Tafuta

Unaweza kutafuta ndugu zako mliopotezana hapa Wanapatikana kirahisi kweli kwa sasa

πŸ‘‰SOMA ZAIDI HAPA...

πŸ‘‰ MSICHANA NA DAWA ZA KULEVYAπŸ‘‡βœ”

MSICHANA NA DAWA ZA KULEVYA

Tatizo la vijana kutumia na kuathirika kwa dawa za kulevya ni njanga la kijamii katika ngazi ya kitaifa na kimataifa. Vijana wengi siku hizi hutumia dawa za kulevya au kutumiwa katika uuzaji, usafirishaji na usambazaji wa dawa hizi bila kuelewa kinagaubaga madhara yake kwao binafsi na jamii kwa ujumla. Dawa hizi huathiri utendaji wao wa kijamii na kihisia, hudhuru afya ya mwili na akili na kumfanya kijana ashindwe kufikia mafanikio ya kimaisha.
Vijana wengi wanaojitumbukiza katika tabia ya kutumia dawa hizi kutokana na urahibu, hupata ugumu wa kujinasua hata pale wanapotamani kuacha. Dawa hizi huchochea mwili na kuusisimua, huleta hisia bandia za kupendeza na kudumaza utendaji wa ubongo na neva.
Kuna aina nyingi ya dawa za kulevya, zingine hutumiwa hadharani na zingine hutumiwa kwa kificho, kutokana na kuzuiliwa kulingana na sheria za nchi kwa sababu ya viwango vikubwa vya madhara yake. Vileo kama pombe, tumbaku, sigara, bangi, mirungi, kokeini, heroin, mandrax na petrol vyote hivi huingia katika kundi la dawa zinazolevya pale vinapotumiwa na binadamu kwa kusudi la kujiburudisha.
Dalili za athari za matumizi ya dawa hizi huwa ni pamoja na kutetemeka, kukosa usingizi, uchangamfu bandia usiokuwa wa kawaida, ulegevu wa mwili, ukali bila sababu bayana au mabadiliko ya kitabia ya ghafla. Ingawa matumizi ya dawa za kulevya huwadhuru vijana wa jinsia zote, wasichana hupata madhara ya dawa hizi haraka zaidi kuliko wavulana.

Baadhi ya athari dawa za kulevya

Athari za Kiafya: Matumizi ya dawa za kulevya husababisha athari zifuatazo:-
β€’ Kuharibika kwa ubongo: ubongo wa mtu anayetumia dawa za kulevya umbo na utendaji wa ubongowake huathirika na kushindwa kufanya kazi zake kama kawaida.
β€’ Huongeza uwezekano wa kupata saratani (kansa) ya bomba la kupitishiwa hewa, mapafu na saratani ya mji wa mimba.
β€’ Dawa za kulevya huhafifisha utendaji wa dawa za kupanga uzazi na kuzuia mimba, hii huongeza hatari ya msichana kupata mimba zisizotarajiwa pale atakapojuhusisha na ngono zembe hata kama anatumia dawa za kuzuia mimba.
β€’ Husababisha magonjwa ya moyo na ini.
β€’ Husababisha magonjwa ya akili.
β€’ Hupoteza hamu ya kula.
β€’ Kukosa usingizi.
β€’ Huleta vidonda vya tumbo.
β€’ Urahibu au hali ya kukosa uwezo wa kujidhibiti na kushindwa kuacha matumizi ya dawa hizo pale anapoamua kuacha. Mtu anayekabiliwa na urahibu wa dawa za kulevya huwa sawa na mtumwa ambaye hana uwezo wa kufanya maamuzi kwa ajili ya Maendeleo yake binafsi na Maendeleo ya jamii.
β€’ Wasichana wengi wanaotumia dawa hizi kabla ya balehe, huchelewa kubalehe.
β€’ Husababisha udhaifu wa mifupa hivyo msichana anayetumia dawa za kulevya anaweza kupata mvunjiko wa mifupa kwa urahisi.
β€’ Maambukizi ya magonjwa kama homa ya ini na UKIMWI utokanao na virusi vya UKIMWI (VVU). Hii huwapata watumiaji wa dawa za kulevya wanaojidunga sindano za kuchangia.
Athari za Kijamii: Katika maswala ya kijamii dawa za kulevya husababisha athari nyingi ikiwa ni pamoja na:-
β€’ Ugomvi, vurugu na tabia za kuendekeza ngono hatarishi.
β€’ Kushindwa kuendelea na masomo au kazi .
β€’ Kuvunjika kwa mahusiano ya kijamii na kifamilia.
β€’ Kudharauliwa na jamii.
Athari za Kiuchumi: Dawa za kulevya huathiri uchumi wa mtu kwa sababu zifuatazo:-
β€’ Kushindwa kuzalisha mali na kufirisika
β€’ Kupoteza uwezo wa kukabiliana na changamoto za maisha.

Baadhi ya sababu zinazotumbukiza vijana katika matumizi na biashara ya dawa za kulevya
o Kuiga tabia za marafiki wenye tabia zisizofaa au kuiga mila mbovu za kigeni zinazoonyeshwa katika vyombo vya habari na kupambwa kama ustarabu wa kisasa au kwenda na wakati. Magazeti, vitabu, televisheni na internet(wavuti) nyingi huonyesha watu wanaotumia dawa za kulevya kama watu wenye mafanikio au watu wenye maisha bora , wanaokwenda na wakati na wasiokuwa washamba. Jambo hili huwachochea vijana wengi kuona matumizi ya dawa hizi kuwa ni jambo la kawaida na linalotamanika.
o Kupoteza mawazo au kuepuka hali ngumu ya maisha – vijana wanaotumia dawa za kulevya kwa sababu hii hupoteza uwezo wao unaohitajika ili kukabiliana na hali ya maisha. Husimamisha na kuhairisha ukuaji wao wa kihisia na kifikra katika kukabiliana na changamoto za maisha.
o Kuacha au kuachishwa shule: vijana wengi wanaofukuzwa shule hujitumbukiza katika janga la kutumia dawa za kulevya kama sababu ya kuachishwa shule haikuwa kutumia dawa hizo.
o Kukataliwa na wazazi, jamii au wapenzi wao: wasichana wanaotumia dawa za kulevya huwa na tabia yisizokubalika katika jamii, hii husababisha wasichana hawa kuwa sawa na kunguru wasiofugika.
o Upweke na matatizo ya kisaikolojia.
o Kukosa heshima kwa wazazi, walimu na viongozi wa kijamii.
o Kukosa makazi na kuwa watoto wa mitaani.
o Kutaka kujionyesha kuwa wanakwenda na wakati na kutafuta umaarufu wa haraka.
o Kupatikana kwa dawa za kulevya kwa urahisi katika mitaa.
o Kupenda utajiri na mafanikio ya haraka kwa njia za mkato bila kufuata kanuni za kimaadili za mafanikio.
Jinsi msichana anavyoweza kuepuka dawa za kulevya
1. Kujifunza maadili mema.
2. Kupata elimu juu ya madhara ya dawa za kulevya.
3. Kufanya kazi kwa bidii na kuepuka tabia ya kukaa vijiweni.
4. Kuepuka makundi rika na marafiki wanaoshawishi utumie dawa za kulevya ili uwe kama wao.
5. Epuka kuanza, kuonja au kujaribu dawa hizi. Ukianza utashindwa kuacha na ukishindwa kuacha utaharibikiwa na kuwa zezeta.
6. Thamini masomo kwa dhati na uwe na malengo ya maisha yako.Mtu asiyekuwa na malengo ni rahisi kuyumbishwa na kujiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya.
7. Jiheshimu mwenyewe na tumia vizuri kila seli ya ubongo wako vizuri, tumia ubongo wako kuendesha maisha yako vizuri.
8. Jihusishe na shughuli za ibada mara kwa mara na kuzingatia mafundisho ya dini. Mafundisho ya dini nyingi huwa ni kinga dhidi ya matumizi ya dawa nyingi za kulevya.

πŸ™‰πŸ™‰πŸ™‰Usisahau kushare posti hii kuhusu (MSICHANA NA DAWA ZA KULEVYA).πŸ‘ Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasomeπŸ’―βœ”

Tafuta ndugu zako hapa Utawapata kirahisi zaidi

πŸ‘‰SOMA ZAIDI HAPA...

wadogo.gif

.