.

misaadas.gif

πŸ‘‰ Jinsi ya kutambua magonjwa ya mbuzi wa maziwaπŸ‘‡βœ”

IMG_20170703_130425.jpg

Imehaririwa na; Melkisedeck Leon Shine. Tarehe 30 Jan 2016 04:17. [Legal & Authority]


Jinsi ya kutambua magonjwa ya mbuzi wa maziwa

Magonjwa Yanayowakabili Mbuzi Wa Maziwa
Unaweza kuhakikisha kuwa unawachunguza mbuzi wako mara kwa mara na kuwapa chanjo ili kuwakinga dhidi ya magonjwa,wadudu hatari na kuwalisha vyakula bora viliyvo na madini muhimu.

Baadhi ya magonjwa yanayowakabili mbuzi ni kama vile:

Ugonjwa Wa Heart Water
o Huu ni ugonjwa wa bacteria unaosababishwa na kupe
o Hata mbuzi wanaofanyiwa zero grazing wanaweza kumbukizwa ugonjwa huu.
o Dalili za ugonjwa huu ni pamoja na kufa kwa mbuzi wengi haswa wachanga,kupoteza hamu ya kula chakula,matatizo ya kupumua,na mara nyingi mbuzi huwa mnyonge.
o Ukiona dalili kama hizi mwite dakatari wa mifugo mara moja
o Waoshe mbuzi wako mara kwa mara ili kuwakinga dhidi ya kupe
Homa Ya Mapafu
o Ni ugonjwa wa kuambukiza mbuzi wakati mbuzi wenye afya nzuri wanapokaribiana na wale wagonjwa
o Dalili za pneumonia ni kama vile ongezeko la joto mwilini na matatizo ya kupumua na vifo kwa wingi haswa katika maeneo ambao ugonjwa huu umeenea
o Ukiona dalili hizi mwone daktari wa mifugo
o Wape chanjo mbuzi wako mara kwa mara
o Zingatia marufuku ya kusafirisha mifugo maarufu kama karantine na uhakikishe kuwa wanyama wamechunguzwa kabla ya kuwasafirisha ama kuhamishwa
Mastitis/Ugonjwa Wa Maziwa
o Kiwele au matiti huvimba na kuwa na uchungu na maziwa huwa na damu
o Ugonjwa huu waweza kuzuiliwa kupitia kudumisha usafi haswa wakati wa kukama maziwa
o Madaktari wa mifugo watakupa dawa aina ya anti biotic ya kupaka katika sehemu zilizoathiriwa.endapo mbuzi wako huambukizwa ugonjwa huu mara kwa mara ni vizuri umpe matibabu ya kutosha.
Rift Valley Fever
o Huu ni ugonjwa wa unaosababishwa na virusi vinavyosambazwa na mbu na hutokea sana sana wakati wa mvua wakati mbu wanapozaana kwa wingi.
o Watu na mifugo wanaweza kuambukizwa kwa kukanyaga kinyesi ama mkojo wa wanyama wagonjwa na kupitia kula ama kukanyaga nyama mbichi
o Dalili za ugonjwa huu ni pamoja na homa ya ghafla,kukosa hamu ya kula,kutoka kwa makamasi yaliyo na usaha puani,kutokwa na jasho jingi,kuhara,vifo visivyo vya kawaida kwa wanyama wachanga na kutoka/kuharibika kwa mimba
o Dalili hizi za ugonjwa huu hufanana na zile za magonjwa mengine na unapaswa kumwita daktari wa mifugo ili akuthibitishie
o Ugonjwa huu unaweza kuzuilika kupitia chanjo na kuwazuia mbu
Minyoo
o Hawa ni wadudu wanaokaa kwenye tumbo la mbuzi
o Huathiri uchangamufu wa mbuzi hususan wale wadogo ambao hufa ikiwa minyoo watakuwa wengi
o Wakati minyoo wanapozaana na kuwa wengine huamia kwenye mapafu na wanaweza kusababisha matatizo ya kupumua
o Minyoo wanaweza kuzuiliwa kwa kuwapa mbuzi dawa ya kuua minyoo mara kwa mara lakini ni muhimu kumshauri daktari wa mifugo kabla ya kuwapa dawa kwani dawa zingine huua aina nyingi ya minyoo huku zingine zikiangamiza aina moja pekee.
Kupe, Chawa, Viroboto
o Kupe huambukiza mbuzi magonjwa na ni vyema kuyazuia magonjwa haya
o Wadudu kama vile viroboto,chawa hufyonza damu na kuwasumbua mbuzi na kuwaathiri
o Tafuta ushauri kutoka kwa daktari wa mifugo kuhusu dawa unayopaswa kutumia kuwaua kupe katika eneo lako

Usisahau kushare posti hii Kwenye Mitandao ya Kijamii

wadogo.gif

.

.

.

Melkisedeck%20Shine.gif

b.gif

Mimi ni Melkisedeck Shine Mmiliki, Mwandishi /Mhariri.Soma%20Zaidi.gif

.

Wasiliana nami;

Kwa maoni, ushauri, nyongeza na hata salamu

Jina lako
Mawasiliano
Andika namba yako ya simu
Mahali unapotoka
Email
Ujumbe wako
Uwe Huru. Ujumbe huu ni siri yangu na wewe.

ABOUT AUTHOR | LEGAL GUIDELINES | CONSULT ME


images-10.jpeg

"Je wajua maelfu ya watu hutembelea blog hii kila mwezi.πŸ˜ƒ Kuwa miongoni mwao na wewe kwa kutembelea blog hii kila siku.."