Kupunguza magonjwa kwa kuku

jarida-la-vichekesho-bomba.jpg

Kupunguza magonjwa kwa kuku

Ufugaji wa kuku una faida kubwa, lakini mkulima anatakiwa kuzuia kadri awezavyo uwezekano wa kuwepo magonjwa shambulizi.

Wafugaji wengi wamekuwa wakiwekeza katika ufugaji wa kuku. Ufugaji huo unalenga kuku wa kisasa au wa kienyeji. Wanajenga mabanda, kununua chakula, pamoja na kuku, wakitarajia kupata faida kubwa kutokana na uwekezaji huo. Hata hivyo, mradi unapoanza mambo huonekana kwenda sawa, mpaka mfugaji anaposhtuliwa na mlipuko wa magonjwa ambayo hupunguza uzalishaji au kuua kuku.

Mfugaji anaweza kufanya nini kupunguza hatari ya magonjwa kwa kuku?

Mbinu zinazotumiwa na wakulima duniani kote zinanaonesha kuwa kuweka banda katika hali ya usafi, kuwalisha kuku ipasavyo na kuwapatia maji safi, ndiyo njia ya kwanza muhimu ya kupambana na magonjwa, kama vile mharo mwekundu, kipindupindu cha kuku, na ndui. Kuwa makini katika ufugaji wa kuku ni pamoja na kutoa chanjo kwa kuku, kuzuia magonjwa kama sotoka au ndigana na ndui.

Taratibu za kufuata ili kuzuia magonjwa kwa kuku

Utunzaji wa banda la kuku ili kujikinga na magonjwa

• Ni lazima nyumba ya kuku iwe safi na kavu muda wote
• Nyumba ya kuku iwe na nafasi za kupitisha hewa ya kutosha ili kuepuka joto na unyevunyevu
• Hakikisha unaondoa matandazo na takataka zote kwenye banda wakati wote. Matandazo na taka zinaweza kuwa mbolea nzuri ya mboji kwa mimea yako.
• Fagia banda na kuhakikisha ni safi wakati wote. Weka matandazo mapya mara kwa mara.
• Weka nafasi ya kutosha kuku kupumzikia, viota vya kutosha, na kuweka maji sehemu ambayo ni rahisi kusafisha.
• Hakikisha unaondoa wanyama kama panya na wadudu nyemelezi kwenye sehemu ya malisho ya kuku kwani wao hubeba vimelea vya magonjwa.

Utunzaji wa kuku

• Toa chanjo muhimu kwa kuku ili kuzuia magonjwa kama utakavyoshauriwa na mtaalamu wa mifugo. Chanjo huanza katika wiki ya kwanza (mfano chanjo ya kuzuia sotoka) na inaweza kurudiwa baadaye.
• Epuka kuweka kuku wengi mahali pamoja kwani ni rahisi magonjwa kuenea kwa haraka kuku wanaporundikana.
• Tenganisha vifaranga na kuku wakubwa (isipokuwa kutoka kwa mama) kwa sababu vifaranga ni rahisi na wepesi sana kushambuliwa na magonjwa.
• Weka mipaka na madaraja ya sehemu za kuku kuzunguka/kucheza.

Ulishaji wa kuku

• Wapatie kuku chakula cha kutosha na chenye virutubisho vyote. Unaweza kuwaongezea majani, makombo, nafaka, mchanga laini, au maganda ya mayai.
• Wapatie kuku maji safi muda wote. Wafugaji wengi wameripoti kuwa na matokeo mazuri baada ya kuchanganya dawa ya kuua vimelea kwenye maji ya kunywa.
• Safisha vyombo vya kulishia na kunyweshea kila siku. Osha, sugua vizuri, kisha suuza kuondoa utando unaobeba bakteria.
• Nunua chakula kwa wauzaji wazuri na wanaoaminika ili kuepuka minyoo na sumu hatarishi.
• Hifadhi chakula cha kuku katika sehemu kavu isiyo na joto na isiwe kwa zaidi ya miezi mitatu ili kuepuka kuharibiwa na fangasi.
• Usiwape kuku chakula chochote kinachoonekana kuoza au kunuka uvundo. Kukabiliana na magonjwa
• Muone mtaalamu wa mifugo mara uonapo dalili zozote za kuumwa kwa mifugo wako.
• Watenge na uwapatie tiba au kuwaua na kuteketeza kabisa kuku wagonjwa kuepuka kuenea kwa magonjwa.
• Ondoa ndege waliokufa mara moja, uwafukie au kuchoma moto. Usile kuku aliyekufa. Baadhi ya magonjwa ya ndege yanaweza kuambukizwa kwa binadamu.
• Endapo kuna mlipuko wa ugonjwa katika eneo lako, usiruhusu watu kutembelea banda lako. Watu wanaweza kuleta maambukizi kwa miguu yao katika mabuti, nguo na mikono. Pia magari yanaweza kuleta madhara kwa mabanda yako kupitia matairi na upakuaji wa mizigo.

Ukaguzi wa mara kwa mara kwa kuku

Kila siku

• Safisha vyombo vya kulishia na kunyweshea pamoja na viota.
• Ondoa kinyesi.
• Waangalie kuku wako kwa makini ili kujua afya na maendeleo yao.

Kwa wiki

• Ondoa matandazo machafu na kuweka mapya.

Kwa mwezi

• Angalia uwepo wa wadudu na chawa, kisha utibu kama kuna ulazima.

Mambo ya kuzingatia kabla ya kuweka mifugo wapya bandani

1. Ondoa matandazo yote, vyombo vya kulishia na kunyweshea.
2. Ondoa uchafu wote unaoonekana bandani.
3. Safisha banda lote kwa kutumia maji na dawa.
4. Suuza na uache likauke.
5. Puliza dawa ya kuua wadudu.
6. Weka matandazo mapya, weka viombo vya kulishia na kunyweshea.

Ofa! Ofa! Ofa!
Jipatie Jarida La Kilimo Cha Mboga kwa bei ya ofa ya Tsh 2000/= tuu kwa leo!, kutoka bei yake ya kawaida ya Tsh 5000/=.

<<<Bofya hapa kujua zaidi>>>

Usisahau kushare posti hii!! Share Facebook, Twitter bila kusahau Whatsapp!!

Toa maoni yako kuhusu, Kupunguza magonjwa kwa kuku. hapa..

Add a New Comment
or Sign in as Wikidot user
(will not be published)
- +
kilimo-bora-cha-mboga.jpg
usikose-jarida-la-vichekesho.jpg

Kwa sasa endelea kusoma posti hizi zifuatazo;

Bidhaa zinazopendwa na wengi ndani ya Ackyshine Shop

kilimo-cha-Mboga.jpg

Jipatie Jarida La Kilimo Cha Mboga kwa Tsh 2000/= tuu.

<<Bofya hapa kuweka Oda>>

vichekesho-vikuu.jpg

Lina kurasa 162

Jipatie Jarida la Vichekesho Vikuu Vikali 300+ kwa Tsh 1900/= tuu.

<<Bofya hapa kuweka Oda>>