Jinsi ya kutenganeza mbolea ya maji

By, Melkisedeck Shine.

vichekesho-bomba-vya-siku.png

Jinsi ya kutenganeza mbolea ya maji

Mkulima anaweza kupunguza gharama, kuongeza rutuba kwenye udongo, mavuno pamoja na kipato kwa kutengeneza mbolea mwenyewe.

Mimea inaweza kukuonyesha inahitaji nini. Ni rahisi sana kugundua endapo mimea haipati virutubisho vya kutosha. Majani kubadili rangi ni ishara tosha kuwa mimea ina upungufu wa virutubisho. Ni lazima mkulima awe tayari kutatua tatizo hilo kwa haraka kabla hali haijawa mbaya. Upungufu wa madini ya nitrojen na fosiforasi ni jambo la kawaida kwa mimea. Virutubisho hivi vinahitajik kwa kiasi kikubwa sana kwenye mimea hasa katika hatua ya ukuaji.

Hata hivyo, ni muhimu kuelewa kwamba utatuzi unategemea hatua za kutunza udongo kwa kipindi chote cha mwaka. Lisha udongo ili ulishe mazao yako; tumia mboji, samadi, mbolea vunde, matandazo na utaratibu mzuri wa kupanda mazao kwa mzunguko.

Kunyunyizia kunafaa zaidi

Mkulima anaweza kusaidia hatua hii ya kulisha mimea inayokuwa kwa njia ya kunyunyizia mbolea ya maji. Kunyunyizia inasaidia kuipatia mimea virutubisho moja kwa moja kupitia kwenye majani na shina.

Unaweza kuona matokeo mazuri ya kuweka mbolea kwa kunyunyizia kulingana na kiwango cha mavuno, uwezo wa mimea kukabiliana na wadudu pamoja na magonjwa, kuvumilia ukame, na kuongeza ubora wa mazao. Mimea inakuwa na uwezo wa kunyonya mbolea mara 20 zaidi ya unapotumia aina nyinginezo za uwekaji wa mbolea kwenye mimea.

Kutengeneza mbolea ya maji

Aina hii ya mbolea hutengenezwa kwa kuchukua kiroba kilichojazwa samadi, aina mbalimbali ya mimea yenye virutubisho na inayoaminika kuwa dawa ya mimea. Kiroba hicho kinafungwa kwenye kijiti, na kutumbukiza kwa kuningโ€™inia kwenye pipa lililojazwa maji. Kiroba hicho ni lazima kichukue kati ya kilo 30-50 za samadi pamoja na aina nyingine za mimea kwa maji lita 200 (tazama mchoro).

Mkulima anaweza kushika upande mmoja wa mti na kunyanyua na kushusha kila baada ya siku tano ili kuchanganya na kuharakisha kutolewa kwa virutubisho zaidi. Kwa kawaida mchanganyiko huo unakuwa na harufu kali sana maana Nitrojeni nyingi inayopatikana hugeuka kuwa Amonia. Ni vizuri kufunika pipa ili kuzuia kuyeyuka kwa nitrojeni. Harufu ikishaisha, ujue mbolea yako ipo tayari kwa matumizi. Ongeza maji na utingishe vizuri kabla ya kutumia. Nyunyizia mimea yako kila wiki mpaka utakapoona mabadiliko.

Tumia mimea peke yake

Kama unatengeneza mbolea ya maji kwa kutumia mimea peke yake, inashauriwa kutumia aina nyingi za mimea kama vile mivule, mibangi mwitu, majani ya minyanya, mwarobaini, mashona nguo, pamoja na vitunguu saumu. Aina hii ya mimea inasaidia sana katika kuzuia magonjwa, wadudu na kutoa virutubisho muhimu kwa mimea vinavyosaidia mkulima kupata mazao bora bila gharama ya ziada ya kununua virutubisho.

Vigezo vya kunyunyizia

Ili mbolea ya kunyunyizia iwe na matokeo mazuri, vigezo vifuatavyo vifuatwe:
โ€ข Inashauriwa kutumia mbolea iliyochanganywa vizuri ili kuepukana na kuunguza mimea.
โ€ข Acha maji utakayotumia kuchanganyia mbolea yako nje katika pipa lililowazi usiku kucha, hii inasaidia kutoa madini hatarishi, na kufanya mchanganyiko wenye faida kwa mimea.
โ€ข Tingisha vizuri. Chembechembe ndogo ambazo hazikuyeyuka zinaweza kuziba mdomo wa bomba la kunyunyizia.
โ€ข Matokeo mazuri yanaweza kupatikana endapo mbolea imechanganywa vizuri na kunyunyiziwa wakati hakuna upepo.
โ€ข Nyunyiza mbolea wakati wa asubuhi au jioni wakati hakuna joto na upepo ukiwa umepungua.

Jinsi ya kugundua upungufu wa virutubisho

Nitrogen

Dalili: Mahindi, maharage na mboga hukua kwa taabu sana, majani yanakuwa na kijani mpauko. Sukumawiki na kabichi majani yanakuwa na mchanganyiko wa rangi ya njano. Majani ya chini ndiyo huathiriwa kwanza, na kiwango cha maua kuchanua hupungua au kuchelewa.
Kutibu: Ongeza kiasi cha kutosha cha mbolea za asili. Panda mimea inayosaidia kuongeza nitrojen kama lablab, desmodium(figiri) na lusina. Weka mboji, samadi na mbolea ya maji yenye nitrojen kwa wingi.

Phosphorous

Dalili: Mahindi, maharage na mbogamboga haikui vizuri. Majani hugeuka na kuwa rangi ya kijani kama bluu na zambarau. Matunda hubakia kuwa madogo. Inaweza kuharibu mizizi au kukosekana kwa Nitrojeni.
Kutibu: Tumia mbolea ya Minjingu ambayo ina Phosphate, au tumia mbolea asili ya maji yenye phosphorus.

Potassium

Dalili: Majani yanakuwa na rangi ya njano kama yanakauka kuzunguka. Kuchanua kwa shida na kutokuwa mpango mzuri wa matunda. Mmea unashambuliwa na magonjwa kirahisi.
Kutibu: Boresha udongo wako kwa kutumia mimea yenye virutubisho vya potassium au weke majivu kwenye shamba lako.


Endelea kusoma makala hizi zifuatazo;

a.gif Jinsi ya kuzuia magonjwa ya kuku

Ufugaji wa kuku una faida kubwa, lakini mkulima anatakiwa kuzuia kadri awezavyo uwezekano wa kuwepo magonjwa shambulizi… soma zaidi

a.gif Jinsi ya Kulima karoti

Nimepanda karoti lakini sitaki kutumia dawa za viwandani kuua magugu mbali na kupalilia kwa mikono ni dawa gani za asili ninazoweza kutumia kuua magugu?.. soma zaidi

a.gif Jinsi ya kujumuisha miti shambani

Upandaji wa miti unalenga kupunguza madhara yanayotokana na uharibifu wa misitu, pamoja na kutumia ardhi kupita kiasi… soma zaidi

[Msemo wa Leo] ๐Ÿ‘‰Thamani ya faida

[Jarida la Bure] ๐Ÿ‘‰Jinsi ya kupika Biskuti za kokoa

[Hadithi Nzuri] ๐Ÿ‘‰Jinsi mke alivyotoboa siri ya Mmme wake

[SMS kwa Umpendaye] ๐Ÿ‘‰Meseji ya kumkaribisha mpenzi wako

a.gif Kwa nini watu wengine wanabaki maskini?

Sababu zifuatazo zinaweza kuwa na ukweli
mtupu;.. soma zaidi

a.gif Jinsi ya kupika kisamvu bila nazi

Kisamvu ni aina ya mboga ya majani inayopatikana kwa wingi na kwa urahisi katika mikoa takriban yote nchini Tanzania.
Pia aina hii ya mboga hupikwa katika mapishi ya aina mbalimbali kulingana na mahitaji ya mpishi… soma zaidi

a.gif Kampeni ya kutetea watoto yatima

Kampeni hii ilianzishwa na Melkisedeck Leon Shine mwaka 2018.
Lengo la kampeni hii ni kuhamasisha watu wote kusaidia kulea na kuwakuza watoto yatima kwa maendeleo bora ya kimwili, kiroho na kijamii kwa manufaa ya watoto wenyewe na kwa manufaa ya watu wote kwa sasa na kwa baadae.
Kampeni hii inaamini kuwa watoto yatima kama walivyo watoto wengine nao ni kama mali ambayo inawekezwa sasa kwa matumizi na maendeleo ya baadae. Japokuwa hawana (wazazi) watu/mtu rasmi wa kuwatunza haimaanishi kuwa hawawezi kuwa watu wa maana baadae… soma zaidi

a.gif Mapishi ya Pilau Ya Bilingani Na Kuku

Mchele wa basmati - 3 vikombe.. soma zaidi

a.gif Kazi ya Roho Mtakatifu.

Kazi ya Roho Mtakatifu… soma zaidi

afya-mapishi-na-lishe.png

.

familia-mapenzi-na-mahusiano.png
KADI-SHUKRANI-MZAZI.JPG
afya-mapishi-na-lishe.png

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.