Tafuta

👉 JINSI YA KUPANDA MPUNGA KWA MBINU ZA KILIMO HAI👇✔

Chagua aina ambazo zinafaa kutumika katika mazingira husika.
Mpunga hujipevusha wenyewe. Hii inaruhusu kuchagua mbegu kutoka shambani kwako mwenyewe.
Usipure mbegu ambazo zinatumika wakati wa kusia
Mavuno ya kiangazi ni chanzo kizuri cha mbegu bora.
Tenga kilo 30 hadi 40 za mbegu kwa ajili ya kupanda hekta 1.

Kabla ya mbegu kuchipua:

Anza kutayarisha mbegu kabla ya mvua kuanza.
Mbegu zinazotoka kuhifadhiwa miezi 3 au zaidi zinahitaji kwanza kupashwa joto kwenye jua kwa masaa 3.
Ruhusu mbegu zipoe kabla ya kuziloweka kwa siku 1.
Ondoa mbegu zinazoelea.
Jaza mbegu nusu kiroba kwa ajili ya kuvundika kwa masaa 36. Kagua mbegu mara kwa mara ili joto lisipande sana kwenye jua.

Tengeneza matuta kupunguza upotevu wa udongo.
Epuka usumbuaji wa ardhi usio wa lazima.
Boresha rutuba na hifadhi ya udongo kwa kilimo mseto kwa kutumia mazao yatakayokuwa mbolea za kijani.
Zuia upungufu wa virutubisho kwa kuongeza mbolea za kilimo hai na fospheti ya mawe
Zuia ushindani wa magugu na mbegu zake kuongezeka kwa kufanya palizi ya mara kwa mara kwa muda sahihi.

Vuna pale tu mpunga utakapokuwa umekomaa.
Kupanda aina mchanganyiko kunaweza kusababisha shamba moja likawa na viwango tofauti vya kukomaa vya kukomaa.
Tandaza nafaka zisilundikane wakati wa kukausha kuzuia kuvu.
Tumia mashine sahihi za kukoboa ili kuhakikisha asilimia kubwa ya punje za mchele zinatoka nzima.
Mchele unatakiwa usiwe na makapi, mbegu za magugu na mawe ili kupata bei nzuri.

🙉🙉🙉Usisahau kushare posti hii kuhusu (JINSI YA KUPANDA MPUNGA KWA MBINU ZA KILIMO HAI).👍 Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasome💯✔

Umerahisishiwa kutafuta mliopotezana Ni rahisi sana kutafuta wale uwapendao

👉SOMA ZAIDI HAPA...

ndugu.gif

.