KUCHAGUA MCHUMBA

By, Melkisedeck Shine.

familia-mapenzi-na-mahusiano.png

KUCHAGUA MCHUMBA

SOMO: 1 Wakorintho 7

Mungu alipokuwa akiwaumba watu, alimuumba kwanza mwanamume. Baada ya hapo alimuumba mwanamke kwa namna aliyoona inafaa, baada ya kuona haifai mwanamume awe peke yake (Mwanzo 2:18). Kwa hiyo mpango wa uumbaji ni wa mume na mke kuwa wamoja katika maisha yao yote.

Adamu na Hawa walitakiwa wawe na ushirika katika utukufu wa bustani ya Edeni. Baada ya kumkiuka Mungu, walifukuziwa nje na kuwa na ushirika wa kimapenzi uliowafanya wapate watoto, kwa ajili ya kuendeleza kizazi cha mwanadamu.

Mahusiano yanayojengeka kati ya wazazi na watoto inabidi yabadilike watoto wanapokua, na wanapofikia utu-uzima waanze maisha kikwao kwa kuoa au kuolewa (Mwanzo 2:24). Yesu alifundisha kuwa, mahusiano hayo kati ya mwanamume na mwanamke yanapaswa yawe kitu cha kudumu. Ndivyo Mungu alivyotaka iwe tangu mwanzo(Mathayo 19:4-6).

Talaka iliruhusiwa iwepo tu kwa sababu ya udhaifu wa kibinadamu, wa mtu kushindwa kuitii sheria ya Mungu.

Uhuru wa kutengana na kuoa au kuolewa tena, unatofautiana kati ya nchi na nchi. Katika nchi za magharibi ni mazoea yaliyoingia nyakati hizi, yasiyoruhusiwa kwa wafuasi wa Yesu, na ni pale tu mume anapogundua ya kuwa mke wake amekuwa akifanya mapenzi na wanaume wengine. Hakuna kinachogusiwa kusema kama ruhusa hiyo ya kipekee ilikuwa pia kwa upande mwingine; kama mke aligundua kuwa mumewe alikuwa akifanya mapenzi nje.

Mtume Paulo anayakazia mafundisho haya ya Yesu katika waraka wake wa kwanza kwa Wakorintho, Sura ya 7, mstari wa kwanza na wa pili. Ingawa Paulo hakuoa na alipendelea kubakia hivyo, alitambua ya kwamba wafuasi wa Yesu walio wengi wangependa waoe au kuolewa, na ni wachache tu wangeweza kuwa tayari kuufuata mfano wake (1 Wakor. 7:8,9). Anasema wanapokuwa wamekwisha kuoana wasiachane (1 Wakor. 7:10,11). Ni pale mmojawapo anapokufa tu ndipo aliyebaki anaweza kuoa au kuolewa tena (Warumi 7:1-3).

Dunia ya kisasa inapuuza haya yote na inaruhusu sio kutengana mara moja tu, bali kubadili wapenzi kunakoendelea. Hili ni wazi ni kinyume kabisa cha kusudi la Mungu na ni kinyume cha mafundisho aliyotoa Yesu kwa wafuasi wake. Wanaume kwa wanawake wasio na imani na wanaoukana uwepo wa Mungu, kwa vyovyote hawaoni haja ya kufuata miongozo inayowabana wasifanye wanavyotaka.

Matokeo ya hili yamekuwa kuvunjika kwa maisha ya kifamilia na kuongezeka kwa matatizo yanayowakumba watoto, wanaokosa upendo wa wazazi wanaopendana. Hata hivyo, kwa wanaume na wanawake wanaomwamini Mungu na wanaotamani kuwa wafuasi wa Yesu, kuna haja kubwa sana ya kuwa waangalifu juu ya mada hii ya ndoa.

Ujumbe wa Agano la Kale na Jipya unaosemea hili uko wazi, na unarudiwa-rudiwa mara nyingi. Hata hivyo, Paulo anauhitimisha kwa ajili yetu katika 1 Wakorintho 6:9-10. Hakuna lisiloeleweka juu yake:
- Uasherati unakatazwa
- Uzinzi unakatazwa
- Mapenzi ya jinsia-moja yanakatazwa.

Haisaidii kitu kulalamikia makatazo hayo yaliyo wazi sana kwa kuwa hayo ni mapenzi ya Mungu. Kama tunatamani tufufuliwe kutoka kwa wafu (kama tutakuwa tumekufa kabla Yesu hajarudi), na kuwa na sehemu katika Ufalme wa Mungu unaokuja, na kama tunatamani kuufurahia uzima usio na mwisho na maajabu ya kuwa na sehemu katika mpango wa Mungu kwa ajili ya dunia hii, ni lazima tushikamane na sheria zake hizi.

Tunaweza kuyapindisha maneno hayo na kuyageuza yasiseme kile yanachosema, lakini ipo siku tutatakiwa kusimama mbele ya kiti cha hukumu cha Bwana Yesu Kristo. Tusithubutu kuyapuuza maelekezo haya.

Tunapofikia wakati katika maisha yetu wa kutaka kuchagua โ€˜mwenzaโ€™ wa maisha, inatubidi tuwe macho sana. Msichana mrembo sana au mvulana mtanashati kabisa wanaweza kuonekana wazuri, lakini utahitaji kujiuliza kama watakuwa na ushirika nawe wa imani yako kwa Mungu. Mtaweza kwa pamoja kusaidiana katika njia ya Ukristo kuufikia Ufalme wa Mungu?

Paulo alitambua kuwa, baadhi ya wanaume na wanawake wangekuwa wafuasi waliobatizwa wa Yesu, wakati โ€˜wenzaโ€™ wao watakuwa hawataki kubadilika. Ushauri wake kwa watu hao ni wa busara na wa wema sana(1 Wakor. 7:12-16). La muhimu analosema hapa ni kwamba, mume au mke asiyeamini anapaswa aridhike kwamba, mwenza wake amechagua kumfuata Yesu na asimkwaze katika ibada yake.

Kuna tatizo lingine kwa muumini aliyebatizwa: afanye nini kama hawezi kupata mwenza wa umri wake ambaye naye ni mfuasi wa Yesu? Kuna majibu ya namna mbili hapa. La kwanza ni kwamba kuoana ni sehemu muhimu mno ya maisha ya furaha ya muumini, katika kuweza kuishi kwa imani mbeleni, kiasi kwamba, inaweza kumbidi asafiri kwenda sehemu nyingine ya nchi, au nchi nyingine kumpata mwenza.

Hata hivyo, hili ni rahisi zaidi kwa mwanamume kuliko kwa mwanamke, lakini kuna mifano ya kusisimua katika Biblia ambapo hili lilitokea nyakati za kale (Mwanzo 24 na Ruthu 1 na 2).

Katika Ruthu, Sura ya kwanza, tunamwona Ruthu akionesha tu nia yake ya dhati ya kuwa na mama-mkwe wake, Naomi, lakini tunapofikia Sura ya pili ni wazi Naomi amemwongelea Ruthu juu ya ndugu yao katika ukoo (Boazi) aliyekuwa tajiri katika Bethlehemu, ambaye pengine angevutiwa kuiheshimu sheria ya urithi na kumwoa mke wa ndugu yake aliyekufa.

La pili linalowezekana ni kutafuta mwenza ambaye ni msomaji wa Biblia, anayependa kuwa mfuasi ya Bwana Yesu Kristo. Kwa kuisoma Biblia pamoja, inawezekana, sio tu kumpata mwenza wa kuoana naye, bali pia kupata furaha ya kumleta mtu mwingine katika ufahamu wa Ufalme wa Mungu unaokuja duniani. Hili kwa vyovyote ni mwendelezo wa kazi ya kueneza ujumbe wa Injili, ambao wafuasi wote wa Yesu wameamriwa kuifanya (Marko 16:15, 16).

Kwa hiyo, ipo sababu nzuri sana ya kumpata mwenza na kufaa wa kuoana naye. Hata muumini ambaye amefiwa na mume au mke ni muhimu sana kujali hivyo vigezo kabla ya kufikiri kuoa au kuolewa tena (1 Wakor. 7:39).

Mada hii ya ndoa ilithaminiwa sana na mitume kiasi kwamba, Paulo alipokuwa akiandika waraka wake wa pili kwenda Korintho, aliirudia hiyo amri tena (2 Wakorintho 6:14-16).

Kuwafunga nira wanyama wawili wasio sawa kimwili au kihulka ili walime pamoja shambani au wakokote mzigo, kunaweza kuwa na matokeo mabaya sana. Ile nira, kwa kuwa haiwezi kukaa vizuri itasugua ngozi na kuwatia wanyama hao vidonda, na hasa mmoja. Wanyama hao watavutana na kukuta wakiangushana, badala ya kuvuta majembe au mkokoteni pamoja.

Kwa hakika hii ni namna iliyo sahihi kabisa ya kuielezea ndoa yenye migogoro, lakini inakuwa ni hivyo hivyo kwa mahusiano mabaya ya kikazi au kibiashara. Kwa hiyo Paulo anatuonya ili haya yasitokee.

Kwa upande mwingine kunakuwa na furaha kubwa katika kuwa na imani moja kati ya mume na mke, katika kusoma Biblia pamoja, na kama kuna watoto kuwafundisha kuziheshimu sheria za Mungu na kumfuata Yesu.

Katika waraka wake kwa Waefeso, Paulo anafananisha uhusiano kati ya mume na mke na ule uliopo kati ya Yesu Kristo na kanisa lake. Dhabihu ya damu yake aliyokuwa tayari kuitoa kwa ajili ya wafuasi wake ili waweze kuokolewa kutokana na mauti ya milele, inaonesha upendo unaopaswa kuwepo kati ya mume na mke. Ishara hii haikuwa kitu alichokibuni Paulo, kwa maana Yesu aliitumia mara nyingi katika kuihubiri kwake Injili.

Mfano mzuri upo katika Injili ya Mathayo, Sura ya 25:1-13. Hapa Yesu anaongelea kurudi kwake duniani kunakofananishwa na โ€˜ujio wa bwana-harusiโ€™, kitu kinachotufundisha kuwa macho wakati wote tukimsubiri. Pamoja na hilo, anatufundisha pia kuwa macho juu ya kile tunachokuwa tukifanya wakati anapofika. Kwa wafuasi wale walio na wenza, hakuna namna iliyo bora zaidi, zaidi ya kusaidiana katika umoja wa kiimani na tumaini, kuwa tayari kwa ajili ya siku hiyo njema ya ajabu.


[KichekeshoV.gif] ๐Ÿ‘‰Hii sasa kali!!!

[Kitendawili…!] ๐Ÿ‘‰Hulia chakula rnlirnani bila kuanguka

[Fumbo Fumbo] ๐Ÿ‘‰Je, moshi ulielekea upande gani?

[Video Nzuri] ๐Ÿ‘‰Angalia gari ilivyogongwa na treni

[Chemsha Bongo] ๐Ÿ‘‰Je, hii familia ina watoto wangapi?

Endelea kusoma makala hizi zifuatazo;

a.gif UNATAFUTA NDOTO ZAKO AU MAPENZI YA MUNGU?

Watu husema, na hata wahubiri pia nao husema, โ€˜Fuata ndoto zako!โ€™ Lakini Yesu alisema, โ€˜Nifuate mimiโ€™. Ikiwa utafuata ndoto zako, unajifurahisha mwenyewe tu. Lakini ikiwa utamfuata Yesu, atampendeza yeye. Kama utafuata ndoto zako, basi unajitumikia wewe mwenyewe. Ukimfuata Yesu, utamtumikia yeye na kanisa lake. Kama utafuatisha ndoto zako, unajitengenezea njia yako mwenyewe. Kama utamfuata Yesu, yeye ndiye atakayekuandalia njia.
Kuwaambia wakristo kwamba wanapaswa โ€˜kufuata ndoto zaoโ€™ ama โ€˜kuwa na ndoto ama maono ya maisha yao yajayoโ€™ ni kuwaongoza katika njia isiyokuwa sahihi na kuwadanganya. Hao wanaofundisha mafundisho hayo watawajibika mbele za Mungu kwa kuwadanganya waamini. Hao wanaopokea mawazo ya namna hiyo kwenye mioyo yao nao pia wanawajibika kwa kupokea kitu ambacho hakifundishwi katika biblia na ni kinyume na mafundisho ya Biblia… soma zaidi

a.gif SABABU/ FAIDA 40 ZA KUFUNGA KWA MTU BINAFSI.

SABABU/ FAIDA 40 ZA KUFUNGA KWA MTU BINAFSI.
Hapa chini tunakwenda kuorodhesha faida arobaini na moja (4I) za kufunga.Isaya 58 inafaida 20 kama ifuatavyo.
a) Isaya 58:8-9.. soma zaidi

a.gif KUFUNGA NA KUOMBA KUNAKOONGEA MBELE ZA MUNGU

Kufunga na kuomba kunakoongea ni kufunga na kuomba kunakotoa sauti inayopenya hadi kitini pa Mungu na kuleta mabadilko ya kudumu katika ulimwengu wa mwili. Tunaweza kusema Kufunga na kuomba kunakoongea ni atomic bomb katika ulimwengu wa rohok kwa sababu hutoa matokeo makubwa bila kumuumiza anayetumia silaha hiyo… soma zaidi

[Msemo wa Leo] ๐Ÿ‘‰Mfu wa Mawazo

[Jarida la Bure] ๐Ÿ‘‰Jarida la kilimo bora cha kabichi

[Hadithi Nzuri] ๐Ÿ‘‰Kisa cha baba mzee na mwanae

[SMS kwa Umpendaye] ๐Ÿ‘‰SMS nzuri kwa umpendaye asubuhi

a.gif Namna ya kujitibu chunusi kwa kutumia dawa ya meno au dawa ya mswaki

.. soma zaidi

a.gif Dondoo ya leo!

DONGO LA LEO ……..
Kwa lugha nyepesi ni kwamba ukiajiriwa maana
yake umeshindwa kujitegemea kwa ujuzi wako
(yaani hujui ufanyie nini) hivyo umeona uukabidhi
ujuzi wako kwa wenye "akili na uwezo" wa
kuupangia matumizi ya huo ujuzi wako… soma zaidi

a.gif Madhara ya kuangalia picha za ngono

Kuna watu wanapenda sana kuangalia sinema za ngono… soma zaidi

a.gif Ishara za uhakika za mtu yeyote anayekupenda kimapenzi hata kama hajakwambia

Utajuaje kama unapendwa?
Zifuatazo ni ishara za mwanamme au mwanamke anayekupenda hata kama hajakwambia.. soma zaidi

a.gif MAPISHI YA LADU

Unga - 6 vikombe.. soma zaidi

elimu-sayansi-na-tekinolojia.png

.

familia-mapenzi-na-mahusiano.png
UJUMBE-HONGERA-NDUGUU.JPG
uchumi-biashara-na-ujasiriamali.png

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.