Tafuta

Mtafute ndugu yako mliopotezana Yupo hapa anakutafuta wewe

πŸ‘‰SOMA ZAIDI HAPA...

πŸ‘‰ Jinsi ya kuongeza uzalishaji wa Soya, mahindi na MtamaπŸ‘‡βœ”

Kujitayarisha kwa kupanda…

οƒΎ Badilisha soya na mahindi au mtama ili kuimarisha rotuba ya udongo na kuzuia magojwa.
οƒΎ Panda soya kwenye shamba lenye rotuba, lisilokuwa na vidimbwi au chemi chemi za maji.
οƒΎ Tayarisha shamba vyema kwa kuhakikisha kwamba hakuna kwekwe.
οƒΎ Tafuta mbolea aina ya SYMPAL (0-23-16+), ama mbolea inayofaa kwa upanzi wa soya yako.
οƒΎ Tafuta bacteria asilia (Biofix). Iweke mbali na jua na unyevu.
οƒΎ Tafuta aina ya soya iliyopendekezwa kupandwa katika eneo lako.
οƒΎ Jaribu mbegu ya soya kama inamea kabla ya kupanda ili kuthibitisha kwamba asilimia zaidi ya 80
inamea.

Wakati wa kupanda…

οƒΎ Panda kwa wakati ufaao, hakikisha mchanga una unyevu wa kutosha hasa sana wakati wa mvua za
mwanzo. Mizizi ya soya haiwezi kustahimili mchanga mkavu ama machanga wenye chemichemi.
οƒΎ Changanya soya na bacteria asilia (Biofix) huku ukifuata maagizo.
οƒΎ Panda mara moja baada ya kuchanganya bacteria ya asilia kwa nafasi ya sentimita 45 kwa pango hadi
jingine na sentimita 5 mmea hadi mmea mwingine.
οƒΎ Panda soya ukitumia mbolea ya SYMPAL kwa kiwango cha kilo 50 kwa ekari moja. Hakikisha ya
kwamba mbolea na mbegu haziguzani.

Wakati mmea ungali shambani…

οƒΎ Kagua shamba kila mara.Hakikisha kwamba hakuna kwekwe wadudu waharibifu na magonjwa.
οƒΎ Hakikisha ya kwamba shamba lako halina kwekwe kwa kupalilia vizuri na kwa wakati ufaao.
οƒΎ Tumia dawa iliyopendekezwa ya kuzuia magonjwa na wadudu.
οƒΎ Tumia dawa ya kuzuia magonjwa iliyopendekezwa, kwa kiwango kilichopendekezwa, wakati soya
inapoanza kuweka maua. Rudia kunyunyizia dawa, kulingana na maagizo, mara nyingi huwa siku 21
baada ya kunyunyiza mara ya kwanza.
οƒΎ Ikiwa wadudu wataonekana kwenye mmea, haipendekezwi kunyunyiza majani yaliyo athiriwa. Lakini
ikiwa mizoga imeliwa au maua, tafuta ushauri kabla ya kunyunyiza.
οƒΎ Weka rekodi za kilimo zikionyesha siku ya kunyunyiza, jina la mdudu, jina la dawa uliotumia na pahali
uliponyunyiza.

Wakati wa kuvuna…

οƒΎ Vuna mapema wakati asilimia 90 hadi asilimia 100 ya mizoga imekauka na kubadilika kuwa rangi ya
hudhurungi lakini kabla haijaanza kupasuka.
οƒΎ Kausha mmea uliovunwa kwenye jua. Zuia isinyeshewe na mvua.
οƒΎ Gonga soya na kuondoa uchafu ukiwa umeziweka mahali safi kama mkeka.
οƒΎ Ondoa uchafu kwa mbegu ya soya na ukaushe hadi mbegu ziwe na unyevu wa asilimia 11-12 kwa
sababu soya zilizo na unyevu zaidi ya asilimia 13% huenda zikaoza. Ukikausha zaidi ya asimilia 11
mbegu zitapasuka.
οƒΎ Hakikisha kwamba nafaka ya soya haina wadudu walio hai au harufu isiyo ya kawaida.
Kuhifadhi…
οƒΎ Weka soya iliyokauka kwenye gunia safi, usitumie gunia ya mbolea ama ya dawa ya wadudu au
iliyotumika kuweka kemikali zingine. Gunia ya mradi inaweza tumiwa zaidi ya mara moja.
οƒΎ Tunza/ hifadhi Soya mahali palipo kauka na penye hewa safi.
οƒΎ Peleka nafaka katika kituo cha ununuzi kwa wakati unaofaa.
οƒΎ Hakikisha maelezo yote katika gunia ni sawa, hasa tarehe, aina ya soya, mahali au sehemu na
mkulima.
οƒΎ Ruhusu siku saba ili upate malipo yako baada ya soya yako kukubalika kwenye kituo cha ununuzi.

Chanzo www.n2africa.org

πŸ™‰πŸ™‰πŸ™‰Usisahau kushare posti hii kuhusu (Jinsi ya kuongeza uzalishaji wa Soya, mahindi na Mtama).πŸ‘ Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasomeπŸ’―βœ”

Jinsi ya kutafuta ndugu zako mliopotezana Unaweza kuwatafuta kirahisi sana

πŸ‘‰SOMA ZAIDI HAPA...

Slide3-mliopoteana.GIF

.