Tafuta

Jinsi ya kutafuta ndugu zako mliopotezana Unaweza kuwatafuta kirahisi sana

👉SOMA ZAIDI HAPA...

👉 Kwa nini watu wanaamini kuwa Albino hawana maambukizo ya Virusi vya UKIMWI (VVU)?👇✔

Imani hiyo si kweli kabisa. Inawezekana ni kupotoshwa kwa
makusudi wa ukweli kuhusu jambo hilo kunakofanywa na watu
wachache katika jamii ili kuendeleza matendo yao maovu. Watu
wanaweza kufuata imani potofu na zisizo na msingi wowote ili
kukwepa ukweli kuhusu VVU na UKIMWI. Kwa mfano; imani
kuwa mtu anaweza kupona UKIMWI kwa kufanya mapenzi na
bikira, mlemavu au Albino ni za uongo na hazina msingi wowote.
VVU huambukizwa kupitia majimaji ya mwili, na njia kuu ya
maambukizo ni kujamiiana bila kinga. Njia pekee za kuzuia
maambukizo ni kuacha kabisa kufanya ngono, kuwa na mpenzi
mmoja muaminifu au kutumia kondomu.Watu wanaoeneza imani hizi
potofu wanatafuta njia mbadala ya kuhalalisha tabia zao mbaya.

Wewe pia kama Albino unatakiwa kupambana na imani hizo
potofu kwani zinalenga kueneza madhara kwa watu wanaoishi
na ualbino.

🙉🙉🙉Usisahau kushare posti hii kuhusu (Kwa nini watu wanaamini kuwa Albino hawana maambukizo ya Virusi vya UKIMWI (VVU)?).👍 Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasome💯✔

uliyesoma.gif

.