.

πŸ‘‰ Jinsi ya kuzalisha lishe kwa n'gombe wa maziwa kwa bei nafuuπŸ‘‡βœ”

IMG_20180108_172904.jpg

Imehaririwa na; Melkisedeck Leon Shine. Tarehe 30 Jan 2016 06:27. [Legal & Authority]


Jinsi ya kuzalisha lishe kwa n'gombe wa maziwa kwa bei nafuu

Lishe bora: Ng’ombe hawezi kulaumiwa kwa kushindwa kufanya urutubishaji. Ukosefu wa lishe sahihi husababisha ng’ombe kuwa dhaifu na pia husababisha kutokea kwa magonjwa ambayo huweza kuathiri mfumo wa uzazi.

resheni
Malighafi zinazotumika kutengeneza chakula cha mifugo nyumbani
Kupungua kwa ulaji wa vyakula vya kutia nguvu huathiri joto na hatimae kupunguza uwezo wa uzalishaji kwa ng’ombe. Hii ina maana, lishe hafifu kwa ng’ombe wa maziwa husababisha ng’ombe kutokupata joto kwa wakati uliotarajiwa kwa sababu miili yao haipo katika hali nzuri ya kubeba mimba. Ng’ombe lazima alishwe mlo kamili unaojumuisha wanga, protini, madini na vitamini.

Utafiti unaonesha kwamba ng’ombe aliyeathirika kutokana na utapiamlo, baada ya mwili wake kujijenga kwa upya na kuwa katika hali ya kawaida, huweza kujirudia katika hali ya uzalishaji na akashika mimba kwa haraka sana hata kuliko ng’ombe aliyekuwa akipata mlo kamili kwa wakati wote.

Uzalishaji wa lishe

Ng’ombe anayelishwa nyasi tu hawezi kufikia kiwango kizuri cha uzalishaji maziwa hivyo anahitaji kupatiwa lishe ya ziada. Virutubisho vya ziada kama vile dairy meal inakadiriwa kugharimu asilimia 20% zaidi ya gharama ya jumla ya uzalishaji wa maziwa, hivyo kupunguza faida kwa mfugaji.

Kuongeza virutubisho vinavyochochea uzalishaji wa maziwa kwa kutumia lishe ya asili inayopatikana kwenye mazingira ya mfugaji na yenye gharama nafuu husaidia wafugaji kupata maziwa mengi kwa gharama ya chini. Ili virutubisho vya ziada kuwa na manufaa kwa ng’ombe ni lazima uwepo uwiano wa upatikanaji wa nishati, protini na madini.

Vyanzo vya wanga: Mahindi, makapi ya ngano, molasesi, pumba ya mahindi, na pumba ya ngano.
Vyanzo vya protini: Nyasi, mbegu za pamba, soya, mbegu za alizeti, majani ya sesbania, majani ya kaliandra, na dagaa.
Vyanzo vya madini: Kalishamu, fosifeti, mawe ya chokaa, pamoja na madini ya premix.

Namna ya kuchanganya virutubisho vya uzalishaji wa maziwa

1. Uzalishaji wa kawaida

Kufanya mchanganyiko wa kilo 100;
β€’ Kilo 75 ya lishe ya wanga
β€’ Kilo 23 ya lishe ya protini
β€’ Kilo 2 za madini

Kwa mfano;
β€’ Kilo 57 za mahindi
β€’ Kilo 18 za makapi ya ngano
β€’ Kilo 17 za lusina
β€’ Kilo 6 za soya
β€’ Kilo 2 za fosifeti

2. Uzalishaji wa maziwa kwa kiwango cha juu

Kufanya mchanganyiko wa Kilo 100;
β€’ Kilo 68 za lishe ya wanga
β€’ Kilo 30 za lishe ya protini
β€’ Kilo 2 za lishe ya madini

Kwa mfano;
β€’ Kilo 50 za mahindi
β€’ Kilo 16 za makapi ya ngano
β€’ Kilo 2 za molasesi
β€’ Kilo 14 za mbegu za pamba
β€’ Kilo 12 za lusina
β€’ Kilo 4 za dagaa

Faida za mchanganyiko unaotengenezwa kiasili

β€’ Una ubora sawa na lishe zinazouzwa.
β€’ Gharama yake ni ndogo ukilinganisha na lishe ya kununua.
β€’ Hukubalika kwa ng’ombe.
β€’ Ni rahisi kutunza na kutengeneza.

πŸ™‰πŸ™‰πŸ™‰Usisahau kushare posti hii kuhusu (Jinsi ya kuzalisha lishe kwa n'gombe wa maziwa kwa bei nafuu).πŸ‘ Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasomeπŸ’―βœ”


IMG_20170703_130425.jpg

Ujumbe wangu kwako kwa sasa

"Je wajua maelfu ya watu hutembelea blog hii kila mwezi.πŸ˜ƒ Kuwa miongoni mwao na wewe kwa kutembelea blog hii kila siku."

utotoni.gif

.

.

b.gif

Mimi ni Melkisedeck Shine Mmiliki, Mwandishi /Mhariri. Karibu tena kila siku.

Blog nyingine maarufu ndani ya AckySHINE.com

| Vichekesho | Videos | Picha | Ujasiriamali | Mahusiano | Kilimo & Mifugo | Katoliki | Afya & Mapishi | Hadithi | Misemo | SMS