Jinsi ya kupika vitumbua vizuri vitamu kwa ajili yako na familia yako kama kitafunwa cha asubuhi au wakati wowote

By, Melkisedeck Shine.

ISIKUPITE๐Ÿ‘‰ Mtafute ndugu yako mliopotezana

elimu-sayansi-na-tekinolojia.png

Jinsi ya kupika vitumbua vizuri vitamu kwa ajili yako na familia yako kama kitafunwa cha asubuhi au wakati wowote

Vitumbua ni vitafunwa vizuri na vinavyopendwa na wengi lakini ni wengi wasiojua kupika vitumbua japokua wanavipenda sana. Leo nimekuandalia namna rahisi ya kupika vitumbua kama ifuatavyo;

Mahitaji na Vipimo

Ukitaka kupika vitumbua unahitaji hivi vifuatavyo;

 1. Mchele ๐Ÿ‘‰ 2 mugs
 2. Tui la nazi ๐Ÿ‘‰ 2 mugs
 3. Yai ๐Ÿ‘‰ 1 kubwa
 4. Sukari ๐Ÿ‘‰ยฝ mug, unaweza kuongeza kulingana na ladha unayotaka
 5. Hiliki ๐Ÿ‘‰ ยฝ kijiko cha chai
 6. Hamira ๐Ÿ‘‰ ยฝ kijiko cha chai
 7. Unga wa ngano ๐Ÿ‘‰ 2 vijiko vya chakula
 8. Samli ya kupikia (au mafuta) ๐Ÿ‘‰ kiasi,

Kumbuka: Kikarai cha kukaanga vitumbua

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika/ kukaanga

Kutayarisha na kukaanga vitumbua ni kama ifuatavyo;

 1. Osha na loweka mchele kiasi masaa kuanzia mawili au zaidi.
 2. Saga mchele na tui kwenye mashine ya kusagia (blender) mpaka uwe laini usiwe na chenga.
 3. Tia hiliki, hamira na unga wa ngano saga tena mpaka uchanganyike.
 4. Mimina kwenye bakuli na uache uumuke kiasi.
 5. Ukisha kuumuka changanya sukari na yai
 6. Tumia kama kijiko 1-2 cha chai cha samli kwa kukaangia kila kitumbua.
 7. Mimina mchanganyiko kiasi kwenye kikarai maalumu cha kuchomea vitumbua. (Kikarai chenye vishimo)
 8. Kitumbua kikiiva upande mmoja, geuza upande wa pili mpaka kiwe tayari.
 9. Panga kwenye sahani. unaweza kula vitumbua vikiwa moto au vikipowa.

Vitumbua vyako vitakua tayari kwa kuliwa.


Endelea kusoma makala hizi zifuatazo;

a.gif Mahitaji na jinsi ya kupika uji wa ulezi kwa ajili ya watoto, wagonjwa na mtu yoyote

Uji wa ulezi ni kati ya vyakula vyenye nguvu na vinavyopendekezwa kutumiwa hasa kwa wagonjwa na watoto. Uji wa ulezi unapikwa hivi.. soma zaidi

a.gif Jifunze kitu hapa, watu mara nyingi wanaangalia ubaya wako na sio uzuri wako

#*LEO NILIINGIA DARASANI NIKAANDIKA UBAONI KAMA IFUATAVYO:*.. soma zaidi

a.gif Kama watu wanataka kuacha kuvuta sigara au kunywa pombe wafanyeje?

Kwanza kabisa, watu ni kweli wawe wamedhamiria kuacha.
Hii inataka uamuzi wa wazi na nia imara kwa sababu si rahisi
kuacha.
Pili, mtu anatakiwa kufikiria ni katika mazingira gani huwa
anajisikia kuvuta sigara au kunywa pombe. Hii kwa kawaida ni
pamoja na kundi maalumu la marafiki, katika sherehe, baada ya
kazi ngumu, baada au wakati wa kula. Kwa hiyo, kama wanataka
kuacha kuvuta sigara au kunywa pombe, wanatakiwa kubadili
mtindo wa maisha na kuepuka vishawishi.
Hatua ya kwanza katika kuacha kuvuta sigara au kunywa
pombe, inaweza ikawa ni kujiwekea malengo; kwa mfano, kuacha
kuvuta sigara kwa wiki nzima. Jipongeze kuwa umetimiza lengo
lako. Kama umeshindwa anza tena. Ni watu wachache ambao
wameweza kuacha kabisa katika jaribio la kwanza. Watu
wengine wanapata ugumu kuacha kabisa pombe na sigara… soma zaidi

a.gif Watu wafanye nini iwapo wamelazimishwa kufunga ndoa na mtu wasiyemtaka?

Iwapo mtu amelazimishwa
kuingia katika hali ya ndoa
(kuoa/kuolewa) na msichana/
mvulana ambaye hampendi,
hatua ya kwanza ni kukataa
ndoa hiyo na kuonyesha wazi
wazi. Jadiliana suala hili na
wazazi wako. Waeleze kwa
heshima kwa nini hukubaliani
na ndoa hiyo… soma zaidi

a.gif Mapishi ya Ugali Kwa Mchuzi Wa Nazi Wa Nyanya Chungu/Mshumaa/Ngogwe Na Bamia, Mboga Ya Matembele Na Samaki Wa Kukaanga

Unga wa mahindi - 4.. soma zaidi

a.gif Ushauri wa Imani ya dini kwa watu walio katika ndoa, wakati mmoja au wote wameambukizwa na HIV

๏‚ท Ombeni kwa pamoja kwa ajili ya hekima na ujasiri.
๏‚ท Amueni kwa pamoja, kwa msaada wa Mungu, kuwa
waaminifu wenyewe kwa wenyewe… soma zaidi

vichekesho-bomba-vya-siku.png

.

familia-mapenzi-na-mahusiano.png
nn.gif
afya-mapishi-na-lishe.png

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.