.

👉 Kusadikika👇✔

images-7.jpeg

Imehaririwa na; Melkisedeck Leon Shine. Tarehe 30 Jan 2016 07:22. [Legal & Authority]


Kusadikika

Kusadikika
Hakika najiona kama niko ‘Nchi ya Kusadikika’ aliyoieleza mwandishi maarufu wa riwaya Ndugu, Shabani Roberti kama sijakosea. Hadi nakumbuka enzi zile natumwa na wazazi wangu nikachunge mifugo nikapata bahati ya kujua baadhi ya wanyama walio weledi, walio wakali, walio wapole, walio wachoyo, walio wakaidi na kuburi kwa bwana wao, walio wapumbavu, walio wajinga, walio wavivu, walio na juhudi, wapenda dezo, walio wezi,japo kwa tabia hizo chache. Sikubahatika kuingia mbugani nikajifunza wanyama pori. Nimebahatika tu kuchunga na kufuga wanyama hawa wafuatao: mbuzi, kondoo, punda, ng’ombe, mbwa, paka na simbilisi (jamii ndezi hivi!).
Maisha hayo yote ya kufuga na kuchunga wanyama hawa, aliyenipa shida kuliko wote ukiacha mbwa ambaye nilimfanya kuwa rafiki, pia niliweza kumwacha kuwa huru aende anakotaka na akarudi mwenyewe. Hata hivyo “Mbuzi” alionekana kuwa ni mweledi na ni mwisho wa hao wote kwa sifa nyingi kati ya hizo nilizobainisha hapo juu.
Mbuzi ni mweledi wa upumbavu, si mkali bali mchoyo kiasi cha hata kudiriki kumnyima mwanawe wakumzaa, na hapo asisogee wa jirani kwani anaweza kumvunja miguu kwa kichwa. Mbuzi ni mpole na hujipendekeza endapo anataka kupata kitu kwako, mpumbavu kupindukia hasa anapoona kitu ambacho hakifahamu. Yupo radhi aache yote na kufuata aone huyo adui anafananaje, anafanya nini akisogelea, hata kama anamla mbuzi mwenzake na akibaini anachofanyiwa hawezi acha atajitahidi kumsogelea adui huyo ili amtambue anachotenda hatakama ni kitendo ambacho huweza kusababisha apoteze uhai. Mbuzi ana kiburi na mkaidi kupindukia na kujifanya hasikii hali anazo ‘pina’ za kukombea mawimbi ya sauti vizuri, ukitaka kuthitisha hilo mpitishe pahala palipomwagwa munyu ama pumba za mahindi akilamba tu sehemu hiyo na ukaenda naye maili moja anaweza kukutoroka na kurudi pale palipokuwa pamemwagwa chumvi potelea mbali hata kama atapotea njia asifike pahala pale. Waliochunga huyu mnyama wanaweza wakasadiki au wasisadikia walivyomuona wao, japo binafsi namuelewa kwa namna hizo.
Nimetafakari sana sifa za mnyama huyu baada ya kukumbuka maelezo aliyoandika mwana-Njombe mmoja kuhusu Rais kulindwa na nguzu za giza nikaunganisha na kisa cha mnajimu mmoja wa enzi zile za kinyang’anyiro cha urais wa mwaka 2005. Si muumini wa unajimu, ninajaribu kuona kama upo uhusiano wa utabiri wake na hali inavyokwenda sasa kwa kiongozi wetu mkuu. Mnjajimu huyo kama sikosei nadhani ni yule aliyewahi kutamka kuwa atakayempinga rais wetu katika uchaguzi wa 2010 atakufa, kasha ikazua maswali mengi vichwani mwa watu. Wakati huo nakumbuka aliwahi kutabiri na magazeti yakaandika, na TV zikamuonesha akisema kuwa ‘rais atakayeshinda uchaguzi ule ana uso wa mviringo na kichwa chake mfano wa kile cha mbuzi’.

Sasa ukisoma hadithi hii, sijui huyu mtabiri alifanikiwa au hakufanikiwa katika utabiri wake hata mimi sijui kwani naona mambo hapa ni yale aliyosema shabani Robert katika ile ‘Nchi kusadikika’. Kwani nchi hiyo ilishamiri kwa viongozi weledi wa rushwa, matabaka miongozi mwa wanajamii, ujinga na umaskini uliokomaa, ukosefu wa maadili kwa viongozi k.v. kutumia madaraka kwa manufaa binafsi, kukosekana kwa haki n.k.
Hivyo usishangae kampeni za chumbani kwa chumabani, au za mke na mme au za mama na mtoto kuendeshwa. Tambua hapo ndipo walipofikia, wanapoweza kupamudu kufanya kwa usanifu na ufasaha zaidi, vitani ukizingirwa na adui hata kama huna risasi usimfanye adui akatambua kuwa umeishiwa risasi. Kwa mtaji huo wanajua wamefanikiwa kuwalemaza watanzania waliowengi kiasi cha kujikatia tamaa na kutojishughulisha kabisa kufikiria dhidi ya watawala wao wanafanya nini. Hapa nakumbuka hotuba mojawapo ya Mwl. Nyerere kuwa mtu akipea kipande ‘feki’ cha dhahabu anaondoka huku akishangilia kama zuzu, nimejionea mwenyewe kwa macho yangu kule vijijini Rukwa na Mbeya ndugu zetu wakigombania kofia na vitenge vya mgombea wakishangilia kufanikiwa kupata vitu hivyo, ajabu!!!!!!!!
Nadhani ushindi wa CCM utafanana na jinsi nilivyoona watu wale wakishangilia kwa kuuza haki zao kwa kutotambua methali waliyotungia. Hakika kama wamebaini kuwa vitu walivyopewa ilikuwa ni kamba yakuwafunga kama zezeta ili wapelekwe gulioni na bwana wao anemeke na familia yake, hasira yao itakuwa kali mno tarehe 31/10/2010, hawatadiriki kurudi tena kutazama hata uso wa bwana wao kama mbuzi wangu yule aliyekuwa mweledi kwa upumbavu na ukaidi.
Natoa samahani kwa yule ambaye atakuwa amekerwa na habari hii! Haya ni mawazo na mtazamo wangu tu.

Soma%20Zaidi.gif Napendekeza uendelee kusoma kuhusu; Tujenge Maghorofa: Njia nzuri ya kufanikiwa katika maisha.

🙉🙉🙉Usisahau kushare posti hii kuhusu (Kusadikika).👍 Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasome💯✔

Nini maoni yako kuhusu, Kusadikika? Niandikie hapa
Add a New Comment
or Sign in as Wikidot user
(will not be published)
- +
Kichekesho%20Kipya Kutana na wale mliosoma pamoja Bado wanakumbukia urafiki wa Kishule shule
👉SOMA ZAIDI HAPA...Kizuri

IMG_20180108_171540.jpg

Ujumbe wangu kwako kwa sasa

"Msomaji wangu mpenzi, nakukumbusha kutembelea blog hii kila wakati unapotaka kujifunza kitu. Kwa kufanya hivyo utaweza kujisomea mambo mapya ya kila siku."

nn.gif

.

.

b.gif

Mimi ni Melkisedeck Shine Mmiliki, Mwandishi /Mhariri. Karibu tena kila siku.

MAWASILIANO | KUHUSU MWANDISHI

Blog nyingine maarufu ndani ya AckySHINE.com

| Vichekesho | Videos | Picha | Ujasiriamali | Mahusiano | Kilimo & Mifugo | Katoliki | Afya & Mapishi | Hadithi | Misemo | SMS