Kichekesho%20Kipya Usikose πŸ“•Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKEπŸ‘§πŸ‘—πŸ‘  KinamwelezeaπŸ”ŽMwanamkeπŸ” kinagaubagaβœ”πŸ‘‰Bofya hapa KuchukuaKizuri

.

πŸ‘‰Jinsi ya kuzalisha papaiβœ…


images-11.jpeg

"Kukosa mtu, kitu au jambo fulani kunasababila Moyo kujenga upendo kwenye mtu, kitu au jambo ulilolikosa."


πŸ‘Baada ya kusoma kuhusuπŸ‘‡;

FURAHA-SHINE.jpg
πŸ’‘Leo nimekutayarishiaπŸ’« makala kuhusu🌠 Jinsi ya kuzalisha papaiπŸ‘‡.

πŸ’₯Jinsi ya kuzalisha papaiπŸ‘‡

Imehaririwa na; Melkisedeck Leon Shine. Tarehe 30 Jan 2016 06:26. [Legal & Authority]


Papai ni tunda lenye ladha nzuri, na rahisi kuliwa. Aina hii ya tunda ni chanzo cha virutubisho muhimu mwilini, ambavyo husaidia kujenga mwili.

Zao hili asili yake ni ukanda wa kitropiki ambao hauna baridi kali na joto kiasi.

Udongo

pawpaw 2Mipapai hustawi vizuri kwenye udongo usiotuhamisha maji. Endapo maji yakituama kwenye eneo lililopandwa mipapai kwa muda wa siku mbili, mpapai unaweza kuoza kwa haraka na kufa. Kwa kuwa mipapai haina mzizi mkuu, inahitaji udongo wenye rutuba ya kutosha. Halikadhalika, zao hili halihitaji udongo wenye kina kirefu, hivyo ni muhimu kumwagilia mipapai wakati wa kiangazi. Wakati wa mapapai kuiva kama kuna ukame basi hali hiyo huongeza ubora wa papai ikiwamo kutooza mapema baada ya kuvunwa.

Kupanda

Mipapai ipandwe sehemu ambazo hazina upepo mkali. Hii itasaidia mipapai kukua vizuri bila kuvunjika kwani mti wa mpapai huvunjika kirahisi. Inashauriwa kupanda miti ya kukinga upepo kuzunguka shamba la mipapai. Ili kuwa na tija zaidi, unaweza kupanda aina nyingine ya miti ya matunda kama vile miparachichi, na miembe.

Hakikisha miti ya kukinga upepo inakuwa mirefu kuzidi mipapai. Miti hiyo inaweza kutangulia kupandwa miezi kadhaa kabla ya kupanda mipapai.

Mbegu

Kusanya mbegu toka kwenye mapapai makubwa na yaliyo komaa na kuiva, kisha kausha mbegu vizuri kabla ya kupanda. Inashauriwa kununua mbegu kutoka kwa wazalishaji wanaoaminika na waliothibitishwa, ili kuwa na mazao bora zaidi na yanayoweza kukabiliana na magonjwa.

Mbegu aina ya red royal F1, inasifika zaidi kwa kuwa na uwezo mkubwa wa kukabiliana na magonjwa yanayoshambulia mipapai, na huanza kuvunwa mapema zaidi, kati ya miezi 6 hadi 12. Aina hii huvunwa mfululizo kwa miaka 5 hadi 7.

Uandaaji wa shamba

Inashauriwa kuandaa shamba vizuri kwa kuondoa visiki na magugu yote. Shamba lilimwe vizuri, na kuhakikisha udongo umelainika vizuri.

Mashimo

β€’ Chimba shimo kwa ajili ya kupanda mpapai, liwe na kina cha sentimita 60 na upana wa sentimita 60.
β€’ Weka mboji debe moja kisha changanya na nusu ya udongo uliotoa kwenye shimo, kisha rudishia kwenye shimo.
β€’ Mwagilia maji kwa kipindi cha wiki mbili kabla ya kuotesha.

Kuotesha

Sia miche kwenye kitalu, kasha hamishia shambani inapokuwa na urefu wa sentimita 30. Chomeka mche kwenye ardhi kina cha kati ya sentimeta 1 – 2 chini ya udongo kwenye shimo uliloandaa. Hii itasaidia mche kupata joto la wastani na kuepuka mche kuoza na kufa. Baadhi ya wakulima hupenda kuotesha mipapai moja kwa moja shambani.

Endapo unapenda kufanya hivyo, zingatia haya;

β€’ Kabla ya kupanda mbegu weka mchanganyiko wa majivu na mbolea ya kuku au mboji sehemu unayokusudia kupanda. Mbolea husaidia ukuaji haraka na jivu husaidia kukinga mipapai na magonjwa.
β€’ Panda mbegu 3 – 4 kila shimo, hii ni kwa sababu miche mingine inaweza kufa kutokana na magonjwa, kuliwa na wadudu au ikaota mipapai dume.

Nafasi

Shimo hadi shimo, liwe na nafasi ya mita 3, na mstari hadi mstari mita 3. Hii itasaidia miche ya mipapai kukua vizuri bila kusongamana.

Punguza miche

Baada ya miezi 3 – 5 tangu kupanda, mipapai itaanza kutoa maua na hapo jinsia ya mipapai itajulikana. Inapofikia wakati huo inabidi kupunguza mipapai mingine hasa midume.
Mipapai yenye jinsi zote isizidi asilimia 10 – 20 ya miche yote iliyopo shambani, na midume ibaki mmoja katika kila majike 25.

Utunzaji

Copy of pawpaw plant 2β€’ Weka kilo 2 – 5 za samadi kwenye kila mpapai kwa mwaka ili kuongeza ukuaji na uzalishaji.
β€’ Mabaki ya mimea yanaweza kuwekwa kama matandazo. Hii ni muhimu zaidi kipindi cha kiangazi ili kuzuia unyevu usipotee.
β€’ Chunguza mipapai mara kwa mara ili kuangalia kama kuna magonjwa, ing’olewe na kuchomwa au kufukiwa chini endapo itabainika kuwa na maonjwa.
β€’ Unaweza kunyunyiza dawa zisizo na madhara za kukinga au kukabiliana na magonjwa ya ukungu na virusi.

Kupogoa

β€’ Kata matawi yote yatakayojitokeza pembeni ya mpapai. Hili lifanyike mapema kabla ya tawi kuwa kubwa.
β€’ Ondoa mipapi yote ambayo hayakuchavushwa vizuri na ubakize yenye afya tu.

Palizi

β€’ Mipapai inapopandwa tu inaweza kuwekewa matandazo kuizunguka ili kuzuia uoataji wa magugu.
β€’ Magugu yang’olewe yakiwa machanga.
β€’ Epuka kuchimbua sana wakati wa palizi kwa kuwa mizizi ya mipapai huwa juu juu.

Magonjwa

Zao la papai halina magonjwa mengi sana yanayoshambulia endapo litatunzwa vizuri. Hata hivyo kuna baadhi ya magonjwa ambayo yamezoeleka kwenye zao hili kama vile Ugonjwa wa madoa kwenye majani (Papaya spot) na Ugonjwa wa virusi unaojulikana kama Mozaic virus. Mimea yenye magonjwa inaweza kung’olewa na kufukiwa ili kudhibiti ueneaji kwenye mimea mingine.

Facebook

πŸ‘ŠUsikubali kupitwa na Kijitabu cha Kilimo Bora cha Bamia. Linafafanua Kilimo cha bamia . πŸ‘‰Bofya hapa KuchukuaπŸ‘ˆ

Facebook

18010559_1256919237760740_2925276740254304995_n.jpg

πŸ“Nini MaoniπŸ’­ yako Kuhusu Jinsi ya kuzalisha papai? Niandikie hapaπŸ‘‡

Add a New Comment
or Sign in as Wikidot user
(will not be published)
- +
images-21.jpeg

🐼 Endelea kusoma kuhusu;-πŸ™‰

.

.

images-19.jpeg

"Ukiona unaweza ukakaa siku nzima bila hata kuwa na wazo moja jipya ujue umezeeka akili tayari na kesho unaweza ukawa haupo."

.

.

SHINE-MWENYEWE.jpg

"Kama vile moto unavyozimwa na maji ndivyo vivyo hivyo hasira inamalizwa na maneno ya upole."

.

.

IMG_20170703_130936.jpg

"Kila mtu ni mrithi wake yeye mwenyewe. Mafanikio yako ya baadae ni urithi wako ulioutengeneza hapo awali. Utajiri wako wa sasa unatokana na uliyoyawekeza miaka ya nyuma na utajiri wako ujao ni yale unayoyawekeza sasa.."

.

.

IMG_20170703_130508.jpg

"Endelea kufurahia Blog hii kwa kutembelea kila siku. Furahia posti mpya kila siku unapotembelea Blog hii.,"

.

πŸ“ Misemo ya AckySHINEπŸ‘‡

MA.gif
Kichekesho%20Kipya Usikose Kijitabu cha Kilimo Bora cha Bamia Linafafanua Kilimo cha bamia πŸ‘‰Bofya hapa KuchukuaKizuri

.

.

Habari msomaji wangu…?

images-14.jpeg
Melkisedeck Leon Shine

"Kila mtu ni mrithi wake yeye mwenyewe. Mafanikio yako ya baadae ni urithi wako ulioutengeneza hapo awali. Utajiri wako wa sasa unatokana na uliyoyawekeza miaka ya nyuma na utajiri wako ujao ni yale unayoyawekeza sasa."

Jina langu ni Melkisedeck Leon Shine Mwendeshaji wa blog hii.

images-23.jpeg

"Usikubali kupitwa na Picha Bomba Kali za kila siku. Endelea kuperuzi blog hii kwa Picha."

Usisite kuniandikia maoni,mapendekezo au maswali hapa kuhusu Blog hii kwa ujumla

Jina
Mahali ulipo
Mfano Mkoa, Wilaya n.k
Email
Itatumika kukujibu
Maoni yako

images-12.jpeg

"Ukiona unaweza ukakaa siku nzima bila hata kuwa na wazo moja jipya ujue umezeeka akili tayari na kesho unaweza ukawa haupo."

KUHUSU BLOG HII | MAWASILIANO | ABOUT AUTHOR | LEGAL GUIDELINES