwa au wakati wa kunyonyeshwa.
Ikilinganishwa na wavulana, wasichana wako katika hatari kubwa zaidi ya kupata maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa sababu zifuatazo:-
i. Maumbile ya viungo vya uzazi vya wasichana yanakuwa hayajakomaa hivyo wanapofanya ngono zembe (ngono hatarishi) hupata michubuko kwa urahisi. Wakati wa kujamiiana, uchi wa msichana unapokea virusi vingi vinavyokuwa katika majimaji ya mbegu za uzazi za mwanaume na kuvitunza kwa muda mrefu ikilinganishwa na mwanaume.
ii. Wasichana pia wako katika hatari ya kubakwa zaidi kuliko watu wengine kwa vile wana mvuto mkubwa kingono. Wasichana pia wanakabiliwa na ushawishi mkubwa wa kijiingiza katika ngono hatarishi kutokana na utegemezi wao wa kiuchumi na kutokukomaa kimaamuzi.
iii. Jambo jingine linalochangia wasichana kuwa katika hatari kubwa zaidi, ni mila potofu na kandamizi zinazochangia maambukizi ya virusi vya UKIMWI. Mila hizo ni kama vile ukeketaji na ndoa za utotoni ambazo zinawaathiri wasichana zaidi. Lakini pia wasichana wengi hawana taarifa, elimu na habari za kutosha juu ya swala zima la VVU/UKIMWI.

Njia zinazosaidia msichana kupunguza hatari ya kupata maambukizi ya VVU

• Kuepuka ngono katika umri mdogo na kabla ya ndoa.
• Kupata elimu ya UKIMWI na stadi za maisha.
• Kuepuka kugusana na damu au majimaji mengine ya mwili wa mtu mwingine.
• Kuepuka matumizi ya dawa za kulevya na pombe.
• Kusikiliza mashauri ya wazazi, walimu na viongozi wengine wa kijamii na kidini.
• Kuepuka mazingira hatarishi kama vile kutembea peke yako usiku gizani na mahali penye upweke.
• Kufanya kazi kwa bidii na kuchukia mapato ya aibu.
• Kuwa na elimu ya huduma ya kwanza.

Kuishi kwa matumaini

Msichana kama mtu mwingine yeyote anaweza kupata maambukizi ya VVU bila kutegemea tena kwa bahati mbaya hata kama amejitunza, kwani njia za maambukizi zipo nyingi. Wengi hupata maambukizi kwa sababu ya kubakwa au kulazimishwa kushiriki tendo la ndoa bila ridhaa yao.Wengine hupata maambukizi kama matokeo ya makosa yasiyotazamiwa wala kutarajiwa katika tiba.
Inapotokea msichana akawa na maambukizi ya VVU huwa anajikuta katika wakati mgumu, kijamii, kiuchumi na kihisia lakini anaweza kujifunza jinsi ya kukalibiana na hali yake na kuishi kwa matumaini. Hapa ushauri nasaha ni muhimu sana na kuwa muwazi kwa mtu wa karibu husaidia ili muathirika asibebe mzigo huu pekee. Ushauri nasaha humjengea mhusika uwezo wa kukabili msongo na hali ya kushuka moyo.Humpatia mbinu za kukabiliana na magonjwa nyemelezi na jinsi ya kupangilia lishe bora.
Kuwa na VVU haimaanishi kifo, wapo watu wengi wanaoishi maisha marefu wakiwa wameathirika. Kitu cha kufanya ni kuishi kwa matumaini na kufuata ushauri wa kiafya kutoka kwa wataalamu wa afya na lishe. Hii itasaidia kuishi kwa muda mrefu kati ya miaka 10-15 na kutimiza ndoto nyingi za maisha.Wakati kama huu ni vizuri kula mlo kamili, kuepuka ngono hatarishi kwako na kwa wengine, kunywa maji mengi, kufanya mazoezi, kutibu magonjwa haraka mara yanapojitokeza na kufanya ibada.

Upungufu wa kinga mwilini bila virusi vya UKIMWI

Mbali na Virusi vya UKIMWI yapo magonjwa mengine yanayoweza kusababisha upungufu wa kinga mwilini. Baadhi ya magonjwa hayo ni kama haya yafuatayo hapa chini.
Ugonjwa usiojulikana unaosababisha upungufu wa CD4+ mwilini (Ideopathic CD4+ Lyphocytopenia): Huu ni ugonjwa nadra ambao unasababisha upungufu wa kinga mwili bila kuwa na virusi vya UKIMWI (VVU). Mgonjwa mwenye tatizo hili hupata magonjwa nyemelezi kama ilivyo kwa mgonjwa wengine mwenye UKIMWI. Kwa kawaida ugonjwa huu hugunduliwa pale mtu anapoonyesha dalili za UKIMWI licha ya kuwa haonyeshi ushahidi wa kitaalamu wa kuwa na VVU pale anapopimwa kwa vipimo vya maabara. Pia mgonjwa huyu hana chanzo kingine cha upungufu wa kinga yake.
Sumu mwilini: Sumu mwilini husababisha kushuka kwa kinga mwilini. Sumu zinazopatikana katika vipodozi, mazingira machafu na hewa chafu kama vile nikotini ya tumbaku, lead, mercury, copper, zinc, nickel, cadmium nk ni hatari kwa afya.
Msongo wa mawazo: Msongo wa mawazo husababisha tezi ya Thymus inayozalisha kinga za mwili za CD4+ Thymus Lymphocytes isinyae na kuzeeka kabla ya wakati wake. Msongo wa mawazo pia husababisha uzalishaji wa vichocheo vya mwili vinavyodhuru kinga mwili.
Utapiamlo: Utapiamlo ni hali ya kupungukiwa na lishe bora au kuwa na unene uliokithiri kutokana na viini lishe kuzidi mwilini (obesity). Magonjwa kama kwashiorkor hutokana na upungufu wa lishe na huambatana na upungufu wa kinga mwilini. Magonjwa kama kisukari cha ukubwani huwa huwa na tatizo la kunenepa kupita kiasi.
Baadhi ya dawa za tiba: Dawa za tiba zenye kemikali pia zinaweza kuwa chanzo cha upungufu wa kinga mwilini kama zitatumika bila kufuata maelekezo na ushauri wa kitaalamu kwa usahii. Dawa kama Asprin, Predinisolon, dawa za kutibu kansa, dawa za mzio (Antihistamines) pamoja na dawa zenye homon kama progesterome na Oestrogen zinaweza kusababisha upungufu wa kinga mwilini. Dawa za kutibu mzio (antihistamines) na asprin huathiri chembechembe nyeupe za damu zisizalishe histaminin na kwa sababu hiyo hupunguza kinga ya mwili inayozalishwa na seli hizo.
Matibabu kwa njia ya upasuaji: Matibabu ya aina hii hushusha kinga ya mwili kwa takribani siku saba za mwanzo tokea upasuaji unapofanyika. Uzalishwaji wa chembechembe nyeupe ndani ya damu hupungua kufuatia upasuaji au upandikizaji wa viungo kama figo kwa mgonjwa toka kwa mtu mwingine. Hali hii husababisha uambukizo wa bakteria baada ya upasuji kufikia kati ya asilimia 5-20 hata kama upasuaji umefanyika katika hali ya usafi wa hali ya juu na kwa kutumia vyombo vilivyotakasika kikamilifu.
Mionzi: Mionzi kama vile X-ray na mionzi mingine inapotumiwa mara kwa mara au inapopenya ndani ya mwili kwa kiwango kikubwa hupunguza kinga ya mwili.
Uzee: Mwili unapozeeka uwezo wake wa kuzalisha kinga mwili hupungua pia ndiyo maana magonjwa nyemelezi kama vile mkanda wa jeshi (shingles) huwatokea wazee mara kwa mara kuliko vijana.
Ujauzito: Wakati wa ujauzito katika hali ya kawaida kinga ya mwili hupungua kidogo. Lakini hali inaweza kuwa mbaya kwa msichana nayepata ujauzito katika umri mdogo hasa pale hali ya lishe inapokuwa ya wasiwasi. Wasichana wengi katika kipindi hiki huwa hawana uwezo wa kiuchumi na huwa tegemezi hasa kwa wazazi ambao hawafurahii hali ya binti yao kuwa mjamzito kabla ya ndoa.
Magonjwa ya utumbo (inflammatory Bowel Diseases): Magonjwa haya hufanya viini lishe visisharabiwe na visichukuliwe kuingia mwilini pale tunapokula chakula. Kutokana na hali hiyo mwili hupungukiwa na lishe bora ambayo ni muhimu kwa uimarishaji wa kinga ya mwili pia utumbo hushindwa kusharabu chakula vizuri.
Kutumia sukari kwa wingi: Sukari inapoliwa kwa wingi huharibu utendaji wa vitamin B na C mwilini ambazo ni muhimu kwa utengenezaji na utendaji wa mfumo wa kinga mwilini.
Upungufu wa acid tumboni: Uyeyushaji mzuri wa chakula katika mfumo wa kupokea na kusaga chakula hutegemea sana kiwango cha acid/tindikali ndani yake. Upungufu mkubwa wa acid tumboni huathiri vibaya sana hali ya kinga mwilini.

Jinsi ya kuongeza kinga mwilini

Kunywa maji mengi: Kunywa maji mengi ambayo ni safi na salama angalau glasi 10-12 kwa siku ni muhimu kwa utendaji bora wa mfumo wa kinga mwilini. Chembechembe zote za mwili ikiwa ni pamoja na chembechembe zinazohusika na kinga ya mwili pamoja na ngozi laini za mwili (mucous membrane), huhitaji maji ya kutosha ili kufanya kazi zake vizuri.
Kuvuta hewa safi na ya kutosha: chembechembe nyeupe za damu zinazohusika na kinga mwili hufanya kazi zake vizuri pale zinapopata hewa safi na yakutosha.
Mlo kamili na lishe bora: vyakula vitokanavyo na matunda, mboga za majani, nafaka, kokwa na samaki pamoja na kupunguza mafuta yenye asili ya nyama na sukari katika mlo, huimarisha kinga ya mwili.
Kufanya mazoezi: Kufanya mazoezi kila siku angalau kwa dakika 30, huongeza kinga mwili kwa kuchochea uzalishaji wa endorphins, enkephalins, interleukin-1 na interferon zinazohusika na kinga ya mwili.
Kuepuka matumizi ya vileo: Pombe, sigara, ugoro na vinywaji vyenye kaffein- vitu hivi huathiri kinga ya mwili hasa utendaji wa chembechembe nyeupe aina ya T (T.Cells) na B (B-Cell). Kaffein pia huongeza uzalishaji wa kichocheo cha epinephrine ambacho huathiri kinga mwili pale kinapozalishwa kwa wingi.

[kitendawili Kwako] 👉Chakata kama kisu kikaIi

[chemsha_bongo Kwako] 👉Ni herufi gani tatu zinafuata baada ya hizi?

Endelea kusoma makala hizi zifuatazo;

a.gif NGONO KABLA YA NDOA KWA MSICHANA

Siku hizi ngono kabla ya ndoa hutazamwa na vijana wengi kama jambo la kawaida.Vijana wa kike na wa kiume hawahisi hatia yoyote ya kuwa na uhusiano wa kingono katika umri mdogo. Kwa kufanya hivi vijana hupoteza mwelekeo kwa kuishi kiholela bila ya kuwa na mwongozo unaongoza maisha yenye mafanikio sasa na baadaye. Uwezo, fursa na bahati ya vijana kwa ajili ya maisha bora hupotea bure. Vijana hufikiria kuwa ngono ndilo jibu na ufumbuzi wa hali ngumu wanayokabiliana nayo wakati wa balehe na kupevuka. Wengi wao hupungukiwa uwezo wa kutabili nini kitatokea baadaye kama matokeo ya ngono kabla ya ndoa.
Wasichana wanaojiingiza katika mahusiano ya kingono kabla ya ndoa na katika umri mdogo huweka rehani uaminifu, afya na uvumilivu wao wa hisia kuhusu mahusiano ya kingono wakati watakapo ingia ndani ya ndoa hapo baadaye.Vijana wengi hawaelewi kuwa ngono haramu huzaa wivu, tuhuma mbaya na majanga ya kijamii. Hufanya mwenzi kumfikiria msichana kuwa ana udhaifu wa kimaadili na hali hii hutia alama katika hisia za mwenzi kuhusu hali ya uaminifu wa mwenzake hasa pale anapokuwa mbali naye… soma zaidi

a.gif MAPENZI NA AFYA

Kwa binadamu maisha ni kupata uzoefu wa mapenzi na kujifunza kila siku kuhusu mapenzi. Mapenzi ni hitaji la msingi la kila binadamu tangu siku ya kwanza ya maisha hadi siku ya mwisho wa maisha. Mapenzi ni hitaji la vitoto vichanga, wavulana na wasichana, wanawake na wanaume, wazee na vikongwe, matajiri na maskini, watawala na raia wa kawaida.
Maumbile yetu wenyewe yanashuhudia kuwa sisi ni viumbe tusioweza kutenganishwa na mapenzi. Mapenzi yako ndani ya bongo na akili zetu, katika moyo na roho zetu, katika damu na nyama zetu na katika kila chembechembe yenye uhai inayotengeneza miili yetu.
Maisha yetu hapa duniani yanachomoza kutoka ndani ya mapenzi na yanajengwa juu ya msingi wa mapenzi. Raha ya binadamu kuishi duniani inategemea sana dozi ya mapenzi yaani kupendwa na kupenda. Mapenzi ndiyo ikulu ya maisha ya mwanadamu, ndicho kitovu na nguzo ya maisha, ndicho kichocheo cha furaha na afya. Mapenzi sio ubunifu wa binadamu, asili na chimbuko la mapenzi ni ndani ya moyo wa Mungu aliyetuumba, Yeye ndie muasisi wa mapenzi… soma zaidi

a.gif UREMBO NA MAVAZI YA MSICHANA

Ingawa ni vigumu kueleza kinagaubaga maana halisi ya neno urembo, naweza kusema kuwa urembo ni utumiaji wa mapambo, manukato, marashi, uturi, mavazi na rangi ili kuremba na kuongeza nakshi na umaridadi katika mwonekano, sifa na viwango vya ubora wa msichana au mwanamke kwa lengo la kuvutia au kufurahisha hisia (za kuona, kunusa au kugusa) za mtu mwingine atakayekutana naye… soma zaidi

UJUMBE-WA-ASUBUHI-KWA-NDUGU.JPG

a.gif Ukubwa wa uume si kigezo cha kumridhisha mpenzi wako

Utajuaje kuwa ni kubwa au ndogo? Obviously ni kwa kujipima….lakini wanaume wengi wanapenda au hata kujisifia kuwa wao ni wakubwa, wakidhani ni moja ya sifa au hitaji la muhimu la wanawake… soma zaidi

a.gif SIMU YA MKONONI NA AFYA YA MSICHANA

Simu za mkononi leo zimekuwa kama sehemu ya maisha ya kila mwanadamu katika mabara yote duniani. Imefikia mahali simu zimesababisha urahibu kiasi kwamba mtu asipokuwa na simu anakuwa kama amepungukiwa na kiungo muhimu cha mwili wake. Kama simu ya mkononi (cell phone) itatumika vizuri kwa malengo na kwa wakati unaofaa, ni chombo kizuri na cha uhakika kwa mawasiliano ya haraka, kujifunza mambo mapya, kukuza uchumi na mambo mengine ya maana na hilo halina ubishi wala mjadala.
Tatizo la simu za mkononi linakuja pale tunapoanza kuangalia athari za mionzi inayopenya mwilini kama matokeo ya matumizi ya simu hizi na athari nyingine za kiafya zitokanazo na matumizi ya muda mrefu ya simu pamoja na athari za kijamii zinazotokana na matumizi mabaya ya simu… soma zaidi

a.gif Mapishi ya Ndizi na samaki

Ndizi laini (Matoke 6)
Viazi mbatata (potato 3)
Samaki wabichi wa wastani ( Fresh tilapia 2)
Kitunguu swaum (garlic 6 cloves)
Tangawizi (fresh ground ginger vijiko 2 vya chai)
Nyanya ya kopo (tin tomato 1/2 kopo)
Vitunguu (onion 1)
Pilipili (chilli 1 nzima)
Chumvi (salt to your taste)
Mafuta (vegetable oil)
Limao (lemon 1/2)
Curry powder (1/2 kijiko cha chai).. soma zaidi

a.gif Faida 14 za kufunga chakula

Watu wengi wanafahamu kuwa kufunga kula ni swala linalohusiana na imani zaidi. Wengi hawafahamu kuwa kufunga kula kuna manufaa ya kiafya pia. Kufunga kula ni tendo lenye historia ndefu sana ambayo kimsingi chimbuko lake ni sababu za kiimani. Hata hivyo shuhuda na tafiti mbalimbali zimedhihirisha kuwa kuna manufaa mengine kemkem ya kufunga kula mbali na yale ya kiimani… soma zaidi

a.gif Tabia za mwanamke anayefaa kuoa

A. Alimpa usingizi mwanaume
B. Alimfanyia upasuaji
C. Damu ilitoka kwa wingi kwa mwanaume
D. Nyama ilitolewa kwa mwanaume
E. Mfupa ulitolewa kwa mwanaume
F. Baada ya kufanyiwa hivyo mwanaume ndipo mwanamke akaumbwa akatoka mwanaume akakiri na kusema huyo ni mfupa katika mfupa wangu na nyama katika nyama yangu –hivyo ataitwa mwanamke napenda ujue kuwa Mwanamke amebeba uponyaji wa mwanaume na mwanaume amebeba vidonda kwa ajili ya mwanamke.. soma zaidi

FURSA..! Kuna nafasi za kazi 100.

Au soma zaidi hapa

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.